Tamko chanya la kuanza siku yako.

Jinsi unavyoianza siku yako kuna mchango mkubwa wa jinsi gani siku iyo itakwenda, kama itakuwa ya mafanikio au ya kushindwa. Wengi huzianza siku zao kwa mazoea, wakiwa hawana mikakati wowote hivyo kukimbizana na kila fursa linalopita mbele yao.

Hupaswi kuanza siku yako hivyo, maana hutaweza kufanya makubwa. Unapaswa kuanza kila siku yako kwa tamko chanya litakalokusukuma kufanya zaidi.

Mfano ya tamko za kujiambia kila siku asubuhi ;

Siku ya leo ni baraka nitakayoiheshimu na kuitumia kwa ukamilifu wake. Najua hii ndiyo siku ambayo nina udhibiti nayo.

Kwenye siku hii nitaishi kama kiongozi na siyo mwathirika, kama mtu halisi na siyo feki na kama mwenye maono na siyo mfuasi.

Leo nimechagua kuwa wa kipekee na siyo wa kawaida, jasiri na siyo mwoga na kuwa shujaa na siyo mlalamikaji.

Leo nitatenga muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina, kuepuka yote yanayopoteza muda na kufanya kazi zangu kwa viwango vya kuu kabisa.

Leo nitatimiza kila ninachoahidi na kupeleka umakini wangu wote kwenye yale muhimu niliyochagua kufanya.

Nitatenga muda wa kupumzika na kuuheshimu kwa sabau najua bila mapumziko siwezi nikafanya makubwa.

Siku ya leo nitakuwa mwema kuliko Jana, nitafanya yale yenye manufaa makubwa kwa wengine na siyo kujiangalia mimi mwenyewe.

Sitakubali kuhairisha kirahisi yale niliyopanga, kwa sababu mimi ni mfanyaji na siyo mwongeaji.

Nitamaliza siku yangu kwa kuitathmini jinsi ilivyokwenda, kujua yale niliyofanya na namna ya kuboresha zaidi kwenye siku unafuata.

Chukua hatua, jiambie tamko kama hili kila unapoianza siku yako kwa mwongozo wa tamko hili. Hivyo ndivyo unavyoweza kujenga maisha ya mafanikio.

Mimi akujaliye.

Maureen Kemei.

Blog, kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment