-
Sababu 7 za kujihurumia.
Rafiki yangu unaweza kuwa unajiuliza kwamba kujihurumia huku ni nini hasa,ni nafasi mbaya ya kichwa tunayoweza kuingia tunapojiskia kuwa hali ya chini.
Tunajionea huruma kwa magumu tunayovumilia. Huzuni hii ya kujieleza mara nyingi hutufanya tujisikie vibaya zaidi au kutenda kama kilio cha kuomba msaada,tukitumaini wengine watatuona na kutufariji .
Kujihurumia kunajidhihirisha tofauti kwa kila mtu. Hapa kuna baadhi ya mawazo ya kawaida ya kujihurumia yanaweza kusababisha :
- Watu hawakupendi.
- Wewe ni wa kushindwa tu.
- Una bahati mbaya.
- Maisha huwa magumu kwako kila wakati.
- Maisha hayana aki.
- Mabadiliko hayapatikani.
Kupambana na mawazo haya hasi au ya kiotomatiki,iwe huna uzoefu wowote au yote,kunaweza kukua sana,na kuchangia kushuka kwa kasi.
Kujihurumia sio mbaya kwa asili . Ni hali ya kawaida ya akili wakati mambo mabaya yanapotokea. Kujiskia kuchanganyikiwa kwako mwenyewe kwa sababu jambo muhumu limetokea ni afya,mradi halidumu milele. Kuetegemea kwenye uhasi kwa muda ni sawa lakini isikuwe mtindo wa maisha.
Kujihurumia mara nyingi husababishwa na kuhimizwa na vyanzo sawa, kwa hivyo kubainisha kwa nini unahisi hivi ni hatua ya kwanza ya kukomesha. Hapa kuna sababu za kawaida za kujihurumia:
- Kutokujithamini: Wakati thamani yetu ya ubinafsi imeshuka,tunakuwa na hali ya kujiamini kidogo na uzoefu wa maisha yetu kama yapo nje ya udhibiti wetu.
- Kiwewe: Kuchukuliwa vibaya au kutukanwa kunaweza kutufanya tujisikie kuwa hatuna thamani na kana kwamba maisha ni dhidi yetu.
- Huzuni: Huzuni nyingi huhisi mbaya sana ni vigumu kutojihurumia.
- Hisia za kushindwa: Tunapopata kushindwa,mara nyingi ni rahisi kulaumu nguvu za nje badala ya kuwajibikia.
- Ugonjwa au maumivu ya muda mrefu: Ikiwa kila mtu karibu nasi ana afya na kustawi, usumbufu na mateso yetu yanaweza kuhisi kutotendewa haki.
- Hisia za upweke: Kuhisi kutengwa katika uzoefu wetu mara nyingi hutukuza kujihurumia.
- Dalili za imposter: Baadhi ya mawazo yetu hasi yanaweza kuwa yanatokana na kuhisi kama hatukistahiki au hatufai mahali fulani. Ugonjwa huu wa udanganyifu huenda hauna mantiki,na tunaweza kuibadili kwa kuboresha ujuzi wetu na kujenga kujiamini.
Kujihurumia mara nyingi kunachochewa na wale walio karibu nasi,ikiwa watu wako wa karibu wanashughulikia changamoto za maisha kwa njia hii kuna uwezekano mkubwa utafanya hivyo.
Jaribu kuunda uwajibikaji na jumuiya kwa kujifunza jinsi ya kuacha kujihurumia na watu wa karibu nawe.
Uliza mtu unayemwamini akumbuke unapoonyesha dalili za kujihurumia na uangalie maendeleo. Hii itaongeza kasi ambayo unaimarisha mawazo chanya zaidi.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Vitu 4 muhimu unavyopaswa kuvijua kuhusu wewe mwenyewe.
Kikwazo kikubwa kinachofanya watu kushindwa kuishi maisha halisi kwao ni kutokujitambua na hivyo kujikuta wakiiga watu wengine.
Na hii imekuwa hatari sana kwenye zama hizi ambapo ushauri wa maisha umekuwa mwingi. Wengi wanajikuta wakiiga wengine kwa namna mbalimbali hivyo licha ya kuweka juhudi na muda,bado hawafanikiwi.
Ni muhimu sana kujitambua wewe mwenyewe ili uweze kuishi maisha halisi kwako.
Kwenye ustoa,kuna vitu vinne muhimu ambavyo mtu anapaswa kuvijua kuhusu yeye mwenyewe ili aweze kujitambua na kuishi maisha halisi kwake.
Kitu cha kwanza ni asili yetu kama binadamu. Sisi binadamu tuna asili inayotutofautisha na viumbe wengine wote hapa ulimwenguni.
Na asili yetu kubwa ni uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi. Hicho ni kitu ambacho kinapatikana kwa binadamu pekee na chenye nguvu kubwa.
Lazima ujue asili hii na uweze kuitumia Ili kuishi maisha halisi kwako. Kila mara jiulize kama umefikiri na kufanya maamuzi au unafuata tu mkumbo. Wanyama huwa wanafuata mkumbo,wewe usiwe kama wao.
Kitu cha pili ni uwezo na vipaji ulivyonavyo. Kila mtu ana uwezo wa kipekee na mkubwa sana ambao amezaliwa nao. Uwezo ambao hauwezi kupatikana kwa mtu mwingine yeyote. Na kila mtu ana vipaji vyake,vitu anavyoweza kuvifanya vizuri na kwa upekee mkubwa.
Jua uwezo wako na vipaji vyako na kuvitumia,maana hiyo ndiyo njia pekee ya kuishi maisha halisi kwako. Uzuri ni kwamba uwezo mkubwa na vipaji vyetu huwa havipotei,vinabaki na sisi maisha yetu yote.
Kitu cha tatu bahati tunazokutana nazo kwenye maisha. Kuna mambo mengi yanayotokea kwenye maisha yako, ambayo hayapo ndani ya udhibiti wako. Hayo yote huwa yanakuja na fursa nzuri ambazo ukiweza kuzitumia utaishi maisha halisi kwako.
Bahati zinaweza kuwa eneo ulilozaliwa,elimu uliyopata,watu unayokutana nao na kadhalika. Tangu umezaliwa mpaka sasa umepitia mambo mengi ambayo ukiweza kuyatumia vizuri utaishi maisha halisi.
Kitu cha nne ni utashi wetu ambao unabebwa na kusudi na ndoto tunazokuwa nazo. Yale unavyochagua kufanya kwenye maisha yako,ambayo yanatokana na msukumo ulio ndani yako yanakufanya uishi maisha halisi kuliko yale uliyoiga.
Hivyo ni muhimu sana ujue kusudi lako na uwe na ndoto kubwa zinazotoka ndani yako ili kuwa na maisha halisi kwako.
Ustoa unasisitiza sana tujitambue sisi wenyewe ili tusisumbuke na mambo yasiyo sahihi kwetu. Maana kuna mambo wengine wanaweza kufanya na wakafanikiwa vizuri,ila sisi tukafanya tusifanikiwe.
Kuchukua hatua; kuepuka kupoteza muda na nguvu, tujitambue na kuishi kulingana na upweke na utofauti wetu. Kuiga maisha ya wengine ndiyo chanzo cha wengi kuwa na maisha magumu.
Mwandishi wako.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Busara za Babu Warren.
Kutoka kwenye kitabu cha ‘the third door ‘ Alex Banayan anatushirikisha jinsi alivyokutana na wanamafanikio mbalimbali kwenye safari yake ya kutaka kujua nini kiliwafanya wafanikiwe.
Baada ya Alex kuhakikishwa mahojiano na Warren Buffett,Alex aliomba kabla hajatuma barua hiyo ajiandae kwanza Ili atakapopata nafasi atumie vizuri.
Alienda kusoma kila kitu kinachomhusu Warren Buffett. Alikusanya vitabu 15 vya wasifu wa Warren Buffett,na mafunzo mengine yanayomhusu . Mchana alikuwa anasoma vitabu,jioni anasikiliza sauti na usiku anaangalia video za Warren.
Katika kipindi hicho alichota busara nyingi sana kutoka kwa Warren Buffett kupitia maarifa aliyopitia yanayomhusu. Aliweza kupata majibu ya changamoto ambazo yeye na hata marafiki zake walikuwa wanapitia.
Alijifunza jinsi Warren Buffett alivyoanza biashara akiwa na umri wa miaka 6. Alijifunza jinsi alivyoanza uwekezaji mapema na kuwa dalali wa soko la hisa.
Wakati anaanza ilikuwa vigumu kupata mkutano na matajiri aliolenga kuwauzia hisa. Hivyo alitafuta ushawishi mzuri zaidi ambapo aliwaambia ana njia ya kuwasaidia kupunguza kodi wanayolipa na hapo kila mmoja alikuwa tayari kukutana naye.
Hapo alijifunza kwamba watu wanaweza kukataa kukutana na wewe kwenye kile ulicholenga,lakini kuna kitu wanachohitaji,ukiweza kukijua na kuitumia,watakubali kukutana na wewe.
Pia alijifunza umuhimu wa kuchagua kazi inayokupa ujuzi na uzoefu kuliko inayokulipa sana. Wakati Warren anahitimu shahada yake ya uzamivu kwenye biashara (MBA ). Alikuwa na fursa ya kupata kazi ambayo ingemlipa sana. Lakini yeye hakufanya hivyo,aliomba kufanya kazi kwa aliyekuwa mwekezaji maarufu na mwalimu wake Ben Graham.
Kwa miaka miwili maombi yake yalikataliwa,hata alipokuwa tayari kufanya kazi bure bado alikataliwa. Lakini kwa ung’ang’azi wake alifanikiwa kupata kazi hiyo.
Alifanya kwa miaka miwili na kujifunza mengi na Graham alipostaafu, Warren alienda kuanzisha kampuni yake ya uwekezaji na wateja wote wa Graham wakawa wake.
Alex aliwasimulia marafiki zake yale yote aliyojifunza kwa Warren na mara zote walipata majibu ya changamoto zao. Na wote walimchukulia Warren kama babu yao na kutegemea sana busara zake katika maisha yao .
Kuchukua hatua, Warren Buffett ni mfano mzuri kwetu tukijifunza kutoka kwake tutaweza kuwekeza na kufanya biashara kwa mafanikio makubwa,bora tu tuwe tayari kujifunza na kuchukua hatua.
Akupendaye sana.
Mwandishi Maureen,
www.uamshobinafsi.com.
-
Mambo 7 ya kujifunza Kwa Warren Buffett.
Tumeshaona jisni ambavyo hatujifunzi somo sahihi kutoka kwa Warren Buffett kuhusu uwekezaji ambalo ni kuanza mapema na kuacha riba mkusanyiko ifanye maajabu yake.
Kuna mengine ya kujifunza kwake,hasa ambayo hakuyafanya na hivyo kuepuka kupoteza utajiri wake. Tujifunze Ili tujue vitu vya kuepuka kama tunataka kupata na kubaki kwenye utajiri.
Yafuatayo ni mambo mengine muhimu kujifunza kwa Warren Buffett;
- Hajawahi kukopa kupitiliza.
- Hakuwahi kutaharuki na kuuza uwekezaji wake katika midororo ya uchumi 14 ambayo ameipitia katika maisha yake.
- Hajawahi kuharibu jina na sifa yake kwa kufanya mambo yasiyo sahihi.
- Siyo mtu wa kun’gang’ana na njia au mtazamo mmoja.
- Amekua akiwekeza kwa sehemu kubwa fedha zake mwenyewe na siyo kutumia fedha za wengine.
- Hakujichosha na kuamua kustaafu uwekezaji,badala yake amekuwa akienda taratibu bila kuchoka.
- Amevuka magumu na mabaya mengi na kubaki akiwa kwenye utajiri wake, tangu akiwa na miaka 11 mpaka sasa miaka 90 hajawahi kuanguka kwa sababu amekuwa anaepuka yasiyo sahihi.
Kuchukua hatua kupitia haya mambo muhimu ambayo tumejifunza tunapata kujua namna ya kuepuka kupoteza utajiri wetu kwa mambo mbalimbali.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei
www.uamshobinafsi.co.ke.
-
Siri kuu ya Warren Buffett.
Warren Buffett ndiye mwekezaji ambaye vitabu vingi zaidi vimeandikwa kuhusu yeye kwenye uwekezaji.
Vitabu zaidi ya 2,000 vimeandikwa na vyote vinajaribu kumwelezea Buffet jinsi alivyo mwekezaji bora.
Lakini vitabu hivyo havielezi siri moja kubwa kuhusu mafanikio ya Buffet,kwamba alianza kuwekeza tangu akiwa mtoto .
Mwaka wa 2020,akiwa na umri wa miaka 90,thamani ya utajiri wake ikifikia dola bilioni 84.5 . Lakini kati ya hizo dola bilioni 84.2 amezipata baada ya kuvuka umri wa miaka 50 .
Hapo kumbuka alianza kuwekeza akiwa na miaka 11. Hivyo miaka karibu 40 ya kuwekeza, hakupata utajiri mkubwa,lakini miaka 40 ya baadaye,amepata zaidi ya asilimia 99.999 ya utajiri wake wote.
Iwapo Warren Buffett angeanza kuwekeza akiwa na miaka 60 na kustaafu uwekezaji akiwa na miaka 60,asingefika hata bilioni moja na hakuna ambaye angemjua.
Hivyo siri kuu ya mafanikio ya Warren Buffett kwenye uwekezaji ni msimamo wake kwa zaidi ya miaka 75 kwenye kuwekeza na kuacha uwekezaji ukue kwa riba mkusanyiko bila kuuvuruga.
Kuna wawekezaji wengi ambao wana mbinu za kuzalisha faida kubwa kwa mwaka kuliko Buffet. Mfano Jim Simons amekuwa akitengeneza faida ya 66% kila mwaka tangu mwaka 1988. Kwa wastani Buffet anazalisha faida ya 22% kwa mwaka ,theluthi ya Simons. Lakini Buffet ni tajiri zaidi,kwa sababu ya muda.
Simons ambaye utajiri wake ni dola bilioni 21,alianza uwekezaji akiwa na umri wa miaka 50. Hivyo kama angeanza mapema kama Buffett,na akaenda kwa viwango alivyonavyo,angekuwa na utajiri mkubwa sana kwa sasa.
Hatua ya kuchukua, rafiki yangu tumeona jinsi kuanza uwekezaji mapema ulivyomfanya Buffet kuwa Bilionea na mfano bora kwetu. Kwa hivyo,tunangoja nini rafiki yangu,kama tunataka kuajia watoto wetu uridhi mzuri na wafurahie maisha. Mimi naanza kuwekeza,je wewe unangoja nini?.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Namna ya kupata utulivu wa akili.
Katika zama tunazoishi sasa,ni zama zenye kelele na usumbufu wa kila aina, kupata utulivu wa akili ni kitu kigumu sana .
Hivyo ni kwa sababu kila mtu anawinda umakini wako na kutaka kuteka akili yako.
Kupata utulivu wa akili lazima uzuie kelele na usumbufu visiingie kabisa kwenye akili yako.
Rafiki yangu unaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia haya:
1.Usifuatilie habari kwenye TV,redio,magazeti au mtandao.
2. Ondoka kwenye mtandao wa kijamii.
3. Usibishane na mambo ya siasa, mchezo,dini na mapenzi.
4. Usihangaike kufuatilia maisha ya watu maarufu.
Unaweza kujiuliza utajuaje yale yanayoendelea kama hufuatilii habari. Kwanza mengi yanayoendelea kwenye habari kila siku siyo muhimu.
Na yale muhimu kabisa lazima yatakufikia kupitia watu wengine. Njia bora ya kutumia akili yako ni kujifunza kupitia usomaji wa vitabu na makala zenye maarifa yenye tija na unayoweza kutumia kupiga hatua.
Kwani rafiki yangu habari nyingi ni hasi na za kusisimua , unapaswa uachane nayo maana yatakufanya uwe hasi kwenye mambo mengi kimaisha.
Uhasi ukianzia akilini utaathiri mtazamo wako hivyo unajipata umekuwa hasi kwenye kila kitu,hilo linaathiri sana mafanikio yako .
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Jinsi ya kutambua maono yako.

think it up,feel it ,act it out. Rafiki yangu mpendwa karibu sana,kama una ndoto,au unataka kujua maono yako,kumbuka hili. Mungu anapenda watu kama wewe wenye maono. Anapeana maono na anavutiwa sana na watu kama wewe wanaopenda kuota ndoto kubwa .
Rafiki yangu usisahau kwamba wewe ni wa tofauti,ni wa muhimu na hakuna atakayeweza kuchukua nafasi yako. Hukuumbwa hili uwe kama wengine. Ukiamua kuwa wa kawaida,hatima yako nayo itakuwa wa kawaida tu . Mungu anakutaka utumie kipaji alichokupa na pia kukikuza kipaji hicho.
Ni nini tofauti kati ya mwota ndoto anayeota ndoto na kuielewa na kuifanyia kazi na yule ambaye anaota ndoto wala hachukui hatua yoyote ile kwenye kuifikia ndoto yake?
Anayefanikiwa kwenye ndoto zake anazoota ni yule mwenye maono makubwa na anayefanyia kazi ndoto hizo. Ikiwa mtu huyo atakubali maono hayo juu yake,basi kuna uwezekano wa kuondoka kwenye hali yake ya sasa na kuelekea kwenye kukamilisha kusudi lake la maisha.
Kama unasikia kuvinyiliwa mahali,au huna cha kufanya,hujapewa nafasi ya kufanya kazi yako kwa ubora zaidi. Kama una biashara yako mwenyewe na unataka ikue,kama unataka kujua jinsi ya kukimbiza ndoto zako na malengo yako; kama watoto wako wamekua ama wako shuleni,na unataka kuzingatia ufufuaji wa maslahi ya zamani,au pahali ulipo sasa kwenye maisha,kutambua maono yako yatakusaidia kukamilisha yafuatayo:
1. Kuelewa maono na kwa nini muhimu kwenye mafanikio yako.
2.Kugundua na kuishi kusudi lako.
3. Kutambua maono yako, malengo yako na kukaa kwenye mchakato.
4. Kushinda changamoto wakati unaendea maono yako.
5. Kujifunza ufunguo kamili wa kutimiza ndoto zako.
6. Kutengeneza mpango maalum wa kufikia ndoto zako.
7. Utaishi maisha unayopaswa kuishi.
Kutoka kwenye kitabu cha ‘the principles and powers of vision,’ by Myles Munroe, Munroe anasema kwamba hamu yake ni kuwa tutahamasika,tutashawishika,na kupata changamoto ya kurudi kwenye njia sahihi kuelekea kwenye ndoto zetu,na pia kupata maono ya kutimiza malengo yetu.
Munroe anasema kuwa anataka tuachane na tabia ya kuwa farasi anayetikisa na kuwa farasi hai,yaani maono hai kwetu. Anasema kufanya hilo kunahitaji kuelewa na kufanyia mazoezi kanuni yatakayotuvusha kwenye mwenendo wa kisasa na hata kwenye hekima ya kawaida.
Mafanikio yako haitategemea uchumi wa nchi,au vipaji gani vinahitajika sasa hivi,au soko la ajira liko aje kwa sasa? Hautasumbuliwa na hali yako ya awali ya kukosa rasilimali ama kukwazwa na nini watu wanasema unaweza au huwezi kufanya? Ukifuata kanuni sahihi utaweza kufikia maono yako bila kujali wewe ni nani au umetoka wapi?.
Munroe anasema kuwa ‘wewe ni jumla ya maamuzi na chaguzi unazofanya kila siku,you are the sum total of the choices and decisions you make everyday. Unaweza amua ukae hapo ulipo sasa hivi,au kwenda mbele zaidi kwa kukimbiza ndoto zako.
Anatupa changamoto siku ya leo ya kuacha kulalamikia na kutoa sababu za kwa nini huwezi ukatimiza kila ambacho ulizaliwa kufanya.
Ondoa maisha yako kutoka kwenye usawa na kujifananisha na kila mtu. Mungu amekupa nguvu na majukumu ya kuweza kufikia maono yako.
Watu wengi hufanya mambo kwa sababu wanapaswa kufanya. Wewe rafiki yangu usifanye mambo yako tu kwa sababu unataka tu kufanya,bali kwa sababu ya kutimiza kusudi lako.
Unahitajika kuchagua kufanya jambo kwa sababu ya kukerwa bali sio kwa sababu ya kujihami. Naamini utaweza kuamua na kugundua kwamba umetosheka na kuwa wa “kawaida” na unatangaza utofauti wako. Kumbuka,uliumbwa kuwa wa kipekee sana bali sio kuchang’anywa. Ulibuniwa sio tu uwe wa maana na wa kipekee,bali pia kuwa mtalaamu. Yaani rafiki yangu uliumbwa kukamilisha kitu ambacho hakuna anayeweza kukamilisha.
Never expect anything less than the highest thing you can go after. Yaani usitarajie kitu chini ya kile kilicho juu unachoweza kufikia.
Usiruhusu watu wakuambie “huhitaji kuwa na matarajio makubwa” kila mara ndani yako kuna uwezo wa kuota ndoto kubwa,haijalishi ni changamoto ya aina gani unapitia,usikate tamaa,kwa sababu maono yako ni ufunguo wa kutimiza kusudi la maisha yako.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Namna ya kubadili kufikiri kusiko sahihi.
Rafiki yangu kuna mambo mengi uliyojifunza siku za nyuma ambayo kwa sasa siyo sahihi tena. Maana muda unakwenda kwa kasi sana na mambo yanabadilika.
Kutoka kwenye kitabu Cha “hell yeah or no” jinsi ya kujua thamani kwako kufanya,kilichoandikwa na aliyekuwa mwanamuziki Derek Shivas. Anatushirikisha njia bora ya kurekebisha kufikiri kusiko sahihi.
Anatushirikisha kuwa imani zilizokuwa sahihi huko nyuma kwa sasa siyo sahihi tena. Rafiki yangu ukiendelea kun’gang’ana na mambo ya nyuma,kwa sababu tu yalikuwa na manufaa kwa wakati huo siyo sahihi.
Kwani ukiendelea hivyo,utarudi nyuma kwa mambo mengi ya kiamaendeleo kwenye kazi , biashara na hata maisha kwa ujumla. Unapaswa ufike mahali na kubadili yale unayojifunza ,yaani yale unayolisha akili yako kila siku
Unapaswa kabisa uondoe yale yaliyopitwa na wakati na ambayo kwa sasa siyo sahihi tena na uweke ambayo yanakwenda na wakati na ni sahihi kwa wakati huu.
Kinachokufikisha hapo ulipo sasa siyo kitakachokufikisha mbele zaidi. Hivyo mara zote kuwa tayari kujifunza vizuri vitu vipya na kuboresha zaidi.
Ili kukamilisha hilo, unapaswa kufuata hatua hizi tatu;
1.Kuwa na mashaka na kile unachojua ,usijipe uhakika kwenye kitu chochote.
2. Acha tabia ya kujiambia tayari unajua kitu,kuwa tayari kujifunza upya,hata kama tayari unajua.
3.Kwa kila unachojua tafuta uthibitisho kwamba bado ni sahihi mpaka Sasa. Kama siyo sahihi kibadili.
Kuchukua hatua,kama huendelei kujifunza kila siku,tena kwa makusudi kabisa,hutaweza kujua na badala yake utakuwa unarudi nyuma.
Dunia inakwenda kwa kasi,kuweza kwenda nayo kasi lazima uwe tayari kuacha vile ulivyojifunza huko nyuma na kujifunza vipya zaidi.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@kemeimaureen
-
Umuhimu wa kuwa mwaminifu mara zote.
Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze siku ya leo. Wanasema kuwa uaminifu ni sera bora muhimu sana kwenye maisha hasa kazi na kwenye biashara.
Wale wasiowaaminifu wanaweza kufanikiwa kwa muda mfupi,ila hawawezi kudumu kwenye mafanikio hayo kwa muda mrefu.
Kwa kuwa mwaminifu unaweza ukakosa baadhi ya vitu kwa sasa,lakini hilo litakuweka kwenye nafasi ya kupata makubwa mazuri zaidi kwa baadae.
Msingi bora wa kuzingatia maisha na hasa kwenye mauzo ni kujenga uaminifu kwa kufanya kile kilicho sahihi mara zote .
Hata kama unaona mteja hajui,kama wewe unajua basi fanya kilicho sahihi . Kwa sababu kujua kilicho sahihi itakusumbua wewe mwenyewe kwenye nafasi yako na pia itakupotezea wateja.
Kila unapomhudumia mteja wako,jiulize swali hili ‘je,kama mimi ningekuwa ndiyo huyu mteja na nikawa najua yale niliyojua,je ningefurahia kuhudumiwa na mtu wa aina kama yako?’
Kwa kusimamia sera ya uaminifu kwenye mauzo,utaweza kujenga biashara inayokua kwa muda mrefu na yenye manufaa makubwa.
Mteja mmoja amebeba wateja wasiopungua 250. Kama ambavyo sheria ya Girard 250 inavyosema ‘kila mtu ana watu 250 ambao anajuana nao moja kwa moja’. Hivyo jambo unalofanya kwa mtu mmoja,liwe zuri au baya kitafikaia kwa watu wasiopungua 250.
Kama utamfanyia mteja wako kitu kizuri,jua ana nguvu ya kukisambaza kwa watu wengine 250. Na kama utamfanyia mteja wako mabaya,jua atakusema vibaya kwa watu wengine 250.
Kwa kujua sheria hiyo na kuzingatia utaepuka kupoteza wateja ambayo hujakutana nao na pia utakaribisha wateja ambao hujakutana nao .
Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha au kwenye mauzo ni kuona mteja mmoja na usione kama wa umuhimu wowote,labda usimchukulie kwa uzito.
Kwanza mteja hata akiwa peke yake kwa wakati wote ambao anaweza kununua kwenye biashara yako,analeta faida kubwa sana . Kama utamhudumia kwa uaminifu,ataendelea kununua kwako kwa muda mrefu.
Pili ,huyu mteja siyo kisiwa ana watu wake wa karibu. Chochote unachofanya kwa mteja huyo hakiishii kwake tu,bali kunafikia hawa hao wengine.
Hivyo unapomwangalia mteja mmoja,jua kuna wateja wengine wasiopungua 250 walio nyuma yake.
Hatua ya kuchukua; kuwa mwaminifu kwa kila mteja Ili uweze kujenga sifa nzuri itakayosambazwa kwa wateja ambao nao wanakuamini.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Umuhimu wa kuchagua fursa moja na kuifanyia kazi.
Rafiki yangu nataka leo tujifunze kutokana na tabia ya punda,punda akiwekewa nyasi upande mmoja na maji wa pili anajikuta njia panda . Anakuwa anataka ale nyasi na pia anywe maji.
Hivyo atabaki hapo akiangalia ni jinsi gani anaweza kupata vyote kwa pamoja. Kinachotokea ni anakufa kwa njaa na kiu wakati amezungukwa na nyasi na maji.
Ambacho punda anashindwa kukijua ni kwamba,japo hawezi kufanya vyote kwa pamoja,anaweza kuanza na kimoja kisha kwenda kwenye kingine. Anaweza akaanza kula nyasi Kisha kwenda kunywa maji.
Rafiki ,kabla hujamshangaa punda kwa kufa njaa huku akiwa na nyasi, hebu rudi kwako, ni fursa ngapi nzuri zimekuzunguka? Na je, katika fursa hizo ni ngapi unazifanyia kazi?
Kwa walio wengi hasa kwenye zama hizi za mafuriko ya fursa, wanajikuta hawafanyi chochote. Wana fursa tano mbele yao na wanataka kuzifanyia kazi zote,kitu ambacho hakiwezekani ,hivyo wanaishia kutofanya chochote .
Suluhisho kwenye hali hiyo ni rahisi,chagua fursa moja na ifanyie kazi mpaka itakapokamilika,kisha nenda kwenye fursa nyingine.
Hata kama una fursa tano mbele yako ,ukiipa kila fursa miaka mitano ya kuifanyia kazi kwa uhakika,utapiga hatua kubwa kuliko kusubiri mpaka uweze kufanyia kazi zote kwa pamoja.
Katika fursa nyingi zinazokuzunguka,chagua moja utakayoifanyia kazi kwa uhakika na kusema hapana kwa nyingine mpaka utakapokamilisha hiyo.
Kisha nenda kwenye fursa nyingine kwa mpango huo huo. Muda utakwenda iwe utachukua hatua au la . Hivyo badala ya kupoteza muda, chukua hatua.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com