-
41/100.Baadhi ya tamaduni ni bora kuliko wengine.
Karibu, katika uendelezo wa kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Leo tupo changamoto ya nane kati ya 21 ambayo mwandishi ametushirikisha,ambayo inahusu uhamiaji changamoto nyingine kubwa sana katika karne hii.
Tangu enzi na enzi, kumekuwa na mwingiliano baina ya jamii, watu kutoka eneo moja kuhamia eneo jingine. Na mwingiliano huo ndiyo ulioweza kusambaza maarifa na ujuzi katika jamii hizo.
Katika karne ya 21, uhamiaji umekuwa changamoto, baadhi ya mataifa yamekuwa yanaogopa kupokea wahamiaji kutoa kwenye mataifa mengine, wakiamini wahamiaji hao wanaenda kufurahia matunda ya wenzao huku wao wakiwa wameshindwa kutengeneza mazingira bora kwenye nchi zao.
Wale wanaozuiwa kuingia kwenye mataifa wanayotaka kuhamia nao wanayalaumu mataifa hayo kwa ubaguzi wa rangi au dini. Na sehemu kubwa ya watu wanafikiri changamoto kwenye uhamiaji ni rangi au dini. Lakini changamoto kubwa ipo kwenye utamaduni.
Tafiti zote za kisayansi zimeonesha kwamba tofauti yoyote ya kibaolojia baina ya mtu mweusi na mtu mweupe, au mtu wa dini moja na mtu wa dini nyingine. Hivyo tunachotofautiana watu ni utamaduni ambao umejengwa ndani yetu. Tabia tulizonazo ni matokeo ya yale ambayo tumekuwa tunafundishwa na kusisitiziwa tangu tukiwa wadogo.
Hivyo tunapoangalia eneo la uhamiaji, tujue tunasumbuka na utamaduni na siyo rangi wala dini. Pia lazima tukubali kwamba tamaduni zinatofautiana na kila utamaduni una mambo mazuri na mabaya.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com
-
40/100. Mungu anatumikia taifa.
Karibu, katika kujifunza kwetu kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Tumejifunza na kufahamu baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo katika zama hizi. Leo tunajifunza kuhusu uwepo katika mataifa.
Kwa kipindi kirefu dini zimekuwa na nguvu kubwa Sana kwenye jamii. Katika zama zilizopita dini na serikali zilikuwa kitu kimoja, viongozi wa dini ndiyo waliokuwa wakileta utatuzi na suluhisho la changamoto mbalimbali ambazo watu walikuwa wanapitia. Kama mvua hazikunyesha basi viongozi wa dini walifanya ibada au kutoa kafara na miungu ikajibu kwa kunyesha mvua.
Lakini katika karne ya 21 dini zimepoteza nguvu hiyo ya kutatua changamoto kubwa za kijamii. Lakini bado dini zimebaki na nguvu kubwa ya kuweza kuwaleta watu Pamoja. Watu wana imani kali kwenye dini na wengi wapo tayari kufanya chochote kwa jina la dini zao.
Watu hufanya hata uhalifu kwa kwa kisingizio kutetea dini zao. Kwa sasa mataifa yanayotaka kujitenga yanatumia nguvu ya dini katika kuwaleta watu pamoja. Hivyo dini zinakuwa chombo cha mataifa kuimarisha nguvu zao
Katika karne hii lazima tuelewe kwamba matatizo makubwa tunayokutana nayo hayawezi kupata majibu kwa kutegemea dini pekee. Lazima tujue kwamba kujitenga kwa mataifa kwa mwavuli wa dini kutazidi kutengeneza matatizo makubwa duniani.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei.
Blog kufikirichanya.wordpress.com.
-
39/100. Matatizo ya kimataifa yanahitaji majibu ya kimataifa.
Karibu, tunajifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Kama tulivyoona kwamba sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na kwa sasa dunia nzima inakuwa kama jamii moja. Hii ni kwa sababu changamoto zinazotukabili dunia kwa Sasa haziwezi kuathiri nchi moja na hakuna nchi moja inayoweza kutatua changamoto hizo.
Changamoto kubwa sasa zinazoweza kuathiri dunia kwa ujumla ni vita ya kinyukila au mabadiliko ya hali ya hewa. Iwapo itatokea vita na silaha za kinyukila kutumika, sehemu kubwa ya dunia itaathirika. Na mabadiliko ya hali ya hewa yana athari kwa sehemu kubwa ya dunia.
Licha ya matatizo haya kuwa ya dunia nzima, miaka ya karibuni tunaona mataifa yakitaka kujitenga na kutojishughulisha na mataifa mengine. Uingereza kujitoa kwenye umoja wa wilaya na hata marekani Kutenga ukuta baina yake na Mexico, hizi ni juhudi za kujenga utaifa, lakini zina madhara kwa dunia.
Changamoto tunazokabiliana nazo ni za kimataifa na zina hitaji majibu ya kimataifa. Utaifa haitakuwa na msaada wa taifa husika wala dunia kwa ujumla. Hivyo ni muhimu ushirikiano baina ya mataifa ukaimarishwe ili kutatua changamoto hizo kwa pamoja.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com
-
39/100. Ustaarabu moja tu duniani.
Karibu, tunaendelea kufahamu changamoto za karne ya 21. Kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Dunia imepitia vipindi tofauti ambapo kila jamii ilikuwa na ustaarabu wake na namna ya kufanya mambo yake. Pia ndani kumekuwa na mgawanyiko wa watu kulingana na dini au makabila yao. Hivyo ndani ya jamii moja bado kulikuwa na ustaarabu wa aina tofaut tofauti.
Lakini karne 21 mambo yamebadilika sana, kuna ustaarabu mmoja tu duniani, na jamii zote zinaishi kwa ustaarabu huo. Na hili limerahisisha mwingiliano baina ya jamii tofauti.
Ukichukulia mfano wa mchezo ya Olympic, ambayo inahusisha nchi zote duniani kinachowezesha michezo hii kuwezekana ni kuwepo kwa ustaarabu ambao unakubalika na kila nchi.
Ukiangalia pia kila nchi ina bendera yake, kila nchi ina wimbo wake wa taifa, kila nchi ina sarafu yake, ambayo inaweza kubadilishwa na sarafu ya nchi nyingine.
Hali hii ya kuwepo kwa ustaarabu mmoja duniani inapelekea pia matatizo yanayotokea kwenye jamii moja kuathiri jamii nyingine.
Hivyo leo tunajifunza kuwa tunapaswa kufikiri namna ambavyo kila tunachokifanya kinavyoathiri wengine pia na siyo kujiangalia sisi wenyewe.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog:kufikirichanya.wordpress.com
-
38/100. Umuhimu wa jumuiya.
Ni katika harakati ya kujifunza zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Yale nimejifunza ni kwamba;
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, tumezoea kuwa sehemu ya jamii kubwa. Kupona kwetu kama binadamu ni kwa sababu tuliishi kama jamii tangu enzi na enzi. Jamii ilikuwa msaada kwa wote, wale wenye nguvu na uwezo na wasiokuwa na nguvu na uwezo.
Katika karne ya 21 tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kuvunjika kwa jumuiya nyingi, kuanzia za watu binafsi mpaka za mataifa au kitaifa. Tumeona baadhi ya mataifa kutaka kuvunjika yaliyokuwa yameungana na wengine kuachana. Baadhi ya mataifa yanataka kugawanyika.
Na katika hali binafsi hali ndiyo mbaya zaidi, ile nafasi ya watu kukutana ana kwa ana kama jamii imepungua sana. Sasa hivi watu wamekuwa wanakutana zaidi mtandaoni. Na hata wanaopata nafasi ya kuwa pamoja. Bado muda mwingi wanatumia kwenye mtandao wa kijamii, badala ya kutumia kwa mazungumzo ya pamoja.
Tunajifunza leo kuwa, tunapaswa kurejea kwenye misingi ya jumuiya, kwa kuimarisha ushirikiano wetu na wengine, hasa wa ana kwa ana. Kwa sababu utegemezi wetu kwenye teknolojia na mtandao wa kijamii umeleta hali ya kutengwa ndani yetu.
Tafiti nyingi kwa Sasa zinaonesha kiwango cha msongo na sonona kinaongezeka kwa wengi kwa kukosa nafasi ya kuwa ana kwa ana na wengine na kutegemea zaidi mtandao ya kijamii.
Tukutane tena kesho ili tufahamu changamoto zingine zinazotukabili zama hizi na namna ya kuzitatua au kuepukana nazo.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na ushauri wa maisha.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com
-
37/100.Anayemiliki taarifa anaimiliki kesho.
Karibu Mwana mafanikio, katika harakati ya kujifunza zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Mwandishi anatukumbusha kwamba, dunia imepitia zama mbalimbali, zama za kilimo waliomiliki ardhi ndiyo waliokuwa watawala na wao walimiliki uchumi pia.
Katika zama za viwanda, waliomiliki viwanda ndiyo waliomiliki uchumi. Na sasa tupo kwenye zama za taarifa, wale wanaomiliki taarifa ndiyo wanaomiliki uchumi na wanaimiliki kesho pia.
