Home

  • Mambo 35 Ambayo Nimejifunza Kutoka Kitabu Cha (The Excellent Advice For a living). Na Kevin Kelly.

    Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze mambo hayo 35 muhimu ya kuishi kila siku kwenye safari yetu ya mafanikio.

    Mambo haya muhimu ya ushauri muhimu kwenye maisha ni kama yafuatayo;

    1. Kuwa na shauku kubwa ni sawasawa na kuongeza alama 25 kwenye akili. Kuwa na shauku kubwa mara zote kwa jambo unalofanya inaongeza akili.
    2. Mara zote taka muda wa mwisho, kila jambo unalofanya jiwekee (deadline).
    3. Samehe, msamaha sio kitu unalofanya kwa ajili ya wengine bali ni kwa ajili yako. Samehe kama zawadi yako mwenyewe.
    4. Usipime maisha yako kwa kujipima na rula ya watu wengine. Jipime na watu waliotangulia kwako walifanya nini ili wakafanikiwa.
    5. Sehemu kubwa ya kusafiri ni kuacha vitu nyuma. Kusumbuka kwa mambo mengi ni kikwazo kwenye safari yako.
    6. Lengo bora unayoweza kujiwekea kwa mwaka ni kujifunza kuhusu kitu kimoja hadi ukakielewa kwa kina.
    7. Maumivu hayakwepeki, mateso ni kuchagua.
    8. Weka vitu mahali pale, mara nyingi kwenye maisha tunajua vitu viko wapi, tunapaswa kuweka vitu mahali rahisi kuvipata.
    9. Unapaswa kuchagua kitu kimoja ambacho unakuwa (obsessed) sana kuvipata. Weka lengo lako juu sana utakapofika hautaanguka sana.
    10. Kama unataka kuelewa kitu jaribu kuelezea watu wengine.
    11. Kanuni ya ukuu kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa mwaka uliopita alafu rudia kila siku. Chukua hatua kwa namna tofauti kila siku .
    12. Unapokuwa njia panda, chagua njia inayoleta mabadiliko makubwa .Chukua njia ambacho ni kigumu.
    13. Tabia au hamasa haitafanya chochote, jenga tabia ya kuweka akiba, kuwekeza, kufanya mazoezi. Unafanya bila kufikiria.
    14. Unapaswa kutaka ushahidi wa kutosha ili kabla ya kuchukua hatua kwenye kufanya jambo fulani.
    15. Kuwa bora kuliko wote haitoshi bali kuwa wa kipekee na hilo litakutofautisha sana kwenye maisha yako.
    16. Usichukulie binafsi pale mtu anapokukatalia. Jua ni kawaida ya maisha, jifunze kupokea kukataliwa.
    17. Kufanya kitu bora unapaswa kufanya tena na tena, siri ya kufanya kitu kizuri ni kurudia rudia kufanya ( mafanikio ni kurudia rudia).
    18. Panua akili yako, fikiria kwa miguu na kwa mikono, fikiria unapotembea. Ukitaka kufikiria vema tembea , andika.
    19. Punguza orodha yako ya mambo unayofanya. Hakuna chochote kibaya kitatokea unapoacha kufanya mambo mengine mengi.
    20. Ukitaka kuinuka juu wajibika kwa makosa yako.
    21. Njia Bora ya kuangusha washindani ni wewe kuangaika na wateja wako.
    22. Jifunze kusema hapana.
    23. Kama huanguki mara kwa mara unatembea tu, njia nzuri ya kujifunza ni kuanguka. Ukiona uko sahihi mara zote jua hujui.
    24. Asilimia ya 99 ya mafanikio ni kuonekana. (Keep showing up), kama kukutana na mteja, kuuza, kuandika, kufanya kazi.
    25. Usiwe na haraka ya kutaka vitu kwa haraka, utatapeliwa.
    26. Hakuna ugomo wa kuwa bora, mara zote amini kuna kitu cha kuboresha.
    27. Usipoteze changamoto , changamoto inapokuja ndipo kuna hatua ya kupika, mambo yanapokuwa magumu ndipo watu wanapaswa kuwa wagumu
    28. Wewe ni kile unachokifanya, kile unachokifanya ndio inakujenga wewe.
    29. Mara zote angalia maslahi. Kama jambo lina maslahi kwa mtu atakushauri vizuri.
    30. Jambo linalokufanya uone ni maajabu ukiwa mdogo litakufanya uwe bora ukiwa mkubwa.
    31. Bobea kwenye kitu kimoja , kupenda kitu hakitoshi.
    32. Mtu akikuomba kitu chukulia kama anaomba zawadi, ndio asiporudisha haitakuuma, akirudisha itakuwa kama (surprise) kwako.
    33. Kuwekeza kidogo kwa muda mzuri kunaleta maajabu. Lakini watu wanataka utajiri wa haraka.
    34. Usikubali haraka ya mtu, kuwa mfalme kwa kufanya yale muhimu kwako. Mambo yanayotaka ufanye kwa haraka kwa uhalisia ni utapeli tu.
    35. Ukiona mtu akikulazimisha kuwa huu sio utapeli jua ni utapeli, sio uongo jua ni uongo. Kitu cha kulazimishwa huja kinyume chake.

    Hatua ya kuchukua tunapaswa kuchukua hatua kwenye mambo haya ambayo tumejifunza leo na kuyaishi mambo haya kwenye maisha yetu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Namna Ya Kujua Kuwa Unaambatana Na Marafiki Wabay( bad company).

    Rafiki yangu kuna msemo unasema hivi “Nionyeshe marafiki zako nami nitakuambia tabia yako.

    Marafiki wana uwezo wa kujenga hatima yako au ndoto yako au wakaua kabisa ndoto yako.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini watu waliofanikiwa sana kwenye dunia hii ukiwafuatilia ni kwamba waliambatana na watu sahihi ambao waliwasaidia na kuwaonyesha njia sahihi za kufanikiwa hata kama walikutana na changamoto bado marafiki hao hao waliwabeba na kuhakikisha wamefika kwenye ndoto zao.

    Mara nyingi ni bora kubaki mwenyewe na Mungu wako kwenye safari ya ndoto yako kuliko kuambatana na marafiki wabovu wasioelekea kule unakoelekea wewe.

    Hapa mna njia nne za kujua kama una tabia hii ya kuambatana na marafiki wabovu.

    1. Muda wote unakuwa nao, wao ndio maamuzi wenye maamuzi juu ya maisha yako na siyo wewe.
    2. Unawasikiliza kwa kila kitu hata uwe ushauri mbaya utawasikiliza tu.
    3. Unaamini zaidi kwenye matendo yao.
    4. Unawapa kipaumbele kwa kila kitu, hata ukipata hela watu wa kwanza kujua ni hao marafiki zako.

    Rafiki kitu cha muhimu sana cha kukusaidia kutoka kwenye tabia hii ni kuamua kutoka, unapoamua inakupa nguvu ya kutoka kwao .

    Pili, ni kuanza kujitoa taratibu kwa marafiki wenye tabia zisizofaa.

    Chukua hatua jijengee tabia ya kukaa na watu bora na sahihi ili uweze kufika kwenye ndoto yako.

    Ukiona inakushinda sana Muombe Mungu akutenge na watu ambao siyo sahihi juu ya ndoto yako na akupe watu sahihi juu ya ndoto yako utaona urahisi na uwepesi kwenye safari ya ndoto na utafanikiwa hata kama usipofika kabisa kwenye mafanikio basi utakuwa karibu na mafanikio yako.

    Usishangae mara kuona yanatokea mambo kama haya, mara hawakutafuti tena, mara unazuka tu ugomvi mnagombana na mnaachana, mara wanaanza kukusema vibaya na kukuona wa hali ya chini kuliko wao, tafadhali usijiskie vibaya kwa wakati huo tambua uko kwenye kipindi cha mpito na upo karibu sana kukutana na watu sahihi.

    Marafiki watakujenga au watakubomoa ni jukumu lako kuchagua watu sahihi juu ya ndoto yako.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya Kujua Kuwa Una Tabia Mabaya Ya Matumizi Ya Muda.

    Rafiki yangu mpendwa kuna msemo unaosena hivi time is money ikiwa na maana kwamba muda ni pesa.

    Muda ni moja ya rasilimali kubwa sana kwenye maisha ya mwanadamu katika safari ya kufika kwenye ndoto zako ukilinganisha na rasilimali nyingine, kwa sababu muda ukipita umepita, muda huwa haurudi nyuma ni kama mto ukishuka umeshuka haupandi.

