-
Sifa 10 Za Kuangalia Unapomwajiri Mtu Wa Mauzo.
Rafiki yangu mpendwa kuajiri mtu wa mauzo ni hatua muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
Hapa kuna sifa za msingi unazopaswa kuzingatia;
- Uwezo wa kuwasiliana. Awe na ustadi mzuri wa kuzungumza na kuandika. Aweze kueleza faida za bidhaa au huduma kwa ufasaha.
- Ushawishi na ujuzi wa kujadiliana. Awe na uwezo wa kumshawishi mteja kufanya manunuzi. Aweze kushughulikia upinzani wa mteja kwa busara.
- Ujuzi wa mahusiano ya watu. Awe na uwezo wa kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wateja. Awe na tabia ya kirafiki na uvumilivu.
- Uelewa wa bidhaa au huduma. Awe na uwezo wa kujifunza haraka kuhusu bidhaa au huduma unazouza. Aweze kueleza thamani ya bidhaa kwa mteja kwa ufanisi.
- Uzoefu wa mauzo ( si lazima lakini ni faida). Ikiwezekana awe na uwezo wa kufanya mauzo katika sekta husika. Awe na rekodi nzuri ya kufanikisha mauzo katika kazi za awali.
- Motisha ya ndani na bidii. Awe na malengo binafsi na awe tayari kufanya kazi kwa bidii kuyafanikisha. Awe mtu mwenye juhudi na msukumo wa ndani wa kufanikiwa mauzo.
- Uwezo wa kufanya kazi kwa shinikizo. Aweze kushughulikia changamoto za mauzo bila kukata tamaa. Awe na ustahimilivu wa kushughulika na wateja wagumu.
- Ujuzi wa matumizi ya teknolojia. Awe na uelewa wa matumizi ya kompyuta, program za mauzo, na mitandao ya kijamii ( kama inahitajika). Awe na uwezo wa kutumia CRM (customer relationship management) ikiwa biashara inatumia.
- Ubunifu na uwezo wa kutatua matatizo. Aweze kubuni mbinu mpya za kuvutia wateja. Awe na uwezo wa kushughulikia malalamiko ya wateja kwa njia chanya.
- Uaminifu na nidhamu. Awe mwaminifu kwa biashara yako na awe na maadili mazuri ya kazi. Awe na nidhamu ya kufuata maelekezo na kufanikisha malengo ya mauzo.
Kwa kuzingatia sifa hizi utaweza kupata mtu sahihi wa kufanya mauzo na kuweza kushawishi wateja kukamilisha mauzo.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 5 Ya Kusema Hapana Ambayo Hayana Mchango Kwenye Maisha Yako Na Mafanikio Yako.
Rafiki yangu wanasema ni kwenye muda pekee ndipo penye demokrasia ya kweli duniani. Ndiyo kitu pekee ambacho tumepewa kwa usawa.
Kwa kuwa tumepewa kwa usawa, ila wapo ambao wanafanya makubwa sana kwenye muda huo huo, ina maana kuna vitu wanafanya kwa utofauti.
Dr Kocha Makitita Amani anasema kuwa siri kuu ya kutumia muda vizuri ni kusema hapana kwenye mambo yote ambayo hayana mchango kwenye maisha yako na mafanikio unayotaka.
Mambo hayo ni kama yafuatayo ;
- Kufuatilia habari kwa tv, redio magazeti na vyombo vingine vya habari.
- Matumizi ya mitandao ya kijamii, hii inaleta urahibu wa kuzurura na hamu ya kutaka kujua ni nini jipya kimetokea, watu wengi kwa kufanya hivyo wanajipata wakipoteza muda wao mwingi bila kufanya chochote cha maana.
- Ushabiki wa michezo wa aina yoyote ile, Kocha anasema kwa kuwa mrahibu wa kufuatilia michezo mbalimbali unajipata umepoteza muda wako mwingi.
- Vikao visivyo vya lazima vya jamii na familia. Ukiwa mtu wa kufuatilia na kuhudhuria vikao mbalimbali kwenye jamii hutakuwa na muda wa kutosha wa kufanya shughuli zako za maendeleo.
- Ulevi na starehe mbalimbali . Ukiwa mtu unayependa starehe za anasa na pia kuzungukwa na marafiki wanaopenda starehe kama hizo utajipata hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua; rafiki kwa kusema hapana kwenye hayo, unabaki na muda mwingi ambao unaweza kuutumia kwenye mambo yenye tija zaidi.
Tunapaswa kuilinda sana muda wetu, kwa kutumia neno hapana kwa yote yasiyokuwa na mchango kwenye mafanikio unayoyataka.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 10 Muhimu Kuhusu Kazi.
Rafiki yangu mpendwa kazi ni asili ya wanadamu. Siyo adhabu, kazi ni zawadi toka kwa Mungu, mtu asiyetaka kufanya kazi na asile chakula.
Kazi bora zaidi kuliko zingine ni ile ambayo unaifanya. Fikra na mtazamo wako ndiyo kazi bora unayoifanya.
Mambo kumi kuhusu kazi ni kama yafuatayo;
- Ipende kazi. Kazi yoyote unayoifanya ipende. Ifanye kwa hamasa na utapata mafanikio. Kazi ukiipenda nayo itakupenda. Ukiipenda itakua bora sana.
- Kuwa wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka. Kufanya hivyo itakutofautisha na wengine.
- Unapofanya kazi fanya kazi usihangaike na mambo mengine. Heshimu kazi yako na kuipenda.
- Fanya kazi mbili ya muda ambao wengine wanafanya kazi. Utapata matokeo mara mbili ya wengine . Rafiki pekee anayeweza kukupa msaada mkubwa ni kazi.
- Wanaokuambia unafanya kazi sana, jua hao hawafanyi kazi. Hao wanaokuambia huwa unafanya kazi sana wana wivu ila hawawezi kufanya kama wewe.
- Usiseme sio jukumu langu au siwezi kufanya. Ukipewa jukumu iwe unaweza au hujui kufanya pokea na jifunze namna ya kufanya na fanya.
- Kila siku ni siku ya kazi. Kama jua linachomoza basi ujue ni siku ya kazi kwako. Kila siku amka na hamasa ya kazi. Hakuna siku huli chakula.
- Usilalamike kuwa una kazi nyingi. Kuna wengine hawana kazi kabisa na hawajui wafanye nini. Shukuru na usilalamike.
- Usijidanganye kwamba unamfanyia mtu kazi. Kama ukifanya kazi bora utajijengea thamani kubwa sana. Mtu wa kwanza unayemfanyia kazi ni wewe mwenyewe.
- Kufia kazini ni ushujaa. Ondokana na mawazo ya kukimbia kazi bali weka kazi na jenga urafiki na kazi.
Chukua hatua rafiki yangu tunapaswa kupenda kufanya kazi kwa sababu kazi inatutambulisha kwa watu. Tukifanya kazi kwa bidii tutaheshimika zaidi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
-
Njia 5 Za Kukuwezesha Kuwa Wewe Kwenye Jamii Ya Kisasa.
Kuwa wewe mwenyewe katika jamii ya kisasa kunahitaji uwiano kati ya kujielewa, kukubali mabadiliko, na kushikilia misingi yako.
Hapa kuna njia tano za kufanikisha hilo;
- Kujitambua na kujiamini. Fahamu thamani zako, malengo yako na kile unachokipenda. Usiogope kuwa tofauti kwani ndiyo kunakokufanya kuwa wa kipekee. Jifunze kujikubali na kuepuka kulinganisha maisha yako na ya wengine.
- Endelea kujifunza na kukua. Dunia inabadilika haraka, hivyo endelea kusoma, kusikiliza na kujifunza. Jifunze kuhusu teknolojia,utamaduni, na mienendo bila kupoteza utu wako. Chagua habari na mitazamo inayokuza maarifa yako badala ya kuathiri vibaya mtazamo wako.
- Dumisha mahusiano na uhalisia. Kuwa na mazungumzo ya kweli na maana na marafiki,familia na jamii. Tumia mitandao ya kijamii kwa hekima, usiruhusu maisha ya mtandaoni yakufanye upoteze uhalisia wako. Dumisha maadili yako hata kama dunia inabadilika.
- Kubali mabadiliko lakini chuja mengine. Sio kila kitu cha kisasa kinafaa kwako; chagua kile kinachoendanaa na thamani yako. Jifunze kubadilika bila kupoteza msingi wa utu wako. Usiogope kusema ‘hapana’ kwa shinikizo la jamii ikiwa haliendani na wewe.
- Tumia teknolojia kwa manufaa yako. Badala ya kuwa mtumwa wa teknolojia, itumie kukuza elimu, biashara, na ubunifu wako. Dumisha uwiano mzuri kati ya muda wa mtandaoni na maisha halisi.
Chukua hatua; kuwa wewe kwenye jamii ya kisasa unahitajika kuchangamka, lakini pia kubaki na msingi wako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 10 Ya Kuzingatia Wakati Kipato Kinapoongezeka.
Rafiki yangu kipato kinapoongezeka matumizi yanapaswa kutoongezeka .
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia;
- Tengeneza bajeti mpya iwe chini ya bajeti yako. Mapato yawe chini ya kipato chako.
- Weka akiba kwanza kabla ya kufanya matumizi.
- Kutenga sehemu ya kipato kwa ajili ya uwekezaji.
- Kuzuia matumizi ya anasa . Lazima nijiuliza swali kabla ya kufanya manunuzi ya anasa kama vile, je! ni ya lazima?
- Epukana na shinikizo la kijamii. Usinunue kitu ili kufurahisha wengine.
- Tumia kanuni ya 50/30/20 au 50/10/10/10/10/10 . Lengo ni kuwa na udhibiti.
- Kuweka malengo ya muda mrefu.
- Jifunze kuhusu usimamizi wa fedha binafsi .
- Jipe muda kabla kufanya maamuzi ya kununua weka delay kidogo.
- Fedha inayokuja iingie kwenye mfumo. Tamaa na hofu kinakuja.
Chukua hatua; rafiki kwa kuzingatia mambo haya utaweza kudhibiti matumizi na utaweza kuokoa fedha kwa ajili ya kuweka akiba na kufanya uwekezaji.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Katika Kuukabili Ugumu Wa Maisha, Falsafa Ya Ustoa Inasisitiza Mambo 6 Yafuatayo:
Rafiki yangu mpendwa falsafa ya ustoa ni mtazamo wa kifikra unaohimiza uvumilivu, nidhamu ya kihisia, na kuukabili ukweli wa maisha kwa utulivu.
Mambo hayo 6 ya kuzingatia katika kuukabili ugumu wa maisha ni kama;
- Kubali kile usichoweza kudhibiti. Maisha yana changamoto ambayo haziwezi kuepukika, kama vile magonjwa, kupoteza wapendwa au kushindwa katika mambo fulani. Badala ya kulalamika , Ustoa unahimiza mtu azikubali hali hizo kwa utulivu na aelekeze juhudi zake katika kile anachoweza kudhibiti, kama vile mtazamo wake na matendo yake.
- Zingatia matendo yako, si matokeo. Tunapaswa kuweka juhudi katika kufanya jambo kwa uadilifu bila kuwa na wasiwasi juu ya matokeo, kwani hatuwezi kuyadhibiti kikamilifu.
- Tumia changamoto kama fursa ya kujifunza. Badala ya kuona matatizo kama vikwazo, Ustoa unahimiza kuona ugumu wa maisha kama nafasi ya kukua kiakili na kihisia.
- Fanya mazoezi ya kujizuia ( self discipline). Ustoa unasisitiza mazoea ya kujifunza kustahimili hali ngumu kwa hiari, kama vile kujizoeza kuishi na rasilimali chache ili kuimarisha uimara wa kiakili na kuepuka utegemezi wa starehe kupita kiasi.
- Jifunze kuwa na mtazamo wa busara ( virtue first). Maisha mazuri kwa mujibu wa ustoa yanategemea kuishi kwa maadili mazuri kama vile hekima, ujasiri, haki na kiasi.
- Fahamu kuwa kila kitu ni cha muda. Maumivu,raha, mafanikio,na matatizo yote ni ya kupita. Kutambua hili kunasaidia kuwa na utulivu wa nafsi bila kushikilia sana hali fulani.
Chukua hatua; falsafa ya Ustoa inahimiza mtu kuwa na uvumilivu, nidhamu, na mtazamo chanya mbele ya ugumu wa maisha, kwa kutambua kwamba hatudhibiti kila kitu isipokuwa mawazo na matendo yetu.
Rafiki yako
Maureen Kemei.
-
Nguvu Ya Kujiamini Na Kujitathamini.
Rafiki yangu mpendwa moja ya nguvu muhimu unayopaswa kuwa nayo maishani ni uwezo wa kuwaachia watu waendelee na safari yao—hasa wale wasioona thamani yako.
Kama utaendelea kushikilia mahusiano na watu wanaokudharau au kukufanya ujione mdogo, utapoteza kujiamini na hatimaye utaishi kwa mashaka na hofu.
Leo amua kujiamini! Jipende na jithamini kwa sababu thamani yako haiamuliwi na mtazamo wa wengine.
Usiruhusu maoni ya watu yakutawale au yakuzuie kufanikisha malengo yako.
Kila mtu ana safari yake ya maisha, na safari yako ni ya kipekee—hakuna anayepaswa kukufanya ujihisi huna maana.
Jiamini, jithamini, songa mbele! Muda wako ni wa thamani, tumia kwa ajili ya maendeleo yako na wale wanaokuthamini kweli.
Chukua hatua; rafiki kuanzia leo amini kwenye kujiamini,kijithamini na kujipenda. Achana na watu wanaonakuona kama huwezi chochote au hufai kwa lolote.
Na njia bora ya kujipenda ambayo nimejifunza kutoka kwa Kocha wangu Dr Makitrita Amani, ni kuweka akiba na uwekezaji. Njia bora ya kujilipa mwenyewe, kwa kufanya hivyo unatengeza kesho yako yenye matumaini kwako na wapendwa wako
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mawazo 10 Ya Kusaidia Kuboresha Tabia Ya Kusoma Mara Kwa Mara.
Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze mbinu kumi ya kuboresha tabia ya kusoma mara kwa mara.
- Tengeneza ratiba maalum ya kusoma. Amua muda fulani kila siku wa kusoma na ushikilie ratiba hiyo.
- Soma kwa vipindi vifupi lakini vya mara kwa mara. Badala ya kusoma kwa muda kwa muda mrefu mara moja , jaribu kusoma kwa dakika 20-30 mara kadhaa kwa siku.
- Chagua mazingira mazuri ya kusoma. Tafuta sehemu tulivu, yenye mwangaza mzuri na isiyo na usumbufu.
- Weka malengo ya kusoma. Amua kusoma idadi fulani ya kurasa au sura kwa siku ili uwe na msukumo wa kuendelea.
- Tumia mbinu tofauti za kusoma. Unaweza kusoma vitabu vya kawaida, vitabu vya sauti, au makala mtandaoni kulingana na mazingira yako.
- Chagua vitabu au maudhui unayovutiwa nayo. Kusoma kitu unachopenda kunafanya iwe rahisi kujenga tabia iyo.
- Andika muhtasari wa kile unachosoma. Hii inasaidia kuelewa na kukumbuka vizuri zaidi.
- Tafuta kundi la kusoma. Kujiunga na klabu ya vitabu au kuwa na rafiki wa kusoma kunaweza kukuongezea motisha.
- Tumia teknolojia kukusaidia. Unaweza kutumia programu za vitabu vya PDF readers, au apps zinazokusaidia kusoma kwa ufanisi.
- Jikumbushe faida za kusoma. Kusoma kunakuongezea maarifa, kuboresha msamiati, na kukuza mawazo, hivyo kumbuka kwa nini unataka kuendelea na tabia hii.
Chukua hatua; rafiki unaweza kuanza na mbinu chache kwanza na kuziongeza polepole ili iwe tabia ya kudumu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Njia Ya Ustoa Ya Kutafuta Utulivu Kwenye Maisha.
Rafiki yangu mpendwa falsafa ya kiyunani ya kale ambayo inasisitiza kudhibiti hisia, kujitawala, na kutafuta utulivu na furaha kwa njia ya maisha yaliyothibitiwa.
Baadhi ya mbinu kuu za ustoa unazoweza kutumia ili kupata utulivu kwenye maisha yako ni kama yafuatayo;
- Kudhibiti hisia. Ustoa inasisitiza kwamba hatuwezi kudhibiti matukio ya nje, lakini tunaweza kudhibiti jinsi tunavyojibu kwao. Badala ya kujibu kwa hasira, huzuni, au hofu, tunapaswa kujifunza kukubali na kudhibiti hisia zetu.
- Kubali yasiyoepukika. Kukubali kwamba kuna mambo ambayo hatuwezi kubadilisha ni hatua ya kwanza ya kupata amani ya akili.
- Fikiria mambo makuu. Badala ya kushughulika na mambo ambayo hayawezi kubadilika, ustoa inakuhimiza kuzingatia yale unayoweza kudhibiti, kama vile mitazamo, majibu na tabia yako.
- Tumia muda kwa hekima. Ustoa inasisitiza umuhimu wa kutumia muda wako vizuri na kutokuwa na shinikizo la maisha. Kwa mfano, badala ya kufikiria kuhusu mambo yanayokuja au yaliyopita, chukua hatua za sasa ili kuboresha maisha yako.
- Mazoezi Ya Kujitafakari. Kujitafakari kila siku ili kuona kama umeweza kufanya kazi kwa maadili na bila kujali hali ya nje. Hii inaweza kujumuisha kuandika mawazo yako au kutafakari kwa kimya kuhusu matendo yakona mwelekeo wa maisha.
- Kukubali maumivu. Ustoa inatufundisha kwamba maumivu na changamoto ni sehemu ya maisha na kwamba tunayopitia yote yanaweza kutufundisha na kutufanya kuwa na nguvu. Badala ya kuogopa changamoto, tunapaswa kuziona kama fursa za kujifunza na kukua.
- Kuishi kwa maadili. Ustoa inasisitiza kuishi kwa maadili kama vile hekima, usawa,ujasiri na haki. Kwa kuishi maisha kulingana na maadili kama haya, mtu anapata amani ya akili na furaha ya kudumu.
- Kujua thamani ya kitu kilicho cha maana. Ustoa inataka kujua kilicho muhimu zaidi katika maisha yako. Mambo ya kifedha, umaarufu , na mali hayana maana bila utulivu wa ndani.
Kila kitu kilicho cha nje kinaweza kinaweza kuja na kuondoka, lakini utulivu na maadili ni vitu vya kudumu.
Chukua hatua; kwa kutumia kanuni hizi za ustoa, unaweza kujenga utulivu wa akili na kupunguza hisia za machafuko au wasiwasi katika maisha yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Jinsi Ya Kuvunja Kuanzia Sifuri.
Rafiki yangu mpendwa ukiona mafanikio ya watu wengine ujue kuwa wamepambana hadi wakapata mafanikio hayo.
Hapa kuna baadhi ya mambo ya kufanya ili kuepuka kuanzia sifuri kila mara.
- Badilisha mtazamo kuhusiana na fedha. Akili zetu iwaze mbali na kwa upana zaidi. Mafanikio ya kifedha ni kitu ambacho kinajengwa. Lazima tuijenge kwa watoto wetu kwa kufanya na kujenga utajiri kwa sababu watoto wanaiga yale wazazi wanafanya.
- Kuanza kuweka akiba na uwekezaji. Kuwafundisha watoto kuwa na tabia ya kuweka akiba na uwekezaji mapema.
- Kuondoka kwenye madeni mabaya. Madeni mabaya ni muhimu kuondokana nayo, madeni yanarudisha nyumba. Lazima kuwe na sababu ya kukufanya wewe ukope.
- Tengeneza mtandao wa watu sahihi. Mafanikio yanatokana na kukaa na watu sahihi kushirikiana nao wanatusaidia kufungua bongo zetu.
- Kutambua vipaji ulivyonavyo. Tutambue na kuvitumia vipaji vyetu na tuvinoe. Vipaji vya watoto wetu tuvipalilie na kuweka nguvu kwenye vipaji hivyo ili wakavitumie kuweza kusimama.
- Kutengeneza biashara ambayo haikutegemei wewe na inajiendesha yenyewe na watoto wanaikuta na wanamiliki kwa kufuata mfumo huo huo.
Chukua hatua; rafiki yangu vikiwemo maoni, mfumo na mauzo utakuwa umeewaacha watoto maeneo salama wataweza kuendesha maisha yao salama. Na pia utakuwa umeewaacha alama nzuri duniani.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.