-
24/100. Tabia ya sita ;onyesha ujasiri.
Habari
Karibu Mwana mafanikio tumalizie leo tabia ya sita, ambayo tumekuwa tukijifunza mfululizo. Brandon Burchard anatushirikisha tabia hizi, kwenye kitabu chake cha high performance habits (how extraordinary people become that way).
Baada ya kuwakochi watu wenye mafanikio makubwa. Naamini nasi tukichukua hatua hizi kwa kufanya tabia hizo kila siku, kwa kweli safari yetu ya mafanikio itazaa matunda.
Tabia ya sita ;onyesha ujasiri.
Safari ya mafanikio siyo safari rahisi, ina magumu na vikwazo vingi. Kuna kila hatari ya kushindwa kwenye safari hii na hatari hizi zimewazuia wengi Kuendelea na safari hii ya mafanikio.
Njia pekee tunayoweza Kuendelea na safari hii na kufanikiwa ni kwa kuonesha ujasiri. Tunahitaji ujasiri hili tuweze kufanikiwa zaidi.
Na ujasiri haimaanishi kwamba hatuna hofu kabisa, badala yake ni kuwa tayari kuchukua hatua licha ya kuwa na hofu. Wale wanaoonekana jasiri na mashujaa siyo kwamba hawana hofu, wanakuwa nazo, ila hawaruhusu hofu hizo ziwe kikwazo kwao.
Pia ujasiri unaambukizwa, kadiri unavyochukua hatua za kijasiri kwenye eneo moja la maisha yako, ndivyo unavyoweza kutumia kwenye maeneo mengine pia. Hivyo kama huna ujasiri unaweza kuanza na vitu vidogo na kupata ujasiri wa kufanya vikubwa pia.
Ujasiri haupo tu kwenye kuchukua hatua za kishujaa, lakini pia ujasiri ni kuwa tayari kutokuchukua hatua fulani ambayo ingekuwa kikwazo kwetu. Mfano mtu amekuudhi na hasira zikakujia, lakini ukajizuia usichukue hatua yoyote ukiwa na hasira hizi, hilo pia ni ujasiri.
Katika Kujijengea ujasiri zipo hatua tatu za kuchukua.
MOJA;HESHIMU MAPAMBANO.
Ni nzuri zaidi ukitambua kwamba safari ya mafanikio ni mapambano, ujue kwamba utakutana na magumu na changamoto. Hivyo usikimbie wala kutafuta njia rahisi badala yake, heshimu mapambano na uyapokee vizuri.
Kufikia mafanikio makubwa inahitaji kuweka kazi sana, kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kujifunza kila wakati na kupambana na vikwazo vinvyoibuka kila wakati. Yote hayo yanahitaji ujasiri.
Tunaishi kwenye jamii ambayo inayaremba inawadanganya watu kwamba Kuna njia za mkato za kufanikiwa bila ya kuumia na bila ya kazi. Huo ni uongo na usijisumbue nao.
Uwe tayari kuumia, kuteseka na kuwa jasiri kupambana na hayo yote na mwisho wa siku utafanikiwa sana.
Mbili ;washirikishe wengine malengo yako makubwa.
Malengo makubwa uliyonayo kwenye maisha yeko, usiyafanye kuwa siri. Uwaeleze watu wazi kuhusu malengo haya.
Kwa kufanya hivi wataibuka watu wa kukupinga na kukushangaa. Wapo watakaokuambia umechanganyikiwa, wapo watakaokuambia hauwezi kabisa kufikia malengo haya makubwa. Lakini usiwasikilize hao, badala yake endelea kusimamia malengo yako.
Paza sauti kuelekea malengo yako makubwa ya maisha yako na unayofanyia kazi. Wengi watakupinga na kukucheka, lakini wapo watakaoweza kukusaidia na kuja kwako kuhakikisha unafikia malengo hayo.
Unahitaji ujasiri wa hali ya juu kuweza kuyaweka wazi malengo yako makubwa, kwa kufanya hivyo kunakuongezea ujasiri zaidi.
Pale mambo yanapokuwa magumu kwenye safari yako, ndiyo wakati wa kuuishi misingi yako kwa sababu hapo ndipo unapikwa kwa ajili ya mafanikio yako makubwa.
TATU ;TAFUTA MTU WA KUMPIGANIA.
Unapopewa jukumu la kumlinda mtu mwingine, unajitoa zaidi kujilinda mwenyewe. Mtu mwingine anapokuwa hatarini na wewe ni jukumu lako kumuokoa unapata ujasiri wa kuchukua hatua ambazo wewe mwenyewe usingeweza kuzichukua.
Angalia ni watu wa aina gani uko tayari Kuwapigania, upo tayari kufa kwa ajili yao. Watu hao watakupa wewe ujasiri wa kuwapigania hatua ambazo wewe mwenyewe usingeweza kuzichukua.
Kumbuka unafanya zaidi pale wengine wanapohusika kuliko unapokuwa mwenyewe.
Rafiki, hizi ndizo tabia tunazopaswa kuzijengea ili tuweze kufanikiwa zaidi. Tabia hizo kila mtu anaweza kujijengea bila ya kujali elimu, haiba, rangi, kabila au uwezo. Kazi ipo kwako na kwangu kuzijenga tabia hizo kwa kuchukua hatua tulizojifunza na maisha yetu yataweza kuwa bora.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com
-
23/100.Tabia ya tano ;tengeneza ushawishi.
Habari
Nikukaribishe tuendelee kujifunza kuhusu tabia ya tano leo, kati ya tabia sita, ambazo kocha Brendon Burchard anatushirikisha katika kitabu chake cha high performance habits (how extraordinary people become that way).
Mafanikio yako ni matokeo ya ushawishi wako kwa wengine. Kadiri unavyokuwa na ushawishi kwa wengi ndivyo unavyoweza kufanikiwa zaidi.
Wale wenye ushawishi mkubwa kwenye kazi ndio wanaopata nafasi za kupanda juu zaidi. Wenye ushawishi kwenye biashara ndio wanaopata wateja wengi zaidi. Na wenye ushawishi kwenye maisha yao ndio wanaokuwa na mahusiano bora zaidi.
Njia pekee ya kukuza ushawishi wako kwa wengine ni kuwafanya waone wewe uko upande yao na pia kuwafanya waweze kuwa bora zaidi ya walivyo sasa.
Hatua ya kwanza na muhimu sana kwenye kujenga ushawishi wako kwa wengine ambayo wengi hawatumii ni kuwaomba watu hao wakusaidie kitu. Watu wengi hufikiri ushawishi unatokana na wewe kuwa mwongeaji sana, lakini ukweli ni kwamba ushawishi unatokana na watu kukufikiria wewe mara nyingi. Hivyo unapowaomba watu wakusaidie kitu ata kama ni kidogo wanakufikiria na hivyo unakuwa na ushawishi kwao.
Kuwajali wengine pia kunaongeza ushawishi wako kwao. Zifuatazo ni hatua tatu muhimu katika katika kutengeneza ushawishi wako kwa wengine.
Ushawishi pia unatengenezwa kwa kutoa, pale unapowapa watu kitu bila ya kutegemea kupata chochote, unakuwa na ushawishi mkubwa kwa watu hao. Mtu anapopokea kitu kwako, tena kwa wakati ambao hakutegemea na bila ya kudaiwa kulipa chochote, anamfikiria sana yule aliyempa kitu hicho, na hivyo kuwa ameshashawishika.
MOJA;WAFUNDISHE WATU JINSI YA KUFIKIRI.
Kama utawafundisha watu jinsi ya kufikiri yaani ukiathiri ufikiri wao, unakuwa na ushawishi kwao.
Kuna vitu vitabu ambavyo unapaswa kuwafundisha watu jinsi ya kufikiri, kuhusu wao wenyewe, kuhusu watu wengine na kuhusu dunia kwa ujumla kupitia Kazi unazofanya, hakikisha unawafundisha wengine jinsi ya kufikiri kwa usahihi.
MBILI ;WAPE WATU CHANGAMOTO YA KUKUA ZAIDI.
Unapaswa kuwapa watu changamoto ya kukua zaidi, kutoka pale walipo sasa na kupiga hatua zaidi. Usiwe mtu wa kuwabembeleza watu na kutaka wajione wako vizuri, badala yake kuwa mtu wa kuwaonesha watu ukweli, kwamba wanaweza Kuwa bora zaidi ya walivyo sasa.
Katika kuwasukuma watu wawe bora zaidi, Kuna wengi hawatakuelewa. Wapo ambao watakuona wewe ni mkatishaji tamaa, na wapo wengine wataona ni mtu usiyeridhika. Simamia kuwafanya watu kuwa bora na wale watakaokuwa bora hawatakusahau kamwe.
Yapo maeneo matatu muhimu ya kuwasukuma watu kuwa bora zaidi.
Eneo la kwanza ni kuwasukuma watu kuwa na tabia bora zaidi, kuwafanya wawe waaminifu, wenye uadilifu, wanaojituma na wavumilivu.
Eneo la pili ni kuwasukuma watu ni kwenye mahusiano yao na wengine, kuwafanya waweze kuboresha zaidi mahusiano yao na wengine.
Eneo la tatu ni kuwasukuma watu kwenye mchango wanaotoa kwa wengine, kuwasukuma watoe thamani kubwa zaidi kwa wengine.
TATU ;KUWA MFANO WA VILE UNAVYOTAKA WATU WAWE.
Unaweza kutumia nguvu nyingi sana kuwaambia watu wanapaswa kuwaje, lakini usizae matunda. Lakini wewe unapokuwa kama unavyotaka watu wawe, ujumbe unafika haraka na watu wanakuwa.
Kwa mfano unaweza kuwasisitiza sana watu umuhimu wa kuwahi na usieleweke. Lakini unapoanza kuwa mtu wa kwanza kufika kazini, wale walio chini yako watalazimika kuwahi.
Kile ambacho unataka watu wawe, anza kuwa wewe kwanza na utakuwa mfano mzuri kwao. Watu wanashawishika kwa kukuangalia kuliko kukusikiliza.
Tumejifunza kuwa washawishi wazuri kwa wengine, kwa kuongoza kwa kuwafundisha watu jinsi ya kufikiri, kuwapa changamoto ya kuwa bora zaidi walipo, kuwajali wengine na kuongoza kwa mfano.
Tukutane kesho majaaliwa, makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa ushauri nasaha na mafanikio wa maisha kwa ujumla.
Maureen Kemei.
Blog kufikirichanya.wordpress.com
-
22/100.Tabia ya nne ;ongeza uzalishaji (tija).
Habari Karibu katika uendelezo wa kujifunza tabia zinazoweza kutufikisha kwenye mafanikio makubwa. Tukijifunza kutoka kitabu cha high performance habits, (how Extraordinary people become that way) ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Brendon Burchard. Leo tunaangazia tabia ya za kijamii. Kundi la pili kwenye tabia sita za mafanikio ni tabia za kijamii, tabia ambazo zinawahusisha watu […]
-
20/100.Tengeneza nguvu.
Habari
Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu cha high performance habits, how Extraordinary people become that way. Kilichoandikwa na kocha Brendon Burchard.Leo tunaangazia tabia ya pili ya kati ya tabia sita ambazo Brandon anatushirikisha, zitakazotuwezesha kufikia ubobezi na mafanikio kwa ujumla, nenda nami taratibu tupate kuielewa tabia hizi ahsante.
KUTENGENEZA NGUVU.
Mafanikio yako ni matokeo ya nguvu ulizonazo. Huwezi kufanikiwa kama huna nguvu, kwa sababu safari ya mafanikio siyo rahisi kama wengi wanavyofikiri.Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba nguvu hazitokei tu kwenye maisha, bali zinatengenezwa. Jinsi unavyoendesha maisha yako, kuanzia Kulala kwako ulaji na hata matumizi yako ya muda wa siku yana athari kubwa sana kwenye nguvu zako.
Pia tunapozungumzia nguvu, wengi hufikiria nguvu za mwili pekee, lakini nguvu zinahusisha pia akili na hisia pia. Unaweza kuwa na nguvu nyingi za mwili, lakini akili ikawa haina nguvu na usiweze kuchukua hatua. Au mwili na akili vikawa na nguvu huna hamasa kabisa kwa sababu nguvu za kihisia unakuwa huna.
Ili ufanikiwe sana, unahitaji kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu kimwili, kiakili na kiroho (hisia). Na nguvu hizi zinatengenezwa kwa jinsi unavyoendesha maisha yako.
Hatua tatu za kuchukua ili kutengeneza nguvu zaidi kwenye maisha yako.
Moja,achia msongo weka nia.
Msongo wa mawazo ni sumu kubwa Sana kwenye nguvu zako, ni kitu kinachoua kabisa nguvu yoyote uliyonayo ndani yako.Na msongo wa mawazo umekuwa hautokei tu, bali tumekuwa tunauzalisha kwa jinsi tunavyoendesha maisha yetu. Na tunatengeneza sana msongo pale
Kwenye kufanya kitu kimoja kwenda kufanya kitu kingine.Ili kuepuka kupoteza nguvu, tunapaswa kuchukua hatua ya kuachia msongo na kuweka nia kila tunapobadili kile tunacho fanya.
Pale unapotoka kufanya kitu kimoja kwenda kufanya kingine, usiingie tu moja kwa moja kwenye kufanya. Badala yake funga macho yako kwa dakika moja au mbili, jiambie maneno, “naachia msongo” kwa kurudia rudia huku ukiuweka mwili wako kwa namna ya kuachia kilichopo.
Unaposikia msongo umetoka kwenye mwili wako, Weka nia ya kile unachokwenda kufanyia kazi. Fikiria ni hisia gani unataka kuwa nazo kwenye kufanya kitu hicho na matokeo unayotegemea kupata.
Kwa kufanya zoezi hili litakalokuchukua dakika 2 mpaka 5 utapata nguvu kubwa ya kuingia kwenye kitu kipya huku ukiachana na msongo wa kile ulichomaliza kufanya.
Mbili, tengeneza furaha.
Furaha ni kitu ambacho tunakitengeneza au kukipoteza sisi wenyewe, siyo kitu ambacho kinatokea au kutafutwa. Kutengeneza furaha yako mwenyewe ni moja ya aina za kutengeneza nguvu zaidi kwenye maisha yako. Kwani unapokuwa na furaha unakuwa na hamasa zaidi ya kuchukua na kupiga hatua.Unatengeneza furaha kwa kuwa na hisia chanya kwenye maisha yako. Kupenda kile unachokifanya, kuwapenda wengine, kuwa mtu wa Shukrani ni hisia chanya ambazo zinakuletea furaha zaidi.
Pia unatengeneza furaha kwa kutawala akili yako na fikra chanya za yale mazuri unayotaka na kutengeneza taswira ya matokeo unayotaka kupata na kujikumbusha taswira hiyo mara kwa mara.
Tatu,boresha afya yako.
Afya ni eneo muhimu sana la nguvu zako. Bila ya afya imara huwezi kuwa na nguvu. Ili kuboresha afya yako unahitaji kuweka mkazo kwenye maeneo haya matati muhimu.Eneo la kwanza ni ulaji, kula kwa afya, kula kwa kiasi na kula vyakula ambavyo siyo sumu kwako. Epuka kabisa sugari , ni kitu ambacho kinakuondolea nguvu kwa haraka sana. Kula kiwango kidogo cha wanga, kula mafuta, protini na mboga mboga kwa wingi.
Eneo la pili ni ufanyaji wa mazoezi, kazi za wengi sasa zinahusisha kukaa kwa muda mrefu, kama hufanyi mazoezi, ukaaji wako unapoteza nguvu. Hivyo kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa nusu saa kila siku. Unapofanya mazoezi, mwili unatumia vyakula ilivyohifadhi kuzalisha nguvu zaidi.
Eneo la tatu ni Kulala.
Usingisi ni kiungo muhimu sana cha nguvu zako. Kama hupati usingizi wa kutosha huwezi kuwa na nguvu, kila wakati utajiona umechoka kimwili na kiakili. Tafiti zinaonesha mtu anahitaji masaa 7 mpaka 8 ya kulala ili kuweza kupumzika vizuri. Hivyo Pata usingizi wa kutosha ili kuwa na nguvu.Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa ushauri nasaha na maisha kwa ujumla. Pia anayejifunza kazi ya uandishi kupitia kwa waandishi wengine.
Maureen Kemei
Email
Kemeimaureen32@gmail.com
Blog kufikirichanya.wordpress.com -
19/100.Tabia zitakazotufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Habari
Nikukaribishe sana rafiki tujifunze tabia hizi zinazoweza kutufikisha kwenye mafanikio makubwa, tukilielewa vizuri na kuchukua hatua.Kwenye kitabu cha high performance habits (how extraordinary people become that way). Brandon Burchard anatushirikisha tabia sita zitakazotuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yetu.
Brandon anatushirikisha tabia hizi kutokana na uzoefu wake binafsi, baada ya kuwakochi watu wenye mafanikio makubwa. Lakini pia ameingia kwenye tafiti nyingi za kisayansi na kijamii na kuweza kuona mchango wa tabia hizo kwenye mafanikio.
Kupitia uzoefu huo binafsi na matokeo ya tafiti, Brandon anatudhibitishia kwamba tukiweza kuziishi tabia hizi sita, tutaweza kuwa na mafanikio makubwa sana.
Brandon anatushirikisha tabia hizo sita na hatua tatu za kuchukua kwenye kila hatua hili ziweze kuwa na manufaa kwenye maisha yetu.
Tabia hizi sita amezigawa kwenye makundi mawili, kundi la kwanza ni tabia binafsi na kundi la pili ni tabia za kijamii.
TABIA BINAFSI.
Kundi la kwanza la tabia za kimafanikio ni tabia binafsi, ambazo zinamhusisha mtu pekee.Zifuatazo ni tabia tatu zilizoko kwenye kundi hili.
TABIA YA KWANZA. TAFUTA UWAZI.
Tabia muhimu sana kwenye maisha yetu ni kutafuta uwazi, tu natafuta uwazi kwa kujijua wenyewe, yaani misingi unayoisimamia, uimara wako na hata madhaifu yako.Pia unakuwa na uwazi pale unajua nini hasa unataka kwenye maisha yako, maono yako makubwa pamoja na malengo uliyonayo.
Lakini pia uwazi inahusisha kujua jinsi ambavyo utafikia maono na malengo yako, yaani mipango unayofanyia kazi ili kufika kule unakotaka kufika.
Kama hujijui wewe mwenyewe, hujui unakokwenda na hujui unafikaje, haijalishi unachukua hatua kubwa kiasi gani, huwezi kufikia mafanikio makubwa.
HATUA TATU ZA KUCHUKUA KWENYE TABIA YA KWANZA.
Moja. Tengeneza maono yako kwenye maeneo manne muhimu ya maisha yako.
Eneo la kwanza ni maisha binafsi, hapa unapaswa kuwa na maono yako binafsi, unataka kuwa nani, jione kama tayari umeshafika kule unakotaka kufika na endesha maisha yako kama tayari umeshafanikiwa.Eneo la pili ni maisha ya kijamii, hapa kuwa na maono ya jinsi unavyogusa maisha ya wengine kwenye jamii. Unajiona jinsi unavyohusiana na wengine na kuendesha maisha yako kwa maono hayo.
Eneo la tatu ni ujuzi unahitajika kuwa nao ili kufanikiwa. Kwa kile unachotaka kufikia kwenye maisha, jua ni ujuzi gani unaopaswa kuwa nao ili kufikia, kisha Jijengee ujuzi huo.Eneo la nne ni huduma unayotoa kwa wengine, hapa unajiona jinsi ambavyo unatoa huduma yako kwa wengine na wananufaika sana huduma hiyo. Kila hatua unayochukua leo inakuwa na lengo la kukuwezesha kutoa huduma bora zaidi siku zijazo.
Mbili,amua hisia unazotaka kuwa nazo.
Sis binadamu ni viumbe wa kihisia, huwa tunasukumwa kuchukua hatua kulingana na hisia tunazokuwa nazo.Ili kupata uwazi kwenye maisha yako, lazima uamue ni hisia za aina gani unataka kuwa nazo. Kwa sababu usipoamua hisia unazotaka na kuzitengeneza, dunia itakupa hisia ambazo zitakuwa kikwazo kwako kufanikiwa.
Chagua kuwa na hisia za upendo, furaha, utulivu, amani na epuka kuwa hisia za hofu chuki na wivu.
Tatu, jua kile chenye maana kwako.
Uwazi kwenye maisha unakuja pale unapojua kile chenye maana kwenye maisha yako na kuzingatia hicho.Kila unachofanya kwenye kazi au biashara, kinapaswa kuendana na maana unayotaka kutengeneza kwenye maisha yako.
Tukutane kesho tujifunze zaidi kuhusu tabia hizi. Yameandikwa na mwanafuzi wa maisha na pia ushauri nasaha.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com -
18/100.Tabia zinazowafisha watu kwenye mafanikio.
Habari
Nikukaribishe Mwana mafanikio leo tunaangazia kitabu cha ;High performance habits,how extraordinary people become that way ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Brendon Burchard.KANUNI ZA ZAMANI HAZIFANYI KAZI.
Watu wengi wamekuwa wakijifunza kanuni hizo za mafanikio, ambazo zote zimejengwa kwenye msingi wa fanya kazi kwa juhudi, penda sana unachofanya, jitume kuliko wengine, kuwa na shukrani na kuweka mkazo kwenye ubora wako na siyo madhaifu yako.Kanuni hizo hazifanyi kazi siyo kwa sababu siyo sahihi, ni sahihi sana, na unapokuwa unaanza, kanuni hizo zinakuwezesha kujijengea msingi sahihi.
Lakini kuna hatua unafika,kanuni hizo hazifanyi kazi tena. Hapo ndipo wengi wanapokuwa wamekwama. Kwa sababu wanajua kanuni iliyowafikisha pale walipofika, lakini kadiri wanavyoifanyia kazi haileti tena yale matokeo waliyotegemea kupata.
Mfano wakati mtu anaanza kazi au biashara, kadiri anavyoweka kazi zaidi ndivyo a anapata matokeo mazuri zaidi, na hayo yanamwezesha kukua zaidi.
Lakini anafika hatua fulani ya mafanikio ambayo kadiri anavyoweka kazi zaidi haileti tena matokeo makubwa zaidi.
Hapo ndipo mtu anahitaji vitu vingine ili apige hatua zaidi. Na kinachohitajika katika hatua hii ni tabia ambazo mtu anakuwa nazo.
Watu wengi wamekuwa wanaiishi misingi ya mafanikio, lakini hawajali sana kuhusu tabia zao binafsi.wasichojua ni kwamba, kadiri unavyofanikiwa, ndivyo tabia zako binafsi zinavyokuwa na athari kwenye mafanikio yako.
Hivyo kama umefika hatua ya maisha yako, ambapo umekazana kuiishi misingi ya mafanikio, na mwanzo ilikusaidia ila kwa sasa unaona haikusaidii tena , suluhisho siyo kuacha misingi hiyo, bali suluhisho ni kujijengea tabia bora zaidi.
Unapoishi misingi ya mafanikio, halafu ukajijengea tabia bora, utaweza kufanikiwa sana.
Hatua unazochukua zinaleta matokeo makubwa sana pale ambapo unakuwa na tabia sahihi zinazobeba misingi hiyo.
Tukutane kesho mpendwa ambapo tutajifunza kuhusu tabia hizo tunazopaswa kuwa nazo tukiendelea na safari ya mafanikio.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com -
18/100.Tabia zinazowafisha watu kwenye mafanikio.
-
17/100.Hazina ipo kule ulipotoka.
Habari
Karibu sana katika uendelezo wa somo letu la kutafuta hazina ya maisha. Tukiongozwa na kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Santiago alifika chini ya mapiramidi na kuanza kuchimba akitafuta hazina yake, wakati anaendelea kuchimba walikuja watu ambao walimnyang’anya dhahabu aliyokuwa nayo na kumpiga vibaya.
Baada ya kugundua hakuna kitu kingine cha thamani wanachoweza kuchukua, waliamua kumwacha na kuondoka. Lakini mmoja alimuuliza anafanya nini pale, akamjibu anatafuta hazina yake ambayo aliona kwenye ndoto.
Mtu huyo alicheka sana, akamwambia na wewe unaamini huo ujinga? Akamwambia ata yeye alipata ndoto kama hiyo kwamba hazina yake ipo kwenye kanisa lililopo Uhispania, lakini hajajisumbua nayo.
Baada ya kusikia hivyo, Santiago ndiyo alielewa safari nzima, kumbe hazina yake ilikuwa pale alipoipata ndoto yake. Hivyo alirudi kwenye like kanisa, akachimba na kuikuta hazina. Lakini kilichomnufaisha siyo hazina aliyopata, bali safari nzima ya kutafuta hazina hiyo.
Hii ndiyo funzo kuu la hadithi hii, funzo ambalo ukilielewa maisha yako yatakuwa na maana kubwa.Watu wengi wamekuwa wakipata maono, ndoto au kuweka malengo wakiamini kwamba watakapofikia ndiyo watakuwa na furaha. Furaha haipo kwenye kufikia ndoto, maono au malengo, bali ipo kwenye safari nzima ya kufikia ndoto hiyo.
Hazina yako ipo hapo ulipo sasa, unatembea nayo, hazina yako ni safari unayopita kila siku, ni jinsi unavyovuka vikwazo vya kila aina. Usisubiri mpaka mwisho ndiyo ufurahie, bali furahia kwa kila hatua unayopita.
Mwisho kabisa unapokuwa na ndoto au maono au lengo, ukipambana kuyafikia, usipumzike na kuona umeshashinda, badala yake weka ndoto, maono au lengo jingine. Yaani hakikisha kila siku ya maisha yako Kuna kitu kikubwa unachokifanyia kazi, na hapo maisha yako yatakuwa na maana wakati wote.
Kila siku hakikisha Unapiga hatua kuelekea kwenye hazina ya maisha yako, ambayo unayo hapo ulipo sasa.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha, pia anajifunza kazi ya uandishi kupitia kwa waandishi wengine.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com
Email
kemeimaureen32@gmail.com -
16/100.kuelekea kwenye hazina.
Habari
Karibu sana tuendelee na kujifunza kwetu kuhusu safari ya kupata hazina ya maisha, tukiongozwa na kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Baada ya kupitia hatari mbalimbali Santiago na Alchemist walifika kwenye mapiramidi. Na hapo Alchemist alimwacha Santiago amalize safari yake mwenyewe.
Lakini hakumwacha hivi hivi tu, alitumia ujuzi wake kugeuza madini ya risasi kuwa dhahabu na kisha kugawa dhahabu hiyo vipande vipande, ambapo viwili alimpa Santiago kufidia fedha alizopoteza njiani na kimoja alikiweka akiba iwapo akipoteza dhahabu aliyonayo basi atakuwa na pa kuanzia.
Hapo Santiago alibaki peke yake akiliendea hazina yake ambayo ilikuwa kwenye msingi wa mapiramidi.
Katika safari ya ndoto yako, utakuwa na watu watakaokuongoza na kukusaidia, lakini mwisho wa siku ni wewe mwenyewe utakayeenda kwenye hazina yako.
Hivyo jiandae kwa wakati huo na uwe tayari kupambana peke yao.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha, anayejifunza kazi ya uandishi kupitia kwa waandishi wengine.
Maureen Kemei
Blog:
Kufikirichanya.wordpress.com -
15/100.Unahitaji kufanya miujiza hili kupona.
Habari Karibu katika uendelezo wa somo letu la kutafuta hazina ya maisha, tukiongozwa na kitabu cha “the alchemist “kilichoandikwa na Paulo Coelho. Wakati Santiago na alchemist wanaendelea na safari, walikamatwa na moja ya makundi ya wapiganaji, na wakawatuhumu kwamba ni wapelelezi, ambao wametumwa na maadui na hivyo wanapaswa kuuawa. Alchemist aliwaambia wapiganaji wale kwamba wao siyo wapelelezi, bali ni wasafiri kuelekea mapiramidi na kijana aliyenaye anaweza kufanya miujiza. Aliwaambia anaweza kujigeuza kuwa kimbunga ambacho kinaweza kufunika eneo zima. Kiongozi aliposikia hivyo, akasema ajigeuze kuwa kimbunga la sivyo atawaua. Alchemist akaomba wapewe siku tatu. Baada ya Kuachana na wapiganaji wale, Santiago alimwangalia alchemist kwa mshangao, akamuuliza kwa nini umewaambia naweza kufanya miujiza wakati siwezi? Alchemist akamjibu hilo ndilo unalopaswa kufanya sasa, la sivyo watatuua. Santiago akamuuliza, sasa nitawezaje kujigeuza kuwa kimbunga? Alchemist akamwambia hajui, aulize dunia na asikilize lugha ya dunia. Basi kwa siku mbili Santiago alikaa eneo la mlima na kuweza kuangalia na kuisikiliza dunia, aliangalia kila kitu kwa undani wake, akaanza kupata nguvu kulielewa jua, kulielewa upepo na vitu zingine. Siku ya tatu wapiganaji wale waliwaita ili waje kuonesha miujiza, Santiago aliwaambia wakae eneo la chini na yeye aende kwenye kilima, kisha akaanza kuongea na dunia, jua, upepo alipeleka mawazo yake yote kwenye dunia na ghafla upepo mkali ulianza kumzunguka na kimbunga kuanza kujikusanya. Kilikuwa kimbunga kikubwa ambacho kilifunika kabisa eneo lile, mpaka baadhi ya wapiganaji walipatwa na hofu. Kimbunga kiliendelea kuwa kikali na hawakumwaona tena Santiago, kimbunga kilipokuja kutulia wakimkuta amekaa eneo la tofauti kabisa na pale alipo kwa awali. Miujiza huo uliwafanya waruhusiwe Kuendelea na safari yao. Kuna wakati utakutana na ugumu ambao wewe peke yako hauwezi kuutatua, katika nyakati kama hizi, kinachoweza kukuogoa ni miujiza, ambao unapaswa kuutengeneza wewe mwenyewe. Kila mmoja wetu ana nguvu ya kutengeneza miujiza kama ataisikiliza dunia na kutumia vizuri nguvu ya akili yako. Popote unapokwama tengeneza miujiza wa kukutoa hapo. Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha, anayejifunza kazi ya uandishi kupitia kwa waandishi wengine. Maureen Kemei Blog kufikirichanya.wordpress.com