Siri kuu ya Warren Buffett.

Warren Buffett ndiye mwekezaji ambaye vitabu vingi zaidi vimeandikwa kuhusu yeye kwenye uwekezaji.

Vitabu zaidi ya 2,000 vimeandikwa na vyote vinajaribu kumwelezea Buffet jinsi alivyo mwekezaji bora.

Lakini vitabu hivyo havielezi siri moja kubwa kuhusu mafanikio ya Buffet,kwamba alianza kuwekeza tangu akiwa mtoto .

Mwaka wa 2020,akiwa na umri wa miaka 90,thamani ya utajiri wake ikifikia dola bilioni 84.5 . Lakini kati ya hizo dola bilioni 84.2 amezipata baada ya kuvuka umri wa miaka 50 .

Hapo kumbuka alianza kuwekeza akiwa na miaka 11. Hivyo miaka karibu 40 ya kuwekeza, hakupata utajiri mkubwa,lakini miaka 40 ya baadaye,amepata zaidi ya asilimia 99.999 ya utajiri wake wote.

Iwapo Warren Buffett angeanza kuwekeza akiwa na miaka 60 na kustaafu uwekezaji akiwa na miaka 60,asingefika hata bilioni moja na hakuna ambaye angemjua.

Hivyo siri kuu ya mafanikio ya Warren Buffett kwenye uwekezaji ni msimamo wake kwa zaidi ya miaka 75 kwenye kuwekeza na kuacha uwekezaji ukue kwa riba mkusanyiko bila kuuvuruga.

Kuna wawekezaji wengi ambao wana mbinu za kuzalisha faida kubwa kwa mwaka kuliko Buffet. Mfano Jim Simons amekuwa akitengeneza faida ya 66% kila mwaka tangu mwaka 1988. Kwa wastani Buffet anazalisha faida ya 22% kwa mwaka ,theluthi ya Simons. Lakini Buffet ni tajiri zaidi,kwa sababu ya muda.

Simons ambaye utajiri wake ni dola bilioni 21,alianza uwekezaji akiwa na umri wa miaka 50. Hivyo kama angeanza mapema kama Buffett,na akaenda kwa viwango alivyonavyo,angekuwa na utajiri mkubwa sana kwa sasa.

Hatua ya kuchukua, rafiki yangu tumeona jinsi kuanza uwekezaji mapema ulivyomfanya Buffet kuwa Bilionea na mfano bora kwetu. Kwa hivyo,tunangoja nini rafiki yangu,kama tunataka kuajia watoto wetu uridhi mzuri na wafurahie maisha. Mimi naanza kuwekeza,je wewe unangoja nini?.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment