Home

  • Umuhimu wa kujua kusudi la maisha yako.

    Rafiki yangu mpendwa,hatua muhimu katika kujitambua kwenye kuelekea katika ubobezi wako ni kujua kusudi la maisha yako.

    Wanasema kusudi lakini siyo moja,unaweza kuwa na makusudi mengi na tofauti katika vipindi mbalimbali vya maisha yako.

    Kwa kuanzia na kipindi cha maisha yako,jua kusudi lako kwa sasa. Hapo ndipo pa kuanzia ili uweze kupambana kufikia ubobezi na mafanikio makubwa.

    Katika kujua kusudi lako,jiulize maswali haya manne muhimu.

    1. Kama ungekuwa na uhuru wa kuipangilia siku yako nzima unavyotaka wewe,ni vitu gani ungefanya kwenye siku yako nzima? Swali hili linakuwezesha kujua vitu unavyovipa vipaumbele kikubwa kwenye maisha yako.

    2. Ni vitu gani unapenda kufuatilia sana? Kwenye simu yako ni picha gani zipo kwa wingi zaidi? Swali hili linakuwezesha kujua vitu unavyopenda zaidi kufuatilia na kufanya.

    3. Ni vitu gani ukifanya unajiskia furaha na mwenye nguvu zaidi? Vitu gani huchoki kuvifanya ? Angalia kwenye mwezi uliopita na orodhesha vyote ulivyofanya kisha jua vipi vilikupa furaha na nguvu zaidi. Swali hili linakuwezesha kujua vitu ambavyo unafanya kutoka ndani ya nafsi yako kweli na siyo unafanya kwa sababu unalazimishwa kufanya.

    4. Ni vitu gani ulipendelea sana kufanya ulipokuwa na miaka 12 mpaka 15 ? Na je tangu umekua mapenzi yako kwenye vitu hivyo yameendaje? Swali hili linakuwezesha kujua vitu unavyopenda kufanya kutoka ndani ya nafsi yako na siyo kwa kulazimishwa au kwa sababu unalipwa. Katika umri wa miaka 12 mpaka 15 mtu anakuwa anapambana kuwa huru na hapo hupenda vitu ambavyo ni vya tofauti kabisa na wengine . Katika umri huo mtu anakuwa halisi zaidi kwake. Zaidi ya umri huo jamii inaanzia kumharibu mtu na kumwambia nini anapaswa kufanya na nini hapaswi .

    Maswali hayo manne yatakupa mwanga mkubwa wa nini kusudi lako.

    Majibu utakayoyapata yanaweza kuwa yanakupa hofu kwa sababu ni vitu ambavyo jamii imekuwa inakukataza usifanye.

    Na unapoona kitu kinatoka ndani yako lakini unakuwa na hofu kubwa kukifanya ,basi jua hicho ndiyo sahihi kwako.

    Rafiki yangu baada ya kujua kusudi lako kupitia maswali hayo, kuna hatua muhimu za kuchukua.

    1. Ipangilie siku yako kwa namna ambayo utafanya zaidi vile unavyovipenda kufanya na siyo tu vile unavyolazimika kufanya.

    2. Tafuta jumuiya ya watu wanaofanya kile unachopenda kufanya na jiunge nao, unapofanya na wengine unakuwa na msukumo mkubwa . Pia tafuta menta wa kukufundisha na kukuongoza Ili uweze kufikia ubobezi kwenye eneo hilo.

    3. Soma sana kuhusu eneo hilo ulilochagua . Soma historia la eneo hilo kwa undani kabisa. Soma wasifu wa wale waliofanikiwa sana kwenye eneo hilo. Soma maendeleo na vitu vipya vinavyogunduliwa kwenye eneo hilo. Kwa kifupi unapaswa kujua kila kitu kuhusu eneo ulilochagua. Kwa kuwa ni kitu unachopenda na ulichochagua mwenyewe, kujifunza hakutakuwa kugumu kwako.

    4. Changanya makusudi uliyonayo pamoja. Kama unapenda kitu zaidi ya kimoja,angalia jinsi unavyoweza kuviunganisha pamoja Ili uzalishe kitu cha kipekee sana. Hii ndiyo Siri kubwa ya wale walioweza kuja na vitu vipya na vya kipekee na kufanikiwa sana. Walileta pamoja vitu vyote walivyopenda kufanya kisha wakazalisha kitu cha tofauti.

    5. Chukua hatua. Kila siku chukua hatua katika kufanya yale yaliyo kwenye kusudi lako . Kila siku kuwa bora kwa asilimia 1 zaidi katika ufanyaji. Na kila mara fanya majaribio mbalimbali Ili uweze kuwa bora kwenye kile unachofanya.

    Kwa kuchukua hatua hizi tano, utaweza kuanza kuishi kusudi la maisha yako. Lakini bado watu hawatakuacha kirahisi,bado utakutana na vikwazo na changamoto. Hivyo unapaswa kuwa imara sana.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Je, unajua kuwa hofu siyo kwenye kifo, bali ipo kwenye kuishi?

    Karibu rafiki,watu huwa wanasema kitu kikubwa ambacho watu huwa wanakihofia ni kifo,bali hilo siyo kweli.

    Kitu kikubwa ambacho kila mtu huwa anakihofia ni kuishi maisha yake kwa uhalisia wake. Kwani wengi hawana uthubutu wa kuchagua kuyaishi maisha yao kwa namna wanavyochagua wao,hivyo wanalazimika kujificha kwenye utumwa wa jamii.

    Tumefundishwa kuyaishi maisha yetu Ili kuwaridhisha wengine, wakubaliane na sisi na kutuona ni watu wazuri,hata kama inabidi tuigize maisha hayo.

    Tumezoea kuishi kama wengine wanavyotaka tuishi Ili wakubaliane na sisi. Kuchagua kuwa wewe na kuyaishi maisha yako kwa namna unavyochagua mwenyewe ni kitu ambacho watu wanakihofia zaidi kuliko hata kifo. Wengi wapo tayari wafe kuliko kuchagua kuyaishi maisha yao.

    Maisha ambayo wengi wanaishi,siyo maisha halisi kwao, bali ni maisha ambayo wengine wanawategemea wawe hivyo. Dini ambazo wengi wanazo, kazi wanazofanya na maisha wanayoishi, bali kwa sababu ndiyo jamii inawategemea wawe . Kwa njia hiyo,wengi wanaishi maisha yasiyo yao,maisha ya utumwa .

    Kwa kuwa maisha ambayo watu wanaishi siyo yao,wanaacha kujiheshimu na kujiamini. Wanajiona ni watu ambao hawajakamilika na hivyo kuzidi kutafuta njia za kuwafurahisha wengine ,hapo wanazidi kuwa watumwa zaidi kwenye jamii.

    Watu wamekuwa wakijidharau wao wenyewe ili kuwafurahisha wengine . Wamekuwa wanaumiza miili yao Ili tu kuwafurahisha na kubalika na wengine . Hata watu wazima kuna mambo wanayafanya ambayo hayana manufaa kwao na tena yanawaumiza ,lakini wanataka wakubalike na wengine.

    Watu wanajiumiza na kutokujikubali kwa sababu hawana uthubutu wa kuyaishi maisha yao. Wanajiadhibu na kuruhusu wengine wawaadhibu ili tu wakubalike ndani ya jamii. Hili limewafanya wengine kuendelea kubaki kwenye utumwa.

    Chukua hatua; rafiki yangu Ili tuweze kuishi maisha halisi, yatupasa tuondokane na hali ya kufuata mkumbo . Tunapaswa tujiamini Ili tuweze kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yetu kwenye kufanya makubwa. Na tukifanya hivyo tutakuwa tumeondoka na hofu ya kuishi, Asante sana.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi ya kutokuumizwa na wengine.

    Sisi binadamu huwa tunapenda kuumizana wenyewe,tumeshazoea kuumizwa kiasi kwamba tunawapa watu nafasi mbalimbali za kutuumiza.

    Na tunafanya hivyo kwa kuchukuliwa Kila kitu binafsi,kila ambacho mtu anafikiri au kufanya ,tunaona anatulenga sisi,hata kama haina uhusiano na sisi wenyewe.

    Njia kuu ambayo watu wamekuwa wanaumizana ni kupitia uongo ,kila unapoenda,kuna watu watakudanganya kwa namna moja au nyingine . Unapokuja kujua ukweli unaumia, kwa sababu unaona walitumia uongo kujinufaisha kwa namna moja kupitia wewe.

    Kama unataka kuondokana na maumivu yanayotokana na uongo,tambua kwamba,watu huwa wanadanganya,na hawadanganyi kwa sababu yako,bali kwa sababu zao binafsi.

    Usitegemee watu wakuambie wewe ukweli kwa sababu wanajidanganya hata wao wenyewe. Mtu anapokudanganya ,jua tayari amejidanganya yeye mwenyewe. Kwa kujua hili huumii bali unamwonea huruma.

    Unapochagua kuwaona watu kama walivyo,bila ya kujichukulia wewe binafsi , huwezi kuumizwa na chochote wanachofikiri,kusema au kufanya. Kwa sababu unajua hawafanyi kwa sababu yao au kwa sababu zao binafsi.

    Unachohitaji ili usiumizwe na yeyote yule kwenye maisha ni kujiamini na kujikubali wewe mwenyewe na kisha kuwaona watu kama walivyo na siyo kama unavyotaka uwaone .

    Kwa kujua hayo ,utaona jinsi ambavyo kile wengine wanafanya siyo kwa ajili yako,bali kwa ajili yao wenyewe ,hutaumia tena,bali utawaonea huruma.

    Kuchukua hatua; unapojijengea tabia ya kuchukulia chochote binafsi unaondokana na changamoto nyingi kwenye maisha. Kama hasira,wivu,huzuni na chuki vyote vinapotea kabisa unapoacha kuchukulia vitu kwa ubinafsi.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    Mwasiliano.

    kemeimaureen32@gmail.com.

    http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

  • Jinsi ya kuyakabili mabadiliko.

    Karibu sana rafiki yangu mpendwa, mabadiliko ni sehemu ya maisha ya kila siku. Ni kanuni ya asili kwa vitu kubadilika, hakuna kinachobaki kama kilivyokuwa, mabadiliko ndiyo mwendo wa asili.

    Lakini sisi binadamu tumekuwa hatupendi hilo ,tumekuwa tunataka mambo yabaki,kama tulivyozoea,kwa sababu mabadiliko yanakuja na vitu vipya.

    Maendeleo yako na hata mafanikio yako yanatokana na kufanya mambo ambayo ni magumu. Kwani mambo rahisi kufanya hayana thamani kubwa kwenye maisha.

    Mabadiliko ya kweli kwenye maisha huwa yanatokea kipindi ambacho mtu anapitia magumu kwenye maisha yake.

    Chukua hatua,rafiki yangu usiyakimbie magumu unayokutana nayo kwenye maisha ,bali yatumie kama njia ya wewe kuwa bora zaidi na kuzalisha matokeo makubwa .

    Rafiki unapaswa kutengeneza utulivu mkubwa wa ndani kiasi kwamba chochote kinachotokea nje hakiwezi kukuvuruga.

    Tambu kwamba Ili maisha mapya yazaliwe,lazima maisha ya zamani yafe. Mabadiliko ndiyo njia pekee ya kuweza kufanya makubwa kwenye maisha.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen32@gmail.com.

  • Jinsi Alex Banayan alivyoshinda bahati nasibu.

    Alex mbaye ni mwandishi wa kitabu cha the third door (kitabu kinachoelezea jinsi watu waliofanikiwa sana walivyoanza safari zao za mafanikio)

    Alex alichagua kuwafuatilia watu waliofanikiwa sana kwenye yale wanaliyofanya kwa lengo la kujua kule walikoanzia. Hilo hakukuwa rahisi lilihitaji uvumilivu na unganganizi wa hali ya juu. Kitu ambacho kilimsaidia kukutana na wengi.

    Katika harakati zake za kutafuta waliofanikiwa na kuwahoji , aligundua alihitajika kutumia fedha nyingi kwenye usafiri,Ili kuwatafuta watu hao waliofanikiwa na kuwahoji.

    Ndipo alipoona tangazo hilo la bahati nasibu ,likichezeshwa kwenye tv na mshindi kupata zawadi nono. Aliona hiyo ndiyo nafasi yake ya pekee kupata fedha ya kutimiza ndoto yake.

    Lakini kulikuwa na kikwazo,hajawahi kuangalia mchezo huo na hivyo hajui kunafanyikaje. Alikesha usiku mzima akisoma mtandaoni mbinu za kumwezesha kuwa mmoja kati ya wachache wanaochaguliwa kushiriki.

    Akajifunza kwamba wanaochaguliwa ni wale ambao wanaonekana wa tofauti na wa ajabu. Siku ya kwenda kushiriki akajiweka kwa namna ya tofauti Ili kuongeza nafasi yake ya kuchaguliwa.

    Hilo likafanya kazi ,akachaguliwa kuwa kati ya watano walioshiriki. Baada ya kuingia kwenye ukumbi akaona sasa anahitaji kujifunza mbinu za kushinda mchezo huo. Wakati anatafuta mtandao, simu za washiriki wote zikachukuliwa.

    Aliona hana tena namna ya kushinda, lakini akaamua kumwuliza kila aliyekutana naye amshauri afanye nini ili ashinde zawadi. Ushauri mkubwa aliopewa ni mara zote atoe dau dogo kuliko thamani halisi ya kitu husika. Alifanyia kazi ushauri huo na kweli akaweza kuvuka hatua za awali,ambazo hazikuwa ngumu.

    Ugumu ulikuja kwenye hatua ya fainali,alijikuta akishindwa kabisa kukadiria bei na hapo akalazimika kusikiliza mashabiki waliokuwa wanafuatilia.

    Hilo pia likamwezesha kuwa mashindi namba moja wa bahati nasibu hiyo . Alipewa zawadi ya boti la kifahari lenye kila aina ya starehe ambazo mtu anahitaji wakati wa safari na mapumziko.

    Kile tunaondoka nacho hapa na kwenda kuifanyia kazi ni kuwa na nia ya kutaka kufanya kitu kwa ufanisi mkubwa. Kama ambavyo tumeona Alex alivyoona bahati hilo kwenye TV akawa na nia ya kutaka kushiriki na tena afanye kwa ufanisi mkubwa.

    Tunaona pia nguvu ya unganganizi,Alex ameng’ang’ania zawadi hilo na mwishowe ikawa yake. Pia kutokata tamaa na kuwa wazi yaani kuuliza kile ambacho hukijui na watu wako tayari kukupa unachotaka.

    Hatua ya kuchukua,rafiki yangu kwenye maisha tunapaswa kuwa na nia ya kufanya kitu kwa ufanisi mkubwa. Tunapaswa pia tuwe wanganganizi,wavumilivu na watu waliowazi kuuliza kile ambacho hatukijui. Maana hasili yupo tayari kutupa kile tunachohitaji ikiwa tu tutatafuta na kuuliza.

    Mwandishi wako.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Njia 9 za kutumia Ili kuwashinda wakatishaji tamaa.

    Kwa kuchagua kufanya makubwa ili ufanikiwe,
    Kwa kuchagua kuendelea kujifunza na kujaribu vitu vipya,
    Utazalisha matokeo ya tofauti, matokeo ambayo hayajazoeleka.
    Hilo litaleta kwako kundi kubwa la watu ambao watakukosoa na kukukatisha tamaa.
    Kundi hilo litaonekana kuwa na nguvu na kuwa sahihi kwa namna watakavyokudhalilisha.
    Lazima uwe imara sana katika kukabili kundi hili, la sivyo hutaweza kufika mbali, utakata tamaa na kuishia njiani.

    Kwa kugundua ukubwa wa tatizo hili, Robin anatushirikisha njia tisa za kuwashinda wakatishaji tamaa. Kwa kuzijua njia hizi tisa na kuzifanyia kazi, hakuna atakayeweza kukukatisha tamaa. Na hata pale mtu anapokuja kwako kukukatisha tamaa, unanufaika zaidi na ukatishaji wake tamaa kuliko kuumia.
    Njia hizo tisa ni kama ifuatavyo;

    1. Wakatishaji tamaa ni walimu wako wazuri.
      Wanakuonyesha ni maeneo gani una madhaifu au wapi hujiamini.
      Pale mtu anapojaribu kukukatisha tamaa na hilo likakuingia, ni kiashiria kwamba kuna kitu hakipo sawa kwa upande wako.
      Hivyo tumia hilo kutambua wapi una udhaifu na uhakikishe unakuwa imara sana ili yeyote asiweze kukutikisa.
      Kama ni kuboresha zaidi kile unachofanya au kujiamini zaidi, fanya kile kinachohitajika ili wakatishaji tamaa wasiwe na nguvu kwako.
    2. Wanaoumiza wana maumivu.
      Watu wenye maumivu huwa wanahakikisha wanawaumiza na wengine pia.
      Watu waliokata tamaa huwa wanahakikisha wanawakatisha na wengine tamaa pia.
      Hivyo unapoona watu wanakukatisha tamaa, jua tatizo kubwa siyo wewe bali ni wao wenyewe.
      Wanajaribu kutoa kile ambacho tayari kipo ndani yao.
      Hivyo badala ya kuumia, hebu waonee huruma. Maisha yao yameshawaadhibu kiasi kwamba furaha pekee kwao ni kuwaumiza wengine kama wao walivyoumia.
    3. Mwanga hukaribisha kumbikumbi.
      Ukiwasha mwanga kwenye eneo lenye giza, utaleta nuru, lakini pia jua utakaribisha kumbukumbi kuja kwenye mwanga huo.
      Huwezi kuzima mwanga kwa sababu ya kumbukumbi wengi ambao wamekuja. Bado hawawezi kuzuia nuru ya mwanga.
      Kadhalika kwenye kile unachofanya, unapozalisha matokeo bora, utawanufaisha wengi, lakini pia kuna wachache watakaokuja kama wasumbufu.
      Usiache kutoa thamani yako kwa sababu ya hao wachache, achana nao.
    4. Watu walio juu huwa hawahangaiki kuwaangusha wengine.
      Ni watu walio chini ndiyo huwa wanatumia muda na nguvu zao kuwavuta wengine warudi chini.
      Watu waliojuu kwanza hawana hata muda wa kuhangaika na nini wengine wanafanya, wametingwa sana na kile wanachofanya.
      Lakini hata wakiwa na muda huo, wanawasaidia wengine kupanda juu kama wao na siyo kuwashusha chini.
      Ukiona mtu anakukatisha tamaa, jua hakuna kikubwa kinachoendelea kwenye maisha yake, hana kinachomweka bize kupambania ndiyo maana anapata muda wa kuhangaika na mambo yako.
      Je kweli unataka uachane na ndoto zako kubwa kwa sababu ya watu ambao hawana ndoto zozote? Hilo siyo sahihi.
    5. Wenye chuki wamezika ndoto zao kubwa.
      Sifa nyingine ya wakosoaji na wakatishaji tamaa ni hii, wangependa sana kufanya makubwa kama wewe, lakini hawawezi, hivyo wanakuchukia kwa sababu wewe umeweza kile ambacho wao wameshindwa.
      Wenye chuki kwenye ndoto zako kubwa unazofanyia kazi ni wale ambao wamezika ndoto zao kubwa.
      Wangetamani sana na wao wawe kama wewe ila hawawezi, kwa sababu walishakatishwa tamaa na kukubali.
      Hivyo kikubwa wanachoweza ni kukatisha wengine tamaa, usiwasikilize.
    6. Kazi yenye nguvu hugusa pande mbili kubwa.
      Pale unapofanya kazi yoyote yenye nguvu, inayoleta mapinduzi makubwa, utagusa pande kuu mbili.
      Upande wa kwanza ni wale watakaokupenda sana kwa sababu umekuwa mkombozi wao kupitia kazi yako.
      Na upande wa pili ni wale watakaokuchukia sana kwa sababu umevuruga mazoea waliyokuwa nayo.
      Ili upendwe na baadhi, lazima pia uchukiwe na baadhi ya watu.
      Kama unataka usichukiwe na mtu yeyote, jua pia hutaweza kupendwa na yeyote.
      Kama hakuna anayekuchukia maana yake hakuna kazi kubwa na ya kimapinduzi unayofanya, unafanya vitu vya kawaida tu na ambavyo vimezoeleka
    7. Kuelewa kazi ya tofauti lazima mtu awe na jicho la tofauti.Watu wengi hupinga vitu vipya siyo kwa sababu havifai, ila kwa sababu hawavielewi.Ndiyo maana kila aina mpya ya ugunduzi huwa inakutana na upinzani mkali mwanzoni. Unakuwa ni ugunduzi wenye manufaa kabisa, ila kwa sababu watu hawaelewi, wanapinga.Inawachukua muda watu mpaka waje kuelewa ndiyo waone manufaa ya kitu.Hivyo unapofanya kitu kipya na kuleta matokeo ya tofauti na ukapingwa sana, jua siyo kwa sababu hakifai, ila kwa sababu watu hawajakielewa.Usiache kufanya kitu bora kwa sababu watu hawajaelewa, wewe endelea kufanya na siku moja watakuja kuelewa.
    8. Kukosolewa ni dalili ya ushawishi.Kama wanavyosema, mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe.Kukosolewa na kukatishwa tamaa ni dalili kwamba umekuwa na ushawishi mkubwa, unafanya mambo makubwa.Hakuna mtu anayehangaika na mtu asiye na ushawishi mkubwa.Hivyo tumia kipimo cha wakosoaji na wakatishaji tamaa kujua kwamba ushawishi wako umekuwa mkubwa.
    9. Kazi mpya zinatikisa mazoea.Kuna mazoea ambayo yameshajengeka kwenye kila eneo, na hayo ndiyo yanachukuliwa kama ukweli na kiwango ambacho kila mtu anapimwa nacho.Ukifanya kwa mazoea hayo unazalisha matokeo ya kawaida na utapendwa na wale waliozoea hivyo.Ukifanya kwa namna mpya na ya tofauti utazalisha matokeo ya kipekee, lakini pia utatikisa mazoea yaliyopo.Wale waliozoea mazoea hayo hawatakuacha salama, watakupinga na kukukatisha tamaa kwamba unakwenda kinyume na utaratibu.Lakini hupaswi kuwasikiliza, kwa sababu mapinduzi huwa hayaletwi kwa kukumbatia kilichopo.Tumia njia hizi tisa kuhakikisha unasimama imara kabisa kwenye kile ambacho umechagua kufanya na hakuna yeyote anayeweza kukuyumbisha au kukukatisha tamaa.
    10. La mwisho rafiki yangu ni kwamba zama tunazoishi sasa zina wakatishaji tamaa wengi, usipokuwa imara, hutafika kwenye mafanikio unayoyataka.

    Naamini upo kama mimi unapenda uendelee mbele zaidi na kuhakikisha unavuka vikwazo zote zinazoletwa na wakatishaji tamaa wengi ambao wanatuzunguka . Inakutegemea ni sauti gani usikilize sauti ya nje ya hao wakatishaji tamaa,au yako wewe mwenyewe unaokumbia ‘endelea mbele.’

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@kemeimaureen

    http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

  • Namna ya kufanya mazoezi ya kuchukua hatua hatarishi.

    Namna ya kuchukua viwango vya hatua hatarishi ni jambo muhimu na la kipekee sana kwako rafiki yangu.

    Unapoamua kuongea mbele ya kundi la watu ni jambo la hatari kwa wengine,huku kwa wengine likiwa ni jambo rahisi sana.

    Rafiki yangu unapaswa ujiulize maswali kama yafuatavyo Ili ikusaidie unapokokotoa viwango vya hatari kwenye maisha yako.

    Je kuna uwezekano wowote wa kuingia kwenye gharama? Wakati mwingine kuna gharama unayoingia kama fedha unazowekeza ,lakini saa zingine,lakini gharama kwenye zisizowezekana ambazo inahusiana na hatari,kama hatari ya kukataliwa.

    Je uwezekano wa faida. Zingatia uwezekano wa matokeo chanya kwenye kuchukua hatua hatarishi. Ona kile kitatokea ikiwa hatari hiyo itakuwa wa faida. Utaonaje ukipata faida ya kifedha? Ukiwa kwenye mahusiano mazuri? Afya njema? Kuna mahitaji yako mwenyewe yatakulipa zaidi kuliko za gharama.

    Itanisaidia aje kufikia malengo yangu? Ni muhimu kuchagua malengo yako makubwa na jinsi hatari hiyo inavyoweza kuleta matokeo ya aina gani kwenye malengo yako. Kwa mfano,kama unatarajia kupata fedha nyingi ona jinsi ya kufungua biashara yako mwenyewe itakayosaidia lengo lako unapokokotoa hatari hiyo.

    Je kuna mbadala? Mara zote tunaona hatari tuna machaguo mawili tu yakuchukua hatari ama uachane nayo . Lakini mara nyingi,kuna aina tofauti za fursa zitakazokusaidia kufikia malengo yako. Ni muhimu kugundua mbadala hizo zinazoweza lalia katikati,ndio uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

    Je itakuwa salama kama mazingira ya hatari itakuwa nzuri. Tumia wakati mwingi ukifikiria kuhusu malipo kwa hali hatarishi na jinsi malipo hayo yanavyoathiri maisha yetu. Jaribu kukuwa na matarajio halisi kwenye mazingira na jinsi inavyokufaidi.

    Ni kitu gani kibaya kinachoweza kufanyika na jinsi ya kupunguza hatari hiyo isitokee.Ni jambo la muhimu kukokotoa hatua hatarishi kwenye mazingira na ufikirie kuhusu hatua utakazochukua kupunguza hatari. Kwa mfano unafikiria kuanzisha biashara,utaongezaje uwezekano wa mafanikio?

    Ni kitu gani kibaya sana kinachoweza kutokea kwenye mazingira hatarishi? Kama vile kwa hospitali ,serikali wanayo njia ya kujiokoa kutoka kwenye hatari,itakuwa jambo la maana sana unapotengeneza mpango utakayotumia kama hali mbaya kabisa itatokea.

    Uamuzi huu utakuwa wa umuhimu wa miaka mitano ijayo? Itakusaidia kuweka mpango vizuri,unajiuliza hatari hii itaathiri aje maisha yako ya baadaye! Kama ni hatari ndogo,hutakumbuka hata miaka mitano ijayo kuanzia sasa kama ni hatari kubwa itaathiri sana maisha yako yajayo.

    Itakuwa muhimu sana kuandika majibu yako ili usome mara kwa mara . Jisukume kufanya uchunguzi Ili upate habari za kutosha kama hujui sana kuhusu hatari hiyo. Kwa kufanya hivyo, itakusaidia kukokotoa hatari hiyo vizuri. Kama hauna habari ya kutosha,tatua kwa kufanya maamuzi sahihi uwezavyo na habari unazopata.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi ya kujitenganisha na dunia.

    Tunaishi kwenye dunia ya sasa ambayo tuna muunganiko wa masaa 24 kwa siku 7 za wiki,Ili kuweza kufanya makubwa unahitaji muda wa kujitenganisha.

    Watu wote ambao wameweza kufanya makubwa kwenye maisha yao ;waliweza kuwa na muda ambayo walijitenganisha kabisa.

    Katika muda huo hawakuwa na internet, Tv ,simu, redio au watu. Walitenga muda wa kuwa peke yao bila ya usumbufu wowote ule kwa muda mrefu.

    Na hapo ndipo waliweza kuweka umakini wao kwenye kitu na kuweza kuziona fursa za kipekee ambazo wengine hawazioni.

    Ukimya na utulivu ni hitaji kubwa na muhimu sana kwako Ili kuweza kufanya makubwa.

    Na katika kipindi hicho ndiyo unaweza kujifunza kwa kina na pia kuzalisha kwa viwango vya juu kabisa.

    Ukweli ni kwamba kila mtu anakazana kupata muda au umakini wako ili kukunasa kwenye mambo yake.

    Kila biashara inakutaka uwe mlaji wa kile ambacho inauza na siyo tu mlaji,bali ujenge uraibu wa kukigemea.

    Kila mtandao wa kijamii na huduma na bidhaa nyingine za kidijitali zinakazana kunasa umakini wako ili uzitumie muda wote.

    Huwezi kufanya makubwa kwenye maisha yako kama muda wako umenaswa kwenye vitu mbalimbali.

    Unahitaji kipindi ambacho unajinasua kwa kujitengenisha. Unapaswa kutenga muda ambao hakuna kelele au usumbufu wa aina yoyote unaweza kukufikia.

    Katika kipindi hicho ni wewe tu na kazi yako, hakuna kingine. Zima simu yako, usiwe kwenye mtandao na mtu yeyote anayeweza kukufikia.

    Hiyo ndiyo njia ya kuweza kujitenga. katika zama hizi. Ukiweza kupata siku kadhaa za kufanya hivyo kila mwezi au kila mwaka , itakuwa vyema kama haliwezekani basi pata siku moja ya kufanya hivyo kila siku kwa wiki.

    Na kama huwezi kupata siku nzima kwenye wiki,basi chagua masaa ya kufanya hivyo kwa lwa wiki au kwa siku.

    Na haijalishi unafanya kozi ya aina gani au unategemewa kiasi gani . Kama ni lazima uwe unapatikana kwa masaa yote 24 ya siku na siku 7za wiki,hutaweza kufanya makubwa.

    Huwezi kufanya makubwa kama muda wote umeunganishwa na kukutana na usumbufu ambao wengine nao wanakutana nao pia.

    Kuchukua hatua,panga muda wa kujitenganisha wewe mwenyewe Ili uweze kufanya mambo makubwa zaidi.

    Mwandishi akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

  • Tatizo kuu la kisasi cha Sasa.

    Kwenye jamii ya kisasa, ubinafsi ni tatizo mkubwa sana,kila mtu anapambana na mambo yake kwa namna yake mwenyewe.

    Jamii ya asili walikuwa na ushirikiano mkubwa kuliko jamii ya kisasa.

    Hali hii ya ubinafsi imepelekea matabaka kujengeka baina ya watu kwenye jamii .

    Tabaka kati ya masikini na tajiri ni kubwa na linazidi kuwa kubwa .

    Hali hii inatengeneza upweke ambao umechochea msongo wa mawazo na magonjwa ya akili .

    Watu wengi hawana furaha wala utulivu wa akili na mwili licha ya maendeleo makubwa ambayo yametokeo na yanayoendelea kutokea .

    Tangu enzi na enzi , ushirikiano mkubwa ulikuwa kwenye vitu viwili,chakula na usalama.

    Watu walikuwa tayari kushirikiana kwenye kugawa vyakula Ili kuhakikisha wote wanakuwa na afya njema.

    Kila mmoja alishiriki katika kuhakikisha makazi yao ni salama kwa wote.

    Sasa maendeleo ambayo yametokeo yameondoa hatari hizo mbili na hivyo mtu anaweza kujitegemea kuanzia chakula hadi usalama.

    Hilo limejenga ubinafsi mkubwa ambalo linaendelea kuwa na madhara kwa jamii ,kwa ujumla.

    Vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma ni matokeo ya ubinafsi ambao umejengeka kwenye jamii.

    Mtu anajiangalia yeye mwenyewe tu na haangalii wengine.

    Hatua ya kuchukua,tunahitaji kujenga upya jamii zetu kwa namna ambayo ushirikiano na uwajibikaji unakuwa mkubwa.

    Jamii zinapaswa kujengwa kwa kuanzia ngazi ndogo ndogo ambapo watu wanajuana mmoja mmoja.

    Kujuana kunaongeza ushirikiano na kutegemeana kunaleta uwajibikaji kwa sababu kila mtu anategemewa kutekeleza wajibu fulani.

    Upweke,msongo , ubadhilifu,uuaji na ukuaji wa matabaka ,ni sehemu ya madhara ya jamii ya kisasa.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei

    kemeimaureen7@uamsho

  • Kitu kimoja kinachodhihirisha thamani yako.

    Rafiki yangu unaweza kuwa unasema utakavyo ,lakini watu wataamini zaidi kile kile unachofanya. Maneno ni rahisi,kila mtu anaweza kusema atakavyo. Lakini matendo ni magumu na hayo yanadhihirisha kweli mtu anasimamia wapi.

    Kama kitu ni muhimu kwako utakifanya hutaishia tu kusema nataka hivi,nataka kufanya hiki na hiki. Kama unakitaka kitu kweli utafanya kila namna mpaka ukipate ,hautakubali kuzuiwa na chochote.

    Angalia yale unayofanya ,hayo ndiyo yanaonyesha zaidi ni nini unajali . Hata kwa wengine,usisikilize wanasema nini , wewe angalia wanafanya nini . Kama maneno na matendo ya mtu vinatofautiana, wewe amini zaidi vitendo kuliko maneno.

    Hivyo kwa wale ambao kila mwaka wanaema wanataka kuanza biashara ila hawana mtaji,au uwezo au muda au kingine chochote,jibu unalo hapa kuwa hawataki kuanza biashara.Wangekuwa wanataka kweli wangekuwa wameanza.

    Kuchukua hatua, Ili ukubalike na uaminike katika jamii ni vizuri kuwa watu wa vitendo,watu wenye kutia bidii kwenye kila tunachokifanya. Tukifanya hivyo tutaweza kutengeneza fursa nzuri ya kukubalika na kuaminika na pia maisha yatakuwa mazuri zaidi.

    Kuongea kwingi kunaleta jina ambayo sio nzuri kwenye jamii na pia watu watachoka na wewe kwa haraka. Na kibaya zaidi hutaaminika na fursa zikitokea kwenye jamii utakuwa mtu mwisho kupewa iyo fursa ,hivyo maisha yako yatakuwa magumu kidogo.

    Hivyo tuweke kazi kwenye matendo zaidi kuliko kuongea. Maana maneno ni rahisi na kila mtu anaweza akaongea jinsi awezavyo,lakini matendo ni magumu na wachache sana wanaweka nguvu kwenye matendo na kazi yao.

    Mwandishi wako akupendaye sana.

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com