Zama hizi za taarifa zinatoa uwezo mkubwa sana kwa yeyote anayemiliki taarifa. Wale wenye taarifa na wanaoweza kuzitumia, wanaweza kupiga hatua zaidi kuliko wasiokuwa na taarifa.
Hivyo tunapaswa kuhakikisha tuna taarifa sahihi na kuzitumia vizuri kupata kile tunachotoka. Pia kudhibiti taarifa zetu binafsi zisiende kwa wale ambao wanaweza kuzitumia vibaya na kutugeuza tuwe watumwa wao.
Mwandishi anatushauri tumiliki kesho yetu kwa kuwa na taarifa muhimu za kile tunachokifanya,na tuepuke sana kutoa taarifa zetu binafsi kwa wengine, hasa mitandao ambayo inakusanya taarifa za watu na kuziuza kwa wanaotangaza bidhaa na huduma mbalimbali.
Tukutane kesho tunapofahamu zaidi changamoto hizi za karne ya 21 na namna ya kuzitatua, katika safar yetu ya mafanikio.
Imeandikwa na mwana mafanikio, mwanafunzi wa ushauri nasaha na mwandishi.
Maureen Kemei
Blog kufikirichanya.wordpress.com
-
36/100. Kufuatiliwa kwa ukaribu kuliko tunavyofikiri.
Karibu, tunazidi kujifunza changamoto zinazotukabili zama hizi, ikiwa leo tunaangazia, changamoto ya kufuatiliwa na wanaomiliki taarifa nyingi za watu. Kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Mwandishi anatusimulia kuwa kipindi cha nyuma wakati wa ukoloni, mataifa makubwa yalikuwa yanapigania kushika ardhi kwenye nchi nyingi. Hili lilizalisha ukoloni.
Anatujuza kuwa kwenye karne hii ya 21, Kuna aina mpya ya harakati kwa mataifa makubwa na hata kampuni kubwa. Makampuni haya yanapigania kupata taarifa za watu, kadiri wanavyokuwa na taarifa nyingi kuhusu mtu na kwa watu wengi, ndivyo inavyoweza kutumia taarifa hizi kusukuma watu kuchukua hatua fulani.
Makampuni makubwa kama google, facebook, Amazon, alibaba, Coca-Cola na mengineyo yapo kwenye harakati kubwa za kukusanya taarifa nyingi za watu. Kwa kadiri wanavyokuwa na taarifa nyingi kuhusu watu ndivyo wanavyowasukuma watumie bidhaa zao. Kadhalika kila taifa linakazana kupata taarifa zaidi za watu wake na hata watu wa mataifa mengine.
Hivyo yafaa tufahamu kwamba, tunafuatiliwa kwa karibu kuliko tunavyofikiri. Tunapoingia mtandaoni na kufanya yale yametupeleka uko. Na tukafanya mambo tofauti, tuijue kuwa kuna mifumo ya kompyuta inayofuatilia sana kuhusu sisi, tunapendelea nini na kadhalika.
Limeshaonekana kuwa, google na facebook zinatujua vizuri kuliko tunavyojijjua. Hali hii ni hatari sana kwa sababu itafika wakati tutaiamini mifumo hii ifanye maamuzi kwa ajili yetu na hapo tutakuwa tumechagua utumwa mbaya sana.
Sasa hivi karibu kila mtu anafanya maamuz kwa kutumia google, kama Kuna kitu unataka kujua, unauliza google. Kama Kuna mahali unataka kwenda lakini hupajui, ukiuliza google unapewa mpaka ramani ya kufika.
Kile tunachotoka nacho leo hii ni kuwa, twapaswa kuwa makini na taarifa tunazotoa kwa mifumo hii. Tunapaswa kuweka nguvu kubwa kwenye kujiendeleza sisi wanadamu, kukuza ufahamu wetu ili tusiishie kuwa na mifumo yenye uwezo mkubwa na wanadamu tunabaki na uwezo mdogo.
Kwani tukifikia hatua hii, tutakuwa tumekubali kuwa watumwa kwa vitu tulivyotengeneza sisi wenyewe.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog ;kufikirichanya.wordpress.com
-
36/100. Somo la tatu, unafuatiliwa kwa karibu kuliko unavyofikiri.
-
35/100.Utakapokua huenda usiwe na kazi.
Karibu sana tujifunze zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Zama zilizopita mtu alikuwa anapata kazi moja na kudumu nayo maisha yake yote. Hii ni kwa sababu mabadiliko yalikuwa yanatokea kwa kazi ndogo sana hivyo wengi waliweza kudumu na kazi moja maisha yao yote. Na msukumo mkubwa ukawa kwenye kusoma na kuwa na taaluma ambayo itakuwezesha kuwa na Kazi ya maisha.
Lakini katika karne hii ya 21, mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa mno,kazi nyingi zinapotea kila siku. Mifumo mipya ya teknolojia ya habari inaondoa uhitaji wa watu wengi kwenye kazi. Hivyo wazo la kuwa na Kazi ya maisha halipo tena. Maroboti yanaonekana kuchukua kila aina ya kazi ambazo zinafanywa na watu.
Njia pekee ya kukabiliana na hili ni kuwa tayari kubadilika kila wakati, kutokuishi na kufanya kazi kwa mazoea. Badala yake kujua mabadiliko yanaelekea wapi na kisha kuwa mbele ya mabadiliko hayo.
Angalia kama kazi au biashara unayofanya sasa inaathiriwa na mabadiliko yanayoendelea kwenye teknolojia ya habari na baiolojia, kisha chukua hatua mapema.
Mfano mzuri ni kwenye biashara ya taksi, wapo watu ambao wamekuwa kwenye biashara hii kwa muda mrefu, ikaja huduma au uba ambayo inamwezesha kila mtu kutoa huduma ya usafiri wa teksi, hii ikaathiri sana wale waliotegemea hii kama biashara yao kuu.
Sasa ambacho kitaleta athari kubwa zaidi ni pale magari yanayojiendesha yenyewe yatakapokuwa yanatoa huduma za teksi, hakutahitajika kabisa uwepo wa dereva. Kwa taarifa yako, tayari yapo magari yanayojiendesha yenyewe.
Huu ni upande mmoja tu wa kazi ya udereva lakini kila kazi inaathiriwa na mabadiliko makubwa yanayotokea. Mfano mpaka operesheni kwenye miili ya binadamu kubwa zinaweza kufanya na maroboti na umakini mkubwa kuliko zinavyofanywa na madaktari wanadamu.
Tunapata funzo leo kwamba tusing’ang’ane na kazi au biashara tunayofanya sasa, mambo yanabadilika kwa kasi, hivyo inabidi nasi tubadilike pia.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com
-
34/100.ujasiri
Karibu tunaendelea kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Yale nimejifunza ni kwamba:
Binadamu tumezoea kuishi kwa hadithi, kila zama zimekuwa na hadithi zake, zama za kifashisti hadithi ilikuwa nchi yangu ni bora kuliko nyingine.
Zama za kikomunisti nchi yangu inanijali na kunipatia kila ninachotaka. Zama za huria hadithi imekuwa nchi yangu inanipa uhuru wa kuishi nitakavyo.
Sasa hadithi ya huria inapotea na hakuna hadithi mpya ambayo imeshatengenezwa. Mwandishi anatuuliza kwamba, je tunawezaje kuendesha maisha kwa ubora bila ya hadithi ya nje?
Zipo njia tatu ambazo mwandishi ametushirikisha.
Njia ya kwanza ni kuwa tayari kubadilika, kuchukulia maisha kama mabadiliko na kila siku piga hatua kuwa bora zaidi. Usikubali leo iishe ukiwa kama Jana.kumbuka dunia inabadilika kila siku, ili maisha yawe bora lazima na wewe ubadilike kila siku.
Njia ya pili ni kutengeneza maisha yasiyo na hadithi, Mwandishi anasema maisha siyo hadithi, hivyo tuaje kutafuta hadithi ya kuendesha maisha yetu na badala yake tuishi maisha kwa kuyaelewa mateso. Mateso ndiyo kitu kikuu tunakutana nacho kwenye maisha, tukiyaelewa tutakuwa tumeelewa maana ya maisha yetu.
Njia ya tatu ni kufanya tahajudi. Njia pekee ya kuyaelewa mateso na kujielewa sisi wenyewe siyo kwa kufuatilia maisha ya wengine, kufuatilia habari, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii wala kujipa kila aina ya starehe tunayotaka.
Njia pekee ni kujipa muda wa kuangalia namna akili na mawazo yetu yanavyokwenda. Kwa kuangalia na siyo kujaribu kudhibiti. Njia pekee ya kufanya hili ni kwa kutahajudi ili kuweza kuangalia akili inavyokwenda, kuyaelewa mateso na kujielewa wenyewe.
Mpendwa, tunapitia katika kipindi cha mapinduzi makubwa na maisha mapya yanakuja,ambayo yatatikisa kabisa imani yetu na hata msimamo.
Tunapaswa kuwa imara ili tuweze kustawi katika nyakati hizi za mapinduzi. Tufanyie kazi haya tunayojifunza ili mabadiliko yanayotokea yasituache nyuma.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Akupendaye ;
Maureen Kemei.
Blog kufikirichanya.wordpress.com