- Kuwa na shauku ni sawasawa na kuongeza 25% kwenye akili.
- Mara zote taka jambo la mwisho, kuwa na dead line kwa kila jambo.
- Samehee hii ni kwa ajili yako mwenyewe.
- Usipime maisha yako kwa kutumia rula ya mwingine.
- Sehemu kubwa ya kusafiri ni kuacha mambo mengi nyuma.
- Lengo bora unaloweka kwenye mwaka ni kujifunza kitu kimoja kwa kina zaidi.
- Maumivu hayakwepeki kuteseka ni kuchagua.
- Kama unatafuta kitu ndani alafu hukioni ukikipata usikirudishe hapo kirudishe ulipoanza kukitafuta.
- Unapaswa kuchagua kitu kimoja ambacho unachokitak zaidi ya vyote kukifanya.
- Njia bora ya kujifunza kitu ni kuwafundisha wengine.
- Kanuni ya ukuu ni kuwa bora zaidi kila siku alafu rudia kila siku.
- Unapokuwa njia panda chagua njia inayoleta mabadiliko.
- Unaweza kutegemea tabia zaidi kuliko hamasa.
- Unapaswa kutaka ushahidi usio wa kawaida ili upate matokeo yasiyo ya kawaida.
- Usiwe bora kuwa wa kipekee .
- Usichukulie binafsi, wachukulie kama wewe.
- Fanya kitu kizuri , na ufanye tena na tena na tena.
- Boresha akili yako, fikiria kwa miguu,fikiria kwa mikono, tembea, andika.
- Punguza orodha yako ya vitu unavyofanya.
- Wajibika kwa makosa yako.
- Weka nguvu zako kuwahudhumia wateja wako kuliko kushindana na washindani.
- Hapana ni jibu tosha.
- Kama huanguki mara kwa mara hutembei unazurura, au hujionei aibu kwa mambo ya zamani basi hukui.
- Asilimia 99 ya mafanikio ni kuongea na mteja, kumpigia simu, onekana mara zote.
- Usiwe na haraka, ukiwa na haraka ndio utaibiwa, utatapeliwa.
- Hakuna ukomo wa kuwa bora, kuna kitu cha kuboresha kila siku.
- Usipoteze changamoto , penye changamoto ni sehemu ya kukua na kupiga hatua.
- Wewe ni kile unachofanya.
- Angalia maslahi unapoomba ushauri.
- Jambo unaloliona ni la kitoto ndilo linaweza kukufanikisha, bobea kwenye kile unachokifanya.
- Ukikopesha kitu, chukulia unampa zawadi, kama hatarudisha hutaumia.
- Kuwekeza hela kidogo kunaleta miujiza.
- Usikubali haraka ya mtu iwe dharura. Fanya kulingana na umuhimu sio dharura.
- Ukiona mtu analazimisha kitu, jua Kuna uongo nyumba yake.
- Kama hujishangai yale uliyokuwa ukitenda uko nyuma, basi usishangae ya mwenzio.
Rafiki tuifanyie kazi mambo haya na tutazidi kuwa bora kila siku kwenye maisha yetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com