Karibu, kwenye zama hizi tunazoishi vitu mingi vinaonekana kwa juu juu, hivyo huleta raha ya haraka kisha raha hiyo kupotea kabisa.
Kwa hivyo njia mbadala ya kupata raha ya kudumu ni kukataa ukawaida na kuweka umakini woko wote kwenye kile unachokifanya.
Kwa wakati ambao unakifanya unapata ridhiko kubwa kuliko kukifanya kitu kwa juu juu tu. Ridhiko hicho hukuketea raha ndani ya nafsi yako, hivyo unaendelea kufanya bila kuchoka.
Fursa yoyote unayopata ya kufanya kitu, usichukulie kawaida, itumie kama fursa ya kuzama ndani zaidi na kuweka umakini wako wote, kitu kitakachokufanya ukifurahie kitu hicho na ujifunze kudhibiti umakini wako.
Usikubali mawazo yako yahamehame, yaweke kwenye kile unachokifanya ili ukifanye kwa kina na uishi maisha ya kina pia. Kuna raha kubwa katika kufanya kitu chochote kile kwa kina, usikubali kuikosa.
Chukua hatua, amua kuweka umakini wako kwenye kile unachokifanya na usiruhusu usumbufu wowote ule ikuvuruge. Na kwa kufanya hivyo utapata raha ya kudumu na utaishi maisha halisi, ya furaha na raha kweli kweli.
Akujaliye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Uwe na wakati mwema na #sambazauchanya #fikrachanya.