    Rasilimali nyingine unaweza kuzitafuta kama fedha au watu na zikapatikana lakini muda siyo kitu cha kutafuta kikishapotea.

    Njia ya kujua kwamba una tabia ya matumizi mabaya ya muda.

    1. Hujali muda kabisa. Muda wako unaweza kutumika tu hovyo bila kujali ni nini kitatokea badala ya muda huo kupotea.
    2. Kuruhusu kila mtu kutumia muda wako wote. Ni ile ukipigiwa simu na mtu yeyote bila ratiba yeyote basi unafuata chenye anataka yeye ufanye.
    3. Kushinda kwenye mitandano ya kijamii hasa kwenye page za udaku. Simaanishi mitandao ni mbaya bali matumizi yake yakoje kwako? Huna muda maaalum ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii, na hata ukiingia huna kitu maaalum unachokitafuta ili ujifunze kwa siku hiyo.
    4. Malengo yako na mipango yako hayana muda maalum wa kuyatekeleza.

    Tabia hii ukiiendekeza sana utajikuta ni yule kijana ambaye muda wote unajisemea ningejua ningefanya hivi, ningejua nisingewapa watu muda wangu, ningejua muda niliopoteza na watu ningewekeza kwenye biashara.

    Unabaki na majuto ndani yako. Njia za kutoka kwenye majuto haya ni kama yafuatayo ;

    1. Panga siku yako kabla hujaanza.
    2. Pangilia kila ratiba zako na muda wake.
    3. Malengo yako ya mwaka mzima yaweke kwenye muda maalum wa kuyatimiza.
    4. Si kila mtu ni wa kuonana naye kila wakati.
    5. Punguza matumizi yako ya simu nikimaanisha muda wa kukaa mtandaoni.

    Chukua hatua ; rafiki usikubali yeyote yule akaupoteza muda wako iwe ni mtaani, kazini, kwenye biashara zako na kwenye mahuasino yako.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya Kubadili Ulivyo jifunza.

    Rafiki yangu mpendwa kuna mambo mengi uliyojifunza siku za nyuma ambayo kwa sasa siyo sahihi tena. Muda unakwenda kasi na mambo yanabadilika.

    Imani zilizokuwa sahihi huko nyuma sasa siyo sahihi tena. Njia zilizokuwa sahihi na nzuri uko nyuma kwa sasa siyo sahihi tena. Kuendelea kung’ang’ana na mambo ya nyuma, kwa sababu tu yalikuwa na manufaa kwa wakati huo siyo sahihi.

    Unapaswa ufike mahali na kubadili yale uliyojifunza. Uondoe yale yaliyopitwa na wakati na ambayo kwa sasa siyo sahihi tena na uweke ambayo yanakwenda na wakati na ni sahihi kwa wakati huu.

    Kilichokufikisha hapo ulipo sasa siyo kitakachokufikisha mbele zaidi. Hivyo mara zote kuwa tayari kujifunza vizuri vipya na kuboresha zaidi.

    Ili kukamilisha hilo, unapaswa kufuata hatua hizi tatu;

    1. Kuwa na mashaka na kile unachojua, usijipe uhakika kwenye kitu chochote.
    2. Acha tabia ya kujiambia tayari unajua kitu, kuwa tayari kujifunza upya, hata kama tayari unajua.
    3. Kwa kila unachojua tafuta uthibitisho kwamba bado ni sahihi mpaka sasa. Kama siyo sahihi kibadili.

    Chukua hatua, kama huendelei kujifunza kila siku, tena kwa makusudi kabisa, hutaweza kukua na badala yake utakuwa unarudi nyuma.

    Dunia inakwenda kasi, kuweza kwenda nayo kasi lazima uwe tayari kuacha vile uliyojifunza huko nyuma na kujifunza vipya zaidi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya Kujua Kama Una Tabia Ya Kuonewa Huruma.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini tabia hii ni kama imekuwa sugu sana kwa baadhi ya watu.

    Tabia ya kutaka kuonewa onewa huruma ni tabia inayouwa uwezo wa mtu wa ndani nikimaanisha uwezo wa kuwaza mambo kwa ukubwa na upana zaidi.

    Uwezo wa kutatua na kutafuta suluhu za changamoto zinajitokeza, uwezo wa kufikiria kesho itakuaje na na mengine yanayofanana nayo.

    Njia za kujua una tabia hii ni kama;

    1. Ukipatwa na tatizo kidogo tu, unataka kila mtu ajue na waanze kulifanyia kazi wao siyo wewe.
    2. Unakuwa ni mtu wa kukuza jambo, hata kama ni jambo dogo la kawaida tu la kutatulika basi unalikuza na kutaka kila mtu akuonee huruma.
    3. Unakuwa ni mtu wa kujielezea sana matatizo yako na mapito yako kwa watu kuliko kuelezea ni namna gani unataka kupiga hatua ili uweze kufika kwenye ndoto yako.
    4. Ukionyeshwa fursa yoyote ile ambayo itakusaidia kupata kipato basi unataka upewe na mtaji.

    Tabia ya kuonewa huruma itaua uwezo wako wa kufikiri na kutatua changamoto, na itakuzuia sana kufika kwenye ndoto zako.

    Chukua hatua, jikubali kwamba unaweza kufanikiwa kwenye ndoto yako, jikubali kwamba una uwezo mkubwa ndani yako, usijidharau.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 5 Ya Kuangalia Ili Kujua Kama Una Tabia Ya Uvivu.

    Rafi yangu mpendwa uvivu ni tabia ambayo mtu anajijengea tu yeye mwenyewe siyo kwamba anazaliwa nayo. Anajitengenezea bila yeye kujua ya kwamba anajitengenezea tabia ambayo itaua kabisa ndoto zake.

    Yafuatayo ni mambo matano ya kuangalia ili kujua kama una tabia hiii.

    1. Mpangilio wako wa muda kwa siku nzima. Kuanzia kwenye kuamka, mpangilio wa ratiba zako za siku mzima. Watu wenye maono makubwa hufuatilia ratiba zao bila kuacha kufanya yale wanayopanga. Lakini wenye uvivu hawana ratiba yoyote ile, wanaamka saa yoyote tu na kufanya mambo tu bila mipango.
    2. Utendaji wako wa kazi zako za kila siku siyo wa kuridhisha.
    3. Hujishulishi kkwa chochote kile ambacho kitakusaidia wewe kufika kwenye ndoto yako, unasubiri misaada.
    4. Una malalamiko kila kukicha. Utamlalamikia mzazi, serikali, mwajiri au boss,mwenzio au mpenzi, mchumba wako.
    5. Huwazi cchochote juu ya kesho yako. Hii kwa lugha nyingine mtu anasema bora maisha yaende, maisha ni haya haya tu, hakuna maisha mengine.

    Ikiwa uunataka kujikwamua kutoka kwenye tabia hii ya uvivu, anza leo kujijengea tabia ya kufanya mambo yako kwa bidii hata kama ni jambo dogo sana, wewe lifanye kwa bidii, hii litakusaidia sana kufika kwenye mafanikio makubwa.

    Kama una ndoto kubwa ifanyie kazi kwa bidii bila kukata tamaa na bila kuangalia ni nani anafurahia au nani hafurarahii ndoto yako.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Tabia 4 Za Kujua Kama Una Tabia Ya Ughairishaji Mambo.

    Rafiki yangu tabia ya ughairishaji mambo ni tabia ambayo inapelekea mafanikio ya mtu kuishia njiani au kufa kabisa, watu wenye tabia hii ni watu ambao huwa wanaanza upya kila siku mambo yao hawana muendelezo wa mambo waliyoyaanza.

    Mtu kama huyu ni ngumu sana kumkuta amepiga hatua kwenye malengo yake na siyo kwamba hana muda kabisa au rasilimali fedha na watu la hasha ni tabia ambayo amejijengea yeye mwenyewe pasipo kujua inamvuta nyuma asiweze kufika kwenye ndoto zake.

    Utajuaje una tabia hiii, yafuatayo ni mambo manne yatakayotusaidia kujua.

    1. Kila kitu unakiona hakiwezekani.

    2. Husimamii vilivyo kile ulichozungumza na kukipangilia.

    3. Ukitengwa na marafiki zako, basi mipango yako nayo unaacha kufuatilia unaanza kutafuta kwa nini wamekutenga.

    4. Unakuwa ni mtu wa kukuza changamoto sana. Ukiumwa kidogo tu hata kama ni mafua basi unaanza unakuza ugonjwa, unaghairisha mipango yako yote.

    Chukua hatua; rafiki weka tabia ya kuhakiksha kila jambo ulilolipanga unalifanikisha kwa wakati hata kama itatokea changamoto wewe pambana mpaka ulikamilishe.

    Makala haya nimeandika kwa ajili yangu na wewe pia rafiki yangu ambaye una tabia hii pia.

    Naahidi kubadilika kwa kuchukua hatua haraka bila kughairisha mambo.

    Asante.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mbinu 5 Ya Kulinda Fikra Zako.

    Rafiki yangu mpendwa kulinda fikra zako ni hatua muhimu kwa afya ya akili na ustawi wa kiroho.

    Hapa kuna mbinu mbalimbali za kulinda nakustawisha fikra zako.

    1. Kuchuja taarifa unazopokea. Kwa kuepuka taarifa hasi nyingi, jaribu kuepuka habari ambazo zinaeneza hofu.
    2. Fanya mazoezi ya akili. Unafannya hivyo kwa kusoma vitabu vya kujenga. Na pia fanya mazoezi ya kutatua matatizo kwa kufanya hivyo itaboresha uwezo wako wa kufikiri kwa kina na kuimarisha akili yako.
    3. Kuweka mipaka ya mawasiliano . Epuka watu wenye mawazo hasi. Zingatia kuwa na watu wenye mawazo chanya.
    4. Kutafakari. Fanya mazoezi ya kutafakari ili kujifunza jinsi ya kudhibiti mawazo yako na kutuliza akili. Itakusaidia kuzingatia mambo muhimu na kupunguza msongo wa mawazo.
    5. Jifunze kitu kipya kila siku. Kutafuta maarifa mapya kupitia kujifunza lugha mpya, kuchukua kozi au kuchunguza mada mpya kutasaidia kulinda fikra zako.

    Kuchukua hatua, kwa kutumia mbinu hizi, unaweza kuimarisha uwezo wako wa kudhibiti fikra zako, kuepuka msongo wa mawazo, na kuishi maisha yenye amani na uwazi wa kifikra.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei

  • Kwa Nini Hufai Kuahirisha NdotoZako?

    Rafiki yangu mpendwa kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake. Kuna picha ambayo kila mtu anayo ya namna maisha yako yanataka yawe.

    Lakini kwa bahati mbaya sana, wengi wamekuwa wakiahirisha ndoto zao kila wakati.

    Wakijua kabisa wanapaswa kufanya nini, lakini wanaahirisha na kujiambia hawajawa tayari au muda bado.

    Tunajua jinsi ambavyo hatuna muda wa uhakika hapa duniani. Na tunajua jinsi wengi wanavyokuja kujuta maisha yao yanapofika ukingoni.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini hatupaswi kuwa hivyo, hatupaswi kuwa watu wa kuahirisha ndoto zetu. Badala yake tuzitekeleze ndoto zetu kama tunavyoziona kwenye akili zetu.

    Hata kama wengine hawatatuelewa, tufanye kile tunachojua ni sahihi, maana kama ni majuto sisi wenyewe tutayapata.

    Kwani muda tulionao ndiyo huu, hakuna wakati tutakuwa tayari zaidi ya tulivyo sasa.

    Hatua ya kuchukua; rafiki anza kuishi ndoto zako sasa, kwa pale ulipo na kwa kile ulichonacho sasa. Hiyo ndiyo njia ya kuishi maisha kamilifu kwako.

    rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo Ambayo Nimejifunza Mwezi Huu Wa Tisa Kuhusu Utajiri.

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana nikushirikishe yale ambayo nimejifunza mwezi huu wa tisa kuhusu kujenga utajiri na Doctor Kocha Makirita Amani.

    Jambo la kwanza ni kujua tatizo ambalo watu wengi wanalo na wapo tayari kulipia kutatua.

    Jambo la pili ni kutatua matatizo kwa uhakika kiasi cha kila mwenye nalo kutaka suluhisho hilo.

    Jambo la tatu weka kazi hiyo kwa muda mrefu na msimamo bila kuacha.

    Hatua ya kuchukua ni kwamba naenda kufanya hivyo kwa uhakika na nitapata chochote ninachotoka.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM