Home

  • Hatua ya 1 ya kupata unachotaka.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wengi huwa hawapati wanachotaka kwa sababu hawajui nini hasa wanachotaka.

    Unaweza kushangaa hapo kwamba iweje mtu asijue anachotaka, lakini huo ndiyo ukweli. Watu wanaweza tamani kupata vitu fulani kwenye maisha yao.

    Lakini ni wachache sana wanaoamua nini hasa wanataka na kuamua lazima wakipate bila ya kujali wanapitia nini.

    Hivyo hatua ya kwanza kabisa ya kupata chochote unachotaka ni kufanya maamuzi ya nini unataka na kudhaminiwa kupata hicho unachotaka.

    Unapofanya maamuzi maana yake umekata ushauri, umeitangazia dunia kwamba hicho ndiyo unataka na hutakubali kingine isipokuwa hicho.

    Sasa hebu jiulize ni wapi umefanya maamuzi ya aina hiyo kwenye maisha yako?

    Nini umeamua kwamba lazima ukipate hata iweje? Kama hujafanya maamuzi ya aina hii kwenye maisha yako, unajifurahisha tu na hutapata unachotaka.

    Chukua hatua; amua kile hasa unachotaka na kuwa tayari kukipambania usiku na mchana. Jiambie wazi kwamba utapambana mpaka ukipate au utakufa ukiwa unapambania.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

    www.uamshobinafsi.com.

  • Maamuzi makubwa 3 yakufanya kwenye maisha yako.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna maamuzi makubwa matatu unayoyafanya kwenye maisha yako, eneo unaloishi, watu unaishi nao na kile unachofanya.

    Haya ni maamuzi ambayo yataathiri sana maisha yako, lakini wengi hawayapi uzito unaostahili. Wengi huyafanya kwa mkumbo na siyo kufikiria wapi wanataka kufika kisha kufanya maamuzi hayo kwa mwongozo huo.

    Eneo unalochagua kuishi utakaa kwa muda mrefu na itakuwa na athari chanya au hasi kwenye mafanikio yako, hivyo lichague kwa umakini.

    Mahusiano yako na wengine yana ushawishi mkubwa kwenye kile unachofanya, hivyo chagua vizuri wale unaokwenda kujihusisha nao kwenye maisha yako.

    Kadhalika kazi au biashara unayokwenda kufanya, itachukua sehemu kubwa ya maisha yako na inahusika sana kwenye mafanikio yako, hivyo chagua kwa umakini nini unakwenda kufanya.

    Katika kufanya maamuzi hayo matatu, hakikisha yanatoka ndani yako na siyo unayafanya kwa kufuata mkumbo.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Njia 6 ya kuishughulikia uvumi.

    Rafiki yangu mpendwa uvumi na habari zisizo sahihi zinaweza kudhuru kila mtu mahali pa kazi. Mchongezi anapowasha cheche, mzunguko mbaya wa porojo unaweza kuenea kama moto wa nyika na kuharibu haraka ari na tija ya timu.

    Hapa kuna njia 6 zinazoungwa mkono na sayansi za kukomesha uvumi katika nyimbo zake:

    Njia ya kwanza ni kupuuza uvumi ( badilisha mada) wasengenyaji hutamani uangalifu. Unapoondoa umakini wako, maneno yao yenye sumu hupoteza nguvu. Ikiwa mtu anasengenya kuhusu wengine kwako, kataa kujihusisha naye.

    Mara tu wanapoanza kuongea vibaya juu ya mtu mwingine, funga mazungumzo kwa kusema, ” Sina maoni kabisa, na hii sio kazi yangu.”

    Pili; Weka mipaka iliyo wazi. Mipaka ni kanuni za mahusiano yako. Mipaka yako inawaambia watu jinsi utakavyowaruhusu wakutende, ikiwa ni pamoja na nguvu zao juu yako katika hali ya uvumi.

    Wanasaikolojia wamegundua kwamba watu wanaopiga porojo huwa hawana kujistahi, ambayo inaweza kuwaongoza kushiriki katika mijadala isiyo na mipaka kuhusu maisha ya faragha ya wengine.

    Tatu; Unda utamaduni wa uvumi chanya. Utafiti unaonyesha kuwa wasimamizi wanaojihusisha na porojo hasi, kuhusu wasaidizi wanachukuliwa kuwa wasioaminika. Lakini hii haimaanishi kuwa huwezi kuzungumza juu ya wafanyakazi. Jambo kuu ni kuiweka chanya.

    Nne; Kubaki upande wowote. Ikiwa wewe ni mhasiriwa wa porojo, ni jambo la kawaida kuhisi hasira, kuudhika, au kufadhaika. Baada ya yote, hii ni riziki yako na sifa yako kwenye mistari! Badala ya kupambana na moto kwa moto, chukua mtazamo wa kutoegemea upande wowote.

    Tano; Kuwasiliana kwa uwazi na wahalifu. Ikiwa unahitaji kuzuia uvumi, wafikie wahalifu kwa vidokezo hivi akilini: Hati na ujizoeze,waambie jinsi tabia zao zinavyokuathiri,kaa mtulivu,waue kwa wema,alikaa mtu wa tatu kushuhudia.

    Sita; Mjulishe bosi. Watu wengi huepuka kuwasiliana na wasimamizi. Hata hivyo, hali za uvumi uliokithiri huhitaji uingiliaji kati wa ngazi ya usimamizi. Hakuna aibu kuripoti uvumi wa mahali pa kazi kwa bosi wako au idara ya utumishi.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Ukweli kuhusu kushindwa.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye maisha hakuna kushindwa, bali kuna kushinda na kujifunza.

    Habari njema ni kwamba pale unapopata unachotaka unakuwa umeshinda. Lakini pale unapokosa unachotaka unakuwa umejifunza njia isiyo sahihi ya kupata kile unachotaka.

    Hivyo unachopaswa kufanya ni kujifunza njia iliyo sahihi ya kupata. Unapojifunza kupitia unayokosa, unajua ni njia zipi zisizo sahihi ili usizirudie.

    Kushindwa tu ni pale unapokuwa umekata tamaa au unaporudia makosa yale yale. Lakini unapokuwa tayari kujifunza na kuboresha zaidi, hakuna kushindwa badala yake kuna kujifunza.

    Kukosa kile unachotaka haimaanishi kwamba huwezi kukipata, bali inamaanisha hujajua njia sahihi ya kukipata. Hivyo wajibu wako ni kujifunza njia iliyo sahihi na kuitumia.

    Wewe mwenyewe ni shahidi, magumu mengi uliyopitia kwenye maisha yako na kuona kama umeshindwa, yamekuwa na mchango mkubwa kwako kupiga hatua.

    Chukua hatua; rafiki yangu hakuna unachopitia kisiwe na manufaa kwako utakuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua sahihi.

    Hatua ya kuchukua;

    Kwanza; orodhesha mambo yote mabaya unayohofia yanaweza kutokea. Jiulize yapi mabaya kabisa yanayoweza kutokea.

    Pili; Angalia uwezekano wa kila baya ulilowahi kutokea. Ni kwa kiasi gani linaweza kutokea.

    Tatu; Jiulize hatua unazoweza kuchukua pale lile baya kabisa linapotokea. Angalia kipi unaweza kufanya ili kuendelea.

    Nne; Angalia manufaa makubwa unayoweza kupata kwa kuendelea kufanya.

    Tano; Usikilize mwili wako ili ujue kama unachosikia ni hofu au machale.

    Sita; Itumie hofu kama mwongozo kwako, kile unachohofia zaidi lakini hakitoki kwenye fikra zako, ndiyo unapaswa kukifanya.

    Tano; Kumbuka magumu yote umewahi kupitia na ona mazuri uliyojifunza kupitia hayo.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Mchakato 8 wa kutatua matatizo.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwa kila changamoto unalopitia kwenye maisha yako, kuna namna unavyoweza kutatua.

    Hatua ya 1: Kubainisha tatizo. Kwa kujiuliza tatizo ni nini , unagunduaje tatizo na limeendeleaje kwa muda gani?

    Je, kuna data ya kutosha ili kuwa na tatizo na kulizuia lisipitishwe kwa hatua inayofuata ya mchakato? Ikiwa ndio, weka shida.

    Hatua ya 2: Fafanua tatizo. Ni data Gani inapatikana au inahitajika kusaidia kufafanua, au kuelewa tatizo kikamilifu?

    Je, ni kipaumbele cha juu kutatua tatizo kwa wakati huu? Hakikisha tatizo liko na halipitishwi kwa hatua inayofuata ya mchakato.

    Hatua ya 3: Bainisha malengo. Nini lengo lako la mwisho au haki unayotamani siku zijazo? Je, ukisuluhisha tatizo hili utatimiza nini?

    Je, ni muda gani unaotakikana wa kutatua tatizo hili?

    Hatua ya 4: Tambua chanzo cha tatizo. Tambua sababu zinazowezekana za shida . Zingatia sababu zinazoweza shida.

    Je, kuna taarifa gani au data gani ili kuthibitisha chanzo?

    Hatua ya 5: Tangeneza mpango kazi. Tengenezea orodha ya hatua zinazohitajika kuishughulikia chanzo kikuu na kuzuia shida kuwafikia wengine.

    Mpe mmiliki na kalenda ya matukio kwa kila kitendo. Vitendo vya hali ili kuhamisha kukamilika.

    Hatua ya 6: Tekeleza mpango kazi. Tekeleza mpango kazi ili kuishughulikia chanzo kikuu. Vitendo vya kuthibitisha vimekamilika.

    Hatua ya 7: Tathmini matokeo. Fuatilia na kusanya data. Je, umefikia malengo yako yaliyoainishwa katika hatua ya 3? Ikiwa sivyo, rudia mchakato wa hatua 8.

    Tatizo likitatuliwa, ondoa shughuli ambazo ziliongezwa hapo awali Ili kudhibiti tatizo.

    Hatua ya 8: Kuendelea kuboresha. Tafuta fursa za ziada za kutekeleza suluhisho. Hakikisha tatizo halirudi tena na uwasilishe masomo uliyojifunza.

    Ikihitajika, rudia mchakato wa kutatua matatizo wa hatua 8 ili kuendeleza uboreshaji zaidi.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi Ya Kubadili Tafsiri Yako Ya Hofu.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini changamoto kubwa kwenye hofu ni pale tunaposhindwa kuielewa kwa undani. Unapoiona hofu kwa nje inakuwa inatisha sana.

    Rafiki yangu usipoichambua hofu kwa undani, hutaweza kupiga hatua, maana utaiona ni kikwazo kikubwa.

    Hakuna kitu chochote kinachotokea kwenye maisha chenye maana isipokuwa ile maana ambayo tunavipa vitu.

    Hivyo inapokuja kwenye hofu pia, namna tunavyoitafsiri kunaweza kuwa kikwazo au kichocheo kwetu.

    Pale unapozipata dalili za hofu unaweza kuona ni mwisho na kuiacha.

    Habari njema ni kwamba hupaswi kutafsiri hivyo. Wewe chukulia ni kiashiria kwamba unakaribia kufanya kilicho sahihi.

    Chukua hatua; rafiki yangu mpendwa usiwe na wasiwasi maana pale unapoziona dalili za hofu kwako, jiambie wazi kwamba unakwenda kufanya kilicho sahihi na hakikisha unakifanya kweli.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Njia 2 ya kusema hapana.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini zipo njia mbili za kutusaidia kuepuka kushawishiwa vibaya na kufuata mkumbo.

    Njia ya kwanza ni kukagua uhalisia wa kundi unaloshawishiwa kulifuata. Badala ya kujiunga tu na kundi, angalia kama kweli kundi hilo lipo na kama lipo jua kama kila mtu kwenye kundi hufuata wengine kwa sababu tu ya wingi wao.

    Hili litasaidia kuondoa ile hali ya kufuata mkumbo kwa sababu wengi wanafanya, itatusaidia kujua nini kimewafanya wengi hao wafanye hivyo.

    Njia hii ya kwanza nzuri kutumia pale unapojikuta njia panda au ukiwa na hali ya kutokuwa na uhakika. Badala ya kujiunga tu na kundi, jua kundi hilo linasimamia nini.

    Njia ya pili ni kujiepusha na ujinga wa kundi, pale unapoona kuna jambo halipo sawa, badala ya kujiambia kuna mwingine ameshachukua hatua. Jua kila mtu anafikiria mwingine ameshachukua hatua na hivyo hakuna anayechukua hatua.

    Wewe vunja hilo kwa kuwa mtu anayechukua hatua na hata kama mwingine ameshachukua, hakuna unachokuwa umepoteza.

    Wengi wanaodhurika kwa kufuata mkumbo, kama waliojua kwa kushawishiwa na viongozi wa kidini ni kwa sababu wanakuwa hawapati muda wa kufikiri mwenyewe nje ya kundi wanalokuwepo.

    Kwa kuwa kila anayewazunguka anafanya, wanaona ndiyo kitu sahihi kufanya. Lakini wewe ukiwa mtu wa kukaa nje ya kundi kidogo na kufikiri kwa akili yako, utaona jinsi yale yanayofanyika yasivyokuwa sahihi.

    Chukua hatua; rafiki yangu kwenye maisha tunapaswa kujifunza kusema hapana na kukataa kufuata kundi. Hapo tutaweza kujipa muda wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Hatua 2 Muhimu Ya Kuchukua Katika Kufanya Maamuzi Ya Kifedha.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini katika kufanya maamuzi yetu ya kifedha kwa kuzingatia bahati na hatari, tunapaswa kuchukua hatua mbili muhimu.

    Moja tunapaswa kuwa makini na wale tunaowasifia na kutaka kuwa kama wao na wale tunaowadharau na kuepuka kuwa kama wao.

    Tambua kwamba siyo mafanikio yote yanatokana na juhudi na siyo wote walioshindwa ni wazembe. Fikiria hii kabla hujamhukumu yeyote, hata wewe mwenyewe.

    Mbili acha kuangalia hadithi ya mtu mmoja mmoja na angalia mwelekeo mpana. Unapojifunza kupitia hadithi ya mtu mmoja, huuoni ukweli, kwa sababu kuna bahati na hatari ambazo kwa nje hazionekani kwa urahisi.

    Badala yake jifunze kupitia wengi ambao wamefanya kitu na kufanikiwa. Ni vigumu watu wengi wakapata bahati ya aina moja, hivyo japo kila mtu atakuwa na bahati yake, kuna vitu ambavyo wote watakuwa navyo. Ukijifunza hivyo na kuvitumia, itakusaidia zaidi kuliko kuangalia mtu mmoja.

    Kuchukua hatua; badala ya kumwangalia mmoja aliyefanikiwa sana na kujifunza kwake, angalia watu wengi waliofanikiwa na kile ambacho wanacho kwa pamoja na jifunze hicho.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Jinsi Hofu Ilivyo Mwongozo Kwako.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini changamoto kubwa kabisa kwenye hofu ni pale tunaposhindwa kuielewa kwa undani. Unapoiona hofu kwa nje inakuwa inatisha sana.

    Usipoichambua hofu kwa undani, hutaweza kuchukua hatua, maana utaiona ni kikwazo kikubwa.

    Kwa kila hofu unayokuwa nayo, usiishie tu kuiangalia kwa nje, bali ichimbe kwa undani, uweze kuielewa na kuchukua hatua sahihi.

    Hatua muhimu ya kuchukua ni kujiuliza kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea?

    Kwa chochote unachohofia, usikubali tu hofu hiyo juu juu. Badala yake chimba ndani, jiulize kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea kwenye hilo unalohofia.

    Jiulize kama kweli hofu hiyo itatokea kama unavyohofia, ni mambo gani mabaya kabisa yanayoweza kutokea?

    Orodhesha yote mabaya unayoona yanaweza kutokea kutokana na kile unachohofia. Kisha kwa kila unaloorodhesha jiulize ni hatua zipi unazoweza kuchukua kulikabili kama litatokea.

    Andika hatua zote unazokwenda kuchukua pale jambo baya kabisa linapotokea ili uweze kurudi kwenye mipango yako.

    Kwa kufanya zoezi hili, unagundua wazi kwamba mengi unayohofia hayawezi kutokea na hata kama yatatokea una njia ya kuweza kuyavuka na kuendelea na mipango yako.

    Chukua mfano wa kuanzisha biashara, hofu ni itashindwa. Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni biashara kufa na ukapoteza kila kitu.

    Kama hilo litatokea unaweza kuanza upya, hata kwa kutafuta kazi au kibarua kwanza ili ujenge upya.

    Chukua hatua kwa kuchambua hofu hivi, unaona wazi kwamba unachohofia sana hakipaswi kuwa kikwazo kwako.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kwa Nini Unapaswa Kujua Kuwa Hofu Sio Adui Wako.

    Rafiki yangu mpendwa hofu ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Kila mtu huwa anakutana na hofu, hasa pale unapofanya kitu kipya ambacho hujazoea kufanya.

    Kila mtu huwa anahofia, kila anayefanya kitu kwa mara ya kwanza anakuwa na hofu kubwa. Hata wale wanaoonekana ni majasiri, ndani yao huwa wanakuwa na hofu kubwa.

    Lakini huwa wanaweza kuzishinda hofu hizo. Mabadiliko makubwa ya kimtazamo unayopaswa kuyafanya ili uishinde hofu ni kujua kwamba hofu siyo adui.

    Hofu siyo kitu ambacho kinalenga kukuangusha na kukushinda. Hofu ni tahadhari ambayo akili yako inakupa, kwa lengo zuri tu la kuhakikisha unakuwa hai na salama.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini hofu ndiyo imekiwezesha kizazi chetu binadamu kuendelea kuwa hai mpaka leo. Ni kwa sababu hofu inaleta tahadhari na mtu anapochukua tahadhari hiyo anakuwa salama.

    Hivyo tunapaswa kuchukulia hofu siyo kama kikwazo cha kutufanya tusimame, bali kama tahadhari ya kwenda kwa umakini.

    Habari njema ni kuwa huhitaji kuvunja kabisa hofu ndiyo uweze kufanya makubwa. Unachopaswa kufanya ni kujisikiliza, kuielewa na kuchukua hatua huku ukiwa na tahadhari.

    Hofu huwa inaonekana ina nguvu kwa sababu inagusa zaidi hisia zetu. Na pale kitu kinapogusa hisia, huwa tunakipa uzito zaidi.

    Kwa kuweza kuisikiliza na kuielewa hofu, utaweza kuchukua hatua sahihi na kufanya makubwa. Chukua mfano unataka kuanzisha biashara, lakini unahofia itashindwa . Hiyo haimaanishi kwamba ni uhakika biashara hiyo itashindwa, bali ni tahadhari kwamba upo uwezekano mkubwa wa biashara kushindwa.

    Hivyo unapaswa kuendesha biashara yako kwa umakini mkubwa ili kuepuka hatari za kushindwa.

    Kuchukua hatua ndiyo njia pekee ya kuishinda hofu yoyote unayokuwa nayo. Njia pekee ya kuivuka hofu ni kuchukua hatua kufanya kile unachohofia kufanya.

    Baada ya kuisikiliza na kuielewa hofu, unapaswa, kuchukua hatua. Usiendelee tu kuitafakari, badala yake chukua tahadhari ambazo hofu inakupa na kisha chukua hatua.

    Unapochukua hatua na kupata matokeo mazuri, unazidi kujiamini na kupata hamasa ya kuchukua hatua zaidi.

    Hata pale hofu inapokuwa kali na ukashawishika uache kufanya, usisikilize hofu, badala yake chukua hatua. Hata kama itakuwa hatua ndogo kiasi gani, una nguvu ya kuivuka hofu yoyote unayokuwa nayo.

    Kama unataka kumuuliza mtu kitu na unahofia, jua ni tahadhari gani hofu inakupa kisha muulize mtu huyo kile unachotaka kumuuliza.

    Utashangaa jinsi hilo linavyokuwa rahisi kwako na mtu huyo anakujibu vizuri kuliko hata ulivyotegemea.

    Na hata kama hatakujibu vizuri, bado hakuna hatari kubwa au chochote ulichopoteza kwa kuuliza.

    Hofu pia ni nzuri pale inapokuzuia usifanye mambo yenye madhara kwako. Kama unahofia madeni, unakuwa na nidhamu nzuri ya fedha.

    Kama unahofia magonjwa sugu unalinda afya yako. Kwa kuitazama vizuri, hofu ni rafiki yako mkubwa, anayekujali na kutaka kuona upo salama.

    Chukua Hatua; rafiki yangu tunapaswa tuielewe hofu na kuchukua hatua sahihi. Kamwe tusikubali hofu ituzuie kwenye kuchukua hatua.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.