Njia Ya kuweza Kuitawala Siku Yako.

Rafiki kwa mujibu wa falsafa ya utoa (stoism), kutawala siku yako kunamaanisha kutawala, mawazo matendo na mitazamo yako bali si kujaribu kutawala kila kitu kinachotokea.

Baadhi ya mafundisho muhimu kutoka kwa wanafalsafa wa Ustoa ni kama yafuatayo;

Anza siku yako kwa kusudi. Unapoamka asubuhi jiulize, ‘ leo nitakuwa mtu wa aina gani?’

Fanya jambo moja kwa wakati mmoja. Epuka kurukaruka kutoka kazi moja kwenda nyingine.

Kubali usichoweza kudhibiti. Kwa mfano unapokuwa foleni, au hali ya hewa inapobadilika kama ilikuwa jua na ikaanza kunyesha haifai kukukasirisha kwa sababu huna udhibiti nacho. Pia maoni ya wengine yasikuharibie siku.

Tenda kazi zako kwa nidhamu. Rafiki tunapaswa kufanya yaliyo sahihi atakama hatujiskii kufanya .Ukipanga ratiba yako ya siku unapaswa kufuatilia hadi ukamilishe.

Jitathmini jioni. Rafiki baada ya kufanya mambo zako zote au kufuatilia ratiba yako ya siku unapaswa kujifanyia tathmini ili uchunguze umefanya nini vizuri na nini kinahitajika uboreshe kesho.

Hatua ya kuchukua; Marcus Aurelius alisema kuwa ‘ubora wa maisha yako hutegemea ubora wa mawazo yako .”

Kwa mtazamo wa wastoa, siku nzuri si ile ambayo kila kitu kimeenda kama ulivyotaka, bali ni ile ambayo umeishi kwa hekima, nidhamu, ujasiri, na kujidhibiti licha ya changamoto.

Rafiki kwa kuboresha mawazo yetu kila siku tutaweza kuishi na kuitawala siku yetu bila kuzuiliwa na mambo ya nje ambayo hatuyawezi kuyazuia.

Rafiki yako,

Maureen.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment