Home

  • Kufanya zaidi ya ulivyozoea.

    Karibu, iwe unafanya mambo sahihi au yasiyo sahihi, muda hautakusubiri. Muda utaendelea kwenda na hilo ndilo linawafanya wengi kuja kushtuka baadae na kuona kwamba wamepoteza muda wao mwingi na maisha yao.

    Watu wengi hawaridhishwi na matumizi yao ya muda, siyo kwa sababu hawana muda, ila kwa sababu wanajua namna wanavyoitumia muda wao kwa namna isiyo sahihi. Wanajua wanaweza kufanya zaidi ya wanavyofanya sasa, ila hawaijui wanawezaje kukamilisha hilo.

    Wamekuwa wanafanya mambo ya kawaida ili mtu aendelee kuishi. Kufanya kazi au biashara yanayoingiza kipato, kutunza afya na kuimarisha mahusiano na wengine. Haya yanaonekana kuchukua muda wote ambao mtu anakuwa nayo. Lakini bado ndani yake anaona anapaswa kufanya zaidi.

    Hii ni hitaji la msingi ambalo liko ndani ya kila binadamu, ndiyo chimbuko la ugunduzi wote ulioweza kutokea humu duniani hadi sasa. Kama watu wangeridhika tu na hali zao, dunia isingepika hatua ambazo imepika mpaka sasa.

    Chukua hatua, unaweza kabisa ukafanya zaidi ya ulivyozoea, usiendelee tena kujiuliza utapataje muda wa kutosha wa kupumzika ili uweze kufanya zaidi ya ulivyozoea.

    Hilo ndilo jambo kubwa tunalopaswa kuitafakari siku hii ya leo tunapoendelea na mapambano ya maisha, uwe na siku njema.

    Mimi akujaliye sana, Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

  • Kutumia kila fursa kuyafurahia maisha.

    Katika maisha Kuna mambo mengi sana ambayo yanatufanya tukasirike na kukata tamaa. Lakini haifai tuliruhusu hilo litokee, lazima tutumie kila fursa tunayopewa kufurahia Maisha.

    Maana maisha enyewe ni mafupi mno, hivyo kukasirishwa na vikwazo mbalimbali hayatasadia kusuluhisha au kurahisisha lolote kwenye maisha.

    Kwenye kitabu cha everyday manifesto, Robin anatushirikisha kisa kilichotokea akiwa Dubai kutoa mafunzo kwa wagurunzi wa makampuni.

    Akiwa kwenye lifti alikutana na mtu aliyevaa kofia aliyoipenda sana. Ndani yake akasukumwa Kusifia mtu huyo, lakini akasita kwa kuona huenda mtu huyo asipokee hilo vizuri.

    Lakini akajiambia ni bora tu aseme, maana hatari kubwa kwenye maisha ni kutokuchukua hatua yoyote, akamwambia ameipenda sana kofia lake,mtu yule alitabasamu, kisha akavua kofia na kumpa kama zawadi.

    Robin Alishangazwa na hilo, hakutegemea, alisukumwa tena kuikataa zawadi hiyo, ila akaikubali. Walipotoka kwenye lifti alienda kwenye gari na kuchukua kitabu chake na kumpa tu yule mtu, ambapo naye alikifurahia sana.

    Kisa hiki kinatufunza kutumia kila fursa kuyafurahia maisha, kuwa mwema na kufanya yaliyo sahihi. Ni kwa hatua ndogo ndogo ndiyo mtu unajenga mafanikio yako makubwa.

    Chukua hatua, furahia kila fursa kwenye kila siku yako,vijana wa sasa wanaita chagamkia kila fursa na hapo ndipo utashinda vikwazo na kukasirishwa hovyo na mambo madogo yanayotokea.

    Akujaliaye sana, Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Tamko chanya la kuanza siku yako.

    Jinsi unavyoianza siku yako kuna mchango mkubwa wa jinsi gani siku iyo itakwenda, kama itakuwa ya mafanikio au ya kushindwa. Wengi huzianza siku zao kwa mazoea, wakiwa hawana mikakati wowote hivyo kukimbizana na kila fursa linalopita mbele yao.

    Hupaswi kuanza siku yako hivyo, maana hutaweza kufanya makubwa. Unapaswa kuanza kila siku yako kwa tamko chanya litakalokusukuma kufanya zaidi.

    Mfano ya tamko za kujiambia kila siku asubuhi ;

    Siku ya leo ni baraka nitakayoiheshimu na kuitumia kwa ukamilifu wake. Najua hii ndiyo siku ambayo nina udhibiti nayo.

    Kwenye siku hii nitaishi kama kiongozi na siyo mwathirika, kama mtu halisi na siyo feki na kama mwenye maono na siyo mfuasi.

    Leo nimechagua kuwa wa kipekee na siyo wa kawaida, jasiri na siyo mwoga na kuwa shujaa na siyo mlalamikaji.

    Leo nitatenga muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina, kuepuka yote yanayopoteza muda na kufanya kazi zangu kwa viwango vya kuu kabisa.

    Leo nitatimiza kila ninachoahidi na kupeleka umakini wangu wote kwenye yale muhimu niliyochagua kufanya.

    Nitatenga muda wa kupumzika na kuuheshimu kwa sabau najua bila mapumziko siwezi nikafanya makubwa.

    Siku ya leo nitakuwa mwema kuliko Jana, nitafanya yale yenye manufaa makubwa kwa wengine na siyo kujiangalia mimi mwenyewe.

    Sitakubali kuhairisha kirahisi yale niliyopanga, kwa sababu mimi ni mfanyaji na siyo mwongeaji.

    Nitamaliza siku yangu kwa kuitathmini jinsi ilivyokwenda, kujua yale niliyofanya na namna ya kuboresha zaidi kwenye siku unafuata.

    Chukua hatua, jiambie tamko kama hili kila unapoianza siku yako kwa mwongozo wa tamko hili. Hivyo ndivyo unavyoweza kujenga maisha ya mafanikio.

    Mimi akujaliye.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

  • Maadui makuu mawili.

    Karibu rafiki, tunajifunza leo kuhusu maadui makubwa mawili ambayo wanatukabili kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukiacha hadaa ya sinema za maigizo ambazo zinaonyesha adui mkuu ni kitu cha nje, Kuna maadui halisi ambao unapaswa kuwakabili katika kujenga ushujaaa wako.

    Katika kitabu cha the dedicated by Pete Davis, anatushirikisha kuwa kuna maadui wa ndani, ambapo wapo ndani yako, tukiachana na ya sinema.

    Anasema kuwa adui wa kwanza ni hofu, ziko ndani yako, kuna hofu kuu tatu ambazo ni hofu ya kujutia, hofu ya mahusiano na hofu ya kupitwa.

    Hofu hizo zinakuzuia usijitoe kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu na kuweza kujenga ushujaaa unaohitajika kuleta mabadiliko.

    Adui wa pili ni uchoshi, kwenye sinema za maigizo kila wakati Kuna tukio jipya la kusisimua, ndiyo maana tunaweza kuangalia sinema hizo kwa muda mrefu.

    Lakini kwenye uhalisia, matukio ya kusisimua ni machache sana. Kwa muda mrefu unahitajika kufanya mambo ya kawaida na yanayojirudia rudia kwa muda mrefu.

    Hii inaleta hali ya uchoshi ambayo ni rahisi sana kumkatisha mtu tamaa, hasa pale matokeo yanapokuwa hayaonekani kwa haraka. Ukichangia na wingi wa machaguo na usumbufu unaomzunguka mtu, ni rahisi sana kuacha kile anachofanya pale anapokutana na uchoshi.

    Mashujaa walioweza kufanya makubwa ambao mpaka sasa tunawakumbuka, waliweza kuwavuka maadui hao makubwa wawili na kujitoa kwenye kile walichochagua.

    Waliondokana na hofu za ndani na kuchagua kitu sahihi watakachopambana nacho kwa muda mrefu. Waliweza kuvuka uchoshi waliokutana nao kwa Kuendelea na mchakato bila kuruhusu usumbufu kuwaingilia.

    Chukua hatua leo, kwa kuamua kufanya kitu kwa kuirudia rudia bila kuacha kwa muda mrefu, zinajikusanya na kuleta matokeo makubwa baadae. Sharti hatua hizo ziwe endelevu bila ya ukomo.

    Wengi huja kushangaa wanapoona matokeo na kuuliza imewezekanaje? Ni hatua ndogo ndogo ndizo zinachangia matokeo makubwa, uwe na siku njema.

    Akujaliye sana,

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

    Email, kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kuchochea matokeo chanya.

    Karibu, tunajifunza leo kuhusu kanuni muhimu inayoweza kuchochea uchanya katika maisha yako ya kila siku. Mazingira yako yanaathiri nguvu zako na kuchochea aina ya matokeo unayopata.

    Kila kitu kinachokuzunguka kinaathiri unavyofikiri, unavyohisi na unavyochukua hatua. Kwa hivyo, kama unataka kupata matokeo makubwa, unahitaji kuchagua kwa umakini mazingira yanayokuzinguka.

    Mazingira yanayokuzunguka yanahusisha watu unaoshirikiana nao, watu unaowafutailia, habari unazozifuatilia, vitabu unavyovisoma, vyakula unavyokuwa, vifaa unavyotumia kwenye kazi zako, usafiri unaotumia, maeneo unapotembelea na pale unapoishi.

    Yote haya yanaungana kwa pamoja na kuwa na nguvu ya kukupandisha juu kuelekea kwenye mafanikio au kukushusha chini na kupelekea kushindwa.

    Kuna kanuni kuu muhimu ambao unatumiwa na wale wanaokadiria kuwa chanya wakati wote. Kanuni iyo inasema kwamba “ingiza chanya utoe chanya”. Kama vile vinavyokuzunguka ni chanya, matokeo unayopata yatakuwa chanya. Na kama vinavyokuzunguka ni hasi, matokeo utakayopata yatakuwa hasi.

    Kuchukua hatua leo, huwezi tumia muda wako wote kufuatilia habari, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii, kuangalia watu wanaoigiza maisha alafu utegemee kufanya makubwa kwenye siku hiyo.

    Kwa hivyo, ni lazima ulinde sana muda wako hili kuhakikisha unachoingiza kwenye ubongo wako ni chanya pekee. Ingawa hasi hazikosi husiruhusu zikusumbue. Hasi zinapokuja unaamua kutafuta chanya kwa kutumia njia yoyote ile.

    Mimi wako akujaliye.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

  • Matatizo makuu mawili kwenye zama tunazoishi.

    Karibu rafiki, Kuna matatizo makubwa mawili yanayokumba watu wengi kwenye zama hizi.

    Tatizo la kwanza ni kuishi kwa mazoea na kufuata mkumbo. Yaani kufanya kile ambacho wengine wanafanya na wamezoea kufanya na kusahau upekee ambao upo ndani yao.

    Tatizo la pili ni watu kutokujali kile wanachokifanya, kiwe ni kazi au biashara watu wanafanya tu kwa mazoea. Hawajitumi na wala hawakazani kutoa thamani ya tofauti.

    Matatizo hayo mawili yamezalisha kundi kubwa la watu ambao wanahangaika sana lakini hawapati mafanikio makubwa.

    Hatua ya kuchukua. Kama unataka kuondokana na matatizo haya unapaswa kuwa wa tofauti. Kwa kuepuka kufanya mambo zako kimazoea na kuacha kufuata mkumbo.

    Penda kujifanyia maamuzi jiridhishe peke yako kwa kufanya udadisi wa mambo badala ya kufuata au kungoja wengine waseme badala yako.

    Unapaswa pia kujali sana kazi au biashara yako jitume na utoe thamani kubwa kwa bosi wako au wateja wako na utafanya makubwa.

    Mimi wako akujaliye.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

    Email, kemeimaureen7@gmail.com

  • Kutoogopa kukosea.

    Kila mtu ameumbwa akiwa na uwezo wa kujaribu kufanya vitu vipya. Hivyo, tunapojaribu kufanya vitu hivyo vipya makosa hayana budi kutokea.

    Kwa hivyo hatupaswi kuogopa kukosea maana ni njia moja ya kujifunza na kujiboresha zaidi.

    Anayeogopa kufanya makosa hataki kukuwa au hataki mabadiliko yoyote katika maisha yake. Ndio maana ni muhimu kutumia nguvu iliyo ndani yetu kwa kujaribu vitu vipya.

    Kupitia mchakato huo wa kujaribu vitu vipya tunafanya makosa mengi, ila tunapojifunza kutokana na makosa haya tunakua zaidi na kupata mwanga wa kuwa jasiri na kujua namna ya kuepuka makosa zingine baadae.

    Hatua ya kuchukua leo, kwa vile una nguvu kubwa ulio ndani yako, hupaswi kwa namna yoyote ile Kuhofia kuchukua hatua itakayokuimarisha. Kwa sababu tu Kuhofia kukosea, kukosea ni mchakato muhimu ya kujifunza.

    Lakini kibaya zaidi ni pale unapokosea alafu unalirudia kosa hilo, haitakuwa kosa tena bali, litakuwa mazoea, yaani umefurahia kurudia kosa hilo.

    Mimi wako akujaliye.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

    Email, kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kutengeneza mtazamo sahihi.

    Mtazamo ulionao yana mchango kubwa Sana kwenye matokeo unayopata kwenye maisha yako. Upo hapo ulipo sasa kutokana na mtazamo ambao umejijengea siku za nyuma. Na mtazamo ulionao leo, ndio utakaokujengea kesho yako.

    Watu wengi wana mtazamo hasi na ambao unawazuia kufanikiwa hata kama wamejiwekea malengo makubwa na wanajua kusudi la maisha yao. Mtazamo wa wengi unajengwa na vitu vitatu ;kujiamini, kujitathmini na kujikubali.

    Kujiamini ni pale mtu anapokuwa na imani ndani yake na kuona kwamba anastahili kupata mafanikio makubwa. Kama unaona hustahili huwezi ukafanikiwa.

    Kujitathmini ni pale mtu anapojua kwamba anao uwezo, ujuzi na maarifa. sahihi ya kufikia lengo alikojiwekea. Kama unajidharau wewe mwenyewe huwezi kufanikiwa.

    Kujikubali ni pale mtu anapokuwa na uhakika kwamba kile anachotaka kinawezekana na kipo ndani ya uwezo wake. Ukianza kuamini haiwezekani au huwezi, huwezi fika popote.

    Akujaliye sana.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Kupata mrejesho wa kweli kutoka kwa watu sahihi.

    Unahitaji watu ambao wamebobea kwenye kile unachofanya na ambao wapo tayari kukupa mrejesho wa kweli hata kama utakuumiza.

    Wawe tayari kukuambia ni wapi unakosea au wapi una udhaifu. Watu hawa wanaweza kuwa waalimu, makocha mashauri na mamenta.

    Huwezi kubobea kama hupati mrejesho wa kweli kutoka kwa wale wanaoelewa kile unachofanya.

    Ni rahisi kujidanganya mwenyewe kwamba upo vizuri, ni mpaka wengine wakueleze ukweli ndiyo utajua kama upo vizuri au la.

    Watu wasio sahihi hawawezi kukupa mrejesho na wenye msaada kwako. Badala yake, wakiona unapika hatua za kimafanikio watahakikisha wanakupa mrejesho mbaya kabisa ili kukukatisha tamaa na uachane na hatua hizo.

    Hatua za kuchukua leo, jua wale wanaokupa ushauri sana sana, kama ni watu ambao wana nia nzuri na juhudi zako au wale wanapanga kukuangusha.

    Baada ya kuwajua anza sasa kuwa makini na wao, usiwe mwazi sana kwao kwa kutowafahamisha hatua zako unazochukua.

    Ni mimi wako anayekujali.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Aina za mtazamo.

    Kuna aina mbili za mtazamo, mtazamo mgando na mtazamo wa ukuaji.

    Kila mtu ana mtazamo hii miwili ndani yake, kwenye baadhi ya mambo mtu ana mtazamo mgando na mambo mengine mtu ana mtazamo wa ukuaji.

    Mtazamo wa mgando sanasana unaleta fikra zinazoweza kukukwamisha. Ilhali mtazamo wa ukuaji unaleta fikra chanya zinazokusaidia upige hatua zaidi.

    Unapaswa kuwa au kuchochea Mtazamo wa ukuaji litakusaidia upate ujuzi ulio sahihi kwenye eneo unalofanyia kazi.

    Unakusaidia kuweka juhudi kwenye kuchukua hatua na kusonga mbele zaidi,unakuwa tayari kwa mchakato, unakuwa tayari kupokea mrejesho kutoka kwa wengine na kufanya kwa ubora zaidi.

    Hatua ya kuchukua leo unapaswa kuyaelewa maeneo ambayo huwa yanachochea mtazamo mgando ndani yako inaweza kuwa kujilinganisha na wengine au unapokutana na ugumu au changamoto.

    Kwa kuyajua maeneo hayo na kuyavuka, itakusaidia kutosumbuliwa na mtazamo mgando.

    Mimi anayekujali

    Maureen Kemei

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.