Jinsi ya kujizoeza kuwa na nidhamu binafsi.

Nidhamu binafsi sio kitu ambacho unasema unayo au huna. Ni kitu ambacho kila mmoja wetu anaweza awe nacho na kuongoza. Au kuamua kutokuwa nacho na kuipuuza kabisa. Kusema hapana kwa sahani ya chipsi ama cookies inahitaji uwe na nidhamu ya kiasi.

Kama vile kwa kufanya mazoezi na kama hutaki kuepuka makosa hizi ambazo zinakurudisha nyuma inahitaji msimamo thabiti na bidii .

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia inapokuja kwenye kuwa na nidhamu ya kiasi.

Kujifunza kuvumilia magumu (practice tolerating discomfort) Kama unahisi upweke na unajaribiwa kuchati na ex wako ambaye siye mtu mzuri kwako. Au una uteja wa vyakula ambavyo zinaharibu afya yako. Unapaswa ujifunze uvumilie magumu ya kukosa haya yote. Ingawa watu saa zingine wanajifariji na kusema wakikubali au kufanya kitu hiki itawasaidia. Tafiti zinaonyesha tofauti,kuwa kila mara unapokubali kutovumilia magumu unapunguza uwezo wa kuwa na nidhamu ya kiasi.

Kuwa chanya kwenye maongezi Yako. (Use positive self-talk) kiuhalisia unapojitamkia kauli chanya au uchanya kila mara inakusaidia uepuke majaribu wakati wa udhaifu wako. Kujitamkia kauli kama ” Naweza fanya hiki”ama ‘ninafanyia kazi malengo yangu’ Kujitamkia hivyo inakusaidia kukaa kwenye mchakato.

Fikiria kuhusu malengo yako. (Keep your goals in mind). Kuweka focasi kwenye umuhimu wa malengo yako inapunguza majaribu. Hivyo ukiweka focasi yako kwenye kutimiza malengo na mipango yako kila siku,wiki ,mwezi na mwaka , inakusaidia sana kwenye kujenga nidhamu binafsi.

Jisukume mwenyewe ( impose restrictions on yourself). Kama unajua unaweza ukatumia fedha nyingi ukiwa unatembea na marafiki , amua kutembea na fedha zako chache . Chukua hatua ambazo zitakuwa ni vigumu kwako kushawishika kuingia kwenye majaribu haraka.

Tengeneza sababu za kwa nini hutaki kurudia makosa yaleyale. ( Create a list of all the reasons why you don’t want to repeat your mistakes). Tengeneza orodha yako na utembee nayo,unapojaribiwa kurudia kosa lako la awali . Soma kwa sauti tena orodha yako ,kwa kujizoeza hivyo kunaongeza ushawishi wako wa kukataa kurudia makosa hayo hayo kila mara. Kwa mfano, tengeneza orodha ya sababu yote ya wewe kutembea baada ya kula,unapojaribiwa kukaaa chini na kuangalia Tv badala ya kufanya mazoezi,soma orodha yako na itakuongezea hamasa yako ya kusonga mbele.

Kujenga nidhamu binafsi inaanzia kwenye kuwa na shauku kubwa ya kukua ,kujenga shauku na kuhakikisha upo juu kila wakati. Ili usirudishwe nyuma na maneno ya watu au kukatishwa tamaa.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment