Tatizo linalotokana na kuogopa upweke.

Mara kwa mara tunafungwa na majukumu pia na mahusiano yetu ya kila siku. Saa zingine yanakuwa mzigo kwetu kama hatutaaja au kuamua kutenga muda wa kuwa peke yako na kuamua kujiimarisha zaidi. Kwa bahati mbaya sana,umuhimu au uzuri wa kuwa peke yako mara nyingi zinaepukwa .

Watafiti wengi wanasema upweke wa kutenga muda na kuwa peke yako,una umuhimu mkubwa ambao sanasana wale wanaaogopa kutenga muda wa kuwa peke yao wanaiogopa.

Wastani wa upweke yaani muda wa kuwa pekee una manufaa makubwa sana kwa watoto. Utafiti uliofanywa mwaka wa 1997 ” the emergence of solitude as a constructive domain of experience in early adolescence.” Ilidokeza kwamba wanafunzi watano hadi watisa ,ambao wanatumia muda mwingi wa wastani peke yao wana uwezekano mdogo sana wa kuhusiana na tabia zisizofaa.

Watoto hao pia wanauwezo mdogo sana wa kupatwa na msongo wa mawazo, pia wana uwezo mkubwa wa kufaulu darasani.

Upweke ofisini unaongeza umakini. Ingawa ofisi nyingi inafanyiwa kwenye eneo la watu wengi. Tafiti wa mwaka wa 2000 ambao unaitwa “cognitive stimulations in brainstorming.” Iligundulika kwamba watu wengi wanaweza kufanya vizuri zaidi wakiwa peke yao. Kupata matokeo mazuri inahusishwa na kutenga muda wa kuwa peke yako.

Kuwa peke yako inaongeza uwezekano wa kuwa na huruma kwa wengine.Kwa kadri watu wanaotumia muda mwingi peke yao,wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuonyesha huruma kwa wengine. Kama unatumia muda wako mwingi kuzurura mtandaoni na kuongea sana ,una uwezekano mkubwa wa kushikwa na we’vs them’ ‘mentality’ ambao unaleta tabia ya kutokuwa na roho ya huruma kwa wenzako.

Kwa kutumia muda mwingi kuwa peke yako unaongeza ubunifu. Wengi waliofanikiwa hasa kwenye usanii na uimbaji wao hupenda kutumia muda mwingi kuwa peke yao,husaidia kuwa wabunifu zaidi. Tafiti nyingi zinashauri kutenga muda wa kuwa peke yako inamaana unaongeza ubunifu.

Kuwa peke yako unaongeza uwezekano wa kuwa na afya ya akili. Ingawa kuna msisitizo wa umuhimu wa kushirikiana na wengine, ushahidi unashauri kuwa ,kutenga muda wa kukaa peke yako unastawisha mtu na kufanya awe imara kiakili. Kuweza kuwa peke yako husaidia mtu kuwa wa furaha, kutosheka na pia kuongeza uwezo wa kutawala usongo wa mawazo. Wanaofurahia muda wa kuwa peke yao wanapata asilimia ndogo ya sonona.

Muda wa kuwa peke yako unakusaidia ujitafakari na kukusaidia urejelee utu wako na ujikubali jinsi ulivyo. Pia unakutoa kwenye kufuata mkumbo inaleta fursa ya kujiboresha na kujiongeza . Utafiti unaonyesha kwamba kutenga muda huo wa kuwa peke yako kwa asili inakusaidia uwe upya tena kwa sababu ya mapumziko mazuri ya utulivu.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment