Habari
Karibu sana tuendelee na kujifunza kwetu kuhusu safari ya kupata hazina ya maisha, tukiongozwa na kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Baada ya kupitia hatari mbalimbali Santiago na Alchemist walifika kwenye mapiramidi. Na hapo Alchemist alimwacha Santiago amalize safari yake mwenyewe.
Lakini hakumwacha hivi hivi tu, alitumia ujuzi wake kugeuza madini ya risasi kuwa dhahabu na kisha kugawa dhahabu hiyo vipande vipande, ambapo viwili alimpa Santiago kufidia fedha alizopoteza njiani na kimoja alikiweka akiba iwapo akipoteza dhahabu aliyonayo basi atakuwa na pa kuanzia.
Hapo Santiago alibaki peke yake akiliendea hazina yake ambayo ilikuwa kwenye msingi wa mapiramidi.
Katika safari ya ndoto yako, utakuwa na watu watakaokuongoza na kukusaidia, lakini mwisho wa siku ni wewe mwenyewe utakayeenda kwenye hazina yako.
Hivyo jiandae kwa wakati huo na uwe tayari kupambana peke yao.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha, anayejifunza kazi ya uandishi kupitia kwa waandishi wengine.
Maureen Kemei
Blog:
Kufikirichanya.wordpress.com