Home

  • Mambo 8 Ya Kuzingatia Ili Kuongeza Bahati Yako Kwenye Maisha Yako ( falsafa ya ustoa)

    Rafiki yangu mpendwa habari njema ni kwamba siku ya leo tuna bahati nzuri kabisa, na bahati iyo ni hii hapa. Kwamba leo nakushirikisha jinsi ya kuongeza bahati kwenye maisha yako.

    Usiwe na wasiwasi wowote kwa maana falsafa hii imekuwapo tangu ni falsafa ya kutokudharau kitu chochote na pia kutokuamini kitu chochote.

    Mwanafalsafa Epictetus anatukumbusha kutoka Kitabu chake mambo ya kufanya ili tuongeze bahati kwenye maisha yetu.

    Baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo;

    1. Mara zote fikiria kuhusu kifo na kamwe hautadharau chochote wala kutamani chochote kupitiliza. Unapofikiria kuhusu kifo kuwa ni kitu ambacho kipo, utakuwa unajua sio jambo bora kungangania vitu ambavyo hazileti manufaa kwenye maisha yako. Utajua ni swala la muda mfupi tu. Kujikumbusha kuhusu ufupi wa maisha unaweza kuendea maisha bila hofu wowote, kwa sababu unajua hata ukiogopa mwishowe utakufa na ni bora kudhubuthu kufanya jambo kuliko kukaa bila kufanya chochote.
    2. Unapobadili maisha yako, kwa mfano kuanza biashara, kufanya uwekezaji, kuongeza masomo au kuwa hata bilionea. Watu wengi hawatafurahishwa na hayo. Wataanza kusema unajifanya, au unajiona wewe ni bora kuliko wengine wote ama unajiona unaweza zaidi. Unachopaswa kufanya ni kuendelea kufanya kile unachokifanya bila kuruhusu wengine wakukatishe tamaa, kwani mwishowe utakapofanikiwa watakuwa wa kwanza kufurahia mafanikio yako na watakuheshimu. Unapoacha sasa kupambania matamanio yako, na kusema kuwa watu hao wanakusema vibaya, wanaona unajifanya, mwishowe ukifeli au usopofanikiwa, watu hao watakudharau zaidi na kusema wewe ni mvivu au haufai kabisa. Muhimu hapa ni kutokusikiliza kelele zao unapopambania mafanikio yako.
    3. Unapotaka kufanya kitu ili uonekane na wengine, tayari umeshapoteza. Kwani kuna watu tu hawatafurahia kile unachofanya. Kuwa kile ambacho unataka kuwa wewe, alafu wao watachagua kama watakubaliana na wewe au waende kinyume na wewe.
    4. Tusifanye maisha yetu kuwa ngumu zaidi kwa kutaka kuheshimiwa na wengine. Yote tunayohangaika nayo hatupaswi kufuatilia wengine wanasema nini. Wajibu wako ni kuwa wewe, kufanya yale muhimu kwako. Kutaka kujua wengine wanakuchukulia vipi viko nje ya uwezo wako.
    5. Kuhusu matokeo ambayo wengine wanapata au mafanikio ya wengine. Wengine wamefika na sisi hatujafika kama tunaona watu wamepiga hatua fulani, ni kwa sababu kuna gharama ambao wamelipa ambao sisi hatujalipa. Kwa kila mafanikio ambao tunataka kufikia kwenye maisha tunapaswa kuwa tayari kulipa gharama yoyote ile.
    6. Kitu ikitokea kwa wengine tupo tayari kuwatia moyo, au kuwashauri kwa mfano mtu akipoteza mpenzi wake au mmoja wa familia wake, ni rahisi sana kuwatia moyo, lakini inapokuja kwetu tunaona ni ngumu sana kuelewa kuwa imetokea na hivyo huwa inatuumiza sana. Tunapaswa kuelewa na kujua kuwa ni sehemu ya asili na inapita na maisha lazima iendelee.
    7. Hakuna kitu kibaya kinachotokea kwa asili hapa duniani au kikitokea ni kitu chanya au kitu kizuri. Huwa ni chema kwa ajili ya Dunia nzima, chenye manufaa, huwa ni kitu chenye manufaa kwa dunia hii. Tukijua hilo tutaweza kukabili mambo yanayotokea kwa njia nzuri zaidi.
    8. Ni mara ngapi umewapa watu nafasi ya kuathiri maisha yako? Sina uhakika kama itakufaa, lakini mara nyingi tunaruhusu wengine waharibu rasilimali zetu muhimu kama muda, akili zetu na nafsi zetu. Tunafanya hivyo kwa kushindwa kijiheshimu sisi wenyewe. Kwa kuruhusu watu watuvuruge na hivyo tunashangaa mbona hatupigi hatua kwenye maisha yetu. Tunaruhusu watu watupe uchafu zao ndani zetu kwa kusikiliza habari mbaya, habari hizi huondoa amani na utulivu ndani yetu na kutupa wasiwasi wa muda wote. Habari hizo ni za kutufanya tuishi kwa hofu kila mara, hivyo huathiri fikra zetu kwa sababu watu hawatakuwa na utulivu wa kifikiri kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.

    Chukua hatua; rafiki mbira iko upande wetu sasa tuhakikishe tunasoma na kuelewa falsafa hizi na kuweka kwenye matendo ili tuweze kuishi kama wastoa na kuwa wa tofauti kwenye jamii.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei

    KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

  • Mambo 5 Ambayo Nimejifunza Kutoka Kitabu Cha The Old Man And The Sea.

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana siku hii njema ya leo nikushirikishe yale nimejifunza kutoka hadithi hii fupi cha mzee anayepambana na bahari katika kipindi ambacho anaonekana hana bahati.

    Anafanikiwa kumuua samaki mkubwa, lakini anapitia magumu katika kumpeleka samaki huyo ufukweni. Anatumia kila zana kupambana nguvu, nia na akili.

    Yale nimejifunza ni kama yafuatayo ;

    1. Umuhimu wa kupambana hadi tone la mwisho bila kukata tamaa. Jinsi Santiago pamoja na uzee wake alivyoweza kupambana na japo hakupata alichotaka lakini hakukata tamaa.
    2. Umuhimu wa kuwa na watu wa kutusaidia, kwani mara nyingi Santiago alitamani kijana angekuwa karibu yake amsaidie.
    3. Kufanya maamuzi ni kitu kingine tunajifunza, hasa kupitia kijana ambaye alipenda kujifunza kwa mzee, lakini familia yake ikawa kikwazo. Mwisho kabisa anaamua kutokusikiliza familia yake ili aweze kujifunza.
    4. Umuhimu wa nia na akili katika mapambano yoyote yale, hata kama nguvu zitakuishia, pambana kuvitunza hivyo viwili, kuwa na nia ya dhati na kuhakikisha akili inafikiri sana.
    5. Haijalishi unapitia nini, lazima uhakikishe unakula ili mwili uwe na nguvu na pia na pia akili inapumzika ili akili iweze kufikiri vizuri.

    Chukua hatua; kila mmoja wetu ana mapambano yake, muhimu ni sisi tupambane bila kukata tamaa.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

  • Misingi 8 Ya Kufanikiwa Kwenye Biashara.

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana leo tunajifunza misingi nane ya kuzingatia ili kufanikiwa kwenye biashara yoyote ile, mambo haya nimejifunza kutoka kwa kipindi cha ongea na Kocha Dr Makirita Amani.

    Mambo haya ni kama yafuatayo ;

