-
Sheria 20 Za Ukamilishaji Wa Mauzo Na Grant Gardone.
Rafiki yangu mpendwa leo tunajifunza sheria 20 za kukamilisha mauzo ili tuweze kufanya mauzo makubwa kwenye biashara zetu.
1.Kamilisha na jadiliana ukiwa umekaa.
2.Wasilisha mapendekezo yako kwa maandishi.
3.kuwa na uasilishaji unaoeleweka.
4.Waangalie machoni.
5.Mara zote kuwa na kalamu.
6.Tumia vichekesho kupunguza shinikizo.
7.Mara zote uliza zaidi.
8.kuwa na silaha nyingi za uwasilishaji ili usirudie zile zile.
9.Tumia mda mwingi na mteja.
10.Mchukulie kila mteja ni mnunuaji.
11.Mara zote jua mtafika makubaliano.
12.Mara zote kuwa chanya bila kujali mteja anakujibu nini.
13.Mara zote kuwa na tabasamu.
14.Wachukulie wateja wanaweza.
15.Watambue na kuwasifia wateja.
16.Mara zote kalibiana na mteja usipingane nae.
17.Mara zote tafuta suluhisho.
18.Jali sana kiasi cha kukataa kutokukamilisha.
19.Tumia silaha zote za ukamilishaji.
20.Mara zote jua hakuna kitakacho tokea kama mauzo hayajakamilishwa.
Chukua hatua; tunapaswa kutumia hizi njia zote za ukamilishaji ili tuweze kukamilisha mauzo.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen32@gmail.com
-
Matatizo 2 Makubwa Kwenye Zama Tunazoishi.
Rafiki yangu mpendwa bila shaka una hamu kubwa sana siku ya leo kutaka kujua matatizo hayo yanayokumba watu wengi kwenye zama hizi ni nini haswa! Karibu tujifunze.
Tatizo la kwanza ni watu kuishi kwa mazoea na kufuata mkumbo. Kufanya kile ambacho wengine wanafanya na wamezoea kufanya na kusahau upekee ambao upo ndani yao.
Tatizo la pili ni watu kutokujali kile wanachofanya, iwe ni kazi au biashara, watu wanafanya tu kwa mazoea. Hawajitumi na wala hawatoi thamani ya tofauti.
Matatizo hayo mawili yamezalisha kundi kubwa la watu ambao wanahangaika lakini hawapati nada makubwa.
Rafiki hayo ni matatizo ambayo yanawarudisha watu wengi nyuma, sasa ili kuondokana na matatizo hayo ni bora kujaribu kuondokana nayo kwa kuwa wa tofauti na wengine kwa kufanya yaliyo tofauti nao.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen32@gmail.com
-
Siri Kuu Ya Kufanya Makubwa.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye maisha kuna siri ya kufanya makubwa.
Utajiskiaje kama utakuwa unafanya makubwa kwenye maisha yako kila mara unapochukua hatua ya kufanya kitu hicho.
Unaweza ukafanya makubwa kwenye maisha yako kwa kuwa na ndoto kubwa, na kwa kuanza kidogo na kuchukua hatua sasa.
Kabla ya kufanya maamuzi acha kufikiria ukomo au unachokosa na angalia kile ambacho tayari unacho.
Bila ya shaka yoyote rafiki unaweza kufanya makubwa utakavyo, ila kwa kuanza kidogo kidogo na na kwa kuanza sasa
Chukua hatua; rafiki tunapaswa kuwa na ndoto kubwa, kuwa na malengo na mipango ili uweze kutekeleza mambo makubwa kwenye maisha yako na kwa kuanza sasa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen32@gmail.com
-
Mambo 15 Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Nidhamu Ya Kazi Kutoka Kwa Mwandishi Patrick Bet David.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kuzingatia kwenye maisha yetu kama tunataka kuwa na nidhamu ya kazi.
Kwa sababu bila nidhamu ni ngumu sana kutimiza yale ambayo umepanga kufanya.
Ninajua kabisa kuna baadhi ya mambo umekitaka kulibadili kwenye maisha yako.
Kutoka kwa mwandishi Patrick Bet David tunajifunza mambo ya kuzingatia kwenye kujijengea nidhamu ya kazi.
1. Kuwa unayetabirikaKuwafanya watu waweze kunitegemea. Na kuamini kuwa nakwenda kufanya kwa uhakika na ubora.
2. Kuwa na msimamo nafanya hata kama siyaoni matokeo.
3. Kuwa na maandalizi napanga nafanya nini na nifanye mapema.
4. Nifanye zaidi. Naenda hatua ya ziada kwa kufanya zaidi ya nilivyozoea.
5. Kuwa na mtazamo wa kufanya sasa. Naanza kufanya mara moja.
6. Naongozana na watu sahihi. Watu wanaotaka nifike mbali.
7. Nafanya kazi kwa nguvu na akili.
8. Naondokana na usumbufu.
9. Naweka umakini wangu wote kwenye kazi.
10. Nakuwa na orodha vya vitu vyakufanya. Sitoki nje ya orodha.
11. Na kula kwa usahihi. Naepuka vyakula vinavyochosha mwili na kupunguza kasi ya kazi.
12. Kuziba matundu yanayovuja.Vitu ninavyofanya vinavyopoteza muda wangu naachana nayo.
13. Napunguza mambo ninayofanya. Naweka juhudi zangu kwenye mambo machache yenye matokeo makubwa.
14. Naachana na ukamilifu. Naanza kufanya na nitaendelea na ukamilifu baadae.
15. Naepuka uchovu uliopitiliza kwa kuwa na pa kutorokea. Nafanya ninachopenda maana kwa namna iyo nitaepuka uchoshi mwingi.
Naimarisha nidhamu yangu ya kazi kwa kufanyia kazi hayo ninayojifunza. Kazi ndiye rafiki ya kweli ambaye hawezi kunitupa kwa namna yoyote ile.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Mambo 10 Ambayo Nimejifunza Kuhusu Ustoa.
Rafiki yangu karibu tujifunze leo kuhusu ustoa na yale tunayopaswa kufanya ili tuishi kama wastoa, karibu sana.
Yafuatayo ni mambo kumi ambayo Nimejifunza;
- Kila siku tunapoamka, tunapaswa kutambua kwamba tutaonana na watu wabaya, wasio na shukrani, na wenye chuki na hasira. Tunapaswa kuwa na huruma kwao na kujiandaa kiakili kwa changamoto na tabia mbaya zao kabla ya kuanza siku yetu.
- Katika maisha tutakutana na watu wenye tabia mbaya watu wenye wivu, chuki, ulaghai, au wasio na heshima. Tunapokutana na watu wa aina hii, ni bora tuwajibu kwa busara na utulivu, tukiwa na huruma kwa udhaifu wao, na kulinda amani yetu ya ndani kwa kutofanya hisia zao kuwa sehemu ya maisha yetu.
- Kila mtu ana kusudi lake la kipekee katika maisha. Kutambua nafasi yetu na kuishi kwa mujibu wa asili yetu, bila kujaribu kuiga wengine.
- Muda tulionao una ukomo na hatujui utakwisha lini. Tunapaswa kutenda sasa bila kuchelewa au kungoja wakati mwingine.
- Mabadiliko ni sehemu ya maisha, ni fursa za kujifunza na kukua, hatupaswi kuogopa wala kuyakataa. Kama vile asili inavyobadilika, nasi tunapaswa kubadilika bila kulalamika au kupinga.
- Kuwa na umakini katika malengo yetu wenyewe, kuwa na uvumilivu na kutokupoteza mwelekeo kwa sababu ya kujilinganisha au kuingilia njia za watu wengine. Maisha yetu yanatakiwa kuwa na maana inayotokana na malengo yetu ya ndani, si kwa kuangalia kile ambacho wengine wamekifanikisha au kukifanya.
- Kuwa na uhuru wa ndani wa kufanya maamuzi kulingana na maadili na malengo yetu, badala ya kuongozwa na matarajio au maoni ya watu wengine. Maoni ya nje yanaweza kuwa na thamani, lakini hayapaswi kuwa kipimo cha maisha yetu au maamuzi yetu.
- Maadili yetu ni mwongozo wetu wa ndani wa maisha, na tunapaswa kuyashikilia hata wakati hali zinapokuwa ngumu zaidi. Mambo ya nje yanaweza kubadilika, lakini dhamira yetu ya kuishi kwa haki, uaminifu, na nidhamu haipaswi kubadilika.
- Kujikumbusha kila mara kwamba maisha ni mafupi, na hatupaswi kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi, tunapaswa kuzingatia vitu vya maana tu.
- Kuna mambo mengi katika maisha ambayo yako nje ya uwezo wetu. Hatuwezi kudhibiti kila kitu, tunachoweza kudhibiti ni mtazamo wetu na namna tunavyokabiliana navyo.
Kabla ya kufanya maamuzi, rafiki tunapaswa kuchukua hatua baada ya kujifunza mambo hayo kumi na tutaweza kuishi kama wastoa kwenye zama hizi tunazoishi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Yele Nimejifunza Kuhusu Ustoa.
Rafiki yangu mpendwa karibu sana, leo tunajifunza jinsi ya kuishi kama mstoa, yafuatayo ni mambo kumi ambayo nimeondoka nayo.
1.Kuonesha shukrani kwa kila mtu, kwa yale mazuri ninayopata kutoka kwao.
2. Kuwa kiongozi mwenye busara, mwenye maamuzi mazuri, asiye na haraka, na mwenye kuishi kwa uadilifu.
3. Nidhamu ni siri ya mafanikio haijalishi mazingira ni magumu kiasi gani, nidhamu inaweka msingi wa uthabiti wa kibinafsi.
4. Unyenyekevu ni nguzo ya ukuu. Sifa na utukufu hazipaswi kuwa malengo, bali matokeo baada ya kufanya kazi nzuri.
5. Watu wa karibu wanatujenga au kutuharibu. Kila mmoja ana chembe ya hekima iliyo tofauti, inafaa kuwa na watu walio sahihi kwetu.
6. Hasira ni silaha inayoweza kutuharibu sisi zaidi kuliko watu tunaowakasirikia. Kutawala hisia na kuwa na utulivu wa ndani.
7. Kuwa na shukrani kwa vipawa tulivyonavyo na kutochukulia vya kawaida.
8. Kila mtu anastahili heshima na haki. Hakuna mtu yeyote mwenye sifa ya kudharaulika.
9. Maisha hayana maana bila kumcha Mungu na kufuata amri zake. Kumcha Mungu ni kiini cha utakatifu wa maisha.
10. Maisha bila malengo ni kama meli isiyo na usukani. Kuweka malengo thabiti na kufanya kila juhudi kufikia kile ambacho kitanifanya niwe mimi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
-
Jinsi Ya Kuepuka Kuwa Kama Punda.
Rafiki yangu mpendwa Punda akiwekewa nyasi upande mmoja na maji upande wa pili, anajikuta njia panda. Anakuwa anataka ale nyasi na pia anywe maji.
Hivyo atabaki hapo akiangalia ni jinsi gani anaweza kupata vyote kwa pamoja.
Kinachotokea ni anajikuta anakufa kwa njaa na kiu wakati amezungukwa na nyasi na maji.
Ambacho punda anashindwa kujua ni kwamba, japo hawezi kufanya vyote kwa pamoja, anaweza kuanza na kimoja kisha kwenda kwenye nyingine.
Kabla hujamshangaa punda kwa kufa na njaa huku akiwa na nyasi, hebu rudi kwako, ni fursa ngapi nzuri zimekuzunguka? Na je, katika fursa hizo ni ngapi unazifanyia kazi?
Watu wengi hasa kwenye zama hizi za mafuriko ya fursa wanajikuta hawafanyi chochote. Wanafursa tano mbele yao na wanataka kuzifanyia kazi zote, kitu ambacho hakiwezekani, hivyo wanaishia kutokufanya chochote.
Suluhisho kwenye hali hiyo ni rahisi ni wewe kuchagua fursa moja na ifanyie kazi mpaka itakapokamilika, kisha nenda kwenye fursa nyingine.
Hata kama una fursa tano mbele yako, ukiipa kila fursa miaka mitano ya kufanyia kazi kwa uhakika, utapiga hatua kubwa kuliko kusubiri mpaka uweze kufanyia kazi zote kwa pamoja.
Chukua hatua, katika fursa zote zinazokuzunguka, chagua moja utakayoifanyia kazi kwa uhakika na kusema hapana kwa nyingine mpaka utakapoikamilisha hiyo. Kisha nenda kwenye fursa nyingine kwa mpango huo huo.
Muda utakwenda iwe utachukua hatua au la. Hivyo badala ya kupoteza muda, chukua hatua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Maadili 13 Ya Benjamin Franklin.
Rafiki yangu mpendwa bila shaka leo tunajifunza maadili 13 aliyochagua kuyaishi na kujipima nayo. Marafiki mambo hayo ni kama yafuatayo;
- Ujasiri. Kuwa makini kwenye vyakula na vinywaji.
- Ukimya. Kuepuka mazungumzo yasiyo na maana na kuepuka kutumia maneno machafu.
- Mpangilio. Kila kitu kifanyike kwa mpangilio mzuri.
- Maamuzi. Fanya ulichoahidi bila kuhairisha.
- Ubahili. Kuwa makini na matumizi yako na epuka ubotevu.
- Kazi. Tumia muda wako vizuri na epuka kufanya mambo yasiyo na umuhimu.
- Ukweli. Usidanganye yeyote na kuwa mkweli kwako mara zote.
- Haki. Watendee watu kwa usawa na mara zote fanya kilicho sahihi.
- Kiasi. Epuka kuzidisha chochote kile, kiwe kizuri au kibaya.
- Usafi. Uweke mwili wako, makazi yako na mazingira yako kwenye hali ya usafi.
- Utulivu. Kuwa na amani ya ndani na usisumbuke na vitu vidogo vidogo.
- Uadilifu. Usijihusishe na zinaa.
- Unyenyekevu. Waige wale waliofanya makubwa hapa duniani.
Ili kuhakiksha anayaishi maadili hata 13, Franklin alichagua kuyageuza kuwa tabia kwake. Maana tabia Ina nguvu kuliko kipaji au maamuzi.
Alitengeneza chati ya kujipima kila siku na kabla ya kulala alijitathmini jinsi alivyoishi maadili hayo kwenye siku husika.
Rafiki hapa tunajifunza mambo makubwa mawili;
Moja ni kuwa na maadili ambayo mtu unasimamia na kujipima nayo kwenye maisha yako.
Mbili ni kuyageuza maadili hayo kuwa tabia kwa kujifanyia tathmini kila siku na kurekebisha pale unapokosea.
Chukua hatua, rafiki tunapaswa kufanyia kazi maadili hayo ambayo tumejifunza kutoka kwa muuzaji bora kuwahi kutokea Benjamin Franklin.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Njia Bora 3 Ya Kuboresha Kumbukumbu Zako.
Kwanza, inaboresha msisimko wako wa akili. Kubadilisha utaratibu wako kunahitaji ufanye ubongo wako ufanye kazi, ambayo husaidia kufanya mazoezi ya ubongo wako.
Kujaribu mambo mapya na kubadili unachofanya, hata kitu rahisi kama kutengeneza kichocheo kipya au kujifunza ujuzi mpya. Kinahusishwa na viwango vya juu vya uwezo wa utambuzi maishani.
Ina nguvu sana hivi kiasi kwamba inauupa akili changamoto kwa shughuli mpya mapema maishani kunaweza kusaidia kulinda ubongo dhidi ya hasara ya utambuzi wakati wa uzee.
Pili, inasaidia kurudisha ubongo wako. Ikiwa unafanya mambo yale yale mara kwa mara, huupi mwili na akili yako fursa ya kupingwa.
Kufanya mazoezi ya akili yako kila siku na kuipa fursa mpya za kutatua matatizo mapya huusaidia kufanya ubongo wako kuwa na msisimko na changamoto wa kuboresha kumbukumbu.
Tatu, inakufanya ujiskie furaha zaidi. Sio tu kwamba kutofautiana kwa utaratibu wako kunaboresha afya yako ya utambuzi, lakini pia utajiskia furaha kuhusu hilo.
Watafiti katika utafiti mmoja waligundua kuwa, watu huwa na furaha zaidi wanapoachana na shughuli zao za kila siku na kujipa maeneo mapya na uzoefu mpya wa kuchunguza.
Hata mabadiliko madogo zaidi katika utendaji wako wa kimwili yanaweza kukufanya uwe na furaha na kunufaisha akili yako.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.
-
Uwekezaji Bora Kufanya Kwenye Maisha.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini uwekezaji bora kabisa unaoweza kufanya kwenye maisha yako, tena ambao hautakugharimu sana ni kwenye vitabu.
Kwa gharama ndogo sana utaweza kununua uzoefu wa watu walioishi miaka mingi na kufanya makubwa.
Hivyoo kila unapopata nafasi, fanya uwekezaji huu, nunua vitabu vingi kuliko hata unavyoweza kuvisoma.
Na katika usomaji wa vitabu, jua havifanani. Kuna vitabu utasoma mara moja tu. Halafu kuna vitabu utarudia kuvisoma mara nyingi.
Kwa vitabu vichache bora na unavyochagua kurudia kuvisoma mara nyingi, nunua nakala nyingi za kitabu husika.
Hilo litakuwezesha kuwa na kitabu hicho wakati wote lakini pia utaweza kuwapa wengine kitabu hicho kama zawadi.
Robin kwenye kitabu chake cha (everyday manifesto) anatuambia huwa ana makala mpaka 40 za kitabu kimoja.
Unaporudia kusoma kitabu bora, unajifunza vitu vipya ambavyo utajifunza vitu vipya ambavyo hukujifunza wakati unasoma mwanzo.
Kwa sababu umekuwa mtu mpya na hivyo uelewa wako unabadilika pia.
Chukua hatua, wekeza sana kwenye vitabu na chagua vitabu vichache ambavyo utakuwa unarudia kuvisoma mara kwa mara.
Rafiki yako,
Maurwen Kemei .