Rafiki kabla hujajaribu kuuza chochote kwa mtu, jiulize kama ningekuwa mimi ndiye mteja, ningetaka kuskia nini? Hapo ndipo safari ya mauzo ya kweli inaanza, kwa kuvaa viatu vya mteja.
- Sikiliza kwa makini. Muache aongee hadi mwisho. Njia ya kumuondolea mteja maumivu yake ni kumsikiliza. Msikilize na kutambua hisia zake .
- Zungumza kwa lugha ya mteja. Jaribu kujua mteja wako anapendelea nini .
- Tumia maneno anayopenda mteja. Yafanye kutatua maumivu yao, watu hawawezi kununua kwa kulazimishwa. Uliza maswali ya kimkakati.
- Jenga mahusiano ya kabla ya mauzo. Katikati ya mauziano na baada. Waendelee kunufaika zaidi. Watu ni rasilimali nzuri sana wanaweza kukupandisha au kukushusha.
- Tumia hadithi za watu walionufaika kupitia huduma yako. Kwa kutumia shuhuda za wateja wengine utaweza kuwashawishi wengine wachukue hatua.
- Toa suluhisho bila kushinikiza. Kupitia suluhisho ndipo unapendekeza bidhaa zako kwa wateja.
- Jali maslahi ya wateja wako. Weka ubinadamu kwanza kabla ya mauzo. Wawezeshe kwanza kupata wanachokitaka ndipo umuuzie
- Shiriki nao katika matukio ya kijamii. Tumia mbinu ya kirafiki, Anza kuishi kama mtu anayejali na mwisho umkamilishe.
- Waambie watu kile unachokiuza. Kila unayekutana naye muambie kuhusu huduma yako.
Chukua hatua: mteja hanunui bidhaa, ananunua suluhisho. Ili kuuza kwa mafanikio, vaa viatu vyake, uone kwa macho yake, na usikie kwa masikio yake.
Usiuze tu, saidia. Mauzo ni huduma kwa uelewa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.