Home

  • Mambo Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Excellence Advice For Living.

    1. Kuwa na shauku ni sawasawa na kuongeza 25% kwenye akili.
    2. Mara zote taka jambo la mwisho, kuwa na dead line kwa kila jambo.
    3. Samehee hii ni kwa ajili yako mwenyewe.
    4. Usipime maisha yako kwa kutumia rula ya mwingine.
    5. Sehemu kubwa ya kusafiri ni kuacha mambo mengi nyuma.
    6. Lengo bora unaloweka kwenye mwaka ni kujifunza kitu kimoja kwa kina zaidi.
    7. Maumivu hayakwepeki kuteseka ni kuchagua.
    8. Kama unatafuta kitu ndani alafu hukioni ukikipata usikirudishe hapo kirudishe ulipoanza kukitafuta.
    9. Unapaswa kuchagua kitu kimoja ambacho unachokitak zaidi ya vyote kukifanya.
    10. Njia bora ya kujifunza kitu ni kuwafundisha wengine.
    11. Kanuni ya ukuu ni kuwa bora zaidi kila siku alafu rudia kila siku.
    12. Unapokuwa njia panda chagua njia inayoleta mabadiliko.
    13. Unaweza kutegemea tabia zaidi kuliko hamasa.
    14. Unapaswa kutaka ushahidi usio wa kawaida ili upate matokeo yasiyo ya kawaida.
    15. Usiwe bora kuwa wa kipekee .
    16. Usichukulie binafsi, wachukulie kama wewe.
    17. Fanya kitu kizuri , na ufanye tena na tena na tena.
    18. Boresha akili yako, fikiria kwa miguu,fikiria kwa mikono, tembea, andika.
    19. Punguza orodha yako ya vitu unavyofanya.
    20. Wajibika kwa makosa yako.
    21. Weka nguvu zako kuwahudhumia wateja wako kuliko kushindana na washindani.
    22. Hapana ni jibu tosha.
    23. Kama huanguki mara kwa mara hutembei unazurura, au hujionei aibu kwa mambo ya zamani basi hukui.
    24. Asilimia 99 ya mafanikio ni kuongea na mteja, kumpigia simu, onekana mara zote.
    25. Usiwe na haraka, ukiwa na haraka ndio utaibiwa, utatapeliwa.
    26. Hakuna ukomo wa kuwa bora, kuna kitu cha kuboresha kila siku.
    27. Usipoteze changamoto , penye changamoto ni sehemu ya kukua na kupiga hatua.
    28. Wewe ni kile unachofanya.
    29. Angalia maslahi unapoomba ushauri.
    30. Jambo unaloliona ni la kitoto ndilo linaweza kukufanikisha, bobea kwenye kile unachokifanya.
    31. Ukikopesha kitu, chukulia unampa zawadi, kama hatarudisha hutaumia.
    32. Kuwekeza hela kidogo kunaleta miujiza.
    33. Usikubali haraka ya mtu iwe dharura. Fanya kulingana na umuhimu sio dharura.
    34. Ukiona mtu analazimisha kitu, jua Kuna uongo nyumba yake.
    35. Kama hujishangai yale uliyokuwa ukitenda uko nyuma, basi usishangae ya mwenzio.

    Rafiki tuifanyie kazi mambo haya na tutazidi kuwa bora kila siku kwenye maisha yetu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Umuhimu Wa Kupitia Magumu Kwenye Maisha.

    Rafiki yangu mpendwa dunia inakwenda kwa namna yake yenyewe hivyo matamanio yetu inaweza isiende kama tunavyotarajia.

    Hapa kuna njia tano za kutuwezesha kukabiliana na magumu kwenye maisha.

    1. Magumu siyo kisirani wala bahati mbaya ni sehemu ya maisha. Changamoto huwa ni funzo, kushindwa huwa ni mwalimu mzuri sana , magumu yanaimarisha sana akili zetu. Kwa kupitia kwenye changamoto tuchukue kwa upande chanya na tuone kuwa ni fursa ya kujifunza.
    2. Maisha yasiyokuwa na magumu hayanogi kujifunza au kufundisha wengine. Maisha yanakuwa imara kama utakutana na majaribu na kuyavuka. Huwezi kuwa na akili au bora kuliko wengine kama hujapitia magumu, magumu ni mtihani kaa chini tafuta tiba.
    3. Maumivu yanaimarisha kiroho. Chuma inaimarishwa na moto kwa kuondoa kila aina ya uchafuuchafu. Unaimarika na kujifanya ujifunze na kujiimarisha na kuwa na maandalizi bora kwako. Angalia kila changamoto na uone ni nini kimeongezeka kwako baada ya changamoto.
    4. Bila magumu hauwezi kuwa wa kweli. Maisha yanakuwa na furaha pale unapopitia magumu na kuyavuka. Kwa kupitia changamoto inadhihirisha kuwa wewe ni kiongozi, kila mafanikio ya mtu kuna historia ya magumu yake.
    5. Jinsi unavyochukuliana kukabiliana vema na linalokuja ndiyo uimara wako. Ni lazima uwe na maamuzi imara na utulivu wakati unatatua. Huhitaji hata kukimbilia au kukurupuka ni wewe utulie tu na na huenda yakaisha na pengine ukatatua kwa ubora ila tulia kwanza.

    Hatua ya kuchukua, rafiki jambo lolote linapotokea jiulize ni zuri au ni baya, naweza kuliathiri au siwezi kama huwezi achana nalo.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Njia 15 Za Kutumia Falsafa Ustoa Kuboresha Mahusiano Yetu Na Wengine.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini ikiwa unataka kuboresha mahusiano yako na wengine, falsafa ya ustoa inaweza kuwa mwanga mzuri.

    Hapa chini mna njia kadhaa unavyoweza kuitumia.

    1. Kuelewa na kukabiliana na wengine. Huwezi kubadilisha mtu bali ni kumuelewa na kukubali au kumkubali jinsi alivyo. Kwa hivyo pamoja na udhaifu wake Kuna kitu kizuri unachokipata. Usiangalie ubaya bali angalia ni kitu gani kizuri utapata kwake.
    2. Kudhibiti hisia na mawazo. Tunapaswa kudhibiti hayo ili kuweza kuishi na watu vizuri kama wivi,ghadhabu na mengine. Turuhusu hisia lakini ila tujicheleweshe kuchukua hatua fulani.
    3. Kuishi kwa maadili na heshima. Fanya kilichosahihi na kuheshimu . Tusitafute manufaa binafsi bali tumpe kila mtu heshima yake
    4. Onyesha huruma kwa wengine. Hasa wakati wa changamoto, tuwavumilie na kuwaelekeza wawe bora. Tuwape jukumu lililoko ndani ya uwezo wao.
    5. Thibiti matarajio ya wengine . Binadamu wanabadilika na kukugeuka.
    6. Ishi kwa amani iliyo ndani yako. Usikubali utawaliwe na furaha ya nje. Tegemea kupata wanyanganyi na wadhulumu.
    7. Kuwa mtu wa kuwajibika kwa matendo yako. Kuwa tayari kukiri makosa yako na kuwajibika kwa matendo yako. Uwe mfano wa wema .
    8. Kuepuka tabia zisizofaa. Kukosa maadili na udanganyifu. Mambo mengi yanayotokea siyo mabaya ni kujifunza kutokana na changamoto hiyo.
    9. Uzuri au ubaya wa kitu ni tafsiri ya mtu. Inategemea jinsi utakavyoichukulia.
    10. Ishi kadiri ya uwezo wako. Usiishi maisha ya juu kama kipato chako bado iko chini.
    11. Kukuza sehemu ya mahusiano. Tunaishi kwa kutegemeana katika umoja wa kijumuia. Huwezi ukawa bora ukiwa peke yako lazima uwe na uhusiano na watu.
    12. Usiruhusu mambo ya nje yakuumize.
    13. Jijali na kujipa muda. Watu wengi hawajijali wala hawajipi muda . Unapaswa kujipenda na ndipo uwapende wengine. Jitunze wewe mwenyewe kula vizuri, lala vizuri nk.
    14. Kubaliana na mabadiliko. Kukabiliana na mabadiliko ni sehemu nzuri hivyo pokea..
    15. Uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine.

    Chukua hatua, rafiki tutakuwa bora na tutakuwa na furaha pale tu tutakapokuwa na falsafa ya ustoa.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei .

  • Kwa Nini Watu Huchagua Raha Ya Muda Mfupi Badala Ya Mafanikio Ya Muda Mrefu?

    Swali hili linaakisi changamoto ya kisaikolojia na kijamii inayowakumba watu wengi.

    Kuna sababu kadhaa kwa nini watu huchagua raha ya muda mfupi badala ya mafanikio ya muda mrefu:

    1. Msukumo wa hisia za sasa: Akili ya binadamu hupendelea kuridhika kwa haraka (instant gratification). Raha ya muda mfupi huleta furaha ya papo hapo, ambayo mara nyingi huonekana kuvutia zaidi kuliko juhudi za muda mrefu.
    2. Hofu au kutojiamini: Watu wengine huona mafanikio ya muda mrefu kama jambo lisilo hakika au gumu kufikiwa, hivyo huamua kufurahia kilicho rahisi na hakikisho cha sasa.
    3. Mazingira ya kijamii: Tamaduni au marafiki wanaopenda raha za haraka (kama anasa au starehe za mara kwa mara) huweza kuwashawishi watu kupuuza mipango ya muda mrefu.
    4. Kutokuwepo kwa malengo au mwelekeo: Bila malengo madhubuti, mtu huishi maisha ya “kujaribu tu kufurahia sasa”, bila mpango wa baadae.
    5. Shinikizo la maisha: Watu wanaokumbwa na matatizo ya kiuchumi, msongo wa mawazo, au changamoto za kila siku wanaweza kuona raha ya muda mfupi kama njia ya kujituliza au kutoroka matatizo yao kwa muda.

    Hata hivyo, mafanikio ya muda mrefu yanahitaji uvumilivu, nidhamu, na uwezo wa kujizuia—mambo ambayo yanaweza kujengwa kwa mafunzo na tabia sahihi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya Kuongea Na Watu Uvae Viatu.

    Rafiki kabla hujajaribu kuuza chochote kwa mtu, jiulize kama ningekuwa mimi ndiye mteja, ningetaka kuskia nini? Hapo ndipo safari ya mauzo ya kweli inaanza, kwa kuvaa viatu vya mteja.

    1. Sikiliza kwa makini. Muache aongee hadi mwisho. Njia ya kumuondolea mteja maumivu yake ni kumsikiliza. Msikilize na kutambua hisia zake .
    2. Zungumza kwa lugha ya mteja. Jaribu kujua mteja wako anapendelea nini .
    3. Tumia maneno anayopenda mteja. Yafanye kutatua maumivu yao, watu hawawezi kununua kwa kulazimishwa. Uliza maswali ya kimkakati.
    4. Jenga mahusiano ya kabla ya mauzo. Katikati ya mauziano na baada. Waendelee kunufaika zaidi. Watu ni rasilimali nzuri sana wanaweza kukupandisha au kukushusha.
    5. Tumia hadithi za watu walionufaika kupitia huduma yako. Kwa kutumia shuhuda za wateja wengine utaweza kuwashawishi wengine wachukue hatua.
    6. Toa suluhisho bila kushinikiza. Kupitia suluhisho ndipo unapendekeza bidhaa zako kwa wateja.
    7. Jali maslahi ya wateja wako. Weka ubinadamu kwanza kabla ya mauzo. Wawezeshe kwanza kupata wanachokitaka ndipo umuuzie
    8. Shiriki nao katika matukio ya kijamii. Tumia mbinu ya kirafiki, Anza kuishi kama mtu anayejali na mwisho umkamilishe.
    9. Waambie watu kile unachokiuza. Kila unayekutana naye muambie kuhusu huduma yako.

    Chukua hatua: mteja hanunui bidhaa, ananunua suluhisho. Ili kuuza kwa mafanikio, vaa viatu vyake, uone kwa macho yake, na usikie kwa masikio yake.

    Usiuze tu, saidia. Mauzo ni huduma kwa uelewa.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Njia 7 Za Kuondokana Na Ukomo Wa Akili (Mental Limitations).

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kupunguza ukomo wa akili (mental limitations) kunahusiana na kuondoa imani, mawazo, au mitazamo inayokuzuia kufikia uwezo wako kamili.

    Hapa kuna njia 7 madhubuti za kufanya hivyo:


    1. Tambua Imani Zinazokuzuia (Limiting Beliefs)

    Mfano: “Siwezi kufanya hivi”, “Mimi si mzuri vya kutosha”, “Niliwahi kushindwa”

    Hatua ya kuchukua:

    Andika imani hizo.

    Jiulize: “Je, hii ni kweli kabisa?”

    Badilisha kwa maneno chanya: “Ninajifunza na ninazidi kuwa bora kila siku.”


    1. Jifunze Mambo Mapya Kila Mara

    Kujifunza ni dawa ya ukomo wa fikra.

    Soma vitabu vya kujitambua na maendeleo binafsi

    Tazama video za elimu na motisha

    Jiunge na semina au vikundi vya watu wenye mawazo chanya


    1. Jizungushe na Watu Wenye Maono Makubwa

    Mazingira ya kiakili ni muhimu.

    Tafuta marafiki au mento wanaokutia moyo

    Epuka watu wanaokushusha au kukukatisha tamaa.


    1. Chukua Hatua Ndogo Kila Siku

    Ukomo huishi pale unapochukua hatua.

    Lenga mafanikio madogo kila siku

    Kubali makosa kama sehemu ya kujifunza.


    1. Fanya Mazoezi ya Kujiamini (Self-Affirmations)

    Kila siku, sema maneno chanya kama:

    “Nina uwezo wa kushinda changamoto.”

    “Kila siku ninakuwa bora zaidi.”


    1. Tafakari (Meditation) na Kuandika (Journaling)

    Tenga dakika 5–10 kwa siku kufikiri kimya kimya na kutafakari

    Andika mawazo yako, mafanikio yako ya siku, na malengo yako


    1. Kumbuka: Ukomo Nyingi Tunaweka Sisi Wenyewe

    Kifungo kibaya zaidi ni kile ambacho akili yako imekubali bila kupinga.


    Chukua hatua: rafiki ukomo mkubwa zaidi haupo kwenye mazingira yetu, bali katika akili zetu.

    Ukishaamua kubadilika ndani yako, hakuna kinachoweza kukuzuia nje yako.

    Kumbuka: Kila siku unayoishi ni nafasi mpya ya kuvunja mipaka ya fikra na kujenga toleo jipya la wewe mwenye nguvu,imani, na maono makubwa zaidi.

    Najiamini. Najichochea . Najivunja. Najitimiza.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei .

  • Mambo 10 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Sales Like Crazy By Sabri Suby.

    Rafiki yangu mpendwa kitabu hiki ni mwongozo wenye nguvu kwa mtu yeyote anayetaka kuongeza mauzo kwa njia ya mtandao.

    Kinafundisha mbinu halisi za uuzaji wa kijidali zinazoweza kutumika mara moja.

    Hapa kuna mambo kumi ya kujifunza na kufanyia kazi.

    1. Toa thamani kwanza ( value first). Usianze kuuza moja kwa moja. Toa kitu cha bure chenye msaada, kama ebook, video au kozi, ili kuvutia na kuvuta imani ya wateja.
    2. Elewa wateja wako vizuri. Fahamu matatizo yao, na lugha wanayotumia. Hii itasaidia kuwasiliana kwa njia inayogusa hisia zao.
    3. Tengeneza ofa isiyozuilika (irresistible offer). Ofa yako inapaswa kuwa na thamani kubwa kiasi kwamba mteja hawezi kusema ‘hapana.’
    4. Tumia mfumo wa mauzo ( sales funnel). Anzisha mahusiano na mteja hatua kwa hatua , kutoka kupata taarifa zao, hadi kuwafanya wanunue mara ya kwanza, hadi kuwa wateja wa kudumu.
    5. Onyesha uthibitisho wa kijamii ( social proof). Weka ushuhuda kutoka kwa wateja waliopita, matokeo waliopata, na idadi ya watu wanaonufaika.
    6. Weka udharura ( Urgency) na Uhaba (Scarcity). Toa ofa kwa muda maalum au kwa idadi ndogo ili kuhimiza watu kuchukua hatua haraka.
    7. Tangaza kwa makini. (Targeted Ads). Tumia matangazo ya kulenga ( Facebook, google n.k) kuwafikia watu wanaohitaji kile unachotoa, sio kila mtu.
    8. Andika matangazo yenye nguvu ( compelling copywriting). Matangazo yako yawe na kichwa kinachovutia, suluhisho kwa shida ya mteja, na wito wa kuchukua hatua ( call to action).
    9. Pima na boresha ( track and optimize). Pima kila kitu, matangazo, email,faneli, na ubadilishe kile kisichofanya kazi. Takwimu ni mwongozo wako
    10. Kuwa Na mfumo, sio bahati. Badala ya kutegemea ‘bahati ‘ kupata wateja, jenga mfumo wa kila siku unaoleta wateja wapya kwa kuuza kwa ufanisi.

    Chukua hatua, kwa kuzingatia mambo haya kumi na kufanyia kazi utaweza kupata wateja tarajiwa, kufanya mauzo na kugeuza hao wateja tarajiwa kuwa wateja kamili.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 20 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Tano Za Juma Na Kocha Makirita Amani.

    Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze kuhusu maisha na mafanikio kutoka kitabu hiki kizuri.

    1. Usikosee wito wako. Fanya kile ambacho umeumbwa kufanya kile unafurahia kufanya kwa sababu ni wito wako.
    2. Chagua eneo sahihi. Chagua eneo ambalo ukiwa unafanya jukumu lako haivurugi sana mambo yako.
    3. Epuka madeni. Madeni yanaturudisha nyuma. Epuka sana kuingia kwenye madeni kwa sababu utakuwa mtumwa wa kulipa madeni kila wakati.
    4. Kuwa mvumilivu. Huwezi kufanikiwa kwenye maisha kama huna uvumilivu. Kuna wengi ambao wameanzia chini sana wakavumilia hadi wamepata mafanikio.
    5. Fanya kwa nguvu zako zote. Fanya kazi kwa bidii kwa nguvu zako zote. Kazi ndiye rafiki wa kweli, atakufikisha mbali na kukukutanisha na watu wengi zaidi.
    6. Usitegemee juhudi zako binafsi. Huwezi kufanikisha kila kitu peke yako, hata wengine wana mchango.
    7. Tumia dhana Bora. Chagua dhana bora zitakazokusaidia kufikia mafanikio unayoyataka. Jifunze kutumia mashine mbalimbali zitakazokusaidia kurahisisha kazi yako.
    8. Usiende juu ya biashara yako. Usiishi nje ya kipato chako, watu huwa wanapenda kuanzia juu, wengi hawapendi kuanzia chini. Mara nyingi anzia kwenye level ya kawaida.
    9. Jifunze kitu chenye manufaa. Ukiwa na ujuzi fulani utaweza kuendesha maisha yako. Kuna msemi unaosema ‘mwenye ujuzi halali njaa.’
    10. Ongozwa na matumaini lakini usiwe na haraka na uhakika wa kupitiliza. Usihesanu kuku kabla mayai hayajaanguliwa.
    11. Usitawanye nguvu zako zote.Ukiweza kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu utaweza kufanya makubwa, yaani unakuwa bora kabisa unapofanya kitu kimoja. Chagua eneo moja kuu na ufanye bila kuacha.
    12. Kuwa na utaratibu katika kile unakifanya. Panga utaratibu wa kufuatwa, unapunguza makosa wa kujirudia mara kwa mara.
    13. Soma magazeti au vitu mbalimbali . Kuwa tayari kujifunza kuhusu biashara, maendeleo binafsi na uchumi. Ili kuwa na uelewa wa kile kinachoendelea.
    14. Kuwa makini na kazi za nje. Wale wanaokuzunguka ndio wanaokupoteza zaidi. Epuka ushauri ya watu huku nje kwa sababu hajui kwamba wewe unafanya kazi ya wito wako.
    15. Usimthamini mtu bila amana. Usimwamini mtu au kumpa nafasi ya kipekee bila kujiridhisha kuwa anastahili, kupitia matendo,tabia au historia yake.
    16. Tangaza biashara yako. Iweze kuwafikia watu wengi zaidi na wajue uwepo wako.
    17. Kuwa mpole na mkarimu kwa wateja na watu wako wa karibu. Ni sababu moja ya mtu kukukumbuka kuwa umemtoa katika nyakati ngumu.
    18. Toa msaada. Kwa wenye uhitaji lakini pia kuwa makini kwa wale wale unaowasaidia. Kutoa msaada unakusadia pia.
    19. Usiwe mpayukaji. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na utulivu kidogo. Ukimya ni silaha ya mafanikio. Usiwaambie watu kile unachotaka kufanya kabla hajafanya
    20. Tunza uadilifu wako. Watu wakisha jua wewe sio mwadilifu tena hawataweza kukuamini tena.

    Chukua hatua, kwa kufanyia kazi mambo 20 utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako na kupata mafanikio unayoyataka kwenye maisha yako.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei .

  • Mambo Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Retire Before Mam And Dad Na Rob Berger.

    Rafiki karibu kitabu hiki kinatoa mwongozo wa kipekee wa kifedha kwa mtu yeyote anayetaka kupata uhuru wa kifedha mapema, kabla hata ya wazazi wao kustaafu.

    Hapa kuna mambo makuu ya kujifunza kutoka kitabu hiki:

    1. Uhuru wa kifedha unaanza na mtazamo sahihi. Badala ya kulenga ‘kuwa tajiri’ lenga kuwa uhuru wa kifedha. Huru kifedha una uhuru wa kuchagua namna unavyoishi bila kutegemea mshahara wa kila mwezi.
    2. Kiasi unachoweka akiba ni muhimu kuliko mapato. Usisuburi kuwa na kipato kikubwa ndipo uanze kuwekeza. Fanya akiba kuwa kipaumbele hata 1% ya mapato yako ni mwanzo nzuri. Malengo weka 10% , kisha polepole ongeza hadi 20-30% au zaidi.
    3. Weka bajeti ya maisha inayoakisi vipaumbele vyako. Tumia pesa kwenye vitu vinavyokuletea furaha ya kweli, sio tu fahari. Epuka deni la matumizi kama mikopo ya kadi ya mkopo. Bajeti sio kizuizi, bali ni chombo cha uhuru.
    4. Muda na riba ya mchanganyiko ( compound interest). Kuanzisha uwekezaji mapema kuna faida kubwa, muda ni rafiki yako.
    5. Epuka mitego ya kifedha ya kawaida. Kuishi kwa ‘status’ au mashindano na wengine. Kuchelewesha uwekezaji kwa sababu ya hofu au kutokujua. Kuwa na malengo bila mpango wa utekelezaji.
    6. Fanya uwekezaji rahisi na thabiti. Hakuna haja ya kuwa na akili ya wall street. Hakikisha unaelewa unachowekeza, usiweke pesa mahali kwa sababu tu watu wanasema.
    7. Hatua ndogo ndogo, matokeo makubwa. Anza leo, hata kama ni kwa kiwango kidogo. Shinda tabia mbaya kifedha kidogo kidogo. Weka mfumo wa kufuatilia maendeleo net worth tracker.
    8. Uhuru wa kifedha siyo mwisho, ni njia ya maisha. Lengo si tu kuacha kazi mapema, bali kuwa na uhuru wa kuchagua maisha unayotaka. Unaweza kuendelea kufanya kazi unayopenda, bila kulazimishwa na fedha.

    Chukua hatua. Uhuru wa kifedha si kwa matajiri tu, ni kwa mtu yeyote aliye tayari kuchukua hatua ndogo leo kwa ajili ya maisha makubwa kesho.

    Kipato chako sio kizuizi, bali maamuzi yako ya kila siku ndiyo yanayoamua hatima yako.

    Tunakumbushwa kuwa mafanikio ya kifedha si swala la kuwa na pesa nyingi mwanzoni, bali ni juu ya tabia, nidhamu, na kujitolea kwa muda mrefu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 10 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Quit Like A Millionaire Na Kristy Shen Na Bryce Leung.

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana tujifunze mambo kumi ya kufanyia kazi kama tunataka kufikia uhuru wa kifedha.

    Kwa kupitia njia isiyo ya kawaida na kuishi maisha ya kujitegemea kifedha.

    1. Uhuru wa kifedha siyo kwa matajiri tu. Kitabu kinaonyesha kuwa mtu yeyote, hata asiye na asili ya utajiri, anaweza kufikia uhuru wa kifedha kwa maamuzi bora na nidhamu ya kifedha.
    2. Matumizi makini ni muhimu kuliko kipato kikubwa. Si lazima uwe na mshahara mkubwa ili kuwa millionea. Kilicho muhimu ni jinsi unavyotumia kile ulichopata.
    3. Fikra sahihi kuhusu pesa. Watu wengi hukosa uhuru wa kifedha kwa sababu ya mitazamo potofu kuhusu pesa. Kitabu kinahimiza kubadili mtazamo huo.
    4. Elimu ya kifedha ni nguvu. Kujua kuhusu uwekezaji, ushuru, na usimamizi wa pesa kunaleta tofauti kubwa kwenye maisha yako.
    5. Uwekezaji kwenye soko la hisa ni njia nzuri ya kujenga utajiri. Waandishi walitumia mbinu za uwekezaji kama “index investing” kujenga utajiri wao.
    6. Wekeza mapema na mara kwa mara. Kitabu kinasisitiza umuhimu wa kuanza kuwekeza mapema, hata kwa kiasi kidogo, na kuendelea mara kwa mara.
    7. Kuepuka mtego wa maisha ya kifahari. Unapopata pesa zaidi, usikimbilie kuishi maisha ya kifahari. Kuongeza matumizi mara moja si njia ya kuwa huru kifedha.
    8. Hofu ni adui wa mafanikio ya kifedha. Wengi huogopa kuacha kazi au kuwekeza. Kitabu kinashauri kuchukua hatua kwa kuelimika na kuwa na mpango thabiti.
    9. Kujua gharama ya maisha yako halisi. Fuatilia matumizi yako na ujue kiwango halisi cha pesa unachohitaji kuishi maisha unayotaka.
    10. Uhuru ni muhimu kuliko hadhi. Kuwa na uhuru wa muda na maisha yenye amani ni bora kuliko hadhi ya kazi au maisha ya kifahari yaliyojaa presha.

    Chukua hatua rafiki yangu kwa kufuata mambo huu na kufanyia kazi tutaweza kufikia uhuru wa kifedha.

    Waandishi hao wawili wa kitabu hiki wamesema kuwa utajiri sio suala la kipato pekee, bali ni jinsi unavyofikiri na kutumia pesa. Kuwa na nidhamu, kujifunza kila siku, na kukwepa mitego ya matumizi ni hatua muhimu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.