Home

  • Madhara ya kusahau misingi yako.

    Katika safari ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha na utajiri mkubwa, kujitofautisha na watu wengine ni jambo linalohitajika. Kujiwekea misingi ambayo unasimamia muda wote bila kuyumbishwa na matukio yoyote yanayotokea.

    Unapoacha kuishi misingi uliyojijengea, ndipo unapoanguka. Kuishi misingi yako mwenyewe inakupa uhuru wa kuamua kufanya mambo yako kwa mpangilio mzuri, bila kufuata mkumbo.

    Misingi hiyo inakupa nidhamu kubwa na kukufanya uishi maisha halisi mara zote bila kuiga au kungoja wengine wanaamua nini juu ya maisha yako. Na hapo ndipo utaweza kuzishinda hofu yoyote ile,kama hofu ya kuogopa kuchukua hatua au hofu ya kufanya kitu kipya kwenye maisha yako.

    Lakini unapoacha kuishi tu misingi yako, maisha yako yanavurugika, unakosa utulivu na kuwa na hofu. Ukishajijengea misingi inayokupa mafanikio, kamwe usisahau misingi hiyo baada ya kuwa umefanikiwa.

    Unapokosea kufuata misingi yako uliyojiwekea, usianze kujilaumu kwa makosa hayo, badala yake angalia ipi hatua sahihi kuchukua kisha ichukue. Haijalishi umekosea kikubwa kiasi gani, muhimu kwako ni kuanza kuchukua hatua sahihi.

    Hatua ya kuchukua, jiwekee misingi unayofuata kila siku bila kuacha, na ikitokea umeacha misingi hiyo kamwe usijilaumu bali angalia ni ipi hatua sahihi kuchukua kisha ichukue.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

  • Mambo muhimu mawili  ya kuzingatia ili kujijengea msimamo.

    Kitu kikubwa kinachowazuia watu kuishi maisha halisi kwao ni kukosa msimamo. Wengi huwa wanabadilika badilika kila mara, kiasi kwamba hawawezi kuaminiwa au kutegemewa kwenye kitu chochote.

    Wengi ni watu wa kubadili mawazo yao haraka na ndani ya muda mfupi. Wakati huu wanaamua hiki, ila baada ya muda mfupi wanaamua kingine ambacho ni tofauti kabisa na kile cha awali.

    Kwa kubadilika badilika huko, watu wanashindwa kuwa halisi na hata kutoaminika. Kwa hivyo, wastoa wanashauri mambo muhimu mawili ya kuzingatia ili kujijengea msimamo.

    Jambo la kwanza ni kuchagua aina ya watu unayetaka kuwa na kuwa nayo mara zote. Ukishachagua unakuwa mtu wa aina gani, basi kuwa hivyo bila kubadilika. Haimaanishi hubadili unayofanya kulingana na mabadiliko yanayotokea, bali inamaanisha kuwa mtu wa aina moja mara zote.

    Jambo la pili ni kuwa na maisha ya aina moja, hadharani na faraghani. Watu wengi huwa na maisha ya aina mbili, mbele ya watu wanajionyesha ni watu wa aina fulani, ila wakiwa sirini wanakuwa ni watu wa aina tofauti.

    Wewe chagua kuwa mtu wa aina moja, mwenye maisha ya aina moja, hadharani na sirini. Kusiwe na chochote unachokificha kwenye maisha yako. Ukishakuwa na maisha ya aina mbili, huwezi kuishi kwa uhalisia wako na unakosa msimamo wa ndani.

    Hatua ya kuchukua, maisha yasiyo na msimamo ni maisha yasiyoeleweka. Ni muhimu tujijengee msimamo kwenye maisha yetu kwa kuamua tunakuwa watu wa aina gani na kisha kuchagua kuwa na maisha ya aina moja.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

  • Ni nini kanuni ya kukusaidia kutimiza maono yako.

    Kanuni ya kwanza ni kujua uwezo wako. Ili uweze kufanikiwa katika maono yako, lazima ujue uwezo wako wa kutimiza maono hayo. Kwa kuwa umezaliwa kufanya jambo fulani, Mungu amekupa uwezo wa kuutimiza wito huo.

    Uko katika namna ambayo unapaswa kuliishi kusudi la maisha yako. Uwezo wako unaibuka na kugundulika pale ambapo unasema ndiyo kwenye ndoto zako.

    Sisi ni kama mbegu ambazo ndani yake kuna msitu mkubwa au miti mikubwa ambayo itastawi, lakini haiwezi kustawi au kuonekana hadi pale ambapo zitapandwa.

    Kanuni ya pili ni kwamba, tengeneza mpango wa maono yako. Mpango mkakati ulio wazi na unao eleweka. Mungu anakupa maono, plan unazitengeneza wewe mwanadamu na Mungu huongoza hatua zako.

    Malengo ni ramani ya maono yako! Kuonyesha wapi unakwenda na namna gani utafikia huko.

    Hatua ya kuchukua, jitambue wewe ni nani? Kisha weka malengo kulingana tafsiri halisi ya wewe ni nani? Usianze kabla ya kutengeneza plan yako!

    Chora ramani kwanza ya kile ambacho unaenda kukifanya, kabla ya kuanza kufanya. Kisha anza na kile ambacho unacho sasa.

    Baada ya kuweka malengo yako au plan zako, inakubidi uweke kazi haswa kwenye kile unachofanya. Na pia umwombe na msaada wake ilikusimama na wewe katika maono yako. Chagua sasa ni nini unakitaka katika maisha yako.

    Akujaliye sana.

    Maureen Kemei.

  • Kikwazo kikuu kwenye kufikia utulivu wa kiroho.

    Kikwazo kwetu tunachopata kwenye safari ya kufikia utulivu wa kiroho ambacho ni fikra na hisia zetu. Inaweza kuwa tupo eneo moja au kufanya shughuli fulani lakini fikra zetu zinawaza vitu vingine tofauti kabisa.

    Kwa kuwaza vitu vingine mbali na kile tunachofanya inatukosha kuona uzuri wa kile tunachofanya na pia tunachotarajia hapo mbeleni. Tunapaswa kuweka fikra zetu kwenye kile kilicho mbele yetu na tutajifunza mengi.

    Utaweza kuifikia ufahamu wa juu kwa kuisikiliza sauti yako ya ndani, maana hiyo ndiyo inayojua mengi kuhusu wewe.

    Kwa kupata unachotaka, anza kwa kutoa kile ulichonacho. Usidharau chochote ulichonacho, hata kama ni kidogo kiasi gani, wewe tafuta watu gani wanaweza kunufaika nacho, wafanyie kisha watake wakulipe.

    Kama utatoa thamani kweli, lazima ulipwe maana ni kanuni ya asili ambayo huwa haishindwi.

    Una uwezo wa kufanya miujiza mikubwa kwenye maisha yako, unaweza kufanya yale yatakayowashangaza wengine na wakaona una nguvu zisizo za kawaida. Wapo watakaosema una bahati, wengine watasema unatumia majini.

    Lakini siri kamili ipo kwenye vitu vitatu :kufikiri, kusubiri na kufunga. Hakuna kitakachoweza kushinda nguvu hizo tatu.

    Hatua ya kuchukua, kama ambavyo tumejifunza na kuona kikwazo ipo kwenye fikra zetu, inatupasa tubadili namna tunavyofikiri kwa kukaa yote yaliyo hasi na kujenga fikra chanya kwenye yote tunayofanya. Na hapo tunaweza kujipatia utulivu wa kiroho na kifikra.

    Anayekujali sana

    Maureen Kemei

    Email, kemeimaureen7@gmail.com

  • Maana ya maisha kulingana na Socrates.

    Mtu anaposoma falsafa anataka kuelewa jinsi na kwa nini watu hufanya mambo fulani na jinsi ya kuishi maisha mazuri. Kwa maneno mengine, wanataka kujua maana ya maisha.

    Socrates ambaye ni baba wa falsafa ya kale na mtu wenye busara zaidi katika Ugiriki ya kale. Ingawa hatimaye alihukumiwa kwa hekima yake, maneno yake yaliysemwa bado yanasikilizwa na kufuatwa hadi leo.

    Socrates aliamini kwamba kusudi la maisha lilikuwa ukuzi wa kibinafsi na wa kiroho. Anathibitisha imani hii katika kile ambacho bila shaka ni kauli yake maarufu :”maisha ambayo hayajachunguzwa hayafai kuishi. “

    Hakusema tu kwamba maisha ambayo hayajachunguzwa hayakuwa maisha ya kiungwana au kwamba yalikuwa ni njia ya watu wenye haki kidogo, bali maisha ambayo hayajachunguzwa hayafai kabisa kuishi hata kidogo.

    Socrates aliishi sehemu kubwa ya maisha yake akichunguza mara kwa mara mawazo na na tabia yake mwenyewe. Aliona uchunguzi huo wa kibinafsi, uwe unafanywa na yeye mwenyewe mazungumzo na washirika, kuwa bora zaidi ya maisha yenye thamani ya kuishi.

    Lengo la Socrates lilikuwa kuamua jinsi ya kuwa mwanadamu bora. Katika mtazamo huu Kisokrasia, ubora na endelevu wa umakini tunayolipa kwa kuishi maisha yaliyochunguzwa ndio kiini cha kuishi vizuri.

    Kuchunguza chochote kutasababisha kuelewa. Kuhusu nukuu hiyo ya Socrates “Maisha yasiyo na uchunguzi hayafai kuishi!” inamaanisha kuelewa kile unachoishi ni muhimu zaidi kuliko kuishi haswa.

    Kujielewa mwenyewe, uchaguzi zako, na kwa nini unafanya chaguzi zako ;kuelewa wengine wanaokushawishi au kushawishiwa na wewe. Kweli unaeleza kuelewa nini kufanya tena katika maisha yako ni mambo yote ambayo maisha yako “yamechunguzwe.”

    Kuishi maisha ambayo hayajachunguzwa hayakuwa maisha kungejumuisha kutowahi kuuliza maswali kusaidia kupata maarifa ya kuwa na akili, badala ya kutojua kabisa ulimwengu unaokuzunguka.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

  • Taswira ya mafanikio.

    Mtu wa kawaida huwa anafikiria mawazo elfu mbili mpaka elf tatu kwa saa moja, na sehemu kubwa ya mawazo hayo ni mambo hasi yasiyo na faida yoyote kwa mtu.

    Sasa huo ni kupoteza muda na nguvu zako. Unahitaji kutumia mawazo yako kutengeneza taswira ya mafanikio yako, baada ya kuwa umeweka malengo yako.

    Pata picha ukiwa umeshakamilisha na jione jins unavyokuwa umepiga hatua baada ya kuyafikia malengo hayo. Kisha mara kwa mara ona taswira hii kwenye mawazo yako.

    Muda wote mawazo yako yatawaliwe na malengo ambayo umejiwekea. Kwenye shughuli zozote zile unapaswa kuwa na mtazamo wa tayari umeshinda.

    Muda wote akili yako iwe inaangalia kwenye shindi siyo litakusukuma kufanikiwa, bali pia litakuzuia usikate tamaa njiani. Huwezi kukata tamaa wakati umeshajiona mshindi.

    Kwa malengo uliyojiwekea, kila wakati Pata picha kama tayari umeshayafikia malengo hayo, Pata picha upo kwenye kilele cha mafanikio, ona jinsi inavyokuwa ufahari kwako kupata mafanikio hayo, na hilo litakusukuma zaidi.

    Pia, pata picha changamoto unazoweza kukutana nazo katika safari yako ya mafanikio na jione ukiwa unazivuka changamoto hizo na kuelekea kwenye ushindi.

    Kumbuka kujipa taswira siyo mbadala wa kuweka kazi, kazi lazima uweke sana. Kujipa taswira ni kumiliki akili yako ili isiwe kikwazo kwako. Kwa sababu kama hutajipa mawazo ya mafanikio yako, basi mawazo ya kushindwa yatatawala akili yako.

    Hatua ya kuchukua, Pata taswira ya mafanikio unayotaka kwenye maisha yako, lakini kumbuka kuweka kazi kwenye kuyafikia mafanikio hayo.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei

    Kemeimaureen7@gmail.com

  • Kushughulika zaidi na mambo ya ndani.

    Watu wengi kwenye zama hizi hutamani kupata utulivu wa kiroho, kimwili, kihisia na maisha kwa ujumla. Lakini wengi bila kujua hujikuta wakitafuta utulivu huo huko nje.

    Watu wengi huhangaika na mambo ya nje ili kujaza shimo lililo ndani yao, kitu ambacho huwa hakiwezekani. Wapo watu wanahama dini, kazi, ndoa, mahusiano na vitu vingine, lakini kule wanakoenda wanagundua hakuna kipya ukilinganisha na walikotoka.

    Utulivu wa kweli ni ule unaojitafutia mwenyewe, utulivu wa ndani, unaamua kujitenga na ulimwengu wa kelele mingi na kutumia muda huo kuyatafakari maisha yako.

    Unapotafari hivyo unaafikiana na nafsi yako, yaani unaongea na wewe mwenyewe, kwa kufanya hivyo utajua ni wapi una madhaifu na kuweza kuiboresha. Na pale unapoenda vizuri unajipongeza na kutia bidii zaidi.

    Kwa kufanya hivyo unapata utulivu wa ndani, na utaachana na kuhangaika na mambo ya nje. Hutakwazika wala kuumizwa na watu wanapokusema vibaya maana unajijua mwenyewe.

    Hatua ya kuchukua, jitafakari mwenyewe kama unafuata mambo ya nje, watu wanasema nini juu yako, ama unajielewa mwenyewe, unakuwa na muda wako wa kujitenga kisha kujihoji mwenyewe.

    Kwa kujihoji hivyo, unaweza kujirekebisha na kuweza kusonga mbele zaidi bila msongo wowote.

    Akujaliye sana.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

  • Uhuru ni kuwajibika.

    Watu wengi wanapokuwa kwenye hali ya kukosa uhuru, huwa wanapigana sana kupata uhuru,wakiamini kwamba watakapokuwa huru basi kila kitu kutakuwa rahisi kwao, watapata kila wanachotaka. Lakini huko ni kujidanganya, uhuru ni kuwajibika, kuyabeba majukumu yako na kujisimamia  wenyewe.

    Kwa kuwa wengi hawapendi kuwajibika, uhuru unaishia kuwa mzigo kwao na hivyo kutafuta namna ya kurudi kwenye utumwa au kuwaiga wengine. Kama kweli unataka uhuru kwenye maisha yako, lazima uwe tayari kuwajibika, bila ya kuwajibika uhuru unaotafuta hautadumu muda mrefu.

    Mifano mizuri kwa mtu ambaye ameajiriwa na ajira inamkosesha uhuru, anatamani sana kwenda kujiajiri na anapochukua hatua hiyo ndiyo anagundua kwamba kujiajiri kunamtaka kuwajibika zaidi kuliko alivyokuwa ameajiriwa na kwa kuwa hakujiandaa kuwajibika zaidi, basi wengi huishia kushindwa.

    Hatua ya kuchukua, hili tupate uhuru wa kweli ni lazima tuwajibike kweli kweli,kwenye kazi zetu, biashara na shughuli zote. Hakuna uhuru unaokukujia tu ni lazima kuweka kazi, hili baadae tupate uhuru wa kweli.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

    Blog, kufikirichanya.wordpress.com

  • Ni nini dawa ya hofu zote?

    Mojawapo ya uvumbuzi mkubwa zaidi katika ukuzaji wa “mtu wa utendaji ama aliyefanikiwa” ni kwamba hofu yako na kiwango chako cha kujistahi vina uhusiano wa kinyume au kinyume kwa kila mmoja.

    Kwa maneno mengine, unavyojipenda zaidi, ndivyo unavyoogopa kushindwa na kukataliwa. Viwango vyako vya juu vya kujistahi, ndivyo hofu na mashaka ya chini yanavyokurudisha nyuma.

    Kadiri unavyojithamini ndivyo unavyokuwa tayari kuhatarisha na kuvumilia vikwazo visivyoepukika, vikwazo na kushindwa kwa muda kitatokea.

    Njia ya haraka sana ya kujenga kujistahi kwako na kujiamini, na kupunguza hofu ambayo inaweza kuuzuia, ni kurudia mara kwa mara maneno “Najipenda!” wakati wowote unapohisi kuwa na shaka au kukosa raha, anza kujirudia maneno hayo.

    Tabia muhimu zaidi ya dola millioni unayoweza kukuza ni tabia ya kujijengea kujistahi na kujiamini kwa makusudi kila siku. Kadiri unavyolisha akili yako kwa maneno mazuri, unapopata picha ya mambo mazuri na mawzo ndivyo unavyozidi kujiamini, kuwa na matumaini na kutoogopa.

    Kadiri unavyojipenda zaidi, ndivyo unavyofanya vyema katika chochote unachojaribu. Kadiri unavyojipenda, ndivyo utakavyozidi kuendelea hadi ufanikiwe.

    Hatua ya kuchukua, dawa ya hofu ni kujipenda na kujithamini kila siku, kwa hivyo inatupasa tujipende na tujithamani kwanza kabla ya kuwathamini wengine.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

    Kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kusema hapana kunamaanisha nini?

    Mtu anapoamua kusema hapana anamaanisha kwamba hawezi tena kuendelea na kile ambacho kimekuwa kinafanyika.

    Anaweka wazi mpaka kwamba mambo yamekwenda na kupitiliza mpaka kwa kile anachoweza kukubali.

    Hapana inamaanisha kuna mpaka ambao mtu hapaswi kuuvuka, bila ya kujali mamlaka ambayo mtu anayo.

    Mtu anayejua nini anapchopaswa kufanya kwa muda fulani, anaamini kwenye mipaka na pale inapovukwa hawezi kuvumilia hilo.

    Katika harakati ya kuulinda muda wake ni pamoja na kukataa kile ambacho siyo sahihi. Hakuna mabadiliko makubwa kama hakuna msingi sahihi unaosimamiwa na wale ambao wanavunja msingi huo.

    Anayetarajia kufanikiwa kwa tasnia fulani anasema ndiyo au hapana kwa wakati mmoja. Anasema hapana kwa kile kisicho kuwa sahihi na kusema ndiyo kwa kile kilicho sahihi.

    Hatua ya kuchukua, kwa vile tunaishi zama ambazo kilele mwingi umetuzunguka. Kusema hapana kwa mambo yasiyochangia kwenye mafanikio yetu ni chaguo bora kabisa, ambayo unaweza ukafanya kwenye siku yako. Asante Sana.

    Akujaliaye sana.

    Maureen Kemei.

    Email, kemeimaureen7@gmail.com.