Home

  • Sababu kubwa ya kujijengea umakini.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Ili kujijengea umakini mkubwa kwa kitu chochote unachofanya, unapaswa kuweka fikra zako zote kwenye kitu hicho.

    Kwa kawaida fikra zetu huwa zinazurura hazikai eneo moja kwa muda mrefu. Lakini fikra hizo zinaweza kudhibitiwa na kuwa vile mtu unavyotaka.

    Katika kuzidhibiti fikra hizo,tambua pale zinapotoka kwenye kile unachofanya na kwenda kwenye kitu kingine kisha zirudishe kwenye kile unachofanya.

    Kuwa mlinzi wa fikra zako mwenyewe, hakikisha zinakaa kwenye kile unachofanya badala ya kuzurura kwenye vitu vingine.

    Kufanya jambo moja kwa wakati pia inasaidia sana kujenga umakini wako. Wapo wanaodhani kufanya mambo mengi kwa pamoja ni kuongeza ufanisi. Lakini siyo kweli, inashusha umakini na kuathiri ufanisi.

    Panga kufanya jambo moja kwa wakati, weka fikra zako zote kwenye jambo hilo unalofanya kwa wakati unapofanya mpaka likamilike au muda uliopanga kulifanya uishe.

    Kudhibiti mazingira yako pia ni muhimu kwenye kujijengea umakini. Kama mazingira yana usumbufu mkubwa, umakini wako utasumbuka.

    Kuchukua hatua rafiki yangu fanya kitu kwenye mazingira tulivu ambayo hayahangaishi umakini wako ili fikra zako ziweze kutulia kwenye kile unachofanya.

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Njia 3 za kuondokana na usumbufu.

    Rafiki yangu mpendwa, usumbufu ndiye adui mkubwa wa umakini. Usumbufu unaoanzia ndani yako unakuzwa usiwe na umakini kwenye kile unachofanya.

    Hapa kuna njia tatu za kuondokana na usumbufu Ili uweze kuwa na umakini mkubwa.

    Moja ni kufanya zoezi la kupumua . Kwa kupumua kwa umakini mkubwa, inasaidia akili yako kutoka kwenye usumbufu. Kuna zoezi la kupumua la 4-7-8 ambapo unavuka pumzika ndani kwa kuhesabu mpaka 4, unashikilia pumzika kwa kuhesabu mpaka 7,kisha unatoa pumzi nje kwa kuhesabu mpaka 8. Unarudia hivyo kwa mzunguko minne. Zoezi hili lina nguvu ya kuipa akili yako utulivu mkubwa.

    Mbili ni kufanya kile kinachokupa wasiwasi. Mara nyingi huwa kuna kitu kinakupa wasiwasi na hivyo kukifikiria kwa muda mrefu. Kitu hicho kinaendelea kuwa usumbufu kwako na kukukosesha umakini.

    Chukua hatua kwenye kile kinachokupa wasiwasi,Ili ukiondoe kwenye fikra zako. Kwa kufanya kitu au kukipangilia kwa namna ambayo inaondoa wasiwasi, inakupa utukuvu mkubwa wa kifikra.

    Tatu ni kujenga muda wa usumbufu. Kuna vitu ni lazima uvifanye, kama kuwasiliana na kujibu jumbe na barua pepe za watu mbalimbali. Badala ya kuruhusu hilo kufanyika kila wakati,tenga muda ambao utafanya hayo.

    Kwa kujua muda fulani ndiyo utahangaika na usumbufu wote, utaweka umakini wako kwenye kile unachofanya na kuepuka usumbufu.

    Kuchukua hatua jijengee umakini mkubwa wa kiakili kwa kuweza kuituliza kwenye kile unachofanya na hilo litakuwezesha kuwa na fokasi ya kuweza kufanya makubwa.

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmial.com.

    http://www.uamshobinafsi.com.

  • Mambo 10 muhimu yanayoweza kubadili maisha yako.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini rafiki yangu kwa kupenda unachofanya. Unahitaji uwe na hamasa kubwa kwenye kile unachofanya na kuipenda kuliko kitu chochote.

    Kubadili unachofanya kwa mfano kama unataka kuanzisha biashara, unapaswa ukae chini na kupanga mkakati wa kupata mtaji wa biashara labda ni kupitia kuweka akiba au kuweka fedha za matumizi binafsi iwapo utaacha kazi.

    Kabla hujafanya maamuzi kubali kwamba mabadiliko yapo na yataendelea kuwepo. Ni muhimu kukubali na kukiri kwamba matokeo yanakuja, hutakuwa na mtu wa kumlaumu pale ambapo mabadiliko yanapokukuta hujajiandaa au hujachukua hatua kwenye maisha yako.

    Unahitajika pia kujifunza sana kuhusiana na unachofanya. Yaani ujifunze sana kuhusiana na kile ambacho unakifanya na kufanyia kazi utalaamu wako,kujua mabadiliko kwenye taaaluma yako.

    Kwenye kufanyia kazi eneo la kazi, kama unafanya biashara una majukumu mengi zaidi. Hapa yapo mambo muhimu yanayoweza kukusaidia kwenye uboreshaji wa kazi , biashara na maisha yako kwa ujumla. Mambo hayo ni kama yafuatayo:

    1. Unatakiwa kujijua wewe mwenyewe, kujua uwezo wako, ni vitu gani kwenye biashara yako ambavyo uko vizuri. Pia kujua ni maeneo gani haupo vizuri sana una madhaifu gani.
    2. Ukishajijua wewe mwenyewe unatakiwa kujua biashara yako vizuri, kuijua nje na ndani ya biashara yako.
    3. Uhitaji wa kuwajua wateja wako vizuri, kujua sifa zote za mteja wako. Kujua umri wake, kipato chake, hadhi yake ya maisha, eneo analoishi na hata mahitaji yake kulingana na biashara unayofanya. Hili litakuwezesha kujua njia za kuongeza wateja zaidi na hata pale ambapo wateja wako wanabadilika.
    4. Kujua nani ni mpinzani wako, anaweza kuwa mpinzani wa moja kwa moja au asiye moja kwa moja.
    5. Fanya kwa ubora wa hali ya juu sana, usiweke mazoea.Kwa kufanya kitu cha ziada, kwa kuongeza ubora na thamani, unahakikisha hufanyi mambo kimazoea, unahakikisha leo hufanyi kama vile ulifanya jana.
    6. Nusa mabadiliko, kuwa mdadisi. Kuwa mdadisi usikubali majibu ya haraka, kutokubaliana na kila kitu kuhoji kila kitu, kujihoji mwenyewe.Kutumia udadisi huu kwenye mambo chanya.
    7. Kuchukua hatua mapema.Hili kunufaika na mabadiliko ni vizuri kuijua
      na pia kuchukua hatua ambayo itakuwezesha kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunufaika na mabadiliko hayo.
    8. Kujua kwamba hakuna atayekuja kukutoa hapo
      ulipo. Ni wewe utajikwamua unapoanguka hupaswi kukata tamaa bali kuamka ma kusonga mbele.
    9. Kushirikiana na wengine. Ili kufaulu kwenye chochote unachofanya ni muhimu kuzingatia uwepo wa watu wengine kwenye biashara na kazi zako. Uwe tayari kuwa bora wewe mwenyewe na hapo utavutia watu bora kwenye kazi zako.
    10. Kubali na kusong
      ambele .Yaanii kubali kuwa wewe na
      jiamini zaidi kwenye kazi zako kuwa unaweza ukafanya kazi zako kwa ufanisi mkubwa.

    Kuchukua hatua, ni wakati sasa wa kufanyia kazi maarifa hayo,baada ya kufahamu ni kitu gani sahihi kwetu ni muhimu kuchukua hatua hili tuweze kufanikiwa zaidi.

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@kemeimaureen

    http://www.uamshobinafsi.com

  • Kwa Nini hupaswi kufuata mkumbo?

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na hivyo tunaathiriwa sana na imani, mtazamo, fikra na tabia za watu wengine wanaotuzunguka.

    Tunapokuwa ndani ya kundi,tunajikuta yale yanayofanywa na walio ndani ya kundi hilo bila hata kufikiri.

    Hivi ndivyo watu wengi hujikuta wakifanya mambo ambayo baadae huyajutia kwa sababu waliyafanya wakiwa ndani ya kundi.

    Mwanafalsafa Seneca aliona hatari hii kwa kuangalia michezo na mashindano yanayohusisha umati mkubwa wa watu.

    Pale watu wanapokuja wakishangilia kwa pamoja,hupoteza kabisa uwezo wa kufikiri. Kama ni mchezo wa watu kupigana, watu wanaweza kushangilia na kusema mmoja amuue mwenzake kabisa.

    Seneca alishauri kabisa ili mtu uweze kupata utulivu wa ndani na furaha, unapaswa kuepuka kuwa kwenye kundi na kufanya mambo kwa kufuata mkumbo.

    Seneca anasema ukishakuwa ndani ya kundi,unasukumwa kufanya yale ambayo wengine wanafanya bila hata kufikiria. Unaona kwa kuwa yanafanywa na kila mtu basi ni sahihi.

    Hiyo ni njia mbovu sana ya kuendesha maisha na chanzo cha kufanya makosa ambayo mtu unakuja kuyajutia sana.

    Kuchukua hatua rafiki imani,fikra na tabia zetu zinaathiriwa sana na wale wanaotuzunguka. Tusipokuwa makini na hao,tutashangaa kwa nini maisha yetu hayaendi vile tunavyotoka sisi.

    Lakini habari njema ni kwamba wapo watu sahihi wanaokufanya ufikirie kwanza kabla hujafanya maamuzi. Jukumu lako utafute watu hao watakusaidia kufanya maamuzi ambayo umefikiria wewe mwenyewe na pia umeona ni sawa kwako.

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

    http://www.uamshobinafsi.com

  • Hofu linalotokana na kupenda kufurahisha wengine.

    Pata picha rafiki yangu unafanya kazi na wenzako ofisini lakini wanapenda sana kushusha. Ukikosea kidogo wanakusema vibaya kwa bosi yako,hivi utajiskiaje kama watakuwa wanakusema vibaya kila mara na unajua kabisa wanasema uongo juu yako.

    Bila shaka utajiskia vibaya tena sana na kutamani kubadilisha kazi au kuacha kazi hiyo. Au labda utatamani kujaribu kuwafurahisha wenzako maana unaamini kwa kuwafanya wengine wafurahi ndio watakupenda zaidi.

    Kabla hujafanya màamuzi ya kubadili ofisi unaofanya kazi najua utajaribu kutumia nguvu na akili zako kuwafanya waache tabia hiyo. Maana tayari unajua kwamba kufanya mema ndio njia ya kupata umakini wa wengine.

    Najua nyuma ya akili yako ungetamani wangeacha tabia zao za kukusema vibaya na kukutafutia makosa hata ambayo hujayafanya. Sina uhakika kama itakufaa, lakini labda wewe ni mtu ambaye hutaki mzozo,unajiambia kama ungeweza kuwafanya wenzako waache tabia hiyo ya kuleta mzozo na vurugu( kila kitu kingekuwa sawa kwa uhakika kabisa).

    Anayependa kufurahisha watu kwa mfano akiona gari likija kwa mwendo wa kasi,anamwondokea au anaendesha gari yake kwa kasi zaidi ili amwondokee,kwa sababu anafikiri mwenzake ana araka zaidi na hataki kumkasirisha kwa kuendesha polepole.

    Wanaofurahisha watu wanaogopa sana kukataliwa au kuachwa,hiyo ndio hofu kubwa ambalo wanaiogopa sana. Akili yao wana mentality ya ” kama sitakufanya ufurahi,basi hutanipenda.”

    Kitu kimoja zaidi kwa wanaopenda kufurahisha wengine ni kwamba wanastawi kwa kusifiwa na kupewa uhakikisho kutoka kwa wengine, na kama hawapokei sifa hizi za kuimarishwa vya kutosha, wanabadili tabia zao na kujaribu wawezalo kuwafanya watu wafurahi .

    Kuchukua hatua, rafiki yangu tabia ya kutaka kufurahisha kila mtu inachosha kwa kweli. Ni vizuri kufuata sauti yako ya ndani na kukataa kufuata watu wanasema juu yako. Maana kwa kusikia sana sauti za nje utaumia mwenyewe kwa kutafuta sababu za kuwafurahisha wengine ilhali wewe unaumia .

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    http://www.uamshobinafsi.com

  • Misingi 6 muhimu ya kujenga uaminifu.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa,lakini kutoka kwenye kitabu cha mwongozo cha how I raised myself from failure to success in selling. Mwandishi anatushirikisha misingi muhimu ya kujenga uaminifu.

    Misingi huo ni kama ifuatavyo:

    1. Ili kuaminika na wengine,kuwa mwaminifu,kipimo sahihi siyo kama watu wataamini,bali ni kama wawe utaamini.
    2. Kujiamini na kuwafanya wengine wakuamini, sheria hii; ijue vizuri biashara yako na endelea kujifunza kuhusu biashara yako.
    3. Moja ya njia ya haraka za kuaminika na wengine ni kutumia sheria ya Benjamin Franklin aliyesema, ” kamwe sitamwongelea mtu mwingine vibaya, nitasema yote mazuri ninayoyajua kuhusu wengine,”
    4. Kamwe usiongezee chumvi kwenye jambo lolote,sema ukweli kama ilivyo.
    5. Njia ya haraka ya kuaminika na wengine ni kutumia mashuhuda.
    6. Mara zote kuwa na mwonekano mzuri.

    Rafiki yangu Ili kuaminika na watu au na wateja wako, unapaswa kuwa na mwonekano mzuri, kuvaa vizuri na kuwa nadhifu. Kabla hujadanganya mteja Ili tu ukamilishe mauzo yako,jua una nafasi moja tu ya kufanya hivyo na baada ya hapo unakuwa umempoteza mteja wako milele.

    Kuchukua hatua, kuwa mwaminifu ni sera bora kabisa kwenye maisha na biashara. Ukiweza kutumia sera hii vizuri utaweza kuongeza kukubalika kwenye jamii na mauzo kuongezeka kwenye biashara yako.

    Akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    http://www.uamshobinafsi.com

  • Kwa nini haifai kuwafurahisha wengine.

    Care about other people think and you will always be their prisoner. LAO TZU.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa,lakini hapo zamani nilikuwa najaribu sana kuwafurahisha wengine. Yaani thamani ya maisha yangu ilienda sambasamba na jinsi watu wanasema nini juu yangu.

    Yaani nilienda hatua ya ziada kabisa kwenye kuweka uwezo wangu katika kujaribu kufurahisha kila mtu,lakini kwa bahati mbaya sana sikufanikiwa kabisa.

    Nilikuwa napata picha kwamba labda kwa kufanya hivyo ningeweza kupata furaha na utulivu kwenye maisha yangu na pia kupata kukubaliwa . Lakini kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni maumivu, na majuto baada ya kuvunjwa moyo .

    Lakini kibaya zaidi ndani yangu nilihisi kukataliwa,kuchoshwa na mbaya zaidi nilipoteza marafiki wengi. Naamini upo kama mimi hupendi kuyarudia makosa kama haya yakutaka kufurahisha watu ambao hawakufikirii au haupo kwenye to do list yao.

    Usiwe na wasiwasi kwenye hilo maana upo njia mbadala wa kusuluhisha jambo hili ambalo limenisaidia mimi mwenyewe. Mbadala wa jambo hilo ni kuzama kwenye ndoto zako na malengo yako.

    Watu wengi hudhani kwamba kuwajali sana wengine kunaleta amani,furaha na utulivu kwenye maisha yao. Lakini wasilolijua ni kwamba kushughulika zaidi na mambo yako ya ndani ndio yanaleta utulivu na amani na furaha kwenye maisha.

    Kuna aina mbili ya watu duniani wale wanaopenda kuwafurahisha wengine na wale wanaopenda kufanyia kazi ndoto zao. Ni wale wanaoepuka sana kufanya mambo yanayosahaulika kirahisi,badala yake wanahangaika na mambo yanayowafanya waache alama ya kudumu humu duniani.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu ikiwa utajaribu kufanyia kazi jambo hili la kukataa kuwafurahisha wengine,basi nakuhakikishia utaweza kupata muda wa kutosha wa kuweka sawa malengo yako na pia kufanyia kazi.

    Lakini habari njema ni kwamba unapoanza tu kukimbiza ndoto zako na kuzipigania hautakuwa na wasiwasi lolote kwani utazifikia kama tu hutaka tamaa kirahisi.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    Mawasiliano:

    kemeimaureen7@kemeimaureen

    http://www.uamshobinafsi.com

  • Matatizo 7 yanayotokana na kufikiria yaliyopita

    Rafiki yangu kama kila mara akili yako inafikiria yaliyopita, hutaweza kujipatia muda nzuri wa kukaa chini na kupangilia maisha yako vizuri. Utakuwa unazurura bila kutimiza jambo lolote lenye tija.

    Tatizo la kwanza ni kutoweza kuishi kwenye wakati uliopo. Huwezi furahia wakati uliopo kama bado akili yako inafikiria yaliyopita. Utapoteza fursa nyingi mpya na pia hutaweza kufurahia mambo mazuri yanayokuzunguka.

    Pili ni kwamba kukaa kwa yaliyopita inakufanya uone ugumu kwenye kujitayarisha kwa yajayo. Huwezi ukafanikiwa kwenye kuweka sawa malengo au kujiweka kwenye hali kufanya mabadiliko ilhali umejikita kwenye yaliyopita.

    Tatu ni kwamba kuishi kwa yaliyopita yanakuzuia kufanya maamuzi sahihi. Ukiwa na mambo ambayo hujaweza kusuluhisha. Mawazo hayo yatakuzuia usifikirie vizuri unapofanya maamuzi, hutaweza kufahamu kilicho sahihi kwako.

    Nne ni kuwa kukaa kwa ya zamani hayatakusaidia kwenye kukamilisha chochote Cha maana. Kufikiria kilekile na kuweka fokasi yako kwenye mambo yaleyale ambazo hutawezi ukayatawala hayatabadili chochote.

    Kwani kuweka mawazo yako kwa yaliyopita yanaweza kukuletea sonona,kuwa hasi, hasira na mengi mabaya yanayotokana na kufikiria ya uko nyuma.

    Tano ni kuhisi kwamba ya zamani yalikuwa yanakupa furaha zaidi kuliko ya sasa. Ni rahisi sana kujiambia kuwa hapo zamani ulikuwa unajiamini sana na hukuwa unaumizwa sana na mambo. Yote hayo yanakufanya ulinganishe ya zamani na sasa na yanaweza kukukatisha tamaa kwa sababu unaona ya zamani yalikuwa heri kuliko ya sasa.

    Sita ni kwamba kufikiria sana yaliyopita sio nzuri kwa afya yako . Yaani yanakuletea usongo wa mawazo ambayo yanachangia kwenye kuongezeka kwa maradhi ya mwili. Haya yanatokana na uchunguzi uliofanywa mwaka wa 2013 katika university ya Ohio. Waligundua kwamba kufikiria sana yaliyopita yanakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa kama ya moyo,saratani na dimensia.

    Kuchukua hatua, hivyo mpendwa kama ambavyo tumejifunza hapa tunapaswa kuepuka sana kwenye kuruhusu mawazo ya zamani yatutatawale.

    Maana hata tukisema tufikirie makosa yetu ya zamani hayatatusaidia kwenye kupanga kesho yetu, yatatukosesha amani na utulivu kwenye maisha yetu ya kila siku.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei,

    mawasiliano:

    https://www.uamshobinafsi.com.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Namna ya kuwa mghairishaji mzuri.

    Kujifunza kuwa mghairishaji mzuri ni rahisi,lakini kutekeleza siyo rahisi. Hapa kuna msingi ya kuzingatia ili kuweza kutekeleza hilo.

    Msingi wa kwanza ni kujilipa mwenyewe. Huu ni msingi muhimu sana kwenye eneo la fedha,kwamba unapopokea fedha,ukianza kujilipa mwenyewe kwa kuweka akiba halafu ndiyo matumizi yakafuata,utakuwa na akiba.

    Lakini ukianza na matumizi kwa kutegemea kinachobaki ndiyo ujilipe,hutabaki na chochote na hutaweza kuweka akiba.

    Kanuni hiyo pia inafanya kwenye eneo la muda. Kama unatumia muda wako kwa yale yanayokuja mbele yako ukijiambia baada ya kukamilisha hayo utapata muda wa kufanya yaliyo muhimu unajidanganya,haitakuwa kutokea umalizie kila kitu na ubaki na muda.

    Badala yake unapaswa kujitengea muda wako kwanza,wa kufanya yale muhimu zaidi kwako, bila kujali una mengine mengi kiasi gani ya kufanya.

    Hapa unatenga saa moja mpaka mawili kila siku kwa ajili yako mwenyewe ambayo unatumia muda huo kwa yale muhimu zaidi kwako.

    Haijalishi nini kinaendelea kwenye maisha yako,huachi kutenga muda huo muhimu kwa ajili yako. Kwa kufanya hivi,moja kwa moja yale yasiyo muhimu sana yatakosa muda kwenye maisha yako na hapo unakuwa mghairishaji mzuri.

    Msingi wa pili ni kuweka ukomo kwenye mambo unayofanyia kazi kwa wakati mmoja. Wengi huwa wana mambo mengi wanayofanyia kazi kwa wakati mmoja,wakiona hiyo ni njia nzuri ya kukamilisha mambo mengi kwa wakati mmoja .

    Lakini kinachotokea ni wanashindwa kukamilisha chochote kikubwa kwenye maisha yao. Kama kila wakati unakubali kupokea na kuanzisha kitu kipya unaishia kuzitawanya sana nguvu zako na hakuna kikubwa utakachoweza kukikamilisha.

    Unapaswa kuchagua kufanyia kazi mambo makubwa machache kwa wakati mmoja,yasizidi mambo matatu . Yaani katika wakati wowote wa maisha yako,unapaswa kuwa na mambo makubwa yasiyozidi matatu unayofanyia kazi.

    Msingi wa tatu ni kuheshimu vipaumbele vyako na kuachana kabisa na yale ambayo siyo kipaumbele kwako. Ukishajiwekea vipaumbele,kuna mambo yatakuwa kwako ambayo unaweza kuyaona ni mazuri na yanayofaa.

    Lakini kama hayajaingia kwenye vipaumbele vyako,jua huo ni mtego wa kukuondoa kwenye vipaumbele. Yakatae kabisa mambo yote mazuri unayoshawishika kufanya kama hayapo kwenye vipaumbele vyako.

    Kusema hapana ni hitaji muhimu sana hapa. Na ugumu wa kusema hapana unakuja pale ambapo unachopaswa kukisemea hapana na kitu unachopenda kufanya .

    Kuchukua hatua, rafiki yangu tunapaswa kuelewa kwamba kama tunataka kufanya makubwa, hatuna budi kusema hapana kwenye mambo mazuri tunayovutiwa kuyafanya ila hayapo kwenye vipaumbele vyako.

    Akupendaye sana.

    Mwandishi Maureen Kemei,

    Mawasiliano:

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com

  • Mambo 2 muhumu ya kuzingatia Ili kujijengea msimamo.

    Baada ya kutambua na kujua umuhimu wa kijitambua sisi wenyewe kama binadamu, tunapaswa pia kuzingatia msimamo wetu kwenye maisha .

    Kwani kitu kikubwa kinachowazuia watu kuishi maisha halisi kwao ni kukosa msimamo. Wengi huwa wanabadilika badilika kila mara, kiasi kwamba hawawezi kuaminiwa au kutegemewa kwenye kitu chochote.

    Wengi ni watu wa kubadili mawazo yao haraka na ndani ya muda mfupi. Wakati huu wanaamua hiki,ila baada ya muda mfupi wanaamua kingine ambacho ni tofauti kabisa na kile cha awali. Kwa kubadilika badilika huko,watu wanashindwa kuwa halisi na hata kutokuaminika.

    Wastoa wanashauri mambo mawili muhimu ya kuzingatia Ili kujijengea msimamo:

    Jambo la kwanza ni kuwa na maisha ya aina moja,hadharani na faraghani. Watu wengi huwa na maisha ya aina mbili,mbele ya watu wanajionyesha ni watu wa aina fulani, ila wakiwa sirini wanakuwa ni watu wa aina tofauti.

    Wewe chagua kuwa mtu wa aina moja,mwenye maisha ya aina moja, hadharani na sirini . Kusiwe na chochote unachokificha kwenye maisha yako. Ukishakuwa na maisha ya aina mbili, huwezi kuishi kwa uhalisia wako na unakosa msimamo wa ndani.

    Jambo la pili ni kuchagua aina ya mtu unayetaka kuwa na kuwa huyo mara zote. Ukishachagua unakuwa mtu wa aina gani,basi kuwa hivyo bila kubadilika.

    Haimaanishi hubadili unayofanya kulingana na mabadiliko yanayotokea, bali inamaanisha kuwa mtu wa aina moja mara zote .

    Kuchukua hatua; rafiki yangu maisha yasiyo na msimamo ni maisha yasiyoeleweka . Chukua hatua ya kujijengea msimamo kwenye maisha yako kwa kuamua unakuwa mtu wa aina gani na kisha kuchagua kuwa na maisha ya aina moja .

    Akupendaye sana.

    Mwandishi Maureen Kemei,

    Mawasiliano:

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinasfi.com.