Umuhimu Wa Kupitia Magumu Kwenye Maisha.

Rafiki yangu mpendwa dunia inakwenda kwa namna yake yenyewe hivyo matamanio yetu inaweza isiende kama tunavyotarajia.

Hapa kuna njia tano za kutuwezesha kukabiliana na magumu kwenye maisha.

  1. Magumu siyo kisirani wala bahati mbaya ni sehemu ya maisha. Changamoto huwa ni funzo, kushindwa huwa ni mwalimu mzuri sana , magumu yanaimarisha sana akili zetu. Kwa kupitia kwenye changamoto tuchukue kwa upande chanya na tuone kuwa ni fursa ya kujifunza.
  2. Maisha yasiyokuwa na magumu hayanogi kujifunza au kufundisha wengine. Maisha yanakuwa imara kama utakutana na majaribu na kuyavuka. Huwezi kuwa na akili au bora kuliko wengine kama hujapitia magumu, magumu ni mtihani kaa chini tafuta tiba.
  3. Maumivu yanaimarisha kiroho. Chuma inaimarishwa na moto kwa kuondoa kila aina ya uchafuuchafu. Unaimarika na kujifanya ujifunze na kujiimarisha na kuwa na maandalizi bora kwako. Angalia kila changamoto na uone ni nini kimeongezeka kwako baada ya changamoto.
  4. Bila magumu hauwezi kuwa wa kweli. Maisha yanakuwa na furaha pale unapopitia magumu na kuyavuka. Kwa kupitia changamoto inadhihirisha kuwa wewe ni kiongozi, kila mafanikio ya mtu kuna historia ya magumu yake.
  5. Jinsi unavyochukuliana kukabiliana vema na linalokuja ndiyo uimara wako. Ni lazima uwe na maamuzi imara na utulivu wakati unatatua. Huhitaji hata kukimbilia au kukurupuka ni wewe utulie tu na na huenda yakaisha na pengine ukatatua kwa ubora ila tulia kwanza.

Hatua ya kuchukua, rafiki jambo lolote linapotokea jiulize ni zuri au ni baya, naweza kuliathiri au siwezi kama huwezi achana nalo.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment