Home

  • 33/100.Ukweli.

    Karibu, katika uendelezo wetu wa kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

    Nikafahamu kwamba:

    Kama naona kuwa navurugwa na kuzidiwa na mambo yanavyokwenda kasi duniani, basi nijue nipo mahali sahihi na angalau nina uelewa wa mambo yanavyokwenda.

    Mfumo wa kidunia imekuwa migumu sana kwa mtu mmoja kuweza kuelewa namna mambo yanavyokwenda. Kuujua ukweli imekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu propaganda zimekuwa nyingi mno zama hizi.

    Katika zama zilizopita propaganda zilisambazwa kwa vyombo vya habari kama redio, magazeti, TV na hata vitabu. Hivyo watu wote walipata ujumbe mmoja.

    Lakini zama hizi propaganda zinasambazwa kwa mitandao ya kijamii, hivyo kila mtu anaweza kupata propaganda inayoendana na yeye tu. Hii ni hatari sana kwa sababu watu wanazidi kugawanywa kwenye matabaka mbalimbali.

    Katika matumizi yako ya mtandao ya kijamii, mfumo wa kompyuta ya mitandaoni hiyo inajua kabisa wewe unapendelea nini, uko upande upi kwa yale unayofuatilia au kushiriki. Hivyo mtu anayechagua kusambaza propaganda, anaweza kuchagua propaganda zake ziwafikie watu wa aina gani.

    Ni vigumu sana kuujua ukweli katika zama hizi, hasa kama unafikiri ndani ya kundi. Huwezi kuujua ukweli ukiwa ndani ya kundi. Utaujua ukweli kwa kufikiri nje ya kundi, kwa kuufatuta ukweli kwa juhudi zako.

    Hivyo kitu kikubwa tunalotoka nalo leo ni kutafuta ukweli kwa juhudi zetu wenyewe kwa kufikiri nje ya kundi.

    Tukutane kesho ili tuendelee kujifunza zaidi katika kuyaelewa changamoto za zama hizi na namna tunavyoweza kutatua katika safari ya mafanikio.

    Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog :kufikirichanya.wordpress.com

  • 32/100.Kukata tamaa na matumaini.

    Karibu, katika uendelezo wa kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

    Yale nimejifunza kutoka kitabu hiki ni kama yafuatayo.

    Kwamba kutokana na changamoto kuwa nyingi na kutokutabirika;

    Watu wengi wanaishia kukata tamaa na kuona hawana cha kufanya bali kupokea hali kama ilivyo. Lakini tunapaswa kujua kwamba uwezo wetu kama binadamu ni mkubwa na tunaweza kusimama na kuzishinda changamoto zote tunazopitia.

    Ili kuweza kusimama na kuzishinda changamoto hizi, lazima kwanza tuweze kudhibiti hofu zetu, tuwe na matumaini na kuwa wanyenyekevu kwa yale tunayofanya na hata kufikiri.

    Moja ya vitu vinavyotupa hofu kubwa ni ugaidi na hata uwezekano wa kuwepo kwa vita ya tatu ya dunia. Lakini kwa kuangalia kwa uhalisia inagunduka ni hofu zaidi ya uhalisia.

    Mwandishi anasema kwenye kitabu kuwa, ugaidi unauwa wachache Sana kwa mwaka ukilinganisha na ajali au ugonjwa sugu. Lakini magaidi wanajua hofu zetu ziko wapi na kuzitumia vizuri.

    Mwandishi anatupa mfano wa jinsi magaidi wanavyokamilisha malengo yao kwa kutumia nguvu nyingine. Anatoa mfano kama Kuna mgahawa unataka kuuvuruga lakini huna nguvu, unaweza kukamilisha hilo kwa kuweka mdudu ndani ya sikio la ngombe kisha kumweka kwenye mgahawa huo. Wakati anahangaika kumtoa mdudu kwenye sikio lake, atavunja vunja kila kitu.

    Hivi ndivyo ugaidi unavyoharibu taifa, kwa kuchokoza taifa kubwa na taifa hilo kuharibu taifa jingine. Mfano Marekani na Iraq.

    Katika kuchagua mfumo bora wa kuendesha nchi ata jamii, mfumo wa kidunia secularism unaonekana kuwa bora kuliko mfumo wa kidini religion. Mfumo wa kidunia unaendeshwa kwa misingi mikuu sita.

    Misingi ya kwanza ni ukweli

    Mfumo wa kidunia unaongozwa na ukweli, na ukweli ni ule unaoweza kudhibitishwa na siyo tu kupokelewa na kuaminiwa kama ulivyo. Ukweli ni zao la ushahidi na utafiti na siyo imani.

    Misingi ya pili ni kuwa na huruma.

    Mfumo wa kidunia unasisitiza kuwa na huruma kwa wengine, kutambua mateso ambayo wengine wanapitia na kujali zaidi. Kwa mfumo wa kidunia huibi au kuua siyo kwa sababu dini imekataza, bali kwa kuwa unajua kwa kufanya hivyo unawaumiza wengine.

    Misingi wa tatu ni usawa

    Mfumo wa kidunia unasisitiza kwenye usawa baina ya watu na makundi mbalimbali. Kwa mfumo huu unajua wewe siyo bora kuliko wengine, bali kila mtu ana upekee wae unaomfanya awe bora.

    Misingi ya nne ni uhuru

    Mfumo wa kidunia unampa kila mtu uhuru wa kufikiri, kuchunguza na kujaribu vitu mbalimbali. Mfumo huu unaamini kwenye haki ya mtu kuwa na uhuru wa kuwa na wasiwasi, kuuliza zaidi, kupata maoni ya upande mwingine na hata kujaribu njia mbadala.

    Misingi ya tano ni ujasiri wa kupambana na mfumo kandamizi na yenye upendeleo.

    Mfumo huu unasisitiza kuwa na ujasiri wa kukubali kwamba hujui au umekosea. Mfumo huu unatufundisha tusiwe waoga na kupokea kitu kama kilivyo hata kama siyo sahihi, badala yake tukipinge.

    Misingi wa sita ni majukumu

    Mfumo wa kidunia unampa kila mtu majukumu ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora wa kila mtu kuishi. Hawakutoa jukumu hilo na kukabidhi viongozi au mtu yeyote anageonekana ndiyo wajibu wake, bali wanajua jukumu la kuifanya dunia kuwa bora ni la kila mtu.

    Tumefahamu misingi haya sita, tuyatumie katika maisha yetu binafsi na yatakuwa bora zaidi.

    Mara zote kuwa tafuta ukweli, kuwa wa huruma kwa wengine, pigania usawa kwa wote, tumia vizuri uhuru wako na kuwa jasiri kusimamia kilicho sahihi na usisahau kubeba majukumu yako ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.

    Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei

    Blog ;kufikirichanya.wordpress.com

  • 31/100.Changamoto ya kisiasa.

    Karibu, naendelea kukushirikisha yale ninayojifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

    Kitabu hiki kimeezea kwa kina sana changamoto tunazopitia kwenye karne hii na hatua tunazopaswa kuchukua ili kuzivuka.

    Mbili;changamoto ya kisiasa.

    Tuliangalia Jana changamoto ya kwanza ambayo ni changamoto ya kiteknolojia. Leo tuko kwenye changamoto ya pili ambayo ni ya kisiasa.

    Muungano wa teknolojia ya kibaolojia na na ya habari unaleta mtikisiko kwenye uhuru na usawa. Kwa wale ambao wana umiliki kubwa wa taarifa za wengine wanaweza kuzitumia vibaya kwa manufaa yao binafsi. Wanaomiliki taarifa Wanakuwa tabaka la juu huku wasio na taarifa wakiwa tabaka la chini.

    Suluhisho lolote la changamoto za kiteknolojia lazima lihusishe ushirikiano wa kimataifa, kwa sababu kampuni ya kiteknolojia inaweza kuwa kwenye nchi moja,lakini ikakusanya taarifa za wananchi wa nchi tofauti. Mfano Facebook ipo Marekani lakini ina watumiaji dunia nzima.

    Kikwazo kikubwa kwenye utatuzi wa changamoto za kiteknolojia ni mkwamo wa kisiasa na jamii. Nchi nyingi kwa Sasa zinarudi kwenye utaifa baada ya kujenga ushirikiano wa kimataifa. Mwaka 2016 ulikuwa mwaka ambao dunia iliona mambo yasiyotegemewa kutokea.

    Kitendo cha Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye umoja wa ulaya na Donald Trump kushinda urais wa marekani iliashiria namna ambayo watu wanafikiria utaifa zaidi kuliko ushirikiano wa kimataifa.

    Sera kuu ya Trump imekuwa kuifanya Amerika kuwa bora kwa kujali mambo ya America na siyo nchi nyingine. Ushirikiano bora wa kisiasa unahitajika ili kuweza kuzitatua changamoto hizi kubwa za kiteknolojia.

    Tukutane kesho rafiki tutaona changamoto nyingine inayotukumba karne hii ya 21, nikutakie siku ya mafanikio makubwa.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei

    Blog ;kufikirichanya.wordpress.com

  • 30/100.Changamoto kubwa ya karne ya 21 na jinsi ya kuzivuka.

    Karibu katika uendelezo wa kujifunza kutoka kitabu 21 lessons for the 21st century, ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

    Kimeelezea kwa kina sana changamoto tunazopitia kwenye karne hii na hatua tunazopaswa kuchukua ili kuzivuka.

    MOJA;CHANGAMOTO YA KITEKNOLOJIA.

    Katika hiki kilaelezea changamoto zote za kiteknolojia zinaanzia kwenye mambo mawili.

    Moja ni ukuaji wa teknolojia wa habari INFOTECH ambayo sasa hivi taarifa za wengi zimekusanywa na makampuni makubwa ya kiteknolojia na hivyo kuweza kutushawishi kuchukua hatua fulani.

    Mifumo ya kiteknolojia imeweza kukua sana kiasi cha kuweza kumjua mtu kuliko anavyojijua mwenyewe. Kama umekuwa unatumia Google au Facebook, utagundua mitandao inajua tabia zako kuliko wewe, hivyo inakuletea aina ya vitu unavyopendelea kufuatilia. Hii ni changamoto kubwa kama watu hatutakuwa na udhibiti wa taarifa zetu.

    Mbili ni ukuaji wa teknolojia ya kibaolojia BIOTECH ambao kwa Sasa taarifa za ufanyaji wa kazi wa mwili wa binadamu zimeshakusanywa sana.

    Kwa Sasa tuna uelewa mkubwa sana wa jinsi miili yetu inafanya kazi, jinsi ubongo unayofanya kazi na hata jinsi hisia mbalimbali zinavyoibuliwa kwenye mwili, kupitia kemikali mbalimbali ambazo mwili unazalisha.

    Changamoto kubwa Sana itakuja pale teknolojia hizi mbili zitakapoungana, yaani INFOTECH na BIOTECH, kwa mfano kunaweza kuwepo na kadi ambayo inawekwa kwenye mwili wa binadamu, ambayo inasoma taarifa za mwili na kuzituma kwenye mfumo wa kompyuta kisha kompyuta kufanya maamuzi kwa ajili ya mtu huyo.

    Mfano unapokuwa na huzuni, taarifa zinatumwa kwenye kompyuta kwamba una huzuni na hapo kompyuta inakuchagulia wimbo mzuri wa kusikiliza.

    Kadhalika mgonjwa yatakuwa rahisi kugundulika kabla dalili hazijaanza kuonekana. Magonjwa mengi huanza kwa mabadiliko madogo madogo kwenye mwili ambayo hayana dalili za nje. Uwepo kwa mfumo unaokagua mwili utatoa taarifa haraka kuhusu mabadiliko hayo hivyo kuzuia ugonjwa kabla haujaanza. Magonjwa kama saratani yataweza kuzuilika mapema.

    Mfumo kama huo unaonekana ni mzuri sana, lakini una hatari moja kubwa, taarifa za jinsi mwili wako unavyoendeshwa zikifika kwenye mikono ambayo siyo salama, unageuka kuwa mtumwa.

    Pata picha taifa linaloendeshwa na Rais dikteta halafu ana nguvu ya kuwa na taarifa za wananchi wake wote, anaweza kuwafanya wajisikie vile watakavyo na hata wamtukuze na kumwona yeye ndiye mkombozi wao.

    Kadhalika taarifa hizo zikifika kwenye mikono ya makampuni makubwa, yatazitumia kuhakikisha unakuwa mteja wao na kununua chochote wanachouza.

    Hivyo pamoja na maendeleo haya makubwa yanayoweza kutokea kwenye sekta hizi,tunapaswa kuwa na udhibiti mkubwa wa taarifa zetu ili zisitumike kutufanya watumwa au wateja wa watu wengine.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog
    Kufikirichanya.wordpress.com

  • 29/100.Uwazi ni nguvu mkubwa.

    Karibu

    Namshukuru Mungu kwa uhai na zawadi ya siku nyingine ya ushindi. Tunajifunza leo kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

    Kwenye kitabu hiki, Yuval amezichambua changamoto kubwa 21 zinazotukabili kwenye karne hii ya 21 na kupendekeza hatua tunazopaswa kuchukua ili tusiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.

    UWAZI NI NGUVU KUBWA.

    Tunaishi kwenye zama ambazo Kuna mafuriko ya taarifa. Yaani maarifa na taarifa ni nyingi mno kiasi kwamba, badala ya maarifa na taarifa hizi kuwa msaada kwetu katika kufanya maamuzi, zinakuwa kikwazo.

    Kwa sababu kunapokuwa na maarifa na taarifa nyingi, lakini tukakosa uwazi au tukashindwa au kuzielewa kwa ubaya, tunaishia kubaki katika njia panda tusichukue ni hatua ipi ya kuchukua.

    Wingi wa maarifa na taarifa zilizopo, unapelekea hali kubwa ya upinzani baina ya maarifa na taarifa. Taarifa moja inaweza kuwa inakuambia hiki, huku taarifa nyingine ikipingana na hicho cha mwanzo. Katika hali kama hii, ni vigumu sana kujua ni hatua gani ipi uchukue kama huna uwazi ndani yako.

    UWAZI ni nguvu kubwa katika karne hii ya mafuriko ya taarifa na maarifa. Uwazi unaanza kwa kujijua wewe mwenyewe na kujua unataka nini kwenye maisha yako. Kisha kuchagua taarifa na maarifa yanayoendana na kile unachotaka na kuachana na mengine.

    Ukijua kwamba unachochagua wewe siyo kitachokuwa sahihi kuliko vingine vyote, bali kitakuwa sahihi kwako kulingana na unachotaka kwenye maisha yako.

    Upo usemi unaosema ukifa kwa kiu wakati umezungukwa na maji ni ujinga, lakini zama hizi watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa, huku wanazama kwenye mafuriko ya maarifa.

    Nikafahamu kuwa kinachokosekana zama hizi siyo maarifa, bali uwazi. Nimejifunza kwamba napaswa kuwa mwazi kwangu binafsi na kuwa tayari kuchagua kimoja na kuachana vitu vingine.

    Jambo hili wachache wanaliweza na naweza kuwa mmoja wao ata na wewe rafiki unayesoma nakala hii. Kujua unayotaka kwenye maisha, kuchagua aina ya maarifa yanayoendana na kile unachotaka na achana na mengine yote.

    Tukutane kesho rafiki tutajifunza zaidi kuhusu changamoto ya karne hii ya 21 na yale tunayopsawa kuchukua, hili tuendane na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog
    Kufikirichanya.wordpress.com

  • 28/100.mambo sita ya kufanya kila siku asubuhi ili kuwa na siku ya ushindi.

    Karibu, nikushirikishe ninayozidi kujifunza kutoka kitabu makini mno cha kanuni ya siku ya mafanikio. Iliyoandikwa na kocha Dr Makirita Amani.

    Nimejifunza kwamba;

    Maisha yetu yana maeneo manne muhimu tunayopaswa kuweka nguvu na umakini zetu kama tunataka kuwa na maisha bora.

    Maeneo haya manne ni afya ya mwili, akili, hisia na imani.
    Afya ya mwili inahusisha hali ya mwili na nguvu tulizonazo.
    Akili inahusisha fikra zetu na mtazamo tulionao.
    Hisia inahusisha zile hisia tunazokuwa nazo kwenye maisha.
    Imani inahusisha roho na nguvu kubwa isiyoonekana ambayo inatutawala wote.

    Ili tuwe na maisha yenye mafanikio tunapaswa kuyaboresha maeneo hayo manne kila siku.

    Njia ya kuboresha maeneo haya manne ni kufanya mambo sita yafuatayo.

    Jambo la kwanza; kukaa kimya (silence).

    Hatua ya kwanza kuchukua pale unapoianza siku yako ni Kutenga muda wa kukaa kimya.

    Kukaa kimya kina manufaa makubwa kwenye maisha yetu kama yafuatavyo :

    1.kunaituliza akili
    2.kunaiondoa msongo wa mawazo
    3.kunatuwezesha kujitambua zaidi.

    Baadhi ya vitu tunavyoweza kuvifanya kwenye ukimya wetu ni.

    1.kufanya tahajudi
    2.kusali na kuomba
    3.kutafakari kwa kina
    4.kupumua kwa kina
    5.kushukuru.

    Muda wa kufanya haya ni baada ya kuamka, dakika tano za kwanza.

    Jambo la pili ni kujiambia Kauli chanya (Affirmations).

    Unachagua Kauli chanya ambazo zinaonesha uwezo mkubwa na jinsi ya kuufikia kisha unajiambia Kauli hizi kwa kurudia rudia.

    Jambo la tatu; kutengeneza taswira chanya (visualization).

    Hapa unatengeneza taswira ya jinsi maisha yako yatakuwa baada ya kufikia kule unakotaka kwenda.

    Kisha kuiweka picha hiyo kwenye akili yako na kujiona kama tayari umeshapata kile unachotaka au kufikia.

    Kutengeneza taswira Kuna nguvu kama ya kujiambia Kauli chanya, akili yetu inachukulia ni kitu ambacho kimeshatokea na hivyo kutuweka kwenye mazingira ya kukamilisha hilo.

    Jambo la nne; kufanya mazoezi (exercise).

    Mazoezi ya asubuhi Yana nguvu kubwa zaidi, kwa sababu yananipa manufaa nitakayonufaika nayo siku nzima.

    Mazoezi:
    – yanaboresha afya yetu
    – yanaongeza nguvu
    – yanaimarisha kinga ya mwili.
    – yanaifanya akili ifikiri kwa usahihi.

    Yanashauriwa kutenga muda wa dakika 20 kila siku kufanya mazoezi.

    Jambo la tano; ni kujisomea (reading).

    Njia ya mkato, ya haraka na rahisi kubadili maisha yako ni kupitia usomaji. Unaposoma kitabu, unajifunza mambo ambayo mtu mwingine ametumia muda mwingi katika kuyaishi au kuyatafiti, lakini unatumia muda mchache kuyasoma.

    Kama hujifunzi huwezi ukawa na maisha yenye mafanikio, vitabu vina hazina kubwa.

    Chochote unachokisumbuka nacho kwenye maisha yako, kuna majibu yake kwenye vitabu, ni wewe kujua vitabu gani, uvisome na kisha uchukue hatua.

    Ujiwekee lengo la kusoma kurasa kumi kila siku, kwa mwezi unamaliza vitabu kumi, ukifanyia kazi unayojifunza hutabaki jinsi ulivyo.

    Jambo la sita;kuandika mawazo (scribing).

    Akili yetu huwa linapata mawazo mengi mazuri sana na mabaya.

    Ili kuondokana na hali ya kupoteza mawazo mazuri, hili uyatunze na pia kujikumbusha, lakini pia linakufundisha kupangilia vizuri mawazo yako .

    Kwenye kitabu changu unaandika
    – Mawazo yangu mapya ninayoyapata
    – yale niliyojifunza
    – mpenyo ninaoupata
    – magumu ninayokutana nayo
    – jinsi ninavyovivuka.

    Tukutane kesho katika harakati za kujifunza zaidi kanuni hizi.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog
    Kufikirichanya.wordpress.com

  • 27/100.Mambo ya kufanya kila siku asubuhi ili kuwa na siku ya ushindi.

    Karibu naendelea kukushirikisha yale ninayojifunza kutoka kitabu cha kanunikwanza ya siku ya mafanikio. Iliyoandiyakokwa na kocha Dr Makirita Amani.

    Jambo la kwanza ;ni kuandika hadithi mpya ya maisha yako.

    Badala ya kuendelea na kile kilichojengeka kwa mazoea, unachagua kutengeneza kile unachotaka kuamini.

    Jambo la pili ;amka ukiwa na uwezo wako wote.
    Unaamka kwa ushindi, ukijua ni nini unaenda kufanya.
    Unakataa maisha ya zima moto, maisha ya kuamka bila mpango wowote, na kupoteza muda mwingi wako katika kuperuzi.

    Jambo la tatu;dunia yako ya nje ni taswira ya dunia ya ndani.
    Ukisimama mbele ya kioo alafu kioo ioneshe kwamba sura yako imevimba wakati wewe hutaki ivimbe, kusema kioo inadanganya unajidanganya wewe mwenyewe. Kwa sababu kioo haitengenezi sura yao, bali inakuonesha jinsi ilivyo.

    Kama unataka kile unachokiona kwenye kioo kibadilike, unapaswa kubadili kwanza mwili wako, kama kioo kinakuonyesha una uchafu au uvimbe.

    Hivyo ndivyo kilivyo kwenye maisha yetu pia, tabia kinachoonekana nje yetu ni matokeo ya kinachoendelea ndani yetu.

    MUHIMU.
    Asubuhi ni muda mzuri kwako kubadili imani, mitazamo, taswira ulizojijengea kuhusu wewe na maisha kwa ujumla.

    Bila ya kuvunja izo imani na mitazamo utaendelea kupata matokeo unayopata sasa.

    Jambo la nne;kwa nini uamke asubuhi ya leo?

    Hatua kubwa ya kuwa na mafanikio ni kuwa na sababu kubwa ya kuianza siku yako.
    Unapaswa kuanza siku yako ukiwa na hamasa na mapenzi makubwa ni kwenda kitandani ukiwa na nia ya kuamka ukiwa vizuri.

    Rafiki, tukutane kesho ili tujifunze kuhusu mambo sita tunayopaswa kufanya ili siku yetu iwe bora na mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog;
    kufikirichanya.wordpress.com

  • 26/100. Inawezekana unapoteza maisha kwa kufanya haya kila siku.

    Habari
    Karibu sana nikushirikishe niayojifunza kutoka kitabu kanuni ya siku ya mafanikio iliyoandikwa na kocha Makirita Amani.

    Kumbe kila binadamu ana uwezo mkubwa ulio ndani yake , ambayo labda ametumia asilimia 10 tu. Au ata chini ya iyo.

    Nikaelewa pia kuwa napoteza maisha kwa
    _ kufanya mambo kimazoea
    _kufanya kwa viwango vya chini.
    _Na kutojaribu hatua kubwa za tofauti zinazoweza kunitoa hapa ninapokwama sasa.

    kukazana kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, halafu baadae kunapopata matokeo kama ya wengine, tunaanza kukimbilia kuiga na kushindana nao halafu tunashangaa pale maisha yanapokwamba.

    Hatua ninazochukua ili niache kupoteza maisha yangu ni:

    Kutambua mimi ni wa kipekee sana.
    Chochote ninachokifanya sasa ni cha kiwango cha chini nikilinganisha na uwezo mkubwa nilionao wa kufanya makubwa zaidi.

    Kila siku nnakazana kuwa BORA kuliko jana.

    Nakataa kufanya kwa mazoea

    Nakataa kufikiria kwamba nmeshafikia juu kabisa.

    Njia nzuri ninayoweza kufikia na kutumia uwezo ulio ndani yangu, ni kuwa na udhibiti kwenye asubuhi yangu, kuipangilia na kutumia kufanya yale makubwa na muhimu zaidi kwangu.

    Asante tukutane kesho majaaliwa tujifunze zaidi kuhusu asubuhi ya miujiza ambapo tutaweza kujua na kutumia uwezo ulio ndani yetu.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei
    Blog
    Kufikirichanya.wordpress.com

  • 26/100.Je unafahamu kuwa unaweza fanya asubuhi yako kuwa ya miujiza?

    Habari

    Karibu sana tuendelee kujifunza kutoka kitabu kanuni ya siku ya mafanikio, ambayo imeandikwa na kocha wa mafanikio Dr Makirita Amani.

    Anatushirikisha kwamba kanuni muhimu tunazoweza kuzitumia kila siku ili asubuhi yetu iitwe ya miujiza.

    Waswahili husema nyota njema huonekana asubuhi, anasema tukitaka mafanikio lazima tuamke mapema.

    Kabla siku haijachanganya na kupoteza udhibiti wake, lazima tuwe tumeamka mapema na kukamilisha yaliyo muhimu kwetu kwanza.

    Kumbe tunaweza tukatenga muda mzuri asubuhi na kufanya majukumu makubwa na muhimu.

    Anaelezea kwamba tukiweza kudhibiti asubuhi, kwa kufanya makubwa basi tutaliita asubuhi yetu “asubuhi ya miujiza.”

    Ili tuweze tukajitangazia ushindi, ni lazima pale tunapodhibiti asubuhi yetu na kufanya yaliyo muhimu kwa nidhamu ya hali ya juu.

    Ili kujenga maisha yenye mafanikio lazima tujenge tabia ya kurudia kufanya yaliyo muhimu, bila kujali ni kitu gani tunachokifanya.

    Mafanikio kwenye maisha ni mkusanyiko wa asubuhi nyingi za miujiza ambazo mtu amekuwa nazo.

    Nikushukuru Mwana mafanikio tukutane kesho, ili tujifunze zaidi na hatimaye. Siku yetu iwe ya ushindi kadhalika tukichukua hatua, tunapoendelea na safari yetu ya mafanikio.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

    Maureen Kemei

    Blog kufikirichanya.wordpress.com

  • 25/100.Je, unafahamu kwamba mafanikio ni kila siku?

    Habari

    Karibu Mwana mafanikio leo tukianza kujifunza kutoka kitabu makini sana cha kanuni ya siku ya mafanikio . Ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Dr Makirita Amani.

    Kocha anatushirikisha kwamba mafanikio haiji tu kwa kustukia, au kufikiria kuamka siku moja kama umetajirika, yaani Kulala masikini na kutarajia kuamka tajiri . Anaeleza kwamba mafanikio huja kwa kuamua kuchukua hatua ndogo ndogo kila siku.

    Anaeleza kuwa safari ya elfu moja huwa inaanza na hatua moja zitakapofanyika kwa kurudia rudia ndiyo zinakamilisha safari ya mafanikio.

    Kila siku unayoishi ndiyo inachangia kwenye mafanikio yako, anasema kuijua hii ndio ukombozi mkubwa kwenye maisha. Kuliko maarifa yoyote ile.

    Wengi ambao hawajafanikiwa wanaisubiri na hata kukosa furaha kwa sababu wanaisubiri siku moja ya mafanikio. Ambayo haipo huku wakipoteza siku nyingi ambazo ndizo zingechangia mafanikio wanayotaka.

    Kitu kikubwa ambacho tunapaswa mimi na wewe kuondoka nacho kwenye kitabu hiki makini ni kufahamu kwamba mafanikio ni kila siku.

    Badala ya kusubiria siku moja ambayo kwayo utakuwa umepata kila kitu. Ndiyo sasa uanze ufurahie mafanikio yako, unapaswa uanze uishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

    Sababu mkusanyiko wa siku ambazo umeziishi kwa mafanikio ndiyo mafanikio ya maisha yako. Kila siku mambo ya kufanya yanazidi kuongezeka huku muda ukipata ule ule masaa 24.

    Kama shughuli za kufanya zinaongezeka kila siku, muda ukipaki ule ule. Kwa hivyo tunajiuliza tunaweza je, kuuishi mafanikio kwenye masaa 24 tuliyonayo kwenye siku yetu?

    Ili siku yako iwe ya mafanikio ni muhimu uijue na uwe na kanuni utakayoitumia kuendesha siku yako kwa usahihi.

    Tutajifunza namna ya kuvuka kuwa watu wa kufanya mambo kikawaida na kuendesha maisha kwa kubahatisha. Na kujua namna ya kuendesha siku kwa mpangilio maalum, ambayo inatokana na kanuni tunayojitengenezea wenyewe.

    Wanaofanikiwa wamekuwa ni watu wa kuamka asubuhi na mapema, wakati bado dunia imelala na kujipatia muda tulivu wa kufanya mambo ya msingi na muhimu kabisa.

    Mafanikio ni kila siku, yapaswa kuiheshimu sana kila siku tunayoipata. Kutumia vizuri ili kupata matokeo ya tofauti na bora zaidi. Kurudia rudia hivyo kila siku ili kuwa na mafanikio bora yenye thamani kubwa.

    Rafiki, tukutane kesho ili tuzidi kujifunza zaidi kuhusu namna ya kupangilia na kuzifahamu kanuni hizo. Na kutumia ili tupate kuwa washindi kwenye kila siku yetu.

    Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi .

    Maureen Kemei

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com