Home

  • Jinsi ya kuua sauti ya kukatisha tamaa iliyo ndani yako.

    Rafiki yangu mpendwa kila mmoja wetu huwa ana sauti ya kukatisha tamaa ambayo ipo ndani yake. Ni sauti hiyo ndiyo kikwazo kwa wengi kufanya makubwa.

    Bila kuua sauti ya ndani, utakuwa unapanga mambo mengi sana, lakini haitakamilika. Maana sauti hiyo haitaki kukuona ukiteseka, itatumia kila ushawishi kuhakikisha husumbuki na mambo makubwa.

    Tunapaswa kuwa bize sana na kile tunachotaka kiasi kwamba sauti hiyo inakosa kabisa nafasi. Kila kinapotaka kuja haipati nafasi. Msukumo wako kwenye kile unachotaka unakuwa mkubwa kiasi kwamba hakuna kinachoweza kukuyumbisha.

    Rafiki yangu kujilazimisha kufanya kitu, huwa kinachosha, lazima nini na kwa nini kubwa kwenye kile unachotaka.

    Inabidi tubishane na akili yetu na hapo ndipo sauti unapopata nafasi ya kutushawishi, kwa nini yangu inapokuwa kubwa.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Nguvu wa kuwa mkimya.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wengi huchukulia ukimya kuonekana kama ni kutokujua . Hakuna kitu chenye nguvu kama ukimya, hasa inapotumika vizuri.

    Kuna nguvu kubwa mbili za ukimya. Moja ikiwa ni kutokuweka wazi mambo yako.

    Inasemekana kuwa hata mpumbavu akikaa kimya atadhaniwa ni mtu wa hekima. Hakuna kitu kinachowaanika watu kama kuongea sana. Unapokuwa mkimya watu wanashindwa kukuelewa, hivyo wanakuheshimu zaidi.

    Ukiwa mwongeaji sana watu wanakuzoea na kukudharau maana tayari wanajua kila kitu kuhusu wewe.

    Kanuni za madaraka ambazo Robert Green ameandika kwenye kitabu Cha 48 laws of power ambapo inasema, always say less than necessary, akimaanisha mara zote ongea kidogo kuliko inavyohitajika.

    Kadiri unavyoongea zaidi ndivyo unavyoonekana wa kawaida na kudharaulika.

    Pili ni kumsukuma mtu kuongea bila ya kumwonyesha moja kwa moja. Unapokuwa unazungumza alafu ukakaa kimya, watu hao hawatafurahia hali hiyo ya ukimya, watalazimika kuongea zaidi kujaza ombwe.

    Katika kuongea kwao ndipo utajua mengi kuhusu wao na kuweza kuwashawishi.

    Kuchukua hatua; rafiki tunapaswa tuwe wasikilizaji makini pale mtu mwingine anapoongea. Kwa kufanya hivyo utafanya anayeongea aone unajali sana kuhusu kile anachoeleza.

    Kwa yeye kuona unajali anafunguka kukuelezea zaidi na zaidi.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi ya kuacha kijilinganisha wengine.

    Ragiki yangu mpendwa hakuna kitu kinachowaangusha wengi kama kijilinganisha na wengine.

    Kwa sababu haijalishi umepiga hatua kiasi gani, kuna mtu mwingine ambaye amepiga hatua zaidi yako.

    Ukianzia kijilinganisha na watu, unaingiwa na wivu kwa kuona wamekuzidi na hilo litaathiri mahusiano yako na watu hao.

    Sisi binadamu huwa hatuwezi kuficha hisia zetu, hivyo hisia zozote ulizonazo kwa wengine huwa zinajiweka wazi unapokuwa nao. Hivyo hata kama utaficha kiasi gani, bado watu watajua hisia ulizonazo juu yao.

    kuepuka hilo, acha kijilinganisha na yeyote, mpendwa na kumheshimu kila mtu ukijua kila mtu yuko kwenye njia yake ya maisha.

    Muhimu zaidi usiwachukie wale waliofanikiwa kuliko wewe . Kwenye jamii nyingi matajiri wamekuwa wakipewa majina mabaya na kuonekana ni watu wabaya, hakikisha huingii kwenye mkumbo huo.

    Ukiwachukia matajiri kamwe huwezi kuwa tajiri, hivyo wapende wale waliofanikiwa kuliko wewe, wapende kweli kutoka ndani yako na hilo litakufanya uwe tayari kujifunza kutoka kwao na wewe uweze kufanikiwa pia.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu ondokana na fikra na hisia zozote hasi, hizo ni kikwazo kwako kufanikiwa. Mara zote kuwa na hisia na fikra chanya ambazo zitakusuma kufanikiwa zaidi.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Unajua upo zaidi ya unavyojijua?.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini falsafa na mafunzo mengi ya kiroho huwa yanatufundisha kwamba sisi ni zaidi ya tunavyojijua. Kuna nguvu kubwa ambayo iko ndani ya kila mtu, lakini wengi hawajui wala kuifikia kwa sababu wamevurugwa na usumbufu unaowazunguka.

    Pia wengi haitaki jamii wajue wana nguvu, kwa sababu watakuwa huru na jamii haitaweza kuwatumia watakavyo.

    Unapofanya tahajudi, unapata nafasi ya kuijua na kuifikia nguvu kubwa iliyo ndani yako na kuweza kuitumia Ili kuwa huru kabisa na maisha yako na huku ukifanya makubwa.

    Rafiki yangu jinsi ulivyosasa ndiyo jamii imekutengeneza, ili uendane nayo na iweze kukutumia. Kama unataka kuwa na maisha sahihi kwako, lazima uachane na mazoea yote uliyonayo sasa na kuanza kufanya maamuzi yako upya, kwa kuyafikiri mwenyewe kwa kina.

    Kuchukua hatua; idhibiti akili yako mwenyewe na utaweza kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwako. Utaacha kuwa mtumwa wa jamii na watu na utaweza kufanya makubwa.

    Rafiki yako mkubwa,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    Jiunge na mtandao huu n ataweza kupata makala mazuri zaidi kwenye email yako.

  • Kuchagua kuwa huru.

    Rafiki yangu mpendwa utajiskiaje kama ungepewa uhuru au ungepata uhuru wako mwenyewe, wa kukuwezesha kuendesha maisha yako jinsi unavyotaka.

    Kitu kigumu kabisa kwenye maisha siyo kufanya unachotaka, bali kujua unachotaka. Hiki ndiyo kigumu kwa sababu hakuna anayeweza kukujiambia nini unataka, ni kitu kinachotoka ndani yako mwenyewe.

    Sasa kwa kuwa wengi hawajisikilizi na kujua nini wanataka, wamekuwa wanahangaika na mambo mengi yasiyokuwa sahihi kwao, matokeo yake hawafanikiwi.

    Kabla hujafanya màamuzi rafiki yangu usitegemee yeyote akuambie nini unataka, wengi wanaokuambia unachotaka na hawajui hata wao wenyewe wanataka nini.

    Hilo ni zoezi la wewe mwenyewe kufanya, kwa kujisikiliza na kujaribu vitu mbalimbali mpaka kujua kile hasa unachotaka.

    Naval anatuambia kutoka kwenye kitabu chake cha ‘ The Almanack of naval Ravikant’ kwamba kitu kikubwa kabisa anachothamini kwenye maisha ni uhuru.

    Zamani alikuwa anathamini uhuru wa kuwa na vitu anavyotaka, lakini sasa anathamini uhuru wa ndani, uhuru wa kuepuka vile asivyotaka.

    Anachotaka ni uhuru wa kutokuwa na hasira, kutokuwa na huzuni na kutokulazimika kufanya asichotaka.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu ushauri ambao Naval ansema angejiambia alipokuwa kijana ni kuchagua vile anavyotaka kuwa badala ya kujizuia kwa namna yoyote ile.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    Mawasiliano:

    kemeimaureen7@gmail.com.

    Jiunge na mtandao wetu Ili uweze kupata makala mazuri kama hayo.

  • Namna ya kuchagua kubadilika.

    Rafiki yangu mpendwa Naval anatuambia kutoka kwenye kitabu chake cha ‘ The Almanack of naval Ravikant’ kwamba nguvu kubwa kwenye maisha ni mtu kuweza kujibadili mwenyewe.

    Maisha yataenda kama yanavyotaka kwenda yenyewe. Kuna mambo yatakuwa mazuri kwako na mengine kuwa mabaya kwako. Lakini hayo yote ni matokeo ya tafsiri unayojipa kwenye mambo yanayotokea.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili kuwa bora, lazima uwe tayari kubadilika, lazima uanze kwa kubadili tafsiri uliyonayo kwenye yale yanayotokea na pia uwe tayari kubadili tabia zako.

    Ili kuhakikisha unabadilika kweli, unapaswa kutumia nguvu ya nje kukusukuma. Moja ya njia unazoweza kutumia ni kuwaambia watu unaowaheshimu ni tabia gani unataka kujenga au kuvunja na kuwaomba wakufuatilie.

    Kwa kujua wale unaowaheshimu wanakufuatilia, utajisukuma kuchukua hatua. Kama umejiambia mwenyewe ni rahisi kujidanganya na kuacha kuchukua hatua, hasa pale mambo yanapokuwa magumu.

    Na kama hutaki kuchukua hatua fulani, jiambie wazi na siyo kujidanganya. Badala ya kujiambia hujawa tayari au utafanya kesho, jiambie tu ukweli kwamba hutaki kufanya, na hapo itakuwa dhahiri kwako kwamba unajizuia mwenyewe kuwa na maisha unayotaka.

    Kuchukua hatua; chochote unachotaka kufanya, anza kukifanya mara moja, huna haja ya kusubiri, muda haukungoji wewe, unazidi kuzeeka. Fanya unachotaka kufanya na kifanye sasa, huu ndiyo muda ulionao.

    Kitu kimoja zaidi rafiki kwenye chochote unachofanya, jipe muda, matokeo huwa hayaji kama unavyotaka. Wajibu wako ni kuchukua hatua sahihi, matokeo sahihi yatakuja wakati wake.

    Usiache kuchukua hatua kwa sababu matokeo sahihi hayaji, kama unachukua hatua sahihi, jua matokeo sahihi yatakuja kwa muda wake.

    Asante sana,

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    Jiandikishe hapa hili uweze kupata makala mazuri zaidi kwenye email yako.

  • Namna ya kuchagua kuwa wewe.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini umekuwa unahangaika kujiambia unapaswa kuwa hivi, kufanya kile au kuwa kama wale. Yote hayo huyahitaji.

    Unachopaswa kufanya ni kile unachotaka kufanya, kile kinachotoka ndani yako na siyo kuiga wengine. Unapochagua kufanya kile unachotaka, kwa kujisikiliza wewe mwenyewe, unakuwa umechagua kuwa wewe.

    Kama unataka kuwa wa tofauti duniani na kuepuka ushindani wa wengine, basi chagua kuwa wewe. Hakuna anayeweza kukushinda wewe kuwa, kwa sababu hakuna aliye kama wewe.

    Jifunze kupitia wengine, lakini usijaribu kuiga, usitake kuwa kama mwingine yeyote, jifunze utakavyo, lakini kuwa wewe, ambaye inazidi kuwa bora zaidi kila siku.

    Kila mtu kuna kitu cha pekee alichonacho, kuna ujuzi, uwezo na msukumo wa kipekee ulio ndani yako ambavyo kwa wengine hakuna.

    Mtu anachagua kuwa yeye na kuuishi utofauti wake, hakuna anayeweza kumshinda, kwa sababu hakuna aliye na vile alivyonavyo yeye.

    Lengo lako kwenye maisha ni kutafuta watu ambao wanakuhitaji wewe kweli, wananufaika na kile cha kipekee unachoweza kufanya na Kisha kuwapatia watu hao kitu hicho. Hiyo ndiyo njia ya uhakika kufanikiwa.

    Hatua ya kuchukua; baada ya kuchagua kuwa wewe, unapaswa kuwa na hamasa na msukumo mkubwa wa kufanya kile ambacho wewe tu ndiye unayeweza kufanya.

    Tunapaswa kuwa tayari kukifanya kwa viwango vya juu na kwa muda mrefu hata kama hakuna anayekulipa.

    Ni kiwango hicho cha msukumo ndicho kitazidi kukutofautisha na kuwafanya wengine wawe tayari kukulipa kwa manufaa unayowapa.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi furaha inavyojenga tabia.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini amani na furaha ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza na kujijengea.

    Siyo vitu ambavyo mtu anazaliwa navyo au kurithishwa na wala havitokei kwa bahati mbaya, vinatengenezwa.

    Kila mtu anaweza kujijengea amani na furaha na kukuza viwango vyake kama anaamini inawezekana na kujua hatua sahihi za kuchukua Ili kufikia hilo.

    Kama ilivyo kwenye kazi, mahusiano, biashara na fedha, furaha pia ni ujuzi mbao mtu anaweza kujijengea anapojua hatua sahihi za kuchukua.

    Hatua ya kwanza kwenye kujijengea ujuzi wa amani na furaha ni kukubali na kuamini kwamba vitu hivyo ni ujuzi unaoweza kujijengea.

    Hii ni gumu kwa sababu kwa maisha yako yote imekuwa unaamini tofauti na hivyo. Lakini unapoamini na kuchukua hatua, unapata matokeo ya tofauti.

    Furaha ni matokeo ya tabia ambazo mtu unakuwa umechagua kuziishi kwenye maisha yako. Wakati unazijenga tabia unaweza usione madhara yake, lakini zinapokuwa zimeimarika ndiyo unaona jinsi zilivyo na madhara kwenye maisha yako kwa ujumla.

    Kitu kingine kinachoathiri furaha ya mtu ni mahusiano anayojijengea. Kama mtu anazungukwa na watu wasio na furaha, watu ambao wanafikiri hasi, wamekata tamaa na hawana furaha, ni rahisi kwa watu kubeba tabia hizo kutoka kwa wanaomzunguka. Unapaswa kuwa makini na furaha yako kwa kuhakikisha unaozungukwa nao watu wenye furaha pia.

    Kuchukua hatua; tunapaswa kuchagua kwa umakini watu wa kushirikiana nao kwenye mambo mbalimbali. Na muhimu zaidi tuepuke watu wanaopenda ugomvi, maana hao huwa hawakosi kitu cha kugombana.

    Pia mtu yeyote unayechagua kufanya naye kazi, hakikisha unamkubali kwamba unaweza kufanya naye kazi kwa maisha yako yote, kama huwezi hivyo, usifanye naye hata kwa siku moja.

    Yakubali maisha yako na jihusishe na wale walioyakubali maisha yao na wenye furaha.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Umuhimu wa kuwa na utulivu kwenye maisha yako.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini utulivu ni muhimu sana kwenye maisha yako.

    Blaise Pascal amewahi kusema matatizo yote ya mwanadamu ni matokeo ya mtu kushindwa kukaa peke yake kwa utulivu ndani ya chumba.

    Pata picha kama ukiweza kukaa peke yako kwa angalau nusu saa na bila ya kusumbuliwa au kuhangaika na chochote huku ukiwa na furaha, basi umefanikiwa kweli.

    Lakini siyo kukaa na kufikiria mambo mengine, kukaa na kuwa na utulivu mkubwa, bila ya kufikiria mambo yasiyo hapo ulipo, kuwa na tamaa au hofu.

    Kabla hujafanya maamuzi nataka nikujulishe kwamba, kuwa mwenye furaha ni zao la amani, kama una amani ndani yako, lazima utakuwa na furaha.

    Lakini amani ni kitu kigumu kwa wengi kufikia, kwa sababu huwa tunatafuta amani kwa vitu. Kuna vitu za ndani yetu mwenyewe na vitu za nje kwenye kupambana na wengine.

    Rafiki yangu ukiweza kuepukana kabisa na vita hizo, unakuwa na utulivu wa ndani na hivyo kuwa na furaha.

    Kitu kimoja zaidi furaha na amani vinashahibihiana, amani ni furaha iliyotulia wakati furaha ni amani iliyo kwenye mwendo.

    Huwezi kuvitofautisha hivyo viwili. Ukiwa mtu mwenye amani, kila unachofanya kinakuwa cha furaha.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu huwezi kufikia amani kwa kumaliza matatizo yote ya nje, hayo huwa hayaishi. Pia ili kufikia amani kwenye matatizo ya ndani, ni kuacha kuyaangalia kama matatizo.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    uamshobinafsi.com.

  • Njia mbili za kuishi maisha yako hapa duniani.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna njia kuu mbili za kuishi maisha yako hapa duniani.

    Njia ya kwanza ni kuishi kama ambavyo watu wanataka wewe uishi, Ufanye yale ambayo watu wanakutegemea uyafanye hata kama sio yanayokufurahisha au sio muhimu kwako.

    Ufanye kile ambacho kila mtu anafanya hata kama huna msukumo wowote wa kufanya hivyo, hii ndio njia ya kwanza ambayo asilimia 99 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

    Njia ya pili ni kuishi kama vile ambavyo wewe mwenyewe unataka kuishi kufanya kile ambacho ni muhimu kwako na una msukumo wa ndani wa kukifanya.

    Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuweza kufikia ndoto zako kubwa, bila ya kujali wengine wanafanya nini au wanasema nini.

    Kutokujiwekea ukomo wapi unapoweza kufika na kuwajali wale wanaokujali, hii ni njia ya pili ambayo asilimia 1 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

    Rafiki yangu, umechagua kuishi njia ipi? Huu ni uchaguzi wako, kama hujachagua au hujui uchaguzi wako ni sahihi au la.

    Lakini nikukumbushe kwamba hii ni asilimia 1 wanaoishi maisha kwa njia ya pili, ndio wanaofika mafanikio makubwa sana wanaokuwa na furaha kwenye maisha yao na ambao hawana majuto kwenye maisha yao.

    Hatua ya kuchukua; rafiki yangu habari njema ni kwamba maisha ni kuchagua, na kuna njia mbili za kuweza kuishi yako, naamini upo kama mimi unachagua njia ya kuishi asilimia 1 ambayo utafanya mambo muhimu kwako ili uhakikisha maisha yako yanakwenda vile unavyopanga.

    Akupendaye sana,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.