-
Usikubali Hofu Ikutawale.
Rafiki yangu nikupendaye, hofu ni zao la akili. Ni vitu ambavyo hata havipo, ni vitu ambavyo vinazalishwa ndani ya akili yako.
Pata picha mtu yuko mwezi wa tisa leo, anaanza kufikiria hivi mwezi wa kumi utakuwaje? Rafiki yangu, hata kwa wale wanaosali, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake sala na kwenye sala hiyo hakuna mahali alipoomba mambo ya kesho ila leo tu. Tunayasumbukia yajayo na tunayaacha ya sasa. Utupe leo, mkate wetu wa kila siku, na hajasema kesho, ila leo.
Usihofie mambo kutokea, wewe siyo mdhibiti wa mambo kutokea au kiranja wa dunia wa kutaka dunia iende kama wewe unavyotaka iende.
Acha mambo yatokee kama yalivyopangwa kutokea, usiwe na wasiwasi na kitu chochote kile, asili inakulinda na kukutetea, wewe timiza wajibu wako tu.
Hatua ya kuchukua leo; usihofie kitu chochote kile, nenda kachukue hatua kubwa leo bila hofu, bila sababu yoyote ile.
Unachohofia hata hakipo, ni zao la fikra yako, usijifunge na hofu jifungue kwa kuchukua hatua na utaona mambo yanaenda.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
-
Umuhimu Wa Kuanza Na Wewe Kwanza.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini unapaswa kuanza na wewe kwanza, kama kuna watu hawakupi kile ambacho wewe unataka kwenye maisha yako, anza kwanza wewe mwenyewe kujipa kitu hicho ambacho unataka kutoka kwao.
Kwa mfano, kama unataka upendo kutoka kwa wengine, anza kwanza kujipenda wewe mwenyewe, penda kile unachofanya na kisha wapende wengine na utashangaa vile unavyotaka vitakuja vyenyewe.
Kama watu hawakuamini, huna haja ya kuwalazimisha wakuamini, unachotakiwa kufanya ni kuanza kujiamini wewe mwenyewe kisha wale ambao watakuamini watakuamini bila shaka yoyote ile.
Kama unawapa watu kazi na hawafuatilii maagizo unayowapa, anza wewe kuwafuatilia kwa karibu kwa kudai matokeo unayoyataka na wao watajituma kukamilisha hilo kwa sababu wanajua wasipofanya hawana ripoti ya kutoa.
Kama kuna watu umewakosea, unawaomba msamaha na hawataki, achana nao, jisamehe wewe mwenyewe ila maisha yako yaende.
Kama kuna watu hawakuheshimu, anza kujiheshimu wewe mwenyewe kwanza. Kama kuna watu kwenye biashara yako wanakuambia haiwezekani waoneshe kwa mfano jinsi inavyowezekana kufanyika.
Kile ambacho sisi tunataka kitokee kwetu, tuanze kwanza sisi kukiishi kwa kukifanyia kazi. Watu wakikuambia, huwezi kufanikiwa kwenye lengo lako, waambie inawezekana kwa vitendo. Kuwa bora wewe ili uweze kuwadhihirishia wengine kwamba mambo yanawezekana kama ukiyafanyia kazi.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa mfano wewe mwenyewe wa kuishi kile ambacho wengine unataka wakufanyie.
Kanuni ya dhahabu inasema, watendee wengine kile ambacho wewe ungependa kutendewa. Nenda kalifanyie kazi hili na utakuja kunishukuru baadaye.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kwa Nini Hupaswi Kununua Matatizo Ya Wengine.
Rafiki yangu mpendwa nianze kwa kusema, usinunue matatizo ya wengine. Rafiki matatizo uliyonayo, tayari yanakutosha hivyo usinunue mengine.
Muda uliokuwa nao kufanya vitu vya msingi ni mdogo mno. Ukisema uhangaike na kila kitu kwenye hii dunia basi utakufa haraka.
Ukisema uhangaike na matatizo ya kila mtu hutaweza kuyamaliza. Kwanza matatizo ya watu, huwa yanamalizwa na watu wenyewe. Unaweza kuwa mtu wa huruma sana kusikiliza matatizo ya watu na kutaka kuwasaidia lakini matatizo ya watu huwa yanamalizwa na watu wenyewe.
Matatizo ya watu ni mengi, na wengine wanapenda kuwauzia watu wengine matatizo yao. Hivyo, usipokuwa makini, utajikuta kila siku unasikiliza drama za watu.
Na watu ni waigizaji sana, usipokuwa makini, watakuigizia na kuja kuona kwamba jukumu la maisha yao ni lako.
Watu wengi hawajui kwamba, jukumu la maisha yao, ni la kwao wenyewe. Wafanye watu unaohusiana nao, wajitambue na wajue kwamba jukumu la maisha yao ni lao mwenyewe.
Watu wengi ambao wameanza kupata mafanikio kidogo kwenye jamii zetu, wamekuwa wanapata shida sana, kila mtu anamuona kama ndiyo kimbilio la maisha yake, watu hawajitumi na wanajua nikiwa na shida nitasaidiwa na fulani.Na usipokuwa makini, utakuwa unanufaika matatizo yao kila siku na kushindwa kufanya mambo yako.
Kila mtu afanye kazi na afundishwe kujitegemea na kusimama na mambo yake. Usiruhusu utegemezi ambao hauna maana kwako, na usikubali kununua matatizo ya watu.
Watu wengine wanatengeneza matatizo ili uweze na wewe kuingia kwenye matatizo hayo.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa mkali kwa watu wako wa karibu ambao wanashindwa kujitegemea na kufanya utegemezi kwako.
Wafundishe kujitegemea na kutambua kuwa jukumu la maisha yao, ni lao wenyewe.
Kama mtu ana nguvu, anaweza kufanya kazi, afanye kazi ili maisha yake yaende na siyo kukubali kusaidia majukumu binafsi ya watu ambao wana uwezo wa kufanya kazi.
Watu wana uvivu, uzembe wa kutokufanya kazi. Wanapenda kupata mteremko, usikubali kuwaonesha hilo, wasaidie wasimame na miguu yao na kutambua kuwa jukumu la maisha yao ni lao na siyo lako.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kama Huna Tabia Hizi Mafanikio Makubwa Hayakuhusu.
Rafiki yangu mpendwa kwa kuanzia, hebu tuchunguze tabia zetu kwa tunazoishi kwenye maisha yetu, kwa sababu kila kitu kwenye maisha yetu huwa kinajengwa na tabia.
Watu wengi mambo tunayofanya kila siku yanatokana na tabia ambazo tumejijengea huko nyuma.
Watu hawafanyi kitu kama siyo tabia yao. Vitu vingi ambavyo unafanya ni kwa sababu ni tabia yako kufanya ndiyo maana unafanya hivyo.
Kuna usemi kuwa ‘huwa tunatengeneza tabia, kisha tabia zinatutengeneza.’ Ili uweze kufika au kufanya kile unachotaka kufanya ni lazima ujenge kwanza tabia juu ya kitu hicho.
Sina uhakika kama itakufaa lakini hapa kuna orodha ya tabia kumi ambazo ukiwa nazo utaweza kufika mbali.
1. Tabia ya kuamka asubuhi na mapema na kujiandaa kwa siku husika.
2. Tabia ya kujali na kulinda sana muda, kutokupoteza muda kwa mambo yasiyo muhimu.
3. Tabia ya kwenda hatua ya ziada kwenye kila ambacho mtu anafanya.
4. Tabia ya kujifunza kila siku.
5. Tabia ya kuweka akiba kwenye kila kipato anachoingiza.
6. Tabia ya kuwekeza kwenye kila kipato.
7. Tabia ya kujenga mahusiano imara na wale ambao unahisiana nao.
8. Tabia ya uaminifu na uadilifu wa hali ya juu sana.
9. Tabia ya kutokukata tamaa hata kama nini kimetokea.
10. Tabia ya kukubali majukumu yako.
Hatua ya kuchukua leo; andika tabia hizi mahali na uwe unazipitia kila siku kujikumbusha.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Sheria Za Kuwa Na Maisha Marefu.
Rafiki yangu mpendwa leo tutachunguza kwa kina sheria za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio bilionea na mwekezaji Charlie’s Munger ambaye kwa sasa ana miaka 99.
Aliulizwa na mwandishi aseme siri za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio.
Moja ni usiwe na wivu. Wivu ni hali ya kujiona wewe una stahili kuliko mwingine.Ukiishi maisha ya wivu, hutaweza kufurahia maisha yako.
Waache watu waishi vile wanavyotaka wao na wewe ishi vile unavyotaka wewe.Usiwe na wivu na mtu.
Mbili ni usiwe na chuki. Watu wamekuwa na chuki za kijinga, hawapendi kuona wengine wamewazidi, wanakuwa na chuki ambazo hazina hata maana kwenye maisha yao.
Chuki ni mzigo mzito, usikubali kuubeba, kila siku kuwa mtu wa kusamehe na kuwachukulia watu kama walivyo bila kubeba matatizo yao binafsi.
Tatu ni usitumie zaidi ya kipato chako. Hapa kwenye fedha mchakato ni ule ule, haijalishi unaingiza kipato kikubwa kiasi gani, unatakiwa kutumia chini ya kipato chako.
Usiende juu ya kile unachopata. Na ukizingatia misingi hii, lazima utafika mbali.
Nne ni shauku. Shauku ndiyo sifa namba moja inayolipa zaidi duniani. Ukitaka kukubalika kila eneo la maisha yako basi ongea kwa shauku kubwa. Kila kitu unachofanya, kifanye kwa shauku kubwa.
Ukikutana na watu usiwe kama mtu ambaye hana shauku, ukikosa shauku kubwa kwenye maisha yako, hata kama una kitu kizuri ndani yako watu watakupuuza mara moja.Kuwa na shauku kubwa kwenye kila eneo la maisha yako.
Tano ni jihusishe na watu wanaoaminika. Kama una watu ambao hawaaminiki kwenye maisha yako achana nao kabisa. Anza kujihusisha na watu wanaoaminika na itakusaidia kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako. Ukiaminika kwenye maisha yako, watu wengi watakuwa tayari kufanya kazi na wewe.
Sita ni fanya unachopaswa kufanya. Jua wajibu wako ni nini kisha kuwa tayari kufanya wajibu wako bila kukumbushwa. Watu wengi hawafanyi kile wanachopaswa kufanya, hivyo wewe ukiwa ni mtu wa kufanya kile unachopaswa kufanya bila kuambiwa utafanikiwa sana kwenye maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; ishi sheria hizi sita kwenye maisha yako, na jikumbushe kila siku pale unapoamka na kabla hujaenda kulala.
Sina uhakika kama itakufaa lakini ushauri wa Bilionea Charlie Munger unafanya kazi, kama yeye ni Bilionea na ni Mzee wa miaka 99 ameweza kuishi misingi hii basi na wewe ukiishi bila shaka na wewe utatoboa miaka kama yake au hata na zaidi.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Vitu 3 vinavyosababisha shida yoyote kwenye maisha yako.
Rafiki yangu mpendwa leo tunachunguza vitu vitatu vinavyosababisha shida kwenye maisha yetu.
Mfanyabiashara, mwekezaji na mwandishi Kevin O’Leary anasema kwenye maisha kuna wanaume, wanawake na fedha.
Mwandishi anasema, shida yoyote kwenye maisha, inatokana na vitu hivyo vitatu. Kama husumbuliwi na mwanamke, basi mwanaume anakusumbua. Na kama kwa mwanamke na mwanaume uko vizuri basi fedha itakua inakusumbua.
Kila mmoja wetu ana shida kwenye mahusiano yake au fedha, kama husumbuliwi na fedha basi unasumbuliwa kwenye mahusiano.
Na hakuna mtu ambaye amefanikiwa kupatia maisha kwenye kila eneo la maisha yake. Sina uhakika kama itakufaa lakini mwandishi anasema, sehemu kubwa ya matatizo ya wengi, inatokana na ukosefu wa fedha au tabia mbaya kwenye fedha.
Kwenye fedha kama una fedha basi utakua una tabia mbaya za fedha yaani kwenye kudhibiti fedha na matumizi kiujumla unapigwa chenga. Ila matatizo mengi tuliyonayo, yanatatuliwa na FEDHA tu.Ukiwa na fedha shida nyingi unazimaliza.
Leo nataka nikuulize swali, kama tatizo lako ukiwa na hela linaisha? Kama jibu ni ndiyo, basi huna tatizo. Kaa chini na ona njia zipi unaweza kutumia kupata fedha unazozihitaji ili kutatua tatizo hilo. Kama fedha inaweza kutatua tatizo linalokusumbua, basi tafuta fedha tu na tatizo lako litaisha. Kama tatizo lako halitatuliwi na fedha, basi iachie asili, muda ifanye kazi yake usijisumbue kwa matatizo ambayo hayatatuliwi na fedha.
Kama ni mwanaume au mwanamwake anakusumbua angalia njia ambayo mnaweza kuweka mambo yenu sawa. Kama inashindikana tafuta mwache asili itakusaidia kupambana naye wewe ishi maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; kama fedha inatatua tatizo lako, basi tafuta fedha achana na yale ambayo hayana msingi kwako.
Kumbuka, kwenye maisha kuna wanawake, wanaume na fedha, kipi ambacho kinafanya maisha yako yaweze kwenda? Mwanamke au mwanaume au fedha?
Kitu kimoja zaidi, fedha ndiyo jawabu la mambo yote, ukiwa na fedha utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Faida 5 Za Shukrani Kwa Afya Ya Akili.
Rafiki yangu mpendwa nianze kwa kusema shukrani inaweza kuonekana tofauti kidogo kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, shukrani kwa ujumla hufafanuliwa kama tabia ambayo inaruhusu mtu kutambua na kufahamu vipengele vyema na vya maana vya maisha.
Mwanasaikolojia Nathan Brandon anaelezea shukrani kama njia ya kufikiria kuhusu shukrani ni kwamba mara nyingi huibua hisia changamfu, chanya, ikiwa ni pamoja na furaha, upendo na shangwe.
Shukrani inaweza kusaidia kudhibiti hisia zako. Utafiti unapendekeza shukrani ina jukumu katika uwezo wa mtu wa kutambua na kudhibiti hisia, huku baadhi ya tafiti zikielekeza kwenye uhusiano unaowezekana kati ya shukrani na akili ya kihisia.
Shukrani inaweza kuinua mawazo yako. Wakati mtu anahisi shukrani ambayo inaweza kuelekezewa kama hisia chanya yenyewe, utafiti unaonyesha huwa na uzoefu wa hisia chanya zaidi kwa ujumla.
Shukrani inaweza kukusaidia kujisikia kuunganishwa zaidi na wengine. Shukrani inaweza kuwasaidia watu kuhisi kuwa wameunganishwa zaidi na wengine na ulimwengu unaowazunguka, jambo ambalo linaweza kusababisha furaha zaidi na kupunguza upweke.
Shukrani inaweza kukuhamasisha kuelekea matokeo bora. Unaposhukuru kwa jambo fulani, shukrani hiyo mara nyingi huonyeshwa na kuendana na matokeo yako. Tunapothamini uvumilivu wetu, hilo litaonekana katika mazoea yetu ya kula na mazoezi ya kimwili.
Shukrani inaweza kukulinda kutokana na athari za mafanikio. Uhusiano kati ya shukrani na kuboresha afya ya akili katika uso wa dhiki umetambuliwa na watafiti kwa muda mrefu sana.
Chukua hatua; rafiki yangu tumejua umuhimu wa kuwa na shukrani kