Home

  • Kwa Nini Unapaswa Kujua Sauti Yako.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna kitu cha tofauti ndani yako, kama hujakijua ni kwa sababu umekuwa unaipuuza sauti iliyo ndani yako.

    Lakini habari njema ni kuwa sasa ni wakati wa kuanza kusikiliza sauti hiyo, maana hiyo ndiyo inajua wewe ni nani na nini hasa unachotaka.

    Kuna vitu unasukumwa kufanya japo hakuna mwingine anayefanya.

    Kuna vitu unatamani kuviboresha japo wengine wanafanya kwa mazoea.

    Usiwe na wasiwasi maana ni wakati wa kusikiliza sauti yako na kuchukua hatua, maana hiyo inakujua wewe zaidi.

    Kabla hujafanya maamuzi ni kwamba unaweza kuanzia hapo ulipo sasa na ukawa na mengi ya kufanya.

    Chukua hatua; rafiki yangu habari njema ni kwamba unaweza kusimama na kuchukua hatua za tofauti na wengine wakanufaika.

    Hayo yote yatatokea kwa sababu kinafanya kazi vizuri sana kama utasikiliza sauti yako ya ndani.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com.

  • Siri 3 muhimu za kuishi maisha yenye furaha.

    Rafiki yangu mpendwa Sina uhakika kama itakufaa, lakini akili zetu zimezingatia kuishi. Chochote zaidi ya hayo, lazima ufanyike kazi.

    Rafiki Sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna sababu ya bahati mbaya kwa nini furaha mara nyingi haipatikani, akili zetu haziunganishwa kwa njia hiyo. Badala yake, akili zetu zimebadilika ili kuishi, kujilinda , kutuweka salama. Hakika, tuna nyakati za furaha na vipindi vya kuridhika zina furaha. Lakini watu wengi tunasumbuliwa na hisia hasi zinazoendelea, tumekwama tu.

    Je tunapataje furaha zaidi katika maisha yetu? Kama kitu kingine chochote, inahitaji mazoezi Ili kusitawisha furaha inayoendelea. Kwa maana fulani, tunapaswa kuweka upya msingi wetu. Haitatokea mara moja,lakini hapa kuna mambo 3 ya juu unayoweza kufanya kila siku ili kugundua siri za kuishi maisha ya furaha.

    1. Kuzingatia mawazo chanya ili kupata furaha ya muda mrefu, unahitaji kurejesha ubongo wako kutoka kwa mawazo mabaya hadi mawazo mazuri. Jaribu mambo haya : tumia dakika moja hadi mbili kutafuta chanya katika maisha yako. Fanya hivi mara tatu kwa siku 45, na ubongo wako utaanza kuifanya moja kwa moja.

    Kabla hujafanya maamuzi unapaswa uchague mantra chanya kwa siku, jambo ambalo utajirudia, kama vile ‘siku ya leo ni nzuri’ au Ninahisi shukrani kwa yote niliyo nayo.” Chukua muda kujaribu na kuona kwa mtazamo chanya.

    1. Sherehekea ushindi mdogo.
      Maisha yamejaa heka heka, Lakini katikati tuna ushindi mwingi mdogo ambao hauonekani . Chukua muda kusherehekea ushindi huu mdogo.

    Je umechagua vitu vyote kwenye orodha yako ya mambo ya kufanya ambavyo umekuwa ukiahirisha kuvihusu? Ndio! Je, hatimaye ulifuta barua pepe elfu moja ambazo zimekuwa zikijaza kikasha chako?
    Woohoo! Furahia mafanikio haya madogo.

    1. Tafuta usawa wa maisha yako ya kazini. (Mindfulness)
      Upatanishi wa akili hufanya kazi kwa kuleta fahamu wako na umakini kwa wakati uliopo. Ni juu ya kutokuhukumu na kukubali jinsi unavyohisi. Kufanya mazoezi ya kuzingatia kunamaanisha kuwepo, kufahamu na kudadisi.

    Chukua hatua ; rafiki yangu unapaswa uzingatie mambo haya ili uishi maisha ya furaha.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kwa nini unapaswa uwe na lengo halisi.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwa chochote ambacho mtu unafanya, unapaswa kuwa na lengo halisi linalokuongoza.

    Unapokosa lengo, unajikuta ukihangaika na kila kitu, maana kila kitu kinakuwa na umuhimu kwako.

    Seneca anashauri hata kwenye usomaji wa vitabu, bila malengo mtu anajikuta anahangaika na kila kitabu, akisoma vingi kwa haraka na asiwe na uelewa wowote.

    Kwa Seneca lengo sio umesoma vitabu vingapi, bali lengo ni nini umeelewa kupitia usomaji wa vitabu.

    Pamoja na kusisitiza mtu kuwa na lengo ambalo anafanyia kazi, Seneca pia hajasahau umuhimu wa mapumziko na starehe.

    Kwa Seneca kufanya kazi muda wote bila mapumziko na starehe ni kujinyima furaha kwenye maisha.

    Seneca alikwenda mbali mpaka kuandika kitabu alichokiita on leisure, akielezea umuhimu wa mapumziko na starehe kama sehemu ya kutuliza akili na mwili.

    Utulivu huo ni muhimu kwa furaha na kupata msukumo wa kuendelea kufanyia kazi malengo.

    Seneca pia aliamini furaha yako haitegemei mazingira ya nje, bali hali ya ndani ya mtu . Alieleza unaweza kuwa na furaha ukiwa popote, kama tu hali yako ya ndani iko vizuri.

    Anasema amewahi kuona watu walio ndani ya mahekalu yenye kila kitu ila hawana furaha. Na pia amewahi kuona watu wakiwa peke yao kwenye mazingira magumu ila wana furaha kubwa .

    Hivyo kama huna furaha, kabla hujakimbilia kubadili mazingira ya nje, jichunguze kwanza ndani yako.

    Chukua hatua, kama ndani hakujakaa sawa, hata ukibadili mazingira, utaishia kuwa vilevile.

    Kitu kimoja zaidi, tunapaswa kuhakikisha ndani yetu kuna furaha ili tuweze kuleta mabadiliko hata na mazingira yetu.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Namna ya kujifunza somo, siyo mfano.

    Rafiki yangu mpendwa kwenye kila kitu, kuna somo kubwa unaloweza kujifunza linaloendana na wewe au kile unachofanya.

    Tatizo ni kuwa watu wengi hawajifunzi kwa sababu wanakuwa na ubaguzi. Wanataka mifano inayoendana na kile tu wanachofanya wao.

    Unaweza kupata somo kubwa kutoka kwenye mfano wowote. Kwa mfano kitabu kinachohusu mapishi kinaweza kukufundisha mambo mengi kuhusu biashara.

    Huku kitabu cha biashara kinaweza kukufundisha mambo mengi kuhusu malezi.

    Usiwe na ubaguzi wa wapi unaweza kujifunza nini. Bali kwenye kila kitu, jiulize ni somo gani naondoka nalo hapa linaloendana na kile ninachofanya?

    Kuchukua hatua; rafiki kwa kujifunza kwenye kila kitu, na kujiuliza ni somo gani unaondokana nalo hapa utaweza kuona masomo yalivyo mengi na yenye manufaa.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com.

  • Fanya zaidi kile kinachokutisha.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Derek kwenye kitabu chake cha ‘hell yeah or no,’ anatuambia huwa ana kauli mbiu moja anayoishi kwenye maisha yake, ambayo ni hii; chochote kinachokutisha ndiyo unapaswa kufanya zaidi.

    Anatuambia kwa miaka 30 amekuwa akifuata kauli mbiu hiyo na imemwezesha kufanya makubwa sana.

    Ikiwa chochote unachotaka, ila kinakutisha au kukupa hofu, basi ni kiashiria kwamba hicho ni kitu sahihi kwako.

    Hivyo usiogope na kuacha, badala yake kikabili, na habari njema ni kwamba hapo ndipo penye ukuaji na mafanikio.

    Usiwe na wasiwasi maana ukweli ni kwamba, unapokikabili kile kinachokutisha hukuiogopi tena.

    Kwa sababu kinachofuata baada ya hapo unapata ujasiri mkubwa wa kuendelea kukifanya kwa viwango vya juu zaidi.

    Mwanasaikolojia Abraham Maslow amewahi kunukuliwa alisema : Maisha ni mchakato endelevu wa kuchagua kati ya usalama ( kwa kuhofia na kujilinda) na hatari ( kwa kupiga hatua na kukua ). Chagua zaidi ukuaji kuliko hofu.”

    Chukua hatua; rafiki yangu hivyo ndivyo unapaswa kuyaishi maisha yako, chochote kinachokutisha au kukupa hofu, ndiyo unapaswa kukifanya zaidi.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Je unadhani hujapata unachopenda kufanya?

    Rafiko yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kama unadhani bado hujajua kusudi la maisha yako au hujajua nini unapenda kufanya, basi jua unajikwamisha wewe mwenyewe.

    Nadhani bado unasema huenda unategemea kiwe ni kitu kikubwa na chenye kishindo.

    Badala ya kusubiri kikubwa cha kusisimua, anza na vidogo vidogo vinavyokuvutia kufanya.

    Angalia ni vitu gani unavyopenda kufanya zaidi sasa, ambapo wala hujiskii kuchoka.

    Hapo ndipo penye kusudi na mapenzi yako, weka juhudi zaidi eneo hilo .

    Chukua hatua; anza na vitu vidogo vidogo vinavyokuvutia sasa, vijenge hivyo na ndiyo vitakavyoleta matokeo makubwa.

    Rafiki yangu usisubiri mpaka upate kitu kikubwa kabisa, anza na vidogo vinavyokuvutia sasa.

    Rafiki na mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com.

  • Hadithi yenye funzo kubwa.

    Mkulima mmoja alikuwa na farasi wake mmoja ambaye alimtegemea sana kwa shughuli zake.

    Siku moja farasi yule akapotea na hivyo hakurudi tena. Majirani zake walikuja kumfariji, wakimpa pole na kumwambia ana bahati mbaya kupotelewa na farasi. Mkulima yule aliwasikiliza kisha akawajibu, tutaona.

    Siku chache baadaye yule farasi aliyepotea alirudi, akiwa akiongozana na farasi wengine 20. Mkulima kwa kusaidiana na kijana wake waliwafinga vizuri farasi wote 21.

    Majirani zake wakaja na kumpongeza, wakimwambia ana bahati nzuri kupata farasi hao wengi. Mkulima aliwajibu, tutaona.

    Siku moja wakati kijana wa mkulima yule anafunga farasi wake wapya, farasi mmoja akampiga teke na kumvunja miguu yote miwili.

    Wajirani wake wakaja kumpa pole, wakimwambia ana bahati mbaya kwa kijana wake kuumizwa. Mkulima aliwajibu, tutaona.

    Nchi ya mkulima yule ikaingia kwenye vita. Vijana wote wenye afya walichukuliwa kwenda kwenye mapambano.

    Vita ilikuwa kali na vijana wote waliuawa vitani. Lakini kijana wa mkulima alipona kwa sababu alikuwa amevunjika miguu, hakuchukuliwa kwenda vitani.

    Majirani zake wakampa pongezi, kwamba ana bahati nzuri kijana wake hajafika vitani. Mkulima akawajibu tutaona.

    Tunajifunza kuwa kwenye maisha tunapaswa kuchukulia mambo kama yanavyotokea kwenye maisha. Tusiwe na haraka wa kuongea sana kuhusu mambo haya maana hatujui ni lini kibaya au kizuri kitatokea.

    Rafiki na mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com

  • Kufurahia vitu vidogo vidogo.

    Rafiki yangu mpendwa, watu wengi huwa wanalalamika furaha huwa haidumu kwa sababu wanategemea kupata furaha kwenye mambo makubwa.

    Hivyo wanaweka muda mrefu na juhudi kubwa kupata vitu hivyo vikubwa.

    Wanapovipata wanakuwa na furaha, ila furaha hiyo huwa haidumu kwa muda mrefu.

    Hilo ndiyo huwa linawaumiza watu, kwamba kwa kipindi chote walichopambania ili kukipata kitu, kinaishia kuwa cha kawaida tu kwao?

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili kuondokana na hali hiyo, hakikisha unapata furaha kwenye vitu vidogo vidogo.

    Usisubiri mpaka upate kitu kikubwa ndiyo ukifurahie. Badala yake furahia kila hatua ndogo ndogo unayopiga. Habari njema ni kwamba kila hatua ndogo unayopiga kwenye maisha huwa haipotei.

    Na hapo utakuwa na maisha ya furaha wakati wote. Usiwe na wasiwasi kwa sababu unapofanya kitu na wengine wakanufaika nacho furahia.

    Chukua hatua; rafiki yangu kabla hujafanya maamuzi, tambua kwamba zipo fursa nyingi kwenye kila siku yako za kufurahia, uzitumie vizuri.

    Rafiki na mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kupenda kukosea.

    Rafiki yangu mpendwa pata picha unafanya mambo bila kukosea, yaani hata wakati unajaribu mambo mapya unafanya tu bila kukosea.

    Utajiskiaje kama unafanya mambo tu bila kukosea? Bila shaka hautajua kama unaenda vizuri au huendi vizuri.

    Kama hukosei maana yake unafanya vitu rahisi na unafanya mambo kwa mazoea kabisa. Naamini upo kama mimi kwamba, hupendi kwenda kwa mazoea au kufuata kundi.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini unapojaribu vitu vipya lazima ukosee tena mara nyingi.

    Kwa kuwa watu wengi hawapendi kukosea basi huwa wanaacha kujaribu vitu vipya.

    Watu wengi huona kukosea ni kama udhaifu fulani. Wewe usiwe hivyo, penda kukosea na kuwa tayari kujifunza kutokana na makosa yako.

    Nadhani bado hujaweza, lakini kuwa tayari kufundisha hata na wengine wanaojua zaidi yako.

    Chukua hatua; rafiki yangu habari njema ni kwamba, kadiri unavyokuwa tayari kukosea ndivyo unavyojifunza na kuwa bora zaidi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com.

  • Njia bora ya kukabiliana na malalamiko na kulaumu.

    Pata picha jinsi inavyokuwa rahisi sana kuwalaumu wengine, pale unapokutana na matatizo au changamoto fulani kwenye maisha yako.

    Labda ni watu wamekudanganya, wamekusaliti, wamekuibia au wamekutekeleza.

    Ni rahisi kuwalaumu wengine na kufarijika na kwa lawama hizo, ila sasa hazitakuwa na msaada wowote kwako.

    Njia bora ya kukabiliana na hali kama hizo ni kuchukulia kila kitu ni makosa yako.

    Hata kama kuna mtu kakudanganya, ni wewe umempa nafasi mpaka akakudanganya, ni wewe mwenyewe umemwamini.

    Kwa chochote unachokutana nacho au kupitia, hata kama ni wengine wamefanya, bado wewe una mchango kwenye hilo.

    Unapotambua mchango wako kwenye yote unayopitia, inakuwa rafisi kwako kuboresha ili usijiweke tena kwenye nafasi ya wengine kuweza kufanya mambo ya aina hiyo kwako.

    Kuchukulia kila kitu ni makosa yako ni bora kuliko hata kusamehe. Maana unaposamehe bado unakuwa unaamini uliyemsamehe ndiye mwenye makosa.

    Lakini unapokubali kila kitu ni makosa yako, unajiondoa kwenye hali ya mambo fulani kujirudia rudia kwako.

    Kuchukua hatua; kuwasamehe na kuchukulia kila kitu ni makosa yako inakupa nguvu kubwa ya kuona kila kitu ni wajibu wako na kuweza kuchukua hatua ili kuboresha.

    Rafiki yangu,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.