-
Nini maana ya kuwa na fikra chanya.
Karibu rafiki mpendwa, leo tunajifunza somo nzuri kabisa ambayo itachangia kwa namna nyingine katika safari ya kufikia mafanikio makubwa.
Fikra chanya ni ile hali ya kutumia ugumu wowote unaopitia mtu, au kuchagua tu kuwa na mtazamo bora kwenye kila nyanja ya maisha.
Kuwa na fikra chanya inaanzia kwa kujinenea mazuri au kujitamkia matamshi ya ushindi wakati wote. Licha ya kwamba unaweza kuwa unapitia changamoto ya kukatisha tamaa kabisa.
Lakini unadhamiria kabisa kuwa na mtazamo chanya, kuamua kutupilia mbali maneno hasi. Kuna mambo mengi ya kutosha inayoweza kukukwaza tu, lakini unapoamua kuwa chanya, utaona ni mambo madogo mno.
Hivyo rafiki yangu yatosha leo kuchukua hatua ya kuamua kuwa na mtazamo chanya katika kila hali. Lakini kuwa na mtazamo chanya haitoshi, lazima kuwajibika zaidi kwa malengo na mipango yatakayokufikisha kwenye mafanikio unayotaka.
Nikutakie usiku mwema tukutane kesho, ni mimi wako anayekujali sana.
Mwandishi na mshauri.
Maureen Kemei.
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
59/100. Usiombe msamaha.
Natumai kabisa rafiki umekuwa na siku nzuri ya mafanikio, karibu katika kujifunza kwetu kuhusu mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji. Tunajifunza kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Unaposimama mbele ya wengine usihangaike na kuomba msamaha kwa kitu kidogo ulichokifanya ambacho hakihusiani na mazungumzo unayofanya.
Mfano usianze kwa kuambia watu wakusamehe kwa sauti yako, au mavazi yako au kuchelewa kwako na kadhalika.
Chochote ambacho unawaomba watu wakusamehe ndipo fikra zao zitakapokwenda na hivyo na hivyo kuondoka kwenye mada kuu unayozungumzia.
Na hata wewe utahama kutoka kwenye kufikiria kile unachozungumzia na kufikiria kile ulichoombea msamaha.
Tunajifunza leo kuwa,
Kitu pekee cha kuzingatia ni kile unachosema na na wale ambao unawasemea.
Asante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mshauri na mwandishi.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com.
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
58/100. Usiharakishe.
Habari mpendwa, karibu tuendelee mbele katika kujifunza mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji. Kutoka kitabu chetu pendwa cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Waandishi hawa wanatushirikisha kuwa, tunapozungumza mbele ya wengine, tusiharakishe kuanza wala kumaliza. Jua muda ulionao kwenye kutoa mazungumzo yako. Usiwe mtu wa kuharakisha kuanza kuongea au kuharakisha kumaliza kuongea.
Kuharakisha kwenye jambo lolote ni kiashiria kwamba mtu hana udhibiti na maandalizi ya kutosha na kwenye kuongea mbele ya wengine hilo linatosha kuiba hofu kubwa mbele yako.
Tunajifunza leo kwamba;
Ni bora kuongea vitu vichache kwa utulivu ambapo watu wanaelewa, kuliko kuongea vitu vingi kwa haraka ambayo watu hawaelewi wala kuondoka na kitu cha kwenda kufanyia kazi.
Nikushukuru kwa kusoma nakali hii naamini umejifunza kitu, imeandikwa na mshauri na mwandishi.
Maureen Kemei.
Blog;kufikirichanya.wordpress.com
Maisha bora ni uchaguzi wangu.
-
57/100. Tawala hadhira yako.
Naamini siku yako imekuwa ya mafanikio makubwa, karibu tujifunze kuhusu somo letu la mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji. Kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Kuihofia hadhira hasa kwa ukubwa wake ndiyo chanzo cha watu wengi kupata hofu ya kuongea mbele ya wengine. Wengi wanapokuwa mbele ya kundi kubwa la watu huwa wanajifikiria zaidi wao wenyewe kuliko wanavyowafikiria watu hao au kile wanachokwenda kuongea.
Ili kujijengea kujiamini na kuondokana na hofu ya kuongea mbele ya wengine unapaswa kutawala hadhira yako. Wewe unapaswa kuwa ndiyo nguvu kuu ambayo hadhira inafuatilia.
Utaweza kutawala hadhira yako kwa kujiamini wewe mwenyewe na kuongea kwa mamlaka. Unapoongea kwa mamlaka hadhira inakufuata. Lakini unapoongea kwa hofu na kwa hali ya chini, hadhira inakutawala na hapo utashindwa kuongea vizuri.
Ili kutawala hadhira yako vizuri, unapokuwa mbele ya wengine kuongea, jali vitu viwili pekee, kile unachoongea na wale ambao unawaongelesha. Yaani fikra zako zote zinakua kwenye ukweli ambao unataka watu waujue na watu ambao unataka wajue ukweli. Vitu vingine vyote havina muhimu.
Iko hivi rafiki, kama upo mbele ya wengine na ukaanza kujiuliza iwapo umependeza, hadhira nayo itaanza kufikiria kwa namna hiyo. Lakini unapofikia kuhusu kile unachoongea, basi hadhira nayo inaufuata kwenye hilo.
Somo kuu
Unaposimama kuongea mbele ya wengine, simama kama kiongozi na hadhira iwe inakufuata kwa kile unachozungumzia.
Asante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwandishi na mshauri wako.
Maureen Kemei
Blog, kufikirichanya.wordpress.com.
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
56/100. Tegemea kufanikiwa.
Karibu, katika kujifunza zaidi kuhusu mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji, katika kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Baada ya kuwa na maandalizi mazuri kinachofuata ni kutegemea kufanikiwa. Iko ivi rafiki, kile kinachotokea kwenye maisha yetu ni ambacho tumekuwa tunakitegemea.
Sasa inapokuja kwenye kuongea mbele ya wengine, wengi huwa wanategemea kufanya vibaya. Wanajiambia watasahu, wanajiambia watakosea na mengine mengi. Na haishangazi kwa nini wanapata matokeo hayo kwenye unenaji wao.
Ili ufanye vizuri kwenye kuongea mbele ya wengine, lazima uanze ukiwa unategemea kufanya vizuri. Jione ukiwa unaongea kwa kujiamini na kwa mafanikio makubwa mbele ya wengine. Pata picha ya watu wakiwa wanakusikiliza kwa umakini na kujifunza na kukuelewa.
Unapokwenda kuongea mbele ya wengine, hicho ndiyo kinachotokea. Tofauti na ukiwa na mategemeo ya kushindwa, kila kitu kitakupeleka kwenye kushindwa.
Tunapata funzo kuwa,
Unapata kile ambacho unategemea kupata, hivyo tegemea kilicho bora na utapata kilicho bora.
Asante kwa kuchukua hatua ya kusoma nakali hii, imeandikwa na mwandishi na pia mshauri wako.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
55/100. Kuwa na kitu cha kusema.
Karibu, tunaendelea kujifunza kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Maandalizi ni muhimu sana katika kuongea mbele ya wengine. Kama unakwenda kuongea mbele ya wengine huku ukiwa huna maandalizi sahihi, hofu itakujaa na utafanya vibaya.
Ni muhimu sana uwe na kitu cha kusema na uwe na maandalizi mazuri katika kusema kitu hicho. Lazima uwe unajua kwa kina kile ambacho unazungumzia, iwe ni kwa kujifunza au kwa uzoefu.
Lakini kujua pekee haitoshi lazima pia uwe umejiandaa jinsi ya kusema kile unachojua, kwa namba ambayo watu wataelewa na kukupokea. Hivyo lazima ujiandae kwa kujua kile unachokwenda kuzungumzia na pia kujua njia bora ya kukisema kwa wengine.
Unapokuwa unakijua kwa kina kile unachosema na kuwa na maandalizi mazuri ya jinsi ya kukiongea, unakuwa unajiamini zaidi na hilo linaondoa kabisa hofu unayokuwa nayo wakati wa kuongea mbele ya wengine.
Ukienda kuongea mbele ya wengine bila ya maandalizi, hofu itakutanda na utasahau hata kile kidogo ambacho ulikuwa nacho.
Wanenaji wenye mafanikio makubwa wamekuwa wanafanya maandalizi makubwa. Kwanza wanajifunza sana kuhusu somo wanalonenea, pili wanafanya mazoezi ya jinsi ya kunena.
Wengi wanachukua muda wa peke yao na kusimama mbele ya kioo na kuigiza jinsi wanavyokwenda kuongea mbele ya wengine. Wengi wanarecodi sauti zao is a kujisikia jinsi wanavyoongea na kuboresha zaidi.
Hatua ya kuchukua.
Ni muhimu sana uwe na maandalizi ya kutosha ili uweze kuishinda hofu ya kuongea mbele ya wengine na uweze kuongea kwa kujiamini.
Ahsante sana kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwandishi na mshauri wako.
Maureen Kemei
Bloh:kufikirichanya.wordpress.com
-
54/100. Zama kwenye somo lako.
Karibu, katika kujifunza kuhusu mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji kutoka kitabu cha ; the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Tulijifunza katika somo la kwanza la kitabu hiki kuwa, njia ya kushinda hofu ni kufanya. Ya pili sasa ni kuzama kwenye somo lako.
Kitu kikubwa kinachofanya watu kupata hofu wakati wanaongea mbele ya wengine ni kuruhusu mawazo yao kuzurura kwenye mambo yasiyohusiana na kile wanachozungumzia.
Mtu anakuwa anazungumza, lakini mawazo yake yapo kwenye vitu kama watu wanamchukuliaje, je nguo alizovaa zinaonekanaje kwa watu, au akitoka hapo anakwenda kufanya nini.
Kuruhusu mawazo kuzurura ndiyo imekuwa inachochea sana hofu ya kuongea mbele ya wengine na hata kukaribisha makosa mbalimbali katika uongeaji.
Kuondokana na hali hiyo, zama kwenye somo lako, mawazo yako yanapswa kufikiria kile ambacho unzungumzia pekee. Achana na vitu vingine vyote wakati unapokuwa unaongea na fikiria kile tu ambacho unazungumzia.
Kwa kuweka umakini wako wote kwenye kile unachozungumzia, unaifanya hadhira yako nayo ipeleke umakini wao kwenye unachozungumzia na zile hofu ndogo ndogo zinapotea zenyewe.
Kama tulivyojifunza, hofu huwa inatengenezwa kwenye fikra zetu, hivyo kama utaweka fikra zako kwenye kile unachozungumzia pekee, hutakuwa na nafasi ya hofu kwenye fikra zako.
Hatua za kuchukua.
Unapopata nafasi ya kuzungumza mbele ya wengine jali kitu kimoja tu, ukweli ambao unataka watu hao waujue, mengine yote siyo muhimu kwa wakati ambao unazungumza.
Asante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwana mafanikio na mshauri wako.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
54/100. Njia ya kuishinda hofu ni kufanya.
Karibu rafiki, leo tunajifunza mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji, kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Wametushirikisha maarifa ya kujijengea kujiamini na kuweza kuongea mbele ya wengine kwa kujiamini na kwa mafanikio makubwa.
Moja ; njia ya kuishinda hofu ni kufanya.
Njia pekee ya kuishinda hofu ni kufanya kile kitu ambacho unahofia kufanya. Hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa unayopaswa kuchukua ili kujijengea kujiamini na kuondokana na hofu ya kuongea mbele ya wengine, kwa kuongea zaidi mbele ya wengine.
Lengo linapaswa kuwa kutafuta fursa zaidi za kuongea mbele ya wengine.
Rafiki, hofu huwa ni hali ya kifikra zaidi kuliko uhalisia. Huwa tunatengeneza hofu kwenye fikra zetu kwa kutengeneza picha ambazo haipo.
Lakini tunapofanya kitu matokeo huwa ni tofauti kabisa na picha tuliyokuwa tunajipa awali. Hivyo kwa matokeo tunayopata, hofu inapungua yenyewe.
Mara ya kwanza kufanya kitu chochote huwa tunakuwa na hofu kubwa, lakini kadiri tunavyoendelea kufanya, hofu hiyo inakosa nguvu na kupotea kabisa.
Kinachowafanya wengi kuwa na hofu ya kuongea mbele ya wengine ni kwa sababu hawachukui hatua za kutosha katika kuishinda hofu hiyo.
Hatua za kuchukua.
Kila unapokuwa mbele ya wengine, tafuta nafasi ya kuongea chochote. Anza na vikundi vidogo vidogo kisha nenda kwenye makundi makubwa zaidi.
Kadiri unavyorudia rudia kufanya kitu, ndivyo hofu inavyokosa nguvu na mtu kujiamini zaidi. Tafuta nafasi zaidi za kuongea mbele ya watu na utaweza kuishinda hofu hiyo.
Ahsante kwa kusoma nakala hii, imeandikwa na mwana mafanikio na mshauri wako.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
53/100 . Kutumia tahajudi kuyaelewa maisha.
Karibu, katika kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Tumeona kwamba njia pekee ya kuyaelewa maisha ni kuelewa mateso ambayo tunayapitia. Lakini watu hawpati nafasi ya kuyaelewa mateso wanayopitia kwa sababu hawana udhibiti wowote kwenye akili zao.
Wengi wanaruhusu akili zao zizurure hovyo bila ya kuelewa kwa nini zinazurura. Mtu anafanya kitu hiki, lakini akili na mawazo yake yapo kwenye kitu kingine.
Na pia inapotokea mtu anakutana na ugumu au changamoto, akili haipendi kukaa kwenye ugumu ule, badala yake inahama na kwenda kwenye vitu ambavyo siyo vigumu na wala siyo changamoto. Kwa njia hii inakuwa vigumu mtu kuyaelewa mateso na kuyaelewa maisha.
Jawabu la changamoto hii ni mtu kufanya tahajudi, kutenga muda kwenye siku ambao unaitumia kuangalia akili yako jinsi inavyohangaika na kuzurura. Tofauti na wengi wanavyofikiri kwamba tahajudi ni kudhibiti akili, hapa unatumia tahajudi kuiangalia akili, na kuona namna inavyozurura.
Njia rahisi ya kufanya tahajudi ni kukaa eneo tulivu, kufunga macho yako na kuielekeza akili yako kwenye pumzi zako, unapovuta pumzi ndani fikiria unavuta pumzi ndani, unapoitoa nje fikiria unatoa pumzi nje.
Akili yako inapohama kutoka kwenye pumzi zako na kwenda kwenye mengine ona hilo kwamba akili yako imehama. Ni zoezi rahisi kwa kusoma hapa, lakini jaribu kufanya na hazitapita sekunde kumi akili yako itaanza kuhangaika na vitu vingi kuliko unavyoweza kufikiri.
Tahajudi ndiyo njia pekee tunayoweza kuitumia kujijua sisi wenyewe na baada ya kujijua kuweza kupiga hatua zaidi kiutambuzi. Tahajudi ndiyo zana pekee tuliyonayo ambayo inaweza kutusaidia tusizidiwe utambuzi na maendeleo makubwa yanayotokea kwenye teknolojia, hasa ujio wa maroboti.
Hatua za kuchukua.
Tutenge muda wa kufanya tahajudi kwenye kila siku ya maisha yetu. Mwandishi anasema amekuwa akifanya tahajudi katika kila siku ya maisha yake.
Hilo limemsaidia kuandika vitabu mbalimbali ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa sana kwenye maisha ya mwanadamu.
Ahsante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei.
Blog:kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
-
52/100. Maisha siyo hadithi.
Karibu, katika kujifunza zaidi kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century ambacho kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Swali kubwa ambalo limekuwa linawasumbua watu tangu enzi na enzi ni nini maana ya maisha? Watu wamekuwa wakijiuliza swali hili na mengine kama mimi ni nani? Niko hapa duniani kufanya nini?
Katika kila zama swali la maana ya maisha ufanye nini na maisha limekuwa linapata majibu mbalimbali. Na majibu yote yanakuwa yanaletwa kwa hadithi
Hadithi moja maarufu ambayo imekuwa msingi wa dini nyingi ni kwamba kila mtu amekuwa duniani akiwa na kusudi lake tayari, na mtu akilitambua kusudi hilo na kuliishi basi atakuwa na maisha bora.
Kama hatajua kusudi lake au akalijua na asiliishi, basi maisha yake yatakuwa hovyo sana, hata kama atakuwa na mali nyingi kiasi gani.
Lakini pia zipo hadithi kwamba maana ya maisha ni yale tunayokutana nayo kila siku, mkusanyiko wa kila tunachpitia ndiyo maana ya maisha.
Na hadithi nyingine maisha ni mahaba, kwamba mtu akipata anachopemda na kuweka maisha yake yote kwenye kitu hicho amepata maana ya maisha yake.
Hadithi nyingi za maana ya maisha hazijakamilika na hili ndilo zinawafanya watu wasiridhike na maisha licha ya kuishi hadithi hizo.
Ili hadithi ya maisha ikamilike na iendane na wewe inapaswa kukidhi vigezo viwili, moja ikuhusishe wewe kama mhusika mkuu na pili iwe na maana ambayo ni kubwa kuliko wewe.
Hadithi nyingi tunazoishi kwenye maisha ni za uongo, ni kitu ambacho kimetengenezwa na watu, lakini tunaziamini na kuziishi kwa sababu kila mtu anafanya hivyo. Na wakati mwingine inabidi tuziamini kwa sababu tulishajitoa sana uko nyuma kwa sababu ya hadithi hizo.
Hatua za kuchukua ;
Njia pekee za kujijua wenyewe, njia pekee ya kujua maana ya maisha siyo kwa kuangalia hadithi tunazoishi, bali kwa kuangalia mateso na kuelewa maana yake.
Sehemu kubwa ya maisha yetu ni mateso, hivyo Kuyaelewa maisha tunapswa kuanza na kuyaelewa mateso. Maisha siyo hadithi kama tulivyozoeshwa, bali maana ya maisha ipo kwenye mateso tunayopitia.
Ahsante kwa kusoma nakala hii, imeandikwa na mwanafuzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei.
Blog:kufikirichanya.wordpress.com