Home

  • Je, unajua kila kitu kinawezekana?

    Rafiki yangu mpendwa familia,shule, jamii na dunia kwa ujumla imekuwa inakuaminisha kwamba kuna vitu unaweza na zingine huwezi.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini ni wakati sasa wa kujua nini hasa unachotaka na kupambana mpaka kukipata.

    Cha muhimu ni kuwa tuna ushahidi wa kila aina wa watu ambao waliweza kufanya makubwa ambayo yalionekana hayawezekani.

    Kabla hujafanya maamuzi jua kuwa wapo walioweza kuanzisha biashara na kuikuza licha ya kuanza bila ya kitu kabisa.

    Wapo walioweza kuondoka kwenye madeni makubwa na kufika kwenye utajiri.

    Rafiki yangu nini kinachokusumbua sana kwenye maisha yako, habari njema ni kwamba unaweza kabisa ukaondoka kwenye mkwamo unaoona kama inakusumbua kwa sasa.

    Kuchukua hatua; unapaswa kujiamini na uwe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii bila kuruhusu uzembe,uvivu na kufanya mambo kwa mazoea. Kila la kheri rafiki yangu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Njia 10 za kusuluhisha changamoto.

    Rafiki yangu mpendwa Roger Dawson kwenye kitabu chake cha The Secrets Power Problem Solving. Anatushirikisha njia kumi za kusuluhisha changamoto.

    1. Kwa kila changamoto kuna Suluhisho. Kweli, amini kuwa tatizo lako lina suluhisho na linaweza kupata suluhisho. Kweli ni ngumu na huna suluhisho kwa sasa lakini ei lina suluhisho.
    2. Jaribu kuwa na utulivu wakati wa changamoto. Usihofie, usijaribu kuwa na hasira kuwa hupati hiki, huelewi hicho . Unapaswa kutulia na kuamini kuwa ili changamoto lina suluhisho.
    3. Usitumie nguvu kupata jawabu. Usiseme ooh Mungu wangu nahitaji jawabu la changamoto ili kabla ya ijumaa jioni. Wakati mwingine huwezi kulazimisha, maisha huja jinsi ilivyo, kwa hivyo tumia muda huu kusubiri na kuamini kuwa suluhisho linakuja hatimaye.
    4. Tafuta maarifa sahihi. Fanya uchunguzi ya kutosha kwanza kabla hujasema changamoto lako halina suluhisho.Usitegemee maarifa uliyonayo tu.
    5. Andika yote yaliyo kweli kuhusu hali yako. Unapaswa ufahamu kwanza kuhusu changamoto lako, ujue nini kinaendelea labda unaweza kuja na suluhisho.
    6. Tenga muda wa kuomba / fikiria kuhusu jambo hilo. Tenga muda wa maombi juu ya changamoto hilo, sikiliza nafsi yako. Kama huombi juu ya jambo hilo, unafikiria kuhusu namna ya kupata suluhisho.
    7. Amini na utafute mwongozo wa Mungu. Kama kitabu cha Zaburi 23:1 inavyosema Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
    8. Amini kwenye utambuzi wako na angavu wako. Kuna vitu tunaamini tunaweza fanya na kuna vitu tunajua tunaweza fanya. Tenga muda wa kujisikiliza, inataka muda ili ujue nini uko vizuri, lakini pia una mambo mazuri unayoweza ukafanya.
    9. Tafuta mahali unaweza ukatulia. Unaweza enda kanisani ambapo utaweza imba,sali, soma na kutafakari neno la Mungu na pia kujumuika na waumini wengine.
    10. Mawazo yanayokuja kwenye akili yako linakuwa ni sahihi. Ruhusu mawazo yaje akilini mwako, fuatilia kuhusu hili na uzame ndani zaidi.

    Kuchukua hatua; akili yetu lina nguvu kubwa, linaweza kuleta suluhisho la kila changamoto kama tutaweza tu kutumia vizuri kwa kutulia, kutafakari,kufanya tahajudi na kuruhusu Mungu atawala fikra zetu. Tutaweza kufanya makubwa na kuvuka changamoto za maisha

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kwa Nini Unapaswa Kuamini Nguvu Kubwa Iliyo Ndani Yako?

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Robin Sharma anatushirikisha ujumbe muhimu ambao ulimjia na kusukumwa kuutoa kwa wengine.

    Pata picha wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu, unapaswa kufanya nini? Habari njema ni kuwa umepewa nafasi ya kuamini nguvu iliyo ndani yako.

    Wakati wa mkanganyiko ndipo penye dirisha la kupata uelewa wa juu. Wakati unapohoji kila kitu ndiyo wakati wa ukuaji.

    Wakati unapojiona mpweke ndiyo wakati umeungana na wengine wanaopitia hali kama yako.

    Wakati wa dhoruba kumbuka magumu ambayo umewahi kupitia. Mawimbi makali huishia kuwa maji tulivu.

    Usumbufu unaopitia wakati wa mabadiliko utageuka kuwa tulivu wa hekima mpya. Wewe ni imara zaidi ya unavyojichukulia. Una ujasiri kuliko unavyojijua. Una uwezo wa kukabiliana na chochote ambacho maisha yanakuletea.

    Unapokuwa na hofu, jiulize shujaa angefanya nini? Unapokuwa na wasiwasi, jiulize kujiamini kupoje? Unapokuwa na hasira, jiulize wapi unahitaji kuwa na uelewa?

    Unapokuwa na maumivu, nenda kwenye matumaini. Unapokosa kujiamini, ruhusu uongozwe na upendo.

    Kila kitu kinatokea kwa manufaa yako. Hakuna kinachokuja kuondoa furaha yako. Majaribio unayopitia yatakuletea ushindi mkubwa.

    Matendo yako mazuri yatazalisha mafanikio makubwa. Matokeo mazuri yako njiani kuja kwako.

    Kamwe usikate tamaa.Usilinganishe safari yako na ya mtu mwingine. Unalindwa na nguvu kubwa inayoendesha ulimwengu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    https://www.uamshobinafsi.com.

  • Kitu kinachowafanya watu wakose furaha.

    Kinachowafanya watu wengi kukosa furaha kwenye maisha yao ni kuishi maisha ambayo yako chini ya uwezo wao.

    Kwa mfano, mtu anajijua kwamba anaweza kuwa na maisha bora kuliko aliyonayo sasa, anaweza kufanya kazi yake kwa ubora kuliko anavyofanya sasa na pia anaweza kupata kipato kikubwa kuliko anachopata sasa lakini hakuna hatua anazochukua kufikia ule uwezo uliopo ndani yake.

    Ukitaka kutengeneza maisha ya hovyo, maisha yasiyokuwa na furaha kwa kipindi chote cha maisha yako ni kupanga kuishi chini ya uwezo ulio ndani yako.

    Ni bora upange kuishi kuliko uwezo wako, upange kufanya makubwa zaidi ya unavyoweza na hata ukishindwa basi utakua umeshindwa juu ya pale ulipo sasa.

    Sehemu nzuri ya kuanza kuishi kulingana na uwezo wako au hata juu ya uwezo wako ni kuchukua chochote unachofikiria sasa hivi na kuzidisha mara kumi.

    Kwa mfano, chukua kipato chako unachoingiza sasa, kisha kizidishe mara kumi na hilo ndiyo linapaswa kuwa lengo la kipato unalofanyia kazi.

    Angalia mipango yote uliyojiwekea, zidisha mara kumi na weka juhudi kuhakikisha unafikia mara kumi hiyo.

    Usiendeshe maisha ya mazoea, yasiyo na mpango, maisha ya kusubiri mambo yatokee na wewe ndiyo uone utafanya nini, utakua na maisha yasiyokuwa na furaha, maisha ya hovyo na utakuwa umechagua kupoteza maisha yako wewe mwenyewe.

    Hatua ya kuchukua leo, rafiki yangu usiishi maisha yaliyo chini ya uwezo wako, amua kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yako na utafanya makubwa kwenye maisha yako.

    Rafiki yako.

    Maureen Kemei.

    http://www.uamshobinafsi.com/

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Maneno 40 maarufu ya Alexander the great.

    Rafiki yangu mpendwa mwandishi William Ramirez anatushirikisha maneno 40 maarufu ya Alexander the great.

    1. Moja ya mambo niliyojifunza wakati nilikuwa najadili ni kwamba hadi nitakapojibadilisha, singeweza kubadilisha wengine.
    2. Nani hataki ushindi ambao anaweza kuunganisha maeneo ya ufalme wake, yaliyogawanywa sana na maumbile, na ambayo anaweza kupata nyara kutoka kwa walimwengu wengine walioshinda.
    3. Je! Ni vipi mtu anaweza kumtunza farasi wake mwenyewe, kupaka mkuki na kwato, ikiwa amepoteza tabia ya kujali nafsi yake ambayo ni milki yake ya thamani zaidi?
    4. Zaidi ya hayo, nimejeruhiwa kwa upanga, mkono kwa mkono, na mishale, nimejeruhiwa kutoka kwa manati na mara nyingi nimepigwa kwa mawe na marungu.
    5. Kwa upande wangu, ninaamini kwamba kwa wanaume wa roho, hakuna lengo lingine au mwisho wa kazi zao zaidi ya kazi zenyewe.
    6. Sijali asili ya raia au asili yao ya rangi.
    7. Sasa kwa kuwa vita vinamalizika, ningependa muweze kufanikiwa kwa amani.
    8. Wote wanaoweza kufa tangu sasa waishi kama watu wasio na umeona ambao wanakubali na kufanya kazi kwa maendeleo sawa.
    9. Natabiri mashindano makubwa ya mazishi kunihusu.
    10. Kwa mwenye nguvu! ( Katika kitanda chake cha kifo, haya yalikuwa majibu ya mfalme wa Makedonia kwa nani nafasi yake ipewe).
    11. Siibi mafanikio.
    12. Lengo na lengo la ushindi ni kuepuka kufanya sawa na walioshindwa.
    13. Sina hata sehemu moja ya mwili wangu, angalau mbele, ambayo haina makovu.
    14. Lazima Mungu awapende Waafghan, kwani amewafanya kuwa wazuri.
    15. Kwa mtazamo mzuri, mapungufu ya kujitolea hupote.
    16. Kwa habari ya mipaka ya kazi ya mtu, simtambui yeyote kwa mtu mwenye fadhila, isipokuwa zile ambazo zinapaswa kusababisha mafanikio mazuri.
    17. Bila ujuzi, ujuzi hauwezi kuelekezwa . Bila ustadi, nguvu haiwezi kutumia na bila nguvu, maarifa hayawezi kutumika.
    18. Upendo wa kweli hauna mwisho mzuri, kwa sababu hakuna mwisho wa upendo wa kweli.
    19. Wale ambao wana ujasiri wa kushinda woga wamewekwa huru na wake ambao wameshindwa nayo wanateseka mpaka wawe na ujasiri wa kuishinda, au kifo kitawachukua .
    20. Ngono na kulala peke yangu kunifanya nijue kuwa mimi ni binadamu.
    21. Umeleta mtoti mmoja tu wa kiume ulimwenguni, lakini kila mtu hapa duniani anaweza kuitwa Alexander.
    22. Loo! Mimi mnyonge! Kwa nini sikujifunza kuogelea?
    23. Ikiwa nitangojea, nitapoteza ujasiri na ujana wangu.
    24. Hakuna walimwengu wengine wa kushinda.
    25. Mbingu haiwezi kuvumilia jua mbili, wala ardhi mabwana wawili.
    26. Ninahusika katika nchi ya watu jasiri na jasiri, ambapo kila upande cha ardhi ni kama kisima cha chuma, inakabiliana na askari wangu.
    27. Ingekuwa furaha gani kwangu kuuawa vitani.
    28. Jitihada na hatari ni bei ya utukufu, lakini ni jambo la thamani kuishi na ujasiri na kufa ukiacha umaarufu wa milele. Nina deni kwa baba yangu kwa kuishi, lakini kwa mwalimu wangu Aristotle kwa kuishi vizuri.
    29. Mwishowe, wakati yote yamekwisha, jambo pekee ambalo ni muhimu ni kile umefanya.
    30. Hakuna kitu kinachowezekana kwa yule anayejaribu.
    31. Ningependa kuishi maisha mafupi na matukufu kuliko ya muda mrefu gizani.
    32. Huko Makedonia, kwa vizazi vilivyopita, tumefundishwa katika shule kali ya hatari na vita.
    33. Kila mtu anaapa kuwa Mimi ni mtoto wa Jupiter, lakini jeraha hili linatangaza kuwa mimi ni mwanaume.
    34. Mungu akuokoe na sumu ya cobra, neno ya tiger, na kisasu cha Waafghan.
    35. Ninakufa jwa sababu ya msaada wa madaktari wengi.
    36. Ninaweza kufikiria jinsi heshima zangu za mazishi zitakavyokuwaza kupendeza.
    37. Kwangu nimeacha bora: tumaini.
    38. Ikiwa singekuwa Alexander, ningependa kuwa Diogenes.
    39. Nikingoja nitapoteza nguvu za ujana.
    40. Tutakuwa na tabia kwa njia ambayo watu wote wanataka kuwa marafiki wetu na wote wanaogopa kuwa maadui zetu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi ya kuwa paka kwenye zama hizi.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Mwandishi Jaron katika kitabu chake cha Ten Arguments for Deleting Your Social Media Accounts Right Now, anatushirikisha mfano ya wanyama wawili ambao binadamu tunaishi nao, anasema wanyama hao ni paka na mbwa.

    Anasema mbwa walianza kuishi na binadamu kwa sisi binadamu kuwakamata nakuwafuga, hivyo mbwa wamekuwa wakimsikiliza na kumtii binadamu. Mbwa wamebadilishwa tabia na binadamu kufundishwa kuwa watiifu.

    Lakini paka ni tofauti, paka hakukamatwa na kufungwa na binadamu, paka walikuwa wenyewe na kuanza kuishi na binadamu. Hivyo paka wana uhuru mkubwa kuliko mbwa. Ndiyo maana unaweza kuswaga kundi la mbwa, lakini siyo kundi la paka.

    Paka hajawahi kubadilishwa tabia zake na binadamu, paka anaishi maisha yake kwa uhuru, huwa hafuati hata kundi. Na ndiyo maana tunawapenda sana paka, japo hawana matumizi makubwa kwetu kama kwa mbwa ambao tunawatumia kwa ulinzi.

    Mwandishi anaendelea kuelezea kwamba katika mabadiliko yote yaliyotokea duniani, viumbe wengi wamebadilika isipokuwa paka. Paka hajawahi kukubali kutawaliwa na yeyote, wako huru kuyaishi maisha yao na kufanya maamuzi yao.

    Japokuwa tunawapenda mbwa, hakuna anayependa kuwa na tabia kama za mbwa, za kubadilishwa kitabia na kuwa mtiifu kwa wengine. Kila mtu anataka kuwa huru kufanya maamuzi yake mwenyewe, lakini mitandao ya kijamii imekuja kuwa hatari kwetu.

    Mitandao hiyo kwa njia mbalimbali imekuwa inatubadili tabia kama ambavyo mbwa wanafundishwa utiifu.

    Kitu kimoja zaidi rafiki ni kuwa wapo watu wanatumia mitandao hiyo ya kijamii kutusukuma kufanya vitu fulani bila ya sisi kujua kama tumesukumwa kufanya hivyo.

    Mwandishi anatuambia lengo la kitabu chake ni kutufundisha jinsi ya kuwa paka, kupaki na uhuru wa kufanya maamuzi yetu wenyewe kwenye dunia ambayo mitandao ya kijamii imetawala maisha ya watu na kuwashawishi kufanya vitu visivyo na manufaa kwao.

    Mwandishi anasema kuwa mitandao ya kijamii inatuhadaa kwamba hakuna maisha nje ya mitandao hiyo, lakini huo siyo ukweli, ni njia ya kuifanya iendelee kujinufaisha huku ikivuruga maisha yako.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu tunahitajika kuwa paka kwenye nyakati hizi, yaani kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yetu wenyewe na hivyo kuwa huru.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi Usomaji wa vitabu unavyorefusha maisha.

    Rafiki yangu mpendwa unajua nini kuhusu usomaji wa vitabu na umuhimu wake katika maisha yako kwa ujumla?

    Sitaki kukuchosha na maneno mengi lakini usiwe na wasiwasi maana kusoma huku kunakusaidia kurefusha maisha yako bila shaka.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini iwapo unataka kuwa na afya njema na kuishi muda mrefu, utafiti unaonyesha kwamba ulaji wa chakula bora na kudumisha utaratibu wa kawaida wa mazoezi, ni funguo mbili za kupunguza hatari yako ya kifo. Lakini vipi kuhusu usomaji wa vitabu?

    Habari njema ni kwamba vitabu zinaweza kufanya mengi zaidi kwa ajili ya mwili wako kuliko kulisha tu akili yako?

    Kitu kimoja zaidi ni kwamba vitabu vina uwezo wa kutusafirisha hadi maeneo ya mbali na kutufundisha kuhusu mada za ulimwengu zote za upendo na hasara na furaha na huzuni.

    Hata hivyo utafiti uliofanywa na shule ya afya ya umma ya Chuo Kikuu Cha Yale iliyochapishwa katika jarida la kitaaluma la sayansi na tiba ya jamii pia ulibainisha uhusiano kati ya kusoma na maisha marefu.

    Waandishi wa ripoti hiyo walichunguza kama watu wanaosoma vitabu wanafurahia faida ya maisha marefu zaidi ya watu ambao hawasomi vitabu au kusoma aina nyingine za maudhui kama vile majarida na magazeti.

    Kabla hujafanya maamuzi rafiki yangu ni muhumu kuchukua hatua ya kuanza kusoma vitabu kama ambavyo tumeona umuhimu wake kwenye maisha yetu.

    Rafiku yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Nguvu ya ukaribu kwenye maendeleo binafsi.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu kinachochangia kwenye changamoto zilizopo kwenye jamii za kisasa ni kukosekana kwa ukaribu wa watu.

    Ukaribu wa watu ni muhimu sana kwenye maendeleo binafsi kwani bila hiyo ni vigumu mtu kupata utulivu wa akili.

    Tatizo hili linaanzia utotoni. Wakati kwenye jamii za asili watoto wanalelewa na wazazi kwa muda mrefu, huku wakilala nao pamoja, kwenye jamii la kisasa hilo ni tofauti.

    Watoti hawapati kabisa nafasi ya kulelewa na wazazi kwa karibu na hata kwenye kulala, wanalazwa wenyewe.

    Kwa kukosekana kwa ukaribu huo tangu utotoni, unafanya maendeleo ya watoto hao wasiwe mzuri na baadaye kuwa rahisi kwao kupata upweke, msongo na sonona.

    Ukaribu na mgusano unahitajika sana kwenye maendeleo ya watoto na hata watu wazima.

    Ndiyo maana jamii zenye ukaribu wa watu wake zinakuwa na nguvu kubwa kuliko zisizokuwa na ukaribu

    Kuchukua hatua; nguvu ya jamii inatupa umuhimu wa kujiunga na kujenga jamii sahihi kwetu, ambapo tunajuana kwa undani na wengine, tunashirikiana kwa karibu na tunasukumwa kuwa bora na kufanya makubwa zaidi.

    Bila ya jamii imara, hata tuwe na maendeleo makubwa kiasi gani, tutazidi kuwa na changamoto za upweke, msongo, sonona na hata kujiua. Maana yanakosa maana na hivyo kutokuwa na furaha.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Mahitaji makuu 3 ya maisha.

    Rafiki yangu mpendwa ili tuweze kuridhika na maisha yetu na yawe na maana kubwa kwetu, sisi binadamu tunahitaji vitu vikuu vitatu.

    Kwanza; tunahitaji uhuru binafsi yaani autonomy wa kuweza kujitawala sisi wenyewe na kuchagua namna tunavyoishi maisha yetu. Pale tunapoona tunalazimishwa kuwa na maisha ya aina fulani, yanakosa maana na tunashindwa kuyafurahia.

    Pili; tunahitaji ubobezi competence, uwezo wa kufanya kitu chenye manufaa makubwa kwa wengine. Tunajiona wa thamani pale wengine wanapotutegemea kwenye kitu fulani tunachofanya, pale tunapopewa sifa na hadhi kwa yale tunayofanya.

    Tatu; tunahitaji kuwa sehemu ya jamii community, ambayo inatujua kutujali na kutusukuma kufanya makubwa zaidi. Ni jamii ndiyo inafanya maisha yetu yawe na maana kupitia yale tunayofanya na ushirikiano tunaokuwa nao.

    Mambo hayo matatu ndiyo yanayotengeneza furaha ya ndani, furaha ambayo inadumu kwa muda mrefu.

    Mambo hayo matatu ndiyo yalikuwa yakithaminiwa na kujengwa na jamii za asili. Lakini jamii ya kisasa zimehama kutoka kwenye mambo hayo ya ndani na kwenda kwenye mambo ya nje katika kutafuta furaha.

    Rafiki yangu mambo ya nje yanayopewa nafasi zaidi kwenye zama hizi ni uzuri beauty, fedha money na hadhi status.

    Watu wamekuwa wanakimbizana na mambo hayo wakiamini yatawapa furaha, lakini imekuwa ni ya muda mfupi tu.

    Haishangazi kwa nini kwenye zama hizi, licha ya maendeleo makubwa, bado watu wengi hawana furaha na hawayathamini maisha yao.

    Ni kwa sababu mahitaji ya ndani yamepuuzwa na mahitaji ya nje yamepewa nguvu.

    Kuchukua hatua; rafiki yangu tunapaswa kujenga jamii zinazoweka msisitizo kwenye mahitaji ya ndani ili watu wawe huru, wawe na ubobezi na wawe sehemu ya jamii, kitu ambacho kitayapa maisha yao maana na furaha ya kudumu.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kwa nini hupaswi kufurahisha kila mtu.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Winston Churchill anatushirikisha kwamba kuwa na maadui ni kitu kizuri. Inathibithisha kwamba umewahi kusimamia kitu fulani kwenye maisha yako.’

    Rafiki yangu hupaswi kufurahisha kila mtu. Furahia kuwa na maoni yanayowavuruga watu. Unapaswa kubali kwamba utatengeneza maadui kadiri unavyokuwa unafanikiwa.

    Lazima usimamie kitu ambacho kitawavuruga watu wengi na kuwafanya wakuchukie. Kadiri unavyochukiwa na wengi, ndivyo pia unavyokuwa unapendwa na wafuasi wako.

    Wajibu wako ni kufanya kile ambacho unakipenda sana, kukifanya kwa ubora wa hali ya juu, kukifanya kwa mpango wako mwenyewe na bila kujali wengine wanakuchukuliaje.

    Kitu kimoja zaidi rafiki yangu ni kwamba ambatana na wale wanaokukubali kwa vile ulivyo na unachofanya, wapuuze wale wanaokupinga na kukuchukia.

    Unachohitaji kufanya Ili watu wakuchukie ni kufanikiwa sana kwa kufanya kile unachopenda kufanya. Pale unapoonyesha dalili za kufanikiwa, baadhi ya watu watakupenda na kukuunga mkono, wakati huo huo kuna wengine ambao watakuchukia na kukudharau sana.

    Unachukiwa sana pale unapofanikiwa kwa sababu mafanikio yako yanawafanya wale ambao hawajafanikiwa waonekane ni wazembe. Kwa sababu hawana uthubutu wa kuchukua hatua za hatari kama wewe, furaha pekee wanayokuwa nayo kwenye maisha ni kuwachukia wale ambao wamefanikiwa.

    Kuchukua hatua; rafiki hupaswi kusumbuka na watu hao, tayari maisha yao yanawaumiza vya kutosha, wapuuze na endelea kufurahia mafanikio yako.

    Aliyekuwa mtawala wa Roma na Mwanafalsafa wa Ustoa, mwanafalsafa Marcus Aurelius alikuwa na maneno mazuri ya kutuambia kuhusu kutofurahisha kila mtu . Anasema kila unapoamka asubuhi jiambie kauli hii, ‘ Leo nakwenda kukutana na watu ambao ni waovu, wasio na shukrani, wenye fujo, wasaliti, wenye wivu na wasiojali. Watu hao wako hivyo kwa sababu hawajui kipi kizuri na kipi kibaya.’

    Rafiki usiumie pale unapochukiwa, bali ona hizo ni dalili nzuri kwamba upo kwenye njia sahihi. Wenye chuki wana wajibu mkubwa wa kutimiza kwenye maisha yako, wanakusaidia kujenga vizuri maono yako na kukutangaza kwa wengine.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.