Home

  • Njia 20 Za Kisayansi Za Kutafuta Wateja, Kishawishi Na Kufunga Mauzo.

    Rafiki karibu sana leo tunajifunza kuhusu njia za kusaidia kuunda mfumo wa mauzo.

    Njia hizo ni kama yafuatayo;

    1. Weka mfumo wa mauzo ulio wazi, ( mauzo ya uhakika bila kutegemea bahati). Mchakato unaoeleweka wa kupata wateja.
    2. Gawa majukumu ya mauzo. Kila mmoja kazi yake inakuwa ni kutekeleza majukumu yaliyopo kwenye biashara.
    3. Usitumie muda mwingi na watu wasio na nia ya kununua. Njia ya maswali ni rahisi kukufanya uweze kibaini hili.
    4. Uza kwa njia ya kujenga mahusiano na siyo kulazimisha. Tuwafanye wateja kuwa rafiki zetu.
    5. Wekeza kwenye utafutaji wa wateja kila siku.
    6. Tumia simu na ujumbe wa moja kwa moja kwa ufanisi.
    7. Tengeneza mfumo wa rufaa au (refferal) .
    8. Wekeza katika kuwaelimisha wateja wako.
    9. Andika ujumbe wa mauzo wenye ushawishi mkubwa.
    10. Fuata mfumo wa kujenga uaminifu kwanza, kisha uza.
    11. Hakikisha una data sahihi ya wateja kama jina, namba kwa usahihi.
    12. Kuwa na mfumo wa kufuatilia wateja mara kwa mara hadi waoneshe nia ya kununua .
    13. Usiogope kutafuta wateja wapya ( cold calling) unaanza kwa kwa ujumbe mdogo mdogo baadae unampigia.
    14. Toa huduma bora wauzie kitu ambacho ni bora.
    15. Usitumie bei kama sababu pekee ya kumshinda mteja. Onyesha thamani ya bidhaa yako kwanza, ili usimpoteze baada ya manunuzi ya mwanzo tu.
    16. Wekeza katika mafunzo. Mafunzo ya ndani.
    17. Tumia mitandao ya kijamii vyema.
    18. Tumja shuhuda halisi za wateja wenye mafanikio. Wateja wengi wanapenda kufuata mkumbo.
    19. Tumia mfumo wa kurahisisha malipo, ili usipoteze wateja.
    20. Tumia mfumo wa mrejesho wa huduma ( feedback).

    Chukua hatua rafiki, wewe kama muuzaji uza kila siku, fuatilia wateja wako.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Ushauri Ambao Ningependa Kuwaambia Watoto Au Mtu Yeyote Ili Kuwa Na Maisha Bora Yenye Mafanikio Na Anthony Pompliano Kwenye Kitabu Chake Cha ( How To Live An Extraordinary Life).

    Rafiki yangu mpendwa Anthony aliandikia watoto wake barua, huku anajishauri yeye mwenyewe kuhusu maisha aliyoyapitia.

    Mahali alipopotia yeye aliandika barua 65. Karibu sana tujifunze.

    1. (How you do anything is how you do everything). Kwa mfano mchelewaji ndiyo asili yake, itakuathiri wewe iwe kazi ya mtu au kazi yako.
    2. (Today is a practical of tomorrow). Mafanikio siyo ajali. Tabia za kila siku kidogo kidogo ndiyo mchakato wako wa mafanikio.
    3. Yachonge kwenye jiwe maadili yako, maoni ya watu yaandike kwenye mchanga. Usiivunje maadili yako ya uaminifu.
    4. Smartest people read books 📚. Hautafanikiwa kwa kitu unacholazimishwa kufanya, bali utafanikiwa kwa kulazimishwa kuacha kufanya kwa mfano unapozuiwa kusoma unafaulu.
    5. Kukubali unapokosea. Makosa ni sehemu ya kujifunza. Kwa kukubali kuwa umekosea unajipa fursa mpya ya kufanya tena na kusonga mbele.
    6. Ubora hauna saa. Warren Buffett alianza kuwekeza akiwa na miaka 11, alianza kuwa billionea akiwa na miaka 40. Ukiharakisha mambo unaishia kupoteza.
    7. (Do it right do it light). Watu wanafanya kwa usahihi, linarahisisha mfumo.
    8. (Build things). Ili kuwa na maisha bora lazima kuna kitu unakijenga. Kwa mfano jenga biashara ilete matokeo makubwa, jenga huduma, jitoe ili kitu kiishi miaka mingi baada ya wewe kupita.
    9. (Action). Ukijifunza kitu chochote, chukua hatua.
    10. Maliza kitu ulichoanza. Mafanikio inachukua zaidi ya miaka kumi kwa mtu kufanya kitu na kufanikiwa, jipime mwenyewe.
    11. (Luck is not real). Tunatengeneza bahati zetu wenyewe. Kwenye maisha mambo yanaweza kutafsiriwa kwa uzuri au ubaya. Kwa mfano mtu kufukuzwa kazi na baadaye kupata kazi nyingine nzuri zaidi au kufanikiwa kwenye biashara.
    12. (Write two pages a day). Ndani ya mwaka mtu ana kitabu, andika jukumu moja kwa siku hatimaye unapata mwendo.
    13. Usijilinganishe na walio chini yako, bali jilinganishe na walio juu yako kimafanikio.
    14. Jenga sifa yako. Kwenye kitu ambacho hakiwezi kupotea. Vitabeba jina lako. Tambulika kwa sifa zako mwenyewe sio cheo chako.
    15. Uzoefu wa miaka mbili mara tano au uzoefu wa mwaka moja mara kumi. (Learning curve) Hujifunzi kitu kipya kila wakati. Lazima kila wakati uendelee kuwa bora zaidi, usiwe mzoefu ambaye husogei.

    Chukua hatua, rafiki yangu mpendwa huu ndio ushauri ambao tunapaswa kufanyia kazi sisi wenyewe kwanza kabla ya kuwashuri watoto wetu au watu wengine. Mimi naifanyia kazi sasa hivi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya Kufuata Mkumbo Kwenye Kufanya Manunuzi (social proof).

    Rafiki yangu mpendwa kama wengi wananunua na wewe unakimbilia hapo kununua . Hivyo tunaamini katika wengi, wengi wanaiga kwenye kununua vitu. Wanaofanya maamuzi kwa mantiki ni asilimia 5 tu, wengine wanafuata mkumbo.

    Njia kumi za kutumia kuongeza mauzo kwa kutumia social proof ni kama yafuatayo;

    1. Tumia wateja. Watu wanapenda waone wengine waliotumia bidhaa ndiyo watu wengine wanunue kwa mfano celebrities wakitumia bidhaa fulani inawashawishi wateja wengine kununua.
    2. Onyesha idadi ya wateja wanaotumia bidhaa zako. Kwa mfano vodacome ina wateja zaidi ya 15 millions . Inafanya wateja wengine kutumia mitandao hiyo.
    3. Matumizi ya (influencers) au wenye mamlaka. Tafuta mtu mwenye ubalozi kwenye kutangaza biashara yako. Mfano pepsi na diamond.
    4. Tumia ( user generated content). Wasanii wanaopenda kupata huduma.
    5. Endorsement from big brands kwa mfano NBC bank inavyoshirikiana na vilabu vya Tanzania.
    6. Matumizi ya takwimu na utafiti za masoko . Takwimu zinaongeza imani ya wateja bidhaa au huduma. Kwa mfano benki ikisema 90% ya wafanyabiashara wanatuamini kwa mikopo nafuu.
    7. Matumizi ya kuweka uharaka na uhaba. Watu wanapenda vitu kabla havijaisha. Mfano usiseme mzigo uko vya kutosha. Watu hawaharakishi kuja kununua.
    8. Maoni ya ukadiriaji wa wateja. (Ratings and reviews). Mfano app zina nyota ngapi, reviews za wateja kwa mfano booking.com, wahimize wateja waache maoni. Google reviews.
    9. Matumizi ya teknolojia, chat box. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara, inasaidia wateja waone wanajibiwa haraka.
    10. Kuonesha miradi ya kijamii jinsi inavyofanya kazi. Kwa mfano coca-cola company kujenga visima vijijini. Inaongeza imani kwa wateja. Taasisi zinatoa pole kwa majanga, kwa mfano kariokoo jengo liliporomoka unatuma salamu za pole na kuitambulisha biashara yako. Watu wanaona unajali jamii.

    Chukua hatua, rafiki wengi wanapofanya jambo fulani tunafikiri ndiyo jambo jema, hivyo hufanya wengi zaidi kufanya jambo hiyo hiyo. Kwa sababu penye wengi hapaharibiki kitu, kwa sababu wengi wape, tunapaswa kutumia mbinu hizi kwenye kutangaza biashara zetu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 10 Ya Kufanya Ili Kutenga Muda wa Kusoma Na Kuandika.

    Rafiki yangu mpendwa ikiwa unataka kutenga muda wa ufanisi wa kuandika, kusoma au kufanya mazoezi licha ya ratiba yako yenye shughuli nyingi.

    Hapa kuna mawazo kumi ya kuboresha upangaji ea muda wako.

    1. Unda ratiba ya kipaumbele. Tengeneza ratiba inayoweka vipaumbele kwa kila siku. Amua ni wakati gani unafanya kazi bora zaidi kwa kila shughuli.
    2. Tumia mbinu ya pomodoro. Tumia mbinu ya pomodoro kama dakika 25 za kazi, dakika 5 Za kupumzika. Kwa mfano, unaweza kuandika kwa mzunguko mmoja, kusoma na baadaye kufanya mazoezi.
    3. Anza na shughuli fupi kisha ongeza taratibu. Anza na muda mfupi kwa kila shughuli, kama dakika 10 kwa kila moja, kisha ongeza muda polepole ili kuzoea.
    4. Unganisha shughuli kwa njia ya tabia. Unganisha tabia mpya na tabia zilizopo . Mfano: soma baada ya kifungua kinywa.
    5. Tumia kalenda au programu ya kudhibiti muda. Tumia programu kama Google calendar, notion, au todoist kupanga na kufuatilia maendeleo yako.
    6. Chagua mandhari au sehemu maalum kwa kila shughuli. Tafuta sehemu tulivu kwa ajili ya kusoma na kuandika, na eneo tofauti kwa mazoezi ili kuepuka kuchanganya shughuli.
    7. Punguza mambo yanayovuruga umakini. Zima arifa zisizo za lazima kwenye simu au kompyuta wakati wa kufanya kazi.
    8. Tumia kipindi cha mpito. Badala ya kupoteza muda kati ya shughuli, tumia muda huo kusoma makala fupi, kufanya mazoezi mafupi.
    9. Jenga nidhamu na uwe mvumilivu. Lazima uwe na msimamo. Anza kwa muda mdogo, lakini usikate tamaa. Taratibu, utapata mwelekeo sahihi.
    10. Pitia na rekebisha ratiba kila wiki. Kila mwisho wa wiki, pima ufanisi wa muda wako na fanya marekebisho yanayohitajika ili kuendelea kuboresha mpango wako.

    Chukua hatua, kwa mbinu hizi, utaweza kusawazisha muda wako vyema kwa ajili ya kuandika, kusoma na kufanya mazoezi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Ya kudhibiti Hasira( Ustoa).

    Rafiki yangu mpendwa hasira ni asili ya binadamu ila inatupasa tujidhibiti. Hisia zikiwa juu uwezo wa kufikiri unakuwa chini.

    Tunapaswa kukabiliana na changamoto yoyote ambayo yanajitokeza, kuna mambo yaliyopo ndani ya uwezo wetu na mengine yapo nje ya uwezo wetu.

    Sisi sio viranja wa dunia. Kufanya kazi ipo ndani ya uwezo wetu. Kazi isipokamilika ndani ya muda uliotegemea, utegemee pia hilo linaweza kutokea.

    Karibu tujifunze kutoka kwa wanafalsafa wa kale walisemaje kuhusu hasira.

    1. Watu wanakoseshwa na ‘views’ zao, ni kwa sababu ya tafsiri zetu zinazotokea. ‘Men are not disturbed by their actions but their views on them.’
    2. Usiruhusu hisia zako zikuongoze, zisiwe na nguvu juu yako, angalia tukio kwa utulivu. Ukipata hasira usitoe maamuzi yote kwa pamoja, toka hapo nenda sehemu nyingine. Andika chochote kuhusu mtu huyo. Baada ya muda hasira zinaisha. Waelewe watu ili wasikupe shida.
    3. Ukiwa unaweza kuvumilia basi usilalalamike. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako kinapaswa kutokea, yapokee yalivyo.
    4. Hakuna kinachokufanya ukasirike zaidi ya mawazo yako mwenyewe. Badilisha mawazo yako utapata amani. Mtu asipokuitikia, labda ana mawazo mengine, chukulia vitu vilivyo.
    5. Usiwe mtumwa wa hisia zako. Dhibiti hisia zako na akili zako zitakutii. Wenzi marafiki tumepewa kwa muda. Asili ikizitaka zitawaondoa tu mfano kifo n.k. Ukiwa mu wa hasira utaweza kufa mapema.

    Rafiki hasira inaweza kutukosesha amani na utulivu kwenye maisha yetu. Tunapaswa kubadilisha mawazo yetu ili tupate amani na amani.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Muuzaji Bora Kuwahi Kutokea Joe Girald

    Rafiki yangu mpendwa Joe Girald ambaye ni muuzaji bora kuwahi kutokea alivunja recodi ya dunia akiwa muuzaji bora wa magari huko Michigan.

    Mambo sapa ya kuondoka nayo ni kama yafuatayo;

    1. Nguvu ya mtazamo chanya. Maisha ni mwalimu bora sana hata kama huna chochote ukiwa na mtazamo mkubwa unaweza na ukapambana kwa ukubwa na kwa msimamo unafanikiwa, ila uwe kwenye njia sahihi. Girald alianza kupata mafanikio akiwa na miaka 35.
    2. Kila kitu kinaanza na nia na njia. Joel alianza kwa kuchukua orodha ya wateja na kuanza kuwauzia. Mambo ya msingi kwenye kuuza ni kujua kile mteja anataka, unaweza kupata unachotaka kama utampatia mteja anachohitaji.
    3. Hakuna mteja msumbufu. Usimchukulie mteja kama ni msumbufu bali anataka uhakika. Kama Kuna kitu mteja hajakielewa, hajakiamini tumia kila namna ujibu maswali yao.
    4. Kanuni ya Gerald ya 250 . Kila mtu ana watu 250 walioko nyuma yake hivyo ukiwahudumia vizuri utapata matokeo mazuri. Ukiwahudumia vibaya utapoteza kwa mmoja utapoteza 250.
    5. Zana za mauzo. Alitumia muda mwingi kijA na kufundisha. Kuweka record ya kumbukumbu ya wateja na jinsi ya kuwafuatilia.
    6. Uaminifu. Ndiyo sera bora zaidi ya kuweza kutumia. . Ukifuata utaweza kufanikiwa zaidi. Kuwa mkweli mara zote, watendee wateja kama unavyotaka utendewe wewe.
    7. Fanya intelijensia. Mauzo ni vita baridi. Ukiweza kusanya taarifa nyingi sana kwa wateja wako.

    Rafiki hayo Mambo sapa ya kujifunza ili kuboresha mauzo yetu na hakika tukifanyia kazi tutakuwa wauzaji bora kuwahi kutokea.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Namna Ya Kukamilisha To Do List Yangu.

    Rafiki yangu mpendwa ni changamoto ipi umekuwa unakutana nazo kwenye kupangilia siku yako vyema.

    Leo tunajifunza njia nzuri ya kuipangilia siku yetu vyema. Mambo hayo ni kama yafuatayo;

    1. Anza siku yako kwa kutafakari. Unapoamka asubuhi jiambie leo unaenda kukutana na watu watakaokuzingua, watakaokuangusha.
    2. Weka lengo la siku. Weka jambo moja na ulikamilishe ili kuwa na siku yenye mafanikio. Kufanya kitu kimoja kwa ustadi ni bora kuliko kufukuzana na mambo mengi.
    3. Kuweka vipaumbele. Peleka nguvu zako kwenye mambo ambayo unaweza kuyazithibiti, na mengine achana nayo.
    4. Jitahidi kukamilisha kazi muhimu mapema. Usijaribu kutoroka majukumu, pangilia yaliyo muhimu na msingi zaidi kabla hujavurukwa na mambo mengi. Kila maamuzi unayofanya yanatumia nguvu ya akili. ‘Eat that frog ‘
    5. Jifunze kila siku. Mazoezi ya mwili ni kujifunza. Kujifunza unaokoa muda na una onaongeza ufanisi kwenye kitu hicho unachojifunza.
    6. Weka muda wa kukamilisha vitu vya kawaida. Tenga muda wa usumbufu. Fanya kilicho muhimu yanayobaki ni ya ziada tu.
    7. Jioni tafakari siku yako mzima. Kama kipi nimefanya vizuri Leo? Kipi nimefanya vibaya leo? Vipi ni vitu vya kuboresha leo?.
    8. Kubali mambo yasiyoweza kubadilika. Huwezi kubadilisha upepo lakini unaweza kubadilika wewe ili kuendana na hayo.
    9. Fanya vitu kwa NIDHAMU kali sana. Kuna muda wa kukubali kila kitu na kuna wakati wakukataa vitu vyote. Kadiri unavyokataa vitu vizuri ndivyo unavyoruhusu kitu kilicho bora zaidi like. Nidhamu ndiyo funguo ya uhuru.
    10. Soma vitabu kwa ajili ya maendeleo ya kila siku. Jifunze kitu ambacho utakifanyia kazi moja kwa moja.

    Rafiki kwa kuzingatia mambo haya utaweza kuishi siku yako kwa mafanikio zaidi. Tabia ya kitajiri ni kuwa bora zaidi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 7 Ya Kuzingatia Wakati Wa Kutoa Huduma Kwa Wateja.

    Rafiki yangu mpendwa leo tunajifunza kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutoa huduma bora kwa wateja.

    Mambo hayo ni kama yafuatayo;

    1. Kujifunza kujua mahitaji ya wateja. Kwa kuuliza maswali litasaidia kuhudumia vizuri wateja.
    2. Kuwa na lugha nzuri ya mwili na maneno, tumia lugha ya heshima inayojenga mahusiano na watu.
    3. Kutoa huduma ya haraka na ufanisi. Watu wanahitaji uharaka, mtu wa kupokea wateja kuwasaidia kusubiria kama kuangalia tv, gazeti au pipi.
    4. Kuzingatia maoni ya wateja; kama mmiliki wa biashara, tenga muda wa kupitia wateja wako.
    5. Kujenga uaminifu; hakikisha unatekekeza ahadi zako kwa mfano kama kutoa offers.
    6. Kuwa na muonekano mzuri; Watu wananunua wewe kabla ya bidhaa zako k.m. nywele, mavazi zako.
    7. Kumfuatilia mteja; Kama huduma aliyopata ameifurahia n.k. kama ana maoni kuhusu huduma yako ili waweze kurudi tena.

    Chukua hatua; huduma bora kwa wateja inajenga uaminifu, mahusiano mazuri, na jina zuri la biashara.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Mawazo 10 Ya Kuboresha Kwenye Tabia Ya Kuamka Mapema.

    Rafiki yangu mpendwa karibu leo tujifunze mambo ya kufanya ili tuweze kuamka mapema na kuweza kupanga siku yetu na kufanya yale tumepanga kwa mafanikio makubwa.

    Mawazo haya kumi ni kama yafuatayo;

    1. Panga muda wa kulala. Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kwa kupanga muda wa kulala mapema.
    2. Tumia kengele ya saa. Weka kengele mbali na kitanda chako ili uwe na sababu ya kusimama kuizima.
    3. Andaa mazingira ya kulala. Zima taa na vifaa vya eletroniki kama simu saa moja kabla ya kulala ili kusaidia mwili kupumzika.
    4. Unda ratiba ya asubuhi. Panga shughuli unazotaka kufanya mara baada ya kuamka, kama mazoezi au kusoma, ili upate motisha ya kuamka.
    5. Epuka kutumia simu usiku. Mwanga wa simu unaweza kuchelewesha usingizi. Badala yake, soma kitabu au mediti kabla ya kulala.
    6. Tumja mwanga wa asili. Fungua mara tu unapoinuka ili kupata mwanga wa jua, ambao husaidia kuamsha mwili.
    7. Anza na hatua ndogo. Ikiwa unataka kuamka mapema, badilisha muda wako wa kuamka kwa dakika 15 mapema kila siku mpaka ufikie lengo.
    8. Lala ukiwa umeshiba kidogo. Usilale ukiwa na njaa au umeshiba kupita kiasi. Kula mlo mwepesi kabla ya kulala.
    9. Fanha mazoezi ya mchana au jioni. Mazoezi husaidia kuboresha usingizi, lakini usifanye mazoezi makali muda mfupi kabla ya kulala.
    10. Jiwekee malengo ya asubuhi. Tafuta sababu ya maana ya kuamka mapema, kama muda wa kufanya mazoezi, kujifunza kitu kipya, au muda wa utulivu.

    Chukia hatua; kujifunza kuamka mapema ni mchakato, lakini kwa uvumilivu na nidhamu utafanikiwa.

    Rafikk yako,

    Maureen Kemei.

  • Mawazo 10 Ya Kuboresha Kwenye Mchakato Wa Kuweka Malengo.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini leo tunajifunza mawazo kumi ya kuboresha mchakato wa kuweka malengo.

    1. Tumia Mfumo Wa SMART: Hakikisha malengo yako ni mahususi (special), yanayopimika ( Measurable), Yanayoweza kufikiwa ( achievable), yanayohusiana ( relevant), na yenye kipindi maalum ( time boud).
    2. Gawanya malengo makubwa: Vunja lengo kubwa katika hatua ndogo ndogo ili lisionekane gumu kufanikisha.
    3. Andika Malengo Yako: Kuandika malengo husaidia kuyakumbuka na kuyapa kipaumbele.
    4. Weka Kipaumbele: Jua malengo gani ni ya haraka na muhimu zaidi, kisha uyape nafasi ya kwanza.
    5. Pima Maendeleo Yako Mara Mara: Chukua muda kila wiki au mwezi kitathmini jinsi unavyosonga mbele.
    6. Weka Kipimo Cha Mafanikio: Eleza wazi matokeo unayotarajia na jinsi utakavyopima ikiwa umeyafikisha:
    7. Epuka Kuweka Malengo Mengi Sana: Zingatia malengo machache ili uelekeze nguvu na rasilimali zako vizuri.
    8. Tafuta Usaidizi Au Ushauri. Jadili malengo yako na mtu unayemwamini ili kupata maoni na msaada wa ziada.
    9. Adhibu Au Zawadia Nia Yako: Jipe zawadi unapopata mafanikio madogo, au weka adhabu ndogo kama njia ya kujihamasisha.
    10. Jifunze Kutoka Kwa Kushindwa: Ukishindwa kufanikisha lengo, chunguza sababu, jifunze, na rekebisha mchakato wako ili kuboresha siku zijazo.

    Chukua hatua; rafiki hakikisha unajitahidi kuwa thabiti na kuzingatia lengo la muda mrefu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.