    1. Kuwa na imani yenye nguvu na isiyo yumbishwa. Kama huamini ndani ya nafsi yako kuwa utafanikiwa kwenye biashara yako hivyo, huwezi ukafanikiwa. Kujenga ndani yako imani dhahiri kabisa inakufanya uwe imara kwenye biashara yako.
    2. Kuwa na mapenzi ya dhati. Watu wengi wanaanza biashara kweli vizuri kabisa lakini wakikosa mapenzi ya kweli na kujitoa kwenye kujenga biashara hiyo hiwezi fanikiwa.
    3. Chukua hatua kwa haraka. Kama huwezi ukachukua hatua sasa tena kwa haraka huwezi fanikiwa kwenye biashara.
    4. Kuwa bora zaidi kwenye uimara yako. Kila mmoja wetu ana maeneo yenye uimara na dhaifu, unapaswa kuwa na uimara zaidi kwenye maeneo yako ya uimara.
    5. lazima kuwa na uerefu na umakini. Lazima uzitumue vizuri rasilimali zako, na siyo kuzitawanya ovyo.
    6. lazima kutawala sehemu ya soko au (niche) . Usifanye biashara ambayo unashindana na watu. Tafuta biashara au ona kile ambacho watu wanakitaka sana kisha anza kuifanya kwa ubora zaidi.
    7. Kuwa na mtazamo endelevu kama miaka kumi na kuendelea. Unapaswa kuangalia miaka kumi kutoka sasa utakuwa wapi. Hivyo utaweza kujitoa vilivyo kwa kuweka rasilimali zako kwenye biashara kama muda, fedha, na nguvu zako.
    8. Kuwa wa tofauti kabisa na wengine kuwa tayari kuonekana kichaa. Namna pekee ya kujenga biashara yako ni kuonekana kichaa au mwendawazimu ili uweze kufanya kubwa kwenye biashara yako. Hufau kukaa kistaraabu au kwa mazoea kama wengine unapaswa kuwa wa tofauti, kufanya kwa tofauti kabisa na wengine. Unaenda kinyume na mazoea yaliyo kwenye jamii.

    Chukua hatua ; rafiki tunapaswa kuzingatia mambo hayo nane ili tuweze kufanikiwa kwenye biashara zetu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

  • Dalili Za Mtu Mwenye Msongo Wa Mawazo.

    Rafiki yang mpendwa karibu siku ya leo tunajifunza kuhusu dalili Za kujua kama umeathirika na msongo wa mawazo.

    Dalili hizi ni kama zifuatazo;

    1. Kuchoka akili na mwili. Mtu mwenye msongo wa mawazo anaweza kujiskia mchovu kila wakati, hata baada ya kulala au kupumzika. Ni kama mwili na akili vinakosa nguvu za kufanya shughuli ndogo kila siku.
    2. Wasiwasi na huzuni ya wa kwa mara. Mtu anakuwa na hali ya wasiwasi wa kudumu, ambapo anahisi kuwa mambo hayaendi sawa au kuna hatari inayoikabili, hata kama hakuna msingi wa hofu iyo. Huzuni inakuwa sugu, na mtu anaweza kupoteza hamu ya kufanya mambo aliyokuwa akiyafanya hapo awali.
    3. Kubadilika kwa hamu ya kula. Watu wanaokumbwa na msongo wa mawazo mara nyingi hupata mabadiliko ya hamu ya kula chakula. Wengine wanaweza kupoteza kabisa hamu ya kula, wakati wengine wanakula kupita kiasi kama njia ya kupunguza mawazo.
    4. Kushindwa kulala vizuri ( insomnia). Moja ya dalili Za kawaida ni shida ya kulala au kupata usingizi hafifu. Mtu anaweza kupata taabu kulala, kuamka usiku mara kwa mara, au kuamka mapema sana bila uwezo wa kurudi usingizini.
    5. Kushuka kwa nguvu na Ari ya kufanya kazi. Msongo wa mawazo huathiri uwezo wa kufanya kazi au kufurahia mambo ambayo awali yalikuwa yanavutia. Mtu anaweza kupoteza motisha ya kufanya kazi au shughuli za kila siku hali hii ikiambatana na hisia ya kutokujali au kutoona thamani ya juhudi zake.
    6. Kusumbuliwa na mawazo mbaya. Msongo wa mawazo unaweza kusababisha mawazo hasi ya mara, kama vile kujiona huna thamani, kukosa matumaini, au hata kufikiria kujiua.
    7. Dalili za kimwili ( maumivu ya kichwa na mwili). Mara nyingi, msongo wa mawazo unajidhihirisha kupitia maumivu ya kimwili kama vile maumivu ya kichwa, tumbo, au mgongo bila sababu ya kiafya inayoeleweka.
    8. Kujitenga na watu wengine. Watu wenye msongo wa mawazo wanaweza kujikuta wakiepuka mikusanyiko ya kijamii au hata watu wa karibu kwa sababu ya kutokuwa na Ari ya kushirikiana au hisia ya kuwa mzigo kwa wengine.
    9. Kupunguza kwa umakinifu. Msongo wa mawazo unaweza kuathiri uwezo wa mtu wa kufikiria kwa umakini, kufanya maamuzi sahihi, au kuzingatia kazi. Mtu anaweza kusahau mambo kwa urahisi au kuwa na shida ya kumaliza kazi aliyoanza.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo Ya Kuzingatia Ili Kudhibiti Msongo WA Mawazo( sehemu ya Tatu).

    Rafiki yangu mpendwa tunaendelea kujifunza njia tofauti za kupunguza msongo wa mawazo, karibu sana tujifunze ili tuishi maisha ya furaha kila siku.

    Pamoja na zile njia kumi ambazo tumeshajifunza hii hapa njia zingine sapa za kuzingatia ili kupunguza msongo wa mawazo. karibu sana.

    11. Cheka: Kucheka hutoa kemikali za hisia nzuri kama endorphins, ambazo hupunguza homoni za msongo na kusaidia kupumzisha mwili. Angalia kitu cha kuchekesha au tumia muda na watu wanaokufurahisha ili kupunguza msongo wa mawazo.

    12. Panga vizuri mazingira: Mazingira yaliyojipanga vizuri husaidia akili kuwa na utulivu. Wakati nafasi yako au ratiba yako imejipanga vizuri, unaepuka hisia za kuvurugika na kudhibiti msongo.

    13. Andika shukrani: Kuandika vitu unavyoshukuru kila siku husaidia kuhamisha mtazamo wako kutoka kwa msongo hadi kwa mambo mazuri katika maisha yako. Hii inaboresha hali ya jumla ya furaha na kuridhika.

    14. Kupumzisha Misuli (progressive muscle relaxation): Mbinu hiii inahusisha kubana na kuachia misuli ya mwili, kikundi kimoja kwa wakati, mfano kukunja na kuachia vidole. Kuzungusha shingo, kujinyoosha nk. Hii husaidia kupunguza msongo wa mwili na akili, na kuleta utulivu.

    15. Epuka vichochezi: Kafeini, nikotini, na sukari zinaweza kuongeza wasiwasi na msongo wa mawazo. Kupunguza au kuepuka vichochezi hivi kunaweza kusaidia kudhibiti hisia na kupunguza mawazo.

    16. Jifunze kusamehe: Kuweka kinyongo au chuki inaweza kuongeza mzigo wa kihemko na msongo. Kujifunza kusamehe wengine au hata wewe mwenyewe husaidia kuachilia mzigo wa kihemko na kupunguza msongo wa mawazo.

    17. Tafuta msaada wa kitaalamu: Wakati msongo unakuwa mgumu kudhibiti, kuzungumza na kushauri au mtaalamu na msaada wa kitaalamu.

    Chukua hatua ; rafiki hayo ni mambo ambayo tunashauriwa kufanya ili kupunguza msongo wa mawazo.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Hatua Za Kuzingatia Ili Kupunguza Msongo WA Mawazo (sehemu ya pili).

    Rafiki yangu mpendwa karibu twendelee kujifunze zaidi kuhusu njia hizi za kupunguza msongo wa mawazo ili tuweze kuishi maisha ya furaha.

    Haya ni baadhi ya njia za kupunguza msongo wa mawazo.

    5. Udhibiti wa muda. Kuwa na wakati mzuri wa kupanga majukumu hili kupunguza hisia za kuvurugikana na kuahirisha mambo. Gawa kazi kubwa kuwa sehemu ndogo na weka vipaumbele kwa kuainisha uta anza na kipi na kuishia na kipi, hili litakusaidia kudhibiti muda vizuri.

    6. Msaada wa kijamii. Wakati huu unahitaji watu wa karibu ili wakusaidie, kuwa na uhusiano mzuri na watu wa karibu husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Kuzungumza na marafiki au familia hutoa fursa ya kushiriki hisia zako na kupata mawazo tofauti.

    7. Kuimba. Uimbaji ni tiba ambayo wengi hawaitambui, jiunge na kwaya kanisani au kikundi cha uimbaji kanisani. Sikiliza wimbo ulio tulia usio na midundo mingi, muziki mtulivu ni tiba, husaidia kupunguza mvutano wa mwili na akili. Mbinu hizi hutuliza mwili na kusaidia kudhibiti kiwango cha mawazo.

    8.Jihusishe na burudani sahihi. Kufanya shughuli unazozipenda, kama vile kusoma au kuchora, husaidia akili kupumzika na kuondoa mawazo ya msongo. Hata shughuli ndogo hutoa nafasi ya kufurahia wakati wa sasa na kupunguza mawazo ya kupindukia.

    9. Weka mipaka. Kujifunza kusema hapana kunasaidia kuzuia kuchukia majukumu mengi kupita kiasi ambayo kusababisha msongo wa mawazo. Kujua mipaka yako ni muhimu kwa kudhibiti mzigo wa kazi.

    10.Punguza muda wa vifaa vya digitali. Muda mwingi kwenye mitandano wa kijamii au skrini za simu unaweza kuongeza msongo kwa kulinganisha maisha yako na ya wengine au kwa sababu ya habari za kusumbua. Kupunguza muda wa skrini husaidia akili kupumzika.

    Chukua hatua; rafiki tunapaswa kuzingatia hayo hili kupunguza msongo wa mawazo.

      Rafiki yako,

      Mauree Kemei.

      KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

    1. Hatua Za Kuzingatia Ili Kupunguza Msongo WA Mawazo (sehemu ya kwanza) .

      Rafiki yang mpendwa Sina uhakika kama itakufaa, lakini msongo wa mawazo ni hali inayotokana na fikra nyingi ngumu za maisha.

      Ili kupunguza zingatia hatua zifuatazo:

      1. Mazoezi. Kufanya mazoezi ya mara kwa mara huchochea utoajj wa endorphins, kemikali zinazoboresha hali ya hewa, huku ikipunguza homoni za msongo kama cortisol. Mazoezi oia husaidia kuboresha usingizi, ambayo ni muhimu kwa kupunguza msongo wa mawazo.
      2. Kupumua kwa Kina( deep breathing. Kupumua polepole na kwa kina husaidia kupunguza msongo kwa kudhibiti mfumo wa neva ambao una jukumu la kutuliza mwili. Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kwa sekunde tank, kuishikilia kwa sekunde chache, kisha kuachia polepole.
      3. Maombi ya kushukuru. Maombi haya unamshukuru Mungu kwa mema aliyokutendea, unaweza kuorodhesha kwenye karatasi na kusoma. Hii husaidia kuondoa msongo ya kulalamika na wasiwasi wa baadae, akili yako itatambua kuwa Mungu aliye kutendea haya atakutendea na hilo unalopitia. Maombi ya kushukuru husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
      4. Mtindo wa maisha bora. Kulala kwa muda wa kutosha, kula chakula chenye virutubisho sahihi, na kufanya mazoezi ya mara kwa mara husaidia mwili na akili kuwa na uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo.. Kuepuka kafeini na sukari nyingi husaidia kudhibiti mihemko na kuepuka mabadiliko ya ghafla ya nguvu za mwili.

      Chukja hatua: Rafiki baada ya kugundua ishara za msongo wa mawazo unaweza kujaribu njia hizi na unaweza kupunguza msongo haya.

      Rafiki yako,

      Maureen Kemei.

    2. Tabia 5 Za Kuishi Kila Siku.

      Rafiki yangu mpendwa mafanikio yetu yanajengwa au kubomolewa na tabia tunazoziishi kila siku.

      Ndiyo maana Huwa inasemekana kwamba tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga.

      Tabua hayo 5 ni kama yafuatayo;

      1. Kila siku amka mapema. Ukishaamka usiangalie simu wala usumbufu wowote, bali anza kwa kufanya sala au tahajudi, kisha chukua notebook yako na andika vipaumbele vya siku yako.
      2. Kila siku fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30.
      3. Kila siku soma kitabu kwa angalau dakika 30, chagua kitabu chochote unachotaka kusoma, iwe ni cha maendeleo binafsi au maendeleo ya kitaaluma kisha soma kwa angalau dakika 30 kila siku.
      4. Kwa siku pangilia na dhibiti ulaji wako, punguza kabisa vyakula vya wanga na sugari, kula mboga mboga na matunda kwa wingi, kula nyama kwa kiasi na kunywa maji mengi. Pia dhibiti sana vilevi unavyotumia.
      5. Kila siku mpigie simu mtu mmoja wa karibu, ndugu jamaa na marafiki na kuwa na maongezi naye ya kuboresha mahusiano yenu.

      Chukua hatua; rafiki yangu ni mambo hayo matano tukifanyia kazi bila kuacha tutaweza kufanya makubwa.

      Rafiki Yako,

      Maureen Kemei.

    3. Mambo 4 Muhimu Ambayo Nimejifunza Kutoka Kwa Mwanaharakati Wa Afrika Kusini Desmond Tutu.

      Rafiki yangu mpendwa karibu nikushirikishe mambo makubwa muhimu kutoka kwa maisha ya aliyekuwa na Nelson Mandela katika harakati ya kuikomboa Afrika Kusini na kuponya majeraha ya ubaguzi.

      Yafuatayo ni mambo hayo muhimu;

      1. Kuwa jasiri kusimamia kile kilicho sahihi bila kujali ni nani anayekupinga, lakini pia kuwa tayari kuwasamehe waliokuumiza kwa namna mbalimbali.
      2. Kila binadamu hapa duniani ni muhimu bila kujali rangi, jinsia, dini au utaifa. Na kila mtu anapaswa kuchukuliwa kwa heshima, uelewa na upendo.
      3. Umuhimu wa kila mtu kuishi upekee ambao upo ndani yake, kuvunja minyororo ya ukomo ambayo tumejengewa na kuwa halisi, kitu ambacho kina mchango mkubwa hapa duniani.
      4. Kila mtu ni kiongozi ata kama hana madaraka. Asili huwa haipendi kuwepo kwa utupu, hivyo popote ulipo, asili itakupa wajibu wa kuwa kiongozi ili kujaza ombwe lililopo. Ni wajibu wako kuwa na maono na kuwahamasisha wengine kuyaelewa na kujiunga na maono uliyonayo.

      Sisi binadamu tuna nguvu kubwa ambayo ipo ndani yetu, ni wajibu wetu kuitambua na kuianza kuitumia ili kuweza kufanya makubwa.

      Rafiki yako,

      Maureen Kemei.

    4. Umuhimu Wa Kuishi Maisha Yako.

      Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wengi wamekuwa wakifanya mambo kwa ajili ya kujijengea sifa baada ya kuondoka hapa duniani.

      Wanafanya kwa lengo la kukumbukwa vizazi kwa vizazi kwa majina yao kuandikwa maeneo muhimu au kuchongewa masanamu.

      Lakini kama ilivyo kwenye mambo mengine ya maisha, unapolazimisha kitu, huwa hakitokei. Unapofanya mambo ili ukumbukwe, hakuna anayekukumbuka, kwa sababu unakuwa siyo rahisi.

      Tunapaswa kuachana na msukumo wa kufanya vitu ili tukumbukwe au kuacha alama. Badala yake, tuchague kuishi maisha halisi, tusimamie kile kweli tunachokiamini na tutakuwa na maisha bora huku pia tukiwa na nafasi kubwa ya kuendelea kukumbukwa.

      Watu hawatakukumbuka kwa sababu unataka wakukumbuke, bali watakukumbuka kwa aina ya maisha unayoishi.

      Hivyo wajibu wako mkubwa ni kuyaishi maisha yako kwa uhalisia na ukamilifu wake.

      Rafiki yako,

      Maureen Kemei.