Kuwa Bora Kwa Asilimia 1 Kila Siku.

Rafiki yangu mpendwa sheria ya asilimia moja kila siku ni kukazana kuwa bora zaidi kila siku kwa asilimia moja kuliko ulivyokuwa siku iliyopita.

Kwa kila siku mpya unayoianza, pambana kujiboresha kwa asilimia moja zaidi ya siku iliyopita kwenye kile unachofanya.

Unaweza kuiona asilimia moja ni ndogo na kuidharau, ila hujajua nguvu yake. Kama utaifanyia kazi sheria hiyo kwa mwaka mzima, ukakazana kuwa bora kwa asilimia 1 zaidi kila siku kwa siku 365, unadhani mwisho wa mwaka utakuwa bora kwa asilimia ngapi?

Kwa hesabu ya haraka utasema unakuwa bora kwa asilimia 365, lakini hiyo siyo kweli. Kwa kuwa bora kwa asilimia moja zaidi kila siku, kwa siku 365 unakuwa bora kwa asilimia 3,800.

Ndiyo, yaani unakuwa bora mara 38 ya ulivyoanza na hapo ni kwa mwaka mmoja tu. Kinachofanya ubora wako uwe mkubwa hivyo ni nguvu la ongezeko la mkusanyiko compounding.

Siku ya kwanza unakuwa bora asilimia 1, siku ya pili unakuwa bora kwa asilimia 1 zaidi ya siku ya kwanza.

Siku ya tatu unakuwa bora kwa asilimia moja zaidi ya siku ya pili. Kwa hiyo ubora wako unakua kwa mkusanyiko na siyo kwa mstari.

Chukua hatua, kwa kukazana kuwa bora kwa asilimia moja zaidi kuliko ulivyokuwa siku iliyopita, unajikuta ukiwa umepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja kuliko ambazo wengine wanapiga kwa miaka 10.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafsi.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment