Sifa 5 Za Jaribio Sahihi Kufanya.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini ili ufanye jaribio, lazima uwe na vigezo unavyoviangalia.

Kwenye kitabu cha skip the line mwandishi anatushirikisha vigezo vitano vya kuzingatia unapofanya jaribio.

Moja iwe rahisi kuanza,kwa kuwa utafanya majaribio mengi,basi la kwanza lazima liwe rahisi kufanya. Uweze kuanzia pale ulipo sasa bila kuhitaji kitu chochote cha nyongeza ambacho huna. Hupaswi kutumia muda nyingine kusubiri ili kuanza jaribio, linapaswa kuwa rahisi na uweze kuanza mara moja, ili uone matokeo yake na usonge mbele.

Mbili hatari iwe ndogo na ndani ya uwezo wako. Hatari iliyopo kwenye jaribio unalofanya uwe ndogo na ndani ya uwezo wako kuikabili. Usifanye jaribio ambalo lina hatari kubwa kwako kuweza kupoteza kila kitu kinaweza kudhurika kwa namna fulani. Jua kabisa hatari ya jaribio unalofanya ni ipi,kama litashindwa kabisa, hasara utakayoipata ni ipi. Kisha ona kama ni kitu kipo ndani ya uwezo wako ufanye.

Tatu faida unayoweza kupatikana iwe kubwa. Kwa kuwa majaribio utakayoifanya ni mengi na mengi utaishia njiani unapaswa kuchagua jaribio kwa kigezo kwamba kama litafanikiwa basi faida linapaswa kuwa kubwa sana kufidia majaribu mengine ambayo hayatafanikiwa. Na hata kama siyo faida ya kifedha,basi jaribio liweze kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia husika.

Nne iwe ni kitu ambacho hakijawahi kufanywa. Jaribio linapaswa kuwa kitu kipya ambacho hakijawahi kufanywa kabisa na hivyo hujui matokeo gani yatakayopatikana. Kama wazo lilishafanyika huwezi tena kusema ni jaribio, maana njia ya kufanya tayari inajulikana.

Tano ni kuwepo na kitu cha kujifunza. Katika kila jaribio unalofanya,haijalishi ni matokeo gani utapata, basi uwe na kitu ambacho utajifunza. Hata kama jaribio litashindwa kuleta matokeo uliyotaka, angalau ujifunze kitu ambacho kitakusaidia kwenye majaribio mengine. Katika majaribio unayofanya, hakuna kushindwa, unapata unachotaka au unajifunza kitu kipya.

Rafiki, kwa kuzingatia sifa hizi tano,utaweza kufanya majaribio yenye tija kwako na kama utayafanya mengi, lazima utakutana na jaribio litakaloleta matokeo mazuri na ukafanikiwa.

Na kama Thomas Edison alipoulizwa kuhusu kushindwa mara nyingi katika kutengeneza taa zaa umeme alijibu hakushindwa, bali alijua njia ambazo hazifanyi kazi.

Chukua hatua, rafiki kwa kila jaribio ujifunze ili unapoenda kwenye jaribio jingine uweze kulifanya kwa ubora zaidi kuliko jaribio lililopita.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment