Home

  • Umuhimu wa kuthamini kile ambacho unacho.

    Binadamu kwa asili tunatamani vitu ambavyo hatuna. Tunatamani vile ambavyo wengine wanavyo na kusahau hata vile ambavyo tunavyo.

    Usiweke akili yako kwenye vitu ambavyo huvimiliki na siyo vyako, lakini ni vyema kuhesabu baraka zako kwenye vitu ambavyo unavyo.

    Uhuru kamili ni kutumia kile ambacho unacho. Kile ambacho siyo yako ni utumwa, maana utakaa kuwa na wasiwasi kama mwenyewe ataulisia.

    Kitu kingine ni kutumia kile ambacho unacho vizuri maana Kuna siku utavikosa. Hiyo siku ndio utaumia sana kwa kupoteza kile ambacho ulichonacho.

    Kuna vitu vingi tunavimiliki na hatuvithamini, tukianzia kwenye mahusiano watu wengi huchukua mwenzake kama wa kawaida tu, lakini siku ambayo hayuko ndio utagundua ni wa maana akiwa karibu nawe.

    Vitu kama fedha siku ambayo huna ndio unakumbuka unahitaji fedha ili kununua mahitaji muhimu. Watu wa karibu kama wazazi wengi hawakumbuki kuwatunza wazazi wakiwa hai, siku ambayo hawapo wanaanza kujilaumu mbona hawakuwatunza wakiwa hai.

    Hatua ya kuchukua leo ni kuweka nguvu kwenye kile ambacho unacho sasa. Usipoteze nguvu kwenye kile ambacho huvimiliki.

    Hivyo basi, vyote tunavyovimiliki tumeazimwa na asili kwa muda tu. Kazi yetu ni kuthamini na kuvitumia vizuri hata siku ukija kuondoka hutajutia. Ubaya unakuja pale ulikuwa na kitu alafu hukitumii wala hukithamini.

    Imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Umuhimu wa kudhibiti fikra zetu.

    Katika zama hizi ni vigumu sana kwa watu wengi kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja. Hasa kwenye kusoma au kuandika au kutafakari jambo moja kwa muda fulani.

    Wengi hudhani hawawezi kudhibiti fikra na akili zao, lakini ni jambo linalowezekana kabisa. Nguvu ya udhibiti wa fikra ipo kwa kila mmoja wetu, tunahitaji kuiendeleza kwa kukadiria kabisa kujitafutia utulivu na kujaribu kurudisha fikra kwenye jambo moja.

    Kama vile tunavyoweka juhudi kwenye kutunza miili yetu, kuanzia kulisha, kuisafisha na kuvalisha. Hivyo ndivyo inavyotupasa kuweka juhudi kwenye utunzaji wa fikra zetu, kwa kudhibiti akili zetu kutokuzurura kwenye mambo mengi.

    Unafanya hili kwa kuchagua kuweka  mawazo yako kwenye vitu ambavyo vina manufaa zaidi. Hapo unakuwa umeidhibiti akili yako, lakini pia unakuwa umefikiria na kutafakari kitu ambacho ni muhimu kwenye maisha yako.

    Tumejifunza leo kuwa kwa namna yoyote ile usiache tu akili yako izurure hovyo, badala yake idhibiti kwa kuweka mawazo yako kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu. Na hapo utaweza kwa muda fulani kuona matokeo mazuri, lakini akili na fikra zikizurura kila mara hakuna jambo la maana unaloweza kuitimiza.

    Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Email ;kemeimaureen7@gmail.com

    Bloh;kufikirichanya.wordpress.com

  • Siri kuu ya kufanya makubwa.

    Ndugu yangu nakushirikisha yale ninayojifunza kuhusu mafanikio na maisha kwa ujumla. Kutoka vitabu mbalimbali na pia kujifunza kupitia Kazi za Kocha Dr Makirita Amani.

    Kuna umuhimu mkubwa kuwa na ndoto kubwa katika maisha, maana litakusukuma ujitume zaidi. Hili linanikumbusha wakati tukiwa shuleni mwalimu akisema “hili zoezi nahitaji kabla saa sita mchana,” kila mtu atahakikisha anamaliza kabla ya wakati huo.

    Tukija kwenye maisha sasa bila kujiwekea malengo na namna ya kutimiza hakuna namna utaweza fanya makubwa. Maana hakuna kitu kinachokusuma, utaendelea kufanya kwa mazoea.

    Ili kuondokana na hili ni jambo la busara kujiwekea malengo makubwa, kuwa na ndoto kubwa alafu kuanza kidogo na kuchukua hatua sasa. Acha kufikiria ukomo na unachokosa na angalia kile ambacho unacho.

    Unaweza kufanya makubwa utakavyo lakini kwa kuanza kidogo na kuchukua hatua sasa. Imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Email;kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kutohairisha ndoto zako.

    Kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake, tukiwa wachanga huwa tunaulizwa unataka kuwa nani, majibu huwa ya haraka sana labda daktari, piloti, raisi na mengineyo.

    Lakini unapofikia kiwango cha chuo ukiulizwa unataka kuwa nani wengi huwa tumesahau au tunakwepa kusema ndoto hiyo kubwa iliyo ndani yetu. Tunaanza kuwa wa kawaida kabisa na kufuata jamii wanasema nini juu yetu.

    Kitu kubaya sasa ni pale unapokuwa na msukumo mkubwa wa kufanya jambo, unaanza kuhairisha polepole ukijiambia hujawa tayari, au bado muda unayo.

    Tunajua jinsi ambavyo hatuna uhakika wa muda wetu hapa duniani. Tunajua jinsi wengi wanavyokuja kujuta maisha yao yanapofika ukingoni. Usiwe mtu wa aina hiyo, usiwe mtu wa kuahirisha ndoto zako.

    Badala yake zitekeleze ndoto zako kama unavyoziona kwenye akili yako. Hata kama wengine hawatakuelewa, fanya kile unachojua ni sahihi, mana kama ni majuto wewe ndiye utayeyapata.

    Muda tulionao ndiyo huu, hakuna wakati utakuwa tayari zaidi ya ulivyo sasa. Anza kuziishi ndoto zako sasa kwa pale ulipo na kwa kile ulichonacho sasa. Hiyo ndiyo njia ya kuwa na maisha kamilifu.

    Asante kwa kusoma nakali hii naamini unaishi ndoto zako, ama kama ulikuwa umesahau unaanza kuishi sasa. Imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Email ;kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

    Rafiki tunaendeleza mafunzo yetu kutoka kitabu cha anger book 2,kilichoandiwa na Mwana falsafa Seneca.

    Kila unapotaka kupata hasira juu ya makosa ya wengine, jiulize je unaweza kuwa na hasira kwa mtoto mchanga ambaye haachi kulia? Unapoanza kuwachukulia watu wengine na makosa yao kwa mtazamo huo, ndipo unaona kuwa hasira haina maana yoyote.

    Ili kuondokana na kukasirishwa na wengine, unapaswa kuwa mtu wa kumsamehe kila mtu, binadamu wanahitaji huruma na msamaha kwa sababu kila mmoja wetu ni mkosaji kwa namna moja au nyingine. Unaweza kuwakasirikia wengine waliofanya makosa fulani, lakini kumbuka ata wewe Kuna makosa ulifanya, huenda tu hayachulikani.

    Mtu mwenye hekima huwa hakasirishwi na wengine, kwa sababu anajua watu hawataacha kukosea. Na hivyo anapoamka anajua kabisa katika siku yake atakutana na watu wakosefu, watu wavivu, watu wenye hila na tamaa. Na yeye anajua atakabiliana na tabia hizo kama daktari anavyokabiliana na ugonjwa kwenye mwili wa mtu.

    Daktari hawi na hasira kwa mtu kwa sababu anaumwa, bali anachukua hatua kutibu ugonjwa wake. Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa wakosaji, tusiwakasirikie, badala yake tuwasaidie pale wanapokwama.

    Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

    Je kuna uzuri wowote kwenye hasira? Je Kuna uzuri wowote tunayoweza kupata kwa kuwa na hasira? Haya ni maswali ambayo Seneca alijiuliza na kujipa majibu. Kutoka kitabu chake cha( Anger, book 2.)

    Karibu tujifunze nasi ili tujue namna ya kujizuia wakati tunapatwa na hasira.

    Kinachoibua hasira ndani yetu siyo kile ambacho kimetokea, bali jinsi tunavyofikiria kuhusu kilichotokea. Tunapatwa na hasira pale tunapoamini kwamba tumekosewa na wengine na hivyo kuwa na nia ya kulipa ule ubaya ambao tumefanyiwa.

    Hasira ni zao la kutotumia vizuri fikra zetu, pale hasira zinapoibuliwa ndani yetu na sisi kulipuka kwa hisia hatutumii vizuri fikra zetu. Hivyo kama mtu utasimamia kutumia fikra zako, hasira haiwezi kukutawala.

    Wengi wamekuwa wanajiambia kwamba hawawezi kuacha kuwa na hasira kwa sababu wakosaji ni wengi sana sasa kama utatumia hicho kama kigezo cha hasira, basi hutaacha kuwa na hasira, kwa sababu hakuna siku itakayoanza mpaka iishe asitokee mtu wa kukukosea. Wapo wanaokosea kwa makusudi na wapo wanaokosea kwa kutokujua.

    Kwa namna yoyote ile Seneca anatushauri usimkasirikie mtu yeyote anayekukosea. Asante kwa kusoma nakali hii, imeandikwa na mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Kwa nini ni muhimu kufikiri tofauti.

    Tunaishi kwenye jamii ya ajabu kweli, jamii ambayo kufikiri tofauti kunaweza kukuletea shida. Nakumbuka tukiwa wadogo nyumbani, yaani ukitoa hoja au kuchangia hoja fulani. Wazazi wanakuona kama unataka kuchukua nafasi yao.

    Kwa hivyo wanahakikisha watetea nafasi yao kwa kukunyamazisha tena kwa ukali, lakini hata mtu hauna haja na iyo nafasi. Hili ndilo limechangia pakubwa watu wengi Kuendelea kufanya mambo kimazoea maana wengi tumeguswa hivyo.

    Hiyo hoja ya kufikiri tofauti na mazoea hili kukucha na jambo jipya kitakayoleta mabadiliko katika jamii, inabidi kufikiri tofauti pamoja na kuhoji baadhi ya mambo.

    Ni wakati sahihi wa kujenga jamii inayoamini katika fikra tofauti, kupokea mawazo tofauti ndiyo itajenga maendeleo na kuondoa mazoea.

    Kuna msemo unaosema upumbavu ni kufanya mambo kwa namna ile ile ukitarajia matokeo tofauti. Hivyo inabidi kuhoji mambo, kufanya udadisi na kufikiria nje ya boksi.

    Asante kwa kusoma nakala hii ni mimi mwandishi na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Kufikirichanya.wordpress.com.

  • Unahitaji kujiamini.

    Tofauti kati ya wanaoshinda na wasioshindwa sio akili, fursa au bahati. Bali tofauti ni kuamini na kujiamini. Watu wawili wanaweza kuona fursa moja, mmoja akawa anaamini anaweza kutumia fursa ile vizuri na akaanza kufanyia kazi.

    Akajitoa kweli na anapokutana na changamoto bado imani yake iko dhabiti na hakati tamaa. Mwingine anaona ni fursa nzuri na anaamua kuijaribu katika kujaribu haamini kama anaweza kuifanya kwa mafanikio, yeye anajaribu tu.

    Katika kuifanya anakutana na changamoto na kupitia changamoto hizo anakubali kwamba yeye hawezi kufanikiwa kwenye kitu hicho.

    Bila kuamini kwamba unaweza, hakuna kitu kikubwa kinachoweza kutokea kwenye maisha yako.

    Ni mimi anayekujali mwandishi na mshauri wako.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

  • Hatua za kutengeneza maisha bora na yenye mafanikio.

    Hatua ya kwanza ni taswira, unapaswa kutengeneza taswira ya maisha unayotaka kuwa nayo. Kwenye taswira hii ndiyo unajua kusudi la maisha yako, unaweka maono yako, unakuwa na sababu ya kwa nini unataka kufikia maono hayo na hatua za kuchukua. Ni lazima kwanza uone taswira cha unachotaka kabla hakijatokea kwa uhalisia.

    Hatua ya pili ni utambuzi baada ya kupata picha ya wapi unakotaka kufika, kinachofuata ni kutambua njia unayopaswa kupita ili kufika kwenye maono yako. Anzia hapo ulipo Sasa, kwa hali uliyonayo sasa. Usisubiri mpaka kila kitu kiwe Sawa ndiyo uanze, kwa sababu hakuna wakati ambao kila kitu kitakuwa Sawa. Kuanza ni bora kuliko kusubiri.

    Hatua ya tatu, maboresho unapoanza ukiwa hujawa tayari, utajifunza kadiri unavyokwenda. Hivyo utaona njia bora zaidi za kufika kule unakotaka kufika, na hapo unapaswa kufanya maboresho ili kufika unakokwenda. Kwa kila hatua unayochukua, jiulize unawezaje kuboresha zaidi. Maboresho madogo madogo yanyofanywa kila siku yanakuja kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti kabisa.

    Hatua ya nne ni ubunifu, kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa ni lazima uchukue hatua tofaut na unazochukua sasa. Unahitaji kuwa mbunifu na ubunifu ni kufanya vitu kwa namna tofauti. Unaweza kufanya vitu kwa utofauti kwa kuanza na mtazamo Tofauti, kuangalia kitu kwa namna tofauti na kujaribu vitu vipya ambavyo hujawahi kufanya huko nyuma. Kwa kila unachofanya, jiulize ni kwa namna gani unaweza kufanya kwa utofauti na ukapata matokeo bora.

    Hatua ya tano utekelezaji, mipango haiwezi kukuletea mafanikio, nia njema haitakutoa hapo ulipo sasa, ni mpaka pale utakapochukua hatua ya kutekeleza yale uliyopanga ndiyo utaweza kutoka hapo ulipo Sasa na kufika unakoelekea. Ni kuchukua hatua ndiko kutakakokubadili wewe kutoka hapo ulipo sasa na Kufikia maono yako makubwa. Wanaofanikiwa ni wale wanachukua hatua, wakati wale Wasiofikiria kuchukua hatua wakibaki pale walipo sasa.

    Hatua ya sita ufahamu, kila siku Kuna ufahamu ambao tunaupata kupitia yale tunayofanya. Iwapo tunatambua au kutokutambua ufahamu huo kunaamuliwa na utayari wengi kutenga muda na kutafakari kwa kina kila hatua tunayopiga. Tunapotenga muda wa kutafakari, kukaa kimya, kusikiliza na kuangalia, tunajifunza vitu vingi ambavyo siyo rahisi kuviona kama tumetingwa na majukumu yetu ya kila siku. Ufahamu tunaoupata una mchango mkubwa kwenye mtazamo wetu, unatutengeneza jinsi tunavyofikiri leo kuhusu tunachotaka kufikia kesho.

    Hatua ya sapa ni kujihami, siyo kila kitu kitaenda kama tunavyopanga. Kuna wakati tunapata matokeo hasi na kukutana na watu hasi amabo watakukatisha tamaa kuhusu malengo unayofanyia kazi, kwa kukuambia haiwezekani au huwezi. Watu hawa wanaweza kuwa marafiki, ndugu wa karibu, familia au hata wale unaofanya nao kazi. Jihami na watu hao hasi kama unataka kufanikiwa, kwa sababu uwepo wao kwenye maisha yako utakuwa kikwazo kwako kufanikiwa zaidi. Na hapa haimaanishi kuwatenga, bali kuhakikisha hawaleti ushawishi wao hasi kwenye ndoto zako, kwa kuchagua kutokuwashirikisha ndoto hizo.

    Njia rahisi ya kuwajua watu hasi unaopaswa kujihami nao ni kuangalia watu hao wanakuwa na majibu gani unapowaeleza kuhusu mafanikio makubwa. Kama ni watu wanaoamini haiwezekani, basi waweke kwenye kundi la watu hasi na chukua hatua sahihi kwao.

    Hatua ya nane ni uwekezaji, kufikia yote unayotaka kufikia na ambayo yapo ndani ya uwezo wako unapaswa kuwekeza muda, nguvu, juhudi, moyo na fedha. Kila mtu anataka kufanikiwa na kupata matokeo bora kwake na kwa familia yake, kila mtu anataka kilicho bora. Lakini kipimo sahihi cha nani anachotaka, ni utayari wa uwekezaji amabo mtu anao. Unapowekeza vitu hivyo vitano, ndipo unaiambia dunia umejitoa kweli kufanikiwa na hakuna chochote kitakachokuzuia.

    Unawekeza muda, kwa kutoa muda wako kufanyia kazi malengo yako. Unawekeza nguvu kwa kuweka juhudi katika kuyafikia malengo yako. Unawekeza juhudi kwa kwenda hatua ya ziada kwa Kil unachofanya. Unawekeza moyo kwa kuwa na hisia chanya juu yako binafsi na kile unachofanya. Unawekeza fedha kwa kununua maarifa na ujuzi unaopaswa kuwa nayo ili kufanikiwa.

    Unaleta pamoja vitu hivyo vitano kwenye kile unachokifanya, nguvu kubwa usiyoweza kuielezea kinakuwa kwako na kukuwezesha kufikia malengo ambayo umejiwekea.

    Nakala hii imenakiliwa na mwandish na mshauri.

    Maureen Kemei.

    Maisha yangu, uchaguzi wangu.

  • Fikiria kushinda.

    Tunaendelea kujifunza namna ya kuwa chanya wakati wote, tuliangalia kwamba kuwa chanya au hasi inaanzia kwenye fikra zetu.

    Ili tufikirie chanya au tuwe chanya wakati wote, inabidi tubadili mfumo wote wa kifikra. Kutoka hasi kwenda chanya ili tupate nafasi ya kuona fursa badala ya matatizo.

    Kitu kinachotuzuia wakati mwingine tusifanye jambo bora ni kuwa na mtazamo hasi, hasa kama kitu ni kipya wengi wanakuwa na mtazamo ya kufeli au kushindwa.

    Ili tuweze kushinda hali hii ya kuona kushindwa lazima tukatae kabisa fikra hasi. Hata kama wazo hilo linaonekana kutisha au kuwa ngumu, kuwa na mtazamo chanya kunakusukuma kuchukua hatua ya ziada itakayokuletea ushindi.

    Uzuri sisi binadamu tuna uwezo wa kufikiri na kuamua maisha yetu yanafaa kwenda aje. Unaweza kuamua kufikiri chanya na kuona fursa au kutawaliwa fikra hasi na kuona matatizo mengi.

    Asante kwa kusoma nakali hii imeandikwa na ;

    Maureen Kemei

    Mwandishi na anayekujali sana.

    Maisha mema, chaguzi wangu.