-
Jinsi matatizo yanakufanya uwe imara.
Rafiki yangu mpendwa mwandishi Robin anatushirikisha hadithi ya mwanamuziki Gord Downie, ambaye alikuwa mwimbaji wa bendi maarufu nchini Canada.
Alikuwa anajituma sana kwenye muziki wake na kupendwa na wengi. Siku moja akaanguka na kupata degedege kali.
Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe kwenye ubongo. Uvimbe ambao hauwezi kupona na maisha yake hayakuwa marefu.
Alishauriwa aache shughuli zote nzito na apumzike. Lakini Gord hakukubali, aliandaa ziara ya mwisho na bendi yake ya kuzunguka nchi nzima.
Watu hawakuamini kama angeweza kumaliza ziara hiyo. Lakini kwa kujitoa kwa kipekee alikokuwa nako, aliweza kumaliza ziara na kutoa burudani ambayo inakumbukwa miaka na miaka.
Alikufa kama ilivyotegemewa, lakini aliacha alama kubwa. Usikubali tatizo lolote lile unalopitia likuangushe na kukukatisha tamaa. Bali tumia kila tukio kuwa imara zaidi ya ulivyokuwa awali.
Kuchukua hatua; rafiki yangu mpendwa hata kama utakufa kesho kwa hakika, ishi kishujaa leo, ishi kwa ukamilifu leo na utaacha alama itakayodumu milele.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Hadithi: mfano wa kutotosheka.
Rajat Gupta alizaliwa kolkata India na kukulia kwenye umaskini mkubwa kama yatima. Lakini kwa kujituma aliweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
Akiwa kwenye umri wa miaka 40, na Gupta alikuwa CEO wa McKinsey kampuni kubwa ya ushauri elekezi. Mwaka 2007 alistaafu kazi yake akiwa bado ni kijana lakini aliyefikia uhuru wa kifedha.
Mwaka 2008 utajiri wake ulikadiriwa kuwa dola millioni 100 ( zaidi ya bilionea 200) ni kiasi kikubwa mno cha fedha ukilinganisha alikotoka na ambacho kingetosha kuendesha maisha yake bila shida.
Lakini kiasi hicho hakikumtosha, lengo lake ni alitaka awe bilionea, siyo tu millionea. Gupta alikuwa mjumbe kwenye bodi la wakurugenzi wa benki ya Goldman Sachs hivyo alizungukwa na mabilionea kweli kweli na hilo lilimsukuma kuwa bilionea.
Mwaka huo 2008 aliiona fursa, alipata taarifa za ndani kwamba mwekezaji Warren Buffett anapanga kuwekeza dola bilioni 5 kwenye benki ya Goldman Sachs ambayo kwa wakati huo ilikuwa kwenye hatari ya kufilisika. Kitendo cha Buffett kuwekeza kwenye benki hiyo, ilikuwa ni uhakika lazima hisa zake zitapanda sana.
Kwa kuwa alikuwa mjumbe wa bodi, alipata taarifa mapema, lakini kama mjumbe asingeweza kunufaika moja kwa moja, hivyo alitumia taarifa hizo kuhakikisha ananufaika. Alimpigia mwekezaji Raj Rajaratnam na kumweleza mchakato unaoendelea na hapo Raj alinunua hisa 175,000 kabla taarifa haijawa wazi kwa wote.
Baada ya taarifa kuwa wazi na Buffett kuwekeza, hisa zikaongezeka sana na Raj akapata faida ya dola millioni 1. Hapo ni masaa machache kabla . Baada ya uchunguzi, iligunduka kwamba Gupta alikuwa akitumia taarifa za ndani kujinufaisha na kwa kipindi amefanya hivyo, alikuwa amejiingizia dola millioni 17.
Gupta na Rajaratnam walikutwa na hatia na kufungwa jela, majina yao kuharibika na kupoteza kila walichokuwa wamekitengeneza kwa miaka yote waliofanya kazi.
Sasa rafiki yangu unaweza kuona hapo, mtu anapoteza utajiri wa dola millioni 100 kwa kuhangaikia na kupata dola millioni 17 ya ziada, ambayo inapoteza kila kitu.
Kikubwa ambacho Gupta na wengine wengi waliowahi kufanya maamuzi kama haya walikosa ni kutosheka, tamaa ya kupata zaidi iliwasukuma kuchukua hatua zenye hatari lakini wasione.
Tunayojifunza ni kwamba hatupaswi kuhangaikia na kupata fedha zaidi ambazo hatuhitaji kinaweza tufanye tupoteze fedha ambazo tunazo ambazo tunazihitaji sana.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Namna ya kuepuka fursa mpya.

Kujifunza kwa simba.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini mnyamapori akimwona simba huona kifo machoni pake, lakini habari ni tofauti kwa simba, yeye akimuona mnyamapori anaona ni kitoweo kilichokaribia mdomoni mwake.
Simba akimuona mnyama yoyote yule bila kujali ukubwa na ukatili wake, akili wake huona kitoweo.
Tunajifunza kwamba tunapaswa kutengeneza maono yetu alafu kila siku tuhangaike kuyatimiza.
Kitu kimoja zaidi ni kuwa Simba pia huwatisha maadui na kuchagua mnyama mmoja. Kwa sauti yake na mwonekano wake ili watawanyike na kuweza kuchagua mnyama mmoja ambaye atamkimbiza na kumpata.
Tunajifunza kutong’ang’ania kila fursa kwa sababu zitakushinda.
Kuchukua hatua; rafiki yangu kabla hujafanya maamuzi, ni muhimu kujua kwamba kukimbilia fursa mpya kila siku ni kikwazo kuifikia utajiri ata kama unajua maarifa yote muhimu.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Hatua 3 za kuvunja imani zenye ukomo.
Rafiki yangu mpendwa ili uweze kuwa huru kufikiri na kufanya makubwa, lazima kwanza uvunje imani zote zenye ukomo ulizonazo.
Hapa kuna hatua tatu za kuvunja imani hizo.
Hatua ya kwanza ni kutambua imani za ukomo ulizonazo. Jisikilize sauti zinazotoka ndani yako, kwenye kila unachojiambia huwezi au haiwezekani, jua hapo una ukomo wa kiimani.
Hata kama ni jambo dogo kiasi gani, kama unajiambia huwezi au haiwezekani, jua hapo una ukomo wa kiimani.
Hatua ya pili ni kuangalia ukweli. Mengi unayojiambia huwezi au haiwezekani siyo kweli, ni mazoea tu umekuwa nayo.
Chukua hatua ya kuangalia ukweli kwenye kila eneo ulilojiwekea ukomo. Utagundua kuna wakati uliweza kufanya yale uliyojiambia huwezi.
Na hata kama ulifanya na ukashindwa, matokeo hayakuwa mabaya kama ulivyotegemea yawe. Kwa kuona ukweli huo, utazidi kuona jinsi imani uliyonayo siyo sahihi.
Hatua ya tatu ni kutengeneza imani mpya isiyo na ukomo kwenye maeneo yote ambayo umejiwekea ukomo. Kila unachojiambia huwezi au haiwezekani, jiambie unaweza na inawezekana.
Kwa kubadili imani yako kwenye maeneo uliyokuwa na ukomo, unaacha kuona ukomo na kuanza kuziona fursa mbalimbali za uwezekano.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Mambo 3 ya kuondoa ukomo.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kama kuna chochote unachotaka kwenye maisha yako ila hujakipata, kuna maeneo matatu ambayo utakuwa umejiwekea ukomo.
Eneo la kwanza ni mtazamo ulionao, kwa wengi huwa wana mitazamo hasi na ya kushindwa, kitu kinachokuwa kikwazo kwao kuona uwezekano mkubwa na kuufanyia kazi.
Eneo la pili ni motisha kama huna motisha sahihi, hutapata msukumo wa kuchukua hatua ili kupata kile unachotaka. Safari ya kupata unachotaka siyo rahisi, unahitaji motisha ili kuendelea na mapambano.
Eneo la tatu ni mchakato, namna unavyofanya mambo yako inaweza kuwa kikwazo kwako kupata unachotaka. Lazima uwe na mchakato sahihi utakaokuwezesha kupata kile unachotaka.
Kuchukua hatua; ili kufanya na kufikia makubwa, lazima uondoe ukomo kwenye maeneo hayo matatu.
Kitu kimoja zaidi rafiki yangu ni kwamba, unaweza ukafanya makubwa kuliko unavyodhani sasa.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Umuhimu wa kuwa mnyenyekevu.
Rafiki yangu mpendwa Robin kwenye kitabu chake cha ‘everyday manifesto’ anatushirikisha hadithi ya kipindi akiwa mtoto, familia yao walikuwa mapumzikoni.
Siku moja wakiwa kwenye gari njiani wakapishana na gari la aliyekuwa mpiganaji maarufu Muhammad Ali.
Mama yake Robin alimtaka baba yao aliyekuwa anaendesha gari ageuze na kuifuata gari ya Muhammad Ali.
Walifanya hivyo mpaka kuikaribia na akaanza kumsalimia kwa mbali na kumwomba wapige picha ya pamoja.
Robin na kaka yake waliona ni kitendo cha aibu kwani mtu maarufu kiasi kile asingekubali kupiga picha na watu wasiojulikana.
Lakini cha kushangaza Muhammad Ali alipaki gari pembeni, akawasalimia vizuri kisha akapiga nao picha.
Robin anasema hakuwahi kusahau tukio hilo kwa maisha yao yote. Moja ya picha yao na Muhammad Ali iliwekwa kwenye saa ya ukutani na kuwa inakaa sebuleni kwao.
Kitendo hicho cha unyenyekevu mkubwa walioonyeshwa na mtu aliyekuwa na umaarufu mkubwa kilimpa funzo kubwa Robin.
Hapa tunajifunza umuhimu wa kuendelea kuwa wanyenyekevu hata baada ya kufanikiwa sana.
Kuchukua hatua; rafiki yangu kuna kitu kidogo sana unaweza Kufanya, ambacho hakikugharimu chochote, lakini likawa ni alama kubwa sana kwa wengine.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha.
Rafiki yangu mpendwa mwandishi James W.Murphy
kwenye kitabu chake cha ‘ who says you can’t sell ice to Eskimos.’Kwenye sura ya mwisho, Murphy anamalizia kwa kutuambia kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha ni kuingiza kipato. Anasisitiza kuwa hakuna kingine muhimu kuliko hicho.
Usipoingiza kipato, huwezi kupata chakula. Usipoingiza kipato huwezi kupata nyumba, huwezi kuhudumia familia yako, watoto wako na mahitaji muhimu kwako. Kuingiza kipato ndiyo hitaji la kwanza na la msingi kwa kila binadamu.
Lakini pia ndiyo hitaji ambalo watu wengi wamekuwa hawalipi uzito ambao unastahili. Watu wengi wamekuwa hawajipimi kwa uhakika kwenye eneo la kuingiza kipato.
Badala yake wamekuwa wanajiendea tu kwa mazoea, haishangazi kwa nini wengi wanakuwa na maisha magumu.
Kama kuingiza kipato ndiyo kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha, kinapaswa pia kuwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kwenye maisha.
Kupitia mauzo, mtu unapata fursa kuingiza kipato kisichokuwa na ukomo. Hivyo basi, kwa mtu yeyote ambaye yupo makini na maisha yake na anataka kuwa na maisha bora, anapaswa kuuza.
Matatizo mengi ambayo mtu anayo kwenye maisha, yanaweza kutatuliwa na fedha. Na mtu yeyote anaweza kupata fedha kama atakuwa muuzaji mzuri.
Kuchukua hatua; kwa maana hiyo basi, tunaweza kusema mauzo yanaweza kutatua matatizo mengi kwenye maisha.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Hatua 4 za kuchukua Ili kuepuka tamaa isikupoteze.
Rafiki yangu mpendwa unaweza kujiambia ukifika kwenye utajiri wa juu hutasumbuka kupata zaidi. Lakini unajidanganya, kadiri unavyopata fedha zaidi, ndiyo fursa za kupata fedha zaidi zinavyokuja kwako.
Ili kuepuka tamaa isikuingie na ukapoteza kila unachotengeneza, unapaswa kuzingatia hatua haya manne.
Kwanza; ujiwekee lengo lako la kifedha mapema na kisha jisukume kulifikia. Ukishafikia lengo hilo usihangaike tena na fursa mpya za kuingiza kipato zaidi.
Pili; usijilinganishe na yeyote. Ubebari umefanikiwa kwenye vitu vikubwa viwili, kuzalisha utajiri na kuzalisha wivu, hivi ni vitu viwili vimekuwa vinaenda pamoja. Watu siyo tu wanafuata utajiri, bali pia wanataka kuwapita wengine.
Na hapo ndipo watu wanasukumwa kuingia kwenye mambo yasiyo sahihi. Acha kujisumbua kijilinganisha au kushindana na wengine, haijalishi umefanikiwa kiasi gani, lazima kuna aliyefanikiwa kuliko wewe.
Tatu; kutosheka haimaanishi kukubali kidogo. Wengi wakisikia kutosheka wanaona ni kama kukubali kidogo ulichonacho na kuacha fursa kubwa na nzuri zikupite. Hiyo siyo sahihi. Kutosheka ni kufikia kwenye hatua ambayo unajua hata ukienda zaidi hakuna mabadiliko makubwa utakayoleta na kwa kila hatua unayochukua ina hatari, hatari yoyote unayochukua haiwezi kulipa. Hata chakula, ukisema uendelee kula kwa sababu kipo kitakuwa sumu.
Nne; kuna vitu huvipaswi kuvihatarisha, hata kama manufaa ni makubwa. Unapaswa kujua ni vitu gani unalinda sana kwenye maisha yako, ambayo haupo tayari kuvihatarisha kwa faida yoyote ile.
Kuchukua hatua; kutokutosheka imekuwa chanzo cha wengi kuchukua hatari zinazopelekea kupoteza kila ambacho wameshajitengenezea . Ni muhimu tujifunze kutosheka.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@kemeimaureen
-
Hatua 3 za mabadiliko.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wa kale walikuwa na imani kwamba madini ya risasi yanaweza kugeuzwa kuwa madini ya dhahabu kupitia mchakato ulioitwa Alchemy.
Zoezi la kubadili risasi kuwa dhahabu kutokuwezekana, ilitumika sana kwenye mabadiliko ya watu.
Ili mtu aweze kufanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yake na kuzaliwa upya, alipaswa kupitia hatua tatu muhumu zilizotumika kwenye zoezi la Alchemy.
Hatua ya kwanza ni hatua nyeusi. Hapa risasi inavunjwa na kuyeyushwa kutoka yabisi yaani solid kwenda kumiminika yaani liquid . Kwenye mabadiliko binafsi hapa ni pale unapoondoka kwenye hali uliyokuwa huko nyuma.
Hatua ya pili ni hatua nyeupe. Risasi iliyoyeyushwa inasafishwa na kutakaswa . Hapa uchafu wote unaondolewa . Kwenye mabadiliko binafsi ni kuondoa masalia ya yale uliyokuwa nayo huko nyuma.
Hatua ya tatu ni hatua nyekundu. Risasi iliyosafi inapitishwa kwenye moto mkali na kugeuzwa kuwa yabisi ya kitu kipya ambacho ni dhahabu.
Kwenye maendeleo binafsi, mtu anapitia mchakato wa kujengwa kuwa mpya. Hapa ndipo anapochagua kujitoa kweli kwenye kitu kipya alichochagua.
Kuchukua hatua; rafiki yangu mpendwa kama vile tumeona hatua za mabadiliko ni jukumu letu kukubali mabadiliko inapotokea kwenye maisha yetu.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Nyenzo 5 za kubadili mtazamo.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini vile ulivyo ni matokeo ya mtazamo ambao unao.
Matokeo unayoyapata yanatokana na mtazamo wako. Huioni dunia na mambo kama yalivyo, bali unaona kama ulivyo wewe. Hivyo ili kuona vitu kwa namna ambayo itachangia wewe ufanikiwe, unapaswa kubadili mtazamo ulionao.
Kuna nyenzo tano muhimu za kufanyia kazi ili uweze kubadili mtazamo wako.
Ya kwanza ni fikra unazokuwa nazo, unapaswa kuwa na fikra chanya na za uwezekano badala ya fikra ya hasi na za kushindwa.
Ya pili ni hisia zinazokutawala, unapaswa kuwa na hisia chanya juu ya mambo, hisia zinazokusukuma kuchukua hatua sahihi.
Ya tatu ni maneno unayotumia, unapaswa kutumia maneno chanya na ya kuinua na siyo maneno hasi na ya kuangusha.
Ya nne ni matendo unayofanya, yanapswa kuwa matendo sahihi kwako kukupa matokeo unayotaka.
Ya tano ni ushawishi unaokuzunguka, unapaswa kuzungukwa na ushawishi chanya, unaokusukuma kuwa bora na siyo hasi unaokukatisha tamaa.
Kuchukua hatua; rafiki yangu tukifanyia kazi nyenzo hizi tano, tutabadili kabisa mtazamo wako, tutaiona dunia na mambo yanayokutokea kwa namna bora na kuweza kutumia kufanya makubwa zaidi.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.