-
Bosi mbaya kuliko wote.
Pata picha unafanya kazi chini ya bosi ambaye hajali chochote kuhusu wewe. Hakuamini na haoni kama unaweza kufanya makubwa.
Mara nyingi anakutia hofu kwamba saa yoyote anaweza kukuvuta kazi. Au labda anakukazimisha ufanye kazi masaa mingi alafu unapumzika masaa machache.
Huyo bosi si mwingine, bali unamjua vizuri, sababu ni wewe. Wewe ndiye bosi wa kwanza kwako mwenyewe, lakini umekuwa ndiye bosi mbaya kuliko wote duniani.
Umekuwa hujiamini wewe mwenyewe, hukubali kwamba unaweza kufanya makubwa na umekuwa unajipa hofu kupitiliza.
Chukua hatua, anza kujifunza kuwa bosi mzuri kwako. Anza kujiamini wewe mwenyewe na kujikubali kwamba unaweza kufanya makubwa.
Kisha tengeneza mchakato ambao utakuwa unaufuta kwenye kile unachokifanya. Usifanye kwa kubahatisha, bali kwa mchakato.
Kwa kubadilika hivi, utaweza kuwa na utulivu utakaokuwezesha kufanya makubwa.
Akujaliaye sana.
Mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com
-
Kataa kukaa na watu hasi.
Wanasema ogopa watu hasi kama ukoma. Mtazamo hasi huambukiza haraka kama moto wa karatasi na kuleta madhara. Mtazamo kama mimi na unyonge wangu siwezi nikafanya kitu kikafanikiwa.
Mtazamo hasi kama nilizaliwa hivi na nitakufa hivi, mtazamo hasi kama vile nilizaliwa masikini na nitakufa maskini. Ukiziamini maneno hasi kama hizi inamaana umejikubalia na utakuwa hivyo.
Lakini unapokataa maneno hasi kama hizi haziwezi kukupata. Unapoamua kuchukua hatua ya kuepuka matamshi hasi kama hizi. Inamaanisha umeamua kufanikiwa kwenye maisha yako kwa ujumla.
Kwa hivyo hakikisha watu wenye mtazamo wa ukando au hasi kwenye maisha yao, hawapati nafasi kwenye maisha yako, unaweza ukawasilikiza lakini kwa akili yako unajua kabisa unafaa uondoke eneo la tukio kwa haraka. Ili yasijengeke kwenye akili yako.
Ukizungukwa na watu chanya, watu wenye matumaini na mtazamo wa uwezekano na siyo watu waliokata tamaa kwenye maisha yao. Na lengo lao kubwa ni kuwakatisha wengine tamaa, watu hao wanafaa waepukwe kama ukoma.
Chukua hatua, amua kuwaepuka watu hasi na waliokata tamaa kwenye maisha yao. Maana watakuambukiza na wewe utaanza kukata tamaa Unapokutana na changamoto au kikwazo kwenye yale unayofanya.
Akujaliaye sana.
Mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Email, kemeimaureen7@gmail.com
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
-
Ukweli kuhusu kushindwa
Wakati mwingi huwa nasikiliza wachungaji wa madhehebu mbalimbali wanapohubiri. Lakini kati ya wote Kuna menye nawasikiliza napata tumaini la kusonga mbele zaidi. Hata kama kwa wakati huo kuna jambo ambalo limenikwaza sana.
Mchungaji huyo huwa anapenda kusema kuwa “wakristo huwa hawashindwi au hawapati hasara, bali wanajifunza kupitia kushindwa kwao au hasara kwenye biashara ama kazi yoyote wanayofanya.”
Anasema kuwa Mungu huwaweka watu kwenye darasa kwanza wakikosa wanachotaka ndipo watakuwa wamejifunza njia isiyo sahihi ya kupata kile unachotaka.
Hivyo unachopaswa kufanya ni kujifunza njia iliyo sahihi ya kupata unachotaka. Unapojifunza kupitia unachokosea unajua ni njia zipi zisizo sahihi hili usizirudie.
Kushindwa ni pale tu unapokuwa umekata tamaa na unaporudia makosa yale yale. Lakini unapokuwa tayari kujifunza na kuboresha zaidi, hakuna kushindwa, badala yake Kuna kujifunza.
Kukosa unachokitaka haimaanishi kwamba huwezi kukipata, bali inamaanisha hujajua njia sahihi ya kukipata. Hivyo wajibu wako ni kujifunza njia iliyo sahihi na kuitumia.
Wewe mwenyewe ni shahidi, magumu mengi uliyopitia kwenye maisha yako na kuona kama umeshindwa, yamekuwa na mchango mkubwa kwako kupika hatua.
Chukua hatua, hakuna unachopitia kisiwe na manufaa kwako kama utakuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua sahihi.
Akujaliaye, Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
-
Jinsi ya kutuliza hofu isiwe kikwazo kwako.
Karibu, changamoto kubwa kabisa kwenye hofu ni pale tunaposhindwa kuielewa kwa undani. Unapoiona hofu kwa nje inakuwa inatisha sana. Usipochambua kwa undani, hutaweza kupiga hatua, maana utaona ni kikwazo kikubwa.
Kwa kila hofu unayokuwa nayo, usiishie tu kuangalia kwa nje, bali ichimbe kwa undani, uweze kuielewa na kuchukua hatua sahihi. Hatua muhimu ya kuchukua ni kujiuliza kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea?
Kwa chochote unachohofia, usikubali tu hofu hiyo kwa juu juu. Badala yake chimba ndani, jiulize kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea kwenye hilo unalohofia? Jiulize kama kweli hofu hiyo itakutokea kama unavyohofia, ni mambo gani mabaya kabisa yanayoweza kutokea?
Orodhesha yote mabaya unayoona yanaweza kutokea kutokana na kile unachohofia. Kwa kila unaloorodhesha jiulize ni hatua zipi unazoweza kuchukua kulikabili kama kitatokea.
Kisha andika hatua zote unazokwenda kuchukua pale jambo baya kabisa linapotokea ili uweze kurudi kwenye mipango yako.
Kwa kufanya zoezi hili, unagundua wazi kwamba mambo mengi unayohofia hayawezi kutokea na hata kama yatatokea una njia ya kuweza kuyavuka na Kuendelea na mipango yako.
Kwa mfano unapowaza kuanzisha biashara hofu ni itashindwa. Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni biashara kufa na ukapoteza kila kitu. Kama hilo kitatokea unaweza kuanza upya, hata kwa kutafuta kazi au kibarua kwanza ili uweze kujijenga upya.
Chukua hatua , kwa kuamua kabisa kuchambua kile unachohofia kwa undani, unaona wazi kwamba unachohofia sana halipaswi kuwa kikwazo kwako.
Akujaliaye sana.
Mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com.
Email, kemeimaureen7@gmail.com
#fikrachanya #sambazauchanya.
-
Kutokuacha kusudi.
Karibu, hakuna wakati binadamu atasema amekamilika kwa namna yoyote ile, au kwa vile anavyotaka. Hakuna wakati ambao dunia itakuwa Sawa na kila unachohitaji kitakuwa kimekamilika kama unavyotaka.
Kusubiri hadi kila kitu kiwe Sawa ni kujichelewesha. Unachohitaji ni kuwa na kusudi, kuwa na nia njema ya kufanya na kisha kufuata mchakato sahihi.
Kibaya zaidi ni pale tunaposahau kusudi letu hapa duniani na kuanza kujishughukisha na mambo yasiyokuwa na tija yoyote katika maisha.
Kusuluhisha hali hili la kusahau kusudi la maisha ni kukaa kwenye mchakato sahihi, huku ukisukumwa na nia njema na fursa nzuri zaidi inafunguka enyewe.
Hata pale unapoona hakuna njia kabisa, usikate tamaa au kujizuia, badala yake songa mbele na nia yako na fuata mchakato sahihi, njia zitafunguka na utaweza kusonga mbele zaidi.
Chukua hatua, amua kuwa na kusudi la maisha, alafu ufuate mchakato sahihi, ukiendeshwa na nia njema na kwa kweli utafanya makubwa.
Asante, akujaliye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com
-
Hofu siyo adui
Kila mtu huwa anahofia, kila anayefanya kazi kwa mara ya kwanza anakuwa na hofu kubwa. Hata wale wanaoonekana ni majasiri, ndani yao huwa wanakuwa na hofu kubwa. Lakini huwa wanaweza kuzishinda hofu hizo kwa sababu ya mtazamo wanaokuwa nao.
Mabadiliko makubwa ya kimtazamo inayoshauriwa kuyafanya ili kuyashinda hofu ni kuyajua kwamba hofu siyo adui. Hofu siyo kitu ambacho kinalenga kukuangusha na kukushinda. Hofu ni tahadhari ambayo akili yako inakupa, kwa lengo zuri la kuhakikisha unakuwa hai na salama.
Hofu ndiyo imekiwezesha kizazi hadi kizazi kuwa hai mpaka leo. Ni kwa sababu hofu inaleta tahadhari na mtu anapochukua tahadhari hiyo anakuwa salama. Hivyo tunapswa kuchukulia hofu siyo kama kikwazo cha kutufanya tusimame, bali kama tahadhari ya kwenda kwa umakini.
Hatuhitaji kuivunja kabisa hofu ndiyo tuweze kufanya makubwa. Tunachohitajika kufanya ni kuisikiliza, kuielewa na kuchukua hatua uku tukiwa na tahadhari. Hofu huwa inaonekana ina nguvu kwa sababu inagusa zaidi hisia zetu. Na pale kitu kinapogusa hisia, huwa tunakipa uzito zaidi.
Kuchukua hatua ndiyo njia pekee ya kuivuka hofu yoyote tunayokuwa nayo. Kama tulivyoona, hofu inatuingia kupitia fikra na hisia. Na kadiri unavyoitafakari hofu, ndivyo unazidi kuiba nguvu kubwa.
Njia pekee ya kuivuka hofu ni kuchukua hatua, kufanya kile unachohofia kufanya. Baada ya kuisikiliza na kuielewa hofu, unapaswa kuchukua hatua. Haipaswi uendelee tu kuitafakari, badala yake chukua tahadhari ambazo hofu inakupa kisha chukua hatua.
Unapochukua hatua na kupata matokeo mazuri, unazidi kujiamini na kupata hamasa ya kuchukua hatua zaidi. Pale hofu inapokuwa kali na ukashwishika uache kufanya. Usisikilize hofu, badala yake chukua hatua. Hata kama itakuwa hatua ndogo kiasi gani, Ina nguvu ya kuivuka hofu unayokuwa nayo.
Asante ni haya kwa leo, uwe na wakati mwema na #fikrachanya #sambazauchanya.
Akujaliye sana, Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com
-
Mabadiliko binafsi
Habari na karibu.
Mabadiliko binafsi yanahitaji nafasi hili kutokea. Yaani kujaribu kuleta kitu kipya kwenye maisha yako. Unahitaji sehemu ya kukiweka vitu hivi vipya, hivyo inakubidi uondoe vya zamani.
Tumezoea kuambiwa tuache vitu vibaya na visivyokuwa na manufaa kwetu. Lakini Kuna upande mwingine wa hilo, kuacha vitu vizuri na tunavyovipenda ili kutengeneza nafasi ya vitu bora zaidi.
Ni lazima uache chochote kwenye maisha yako, hata kama unakipenda kiasi gani. Kama kuna kitu unajiambia huwezi kukiacha basi jua hicho kina nguvu ya kukutawala na umeshakuwa na uraibu nayo.
Hili tuwe huru na tuhakikishe tunafanya makubwa, lazima tuhakikishe hatupotezi uhuru wa kuamua kuacha chochote. Hivyo, kufanyia kazi uhuru huo mara kwa mara.
Chukua hatua, kila unapokiona unakitegemea sana kitu na kujiambia huwezi ukakiacha au kukikosa, hapo papo amua kabisa akiache. Hilo litakufundisha kwamba uwezo wako ni mkubwa kuliko chochote kile.
Asante rafika uwe na siku na #sambazauchanya #fikrachanya.
Akujaliaye sana, Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Email, kemeimaureen7@gmail.com
-
Raha ya kudumu.
Karibu, kwenye zama hizi tunazoishi vitu mingi vinaonekana kwa juu juu, hivyo huleta raha ya haraka kisha raha hiyo kupotea kabisa.
Kwa hivyo njia mbadala ya kupata raha ya kudumu ni kukataa ukawaida na kuweka umakini woko wote kwenye kile unachokifanya.
Kwa wakati ambao unakifanya unapata ridhiko kubwa kuliko kukifanya kitu kwa juu juu tu. Ridhiko hicho hukuketea raha ndani ya nafsi yako, hivyo unaendelea kufanya bila kuchoka.
Fursa yoyote unayopata ya kufanya kitu, usichukulie kawaida, itumie kama fursa ya kuzama ndani zaidi na kuweka umakini wako wote, kitu kitakachokufanya ukifurahie kitu hicho na ujifunze kudhibiti umakini wako.
Usikubali mawazo yako yahamehame, yaweke kwenye kile unachokifanya ili ukifanye kwa kina na uishi maisha ya kina pia. Kuna raha kubwa katika kufanya kitu chochote kile kwa kina, usikubali kuikosa.
Chukua hatua, amua kuweka umakini wako kwenye kile unachokifanya na usiruhusu usumbufu wowote ule ikuvuruge. Na kwa kufanya hivyo utapata raha ya kudumu na utaishi maisha halisi, ya furaha na raha kweli kweli.
Akujaliye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Uwe na wakati mwema na #sambazauchanya #fikrachanya.
-
Umuhimu wa kujitambua wewe mwenyewe.
Kikwazo kikubwa kinachofanya watu kushindwa kuishi maisha halisi ni kutokujitambua na hivyo kujikuta wakiiga watu wengine.
Hii imekuwa hatari sana kwenye zama hizi ambapo ushauri wa maisha umekuwa mwingi. Wengi wanajikuta wakiiga wengine kwa namna mbalimbali hivyo licha ya kuweka juhudi na muda bado hawafanikiwi. Ni muhimu kujitambua wewe mwenyewe hili ushi maisha halisi kwako.
Kwenye Ustoa, Kuna vitu vinne muhimu ambavyo mtu anapaswa kuvijua kuhusu yeye mwenyewe ili aweze kujitambua na kuishi maisha halisi kwake.
Kitu cha kwanza ni asili yetu kama binadamu. Sisi binadamu tuna asili inayotutofautisha na viumbe wengine wote hapa ulimwenguni. Na uwezo wetu kubwa ni kuweza kufikiri na kufanya maamuzi. Hicho ni kitu kinachopatikana kwa binadamu pekee na chenye nguvu kubwa. Lazima ujue asili hii na uweze kuitumia ili kuishi maisha halisi kwako. Kila mara ni vizuri kutulia na kujiuliza kama umefikiri vizuri na kufanya maamuzi au umefuata tu mkumbo. Wanyama huwa wanafuata mkumbo, wewe usiwe kama wao.
Kitu cha pili ni uwezo wa vipaji uivyonavyo, kila mtu ana uwezo wa kipekee na mkubwa sana ambao amezaliwa nao. Uwezo ambao hauwezi kupatikana kwa mtu mwingine yoyote. Na kila mtu ana vipaji vyake, vitu anavyoweza kuvifanya vizuri na kwa upekee mkubwa.
Jua uwezo wako na vipaji vyako na kuvitumia, maana iyo ndiyo njia pekee ya kuishi maisha halisi kwako. Uzuri ni kwamba uwezo mkubwa na vipaji vyetu huwa havipotei, vinabaki na sisi maisha yetu yote.
Kitu cha tatu ni bahati tunazokutana nazo kwenye maisha. Kuna mambo mengi yanayotokea kwenye maisha ambayo hayapo ndani ya udhibiti wako. Hayo yote huwa yanakuja na fursa nzuri ambazo ukiweza kuzitumia utaishi maisha halisi kwako. Bahati zinaweza kuwa eneo uliozaliwa, elimu uliyopata, watu unaokutana nao na kadhalika. Tangu umezaliwa mpaka sasa umepitia mambo mengi ambayo ukiweza kuyatumia vizuri utaishi maisha halisi.
Kitu cha nne ni utashi wetu ambao unabebwa na kusudi na ndoto tunazokuwa nazo. Yale unayochagua kufanya kwenye maisha yako, ambayo yanatokana na msukumo ulio ndani yako yanakufanya uishi maisha halisi kuliko yale unayoiga. Hivyo ni muhimu sana ulijue kusudi lako na uwe na ndoto kubwa zinazotoka ndani yako hili kuwa na maisha halisi kwako.
Chukua hatua, Ustoa unasisitiza sana tujitambue sisi wenyewe ili tusisumbuke na mambo yasiyo sahihi kwetu. Maana Kuna watu wengine wanaweza wakafanya na wakafanikiwa vizuri, ila wewe na mimi tunaweza tukafanya na tusifanikiwe.
Ili kuepuka kupoteza muda na nguvu, tujitambue na kuishi kulingana na upekee na utofauti wetu. Kuiga maisha ya wengine ndiyo chanzo cha wengi kuwa na maisha magumu.
Wako akujaliye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Uwe na siku njema na # sambaza uchanya.
-
Chanzo cha hofu.
Karibu.
Tofauti yetu sisi binadamu na viumbe wengine ni uwezo wetu wa kupangilia mambo yajayo. Tuna uwezo wa kufikiri na kutengeneza taswira yoyote kwa mambo yajayo. Ni pale uwezo huo unapotumika vibaya, ambapo mtu anatengeneza taswira mbaya ndipo hofu na wasiwasi huzaliwa.
Sehemu kubwa ya vitu ambavyo huwa tunavihofia huwa havitokei. Na hata pale vinapotokea madhara yake huwa siyo makubwa kama vile tuliyokuwa tunahofia. Hivyo hiyo inatosha kusema kuwa hofu na wasiwasi ni matumizi mabaya ya uwezo mkubwa ulio ndani ya kila mmoja wetu.
Kwenye kitabu cha breakfast with Seneca by David Fideller, Seneca anaeleza kuwa kuna hofu kubwa mbili zinazowasumbua wengi, ambazo ni hofu ya kifo na hofu ya umaskini au tamaa ya utajiri.
Hatua ya kwanza ya kukabiliana na hofu ambayo Seneca anafundisha ni kujua kwamba Kuna mambo yapo ndani ya udhibiti wetu na mengine yapo nje ya udhibiti wetu. Hivyo tunapswa kujua yaliyo ndani ya uwezo wetu na kuyafanyia kazi na yaliyo nje ya uwezo wetu kuyakubali jinsi yalivyo.
Hatua ya pili ni kuwa na tafsiri sahihi ya mambo yanayotokea. Mambo huwa yanatokea kwa namna yanavyotokea. Tafsiri kwamba mambo ni mazuri au ni mabaya ni sisi wenyewe tunatengeneza. Hivyo kwa kuacha kuweka tafsiri mbaya kwenye mambo yanayotokea kunasaidia kupunguza hofu na wasiwasi. Ukiacha kujiambia umeumizwa, dhana ya maumivu haipati nafasi kwako.
Hatua ya tatu ni kuishi kwenye wakati ujao. Kama tulivyoona hofu na wasiwasi ni zao la taswira tunazozijengea kwenye wakati ujao. Kama tukiacha kuhangaika na wakati huo ujao na kuishi kwenye wakati uliopo, tutapunguza sehemu kubwa ya hofu na wasiwasi.
Tuchukue hatua sasa, tuna uwezo mkubwa wa akili zetu zinazotuwezesha kukabiliana na yale yaliyo mbele yetu, sasa badala ya kuhangaika na yajayo ambayo hatujayafikia. Tunapaswa kuhangaika na yale tunayomiliki kwa sasa yale tu ambayo yapo ndani ya udhibiti wetu.
Uwe na wakati mwema na #fikrachanyakilasaa .
Akujaliaye, Mwandishi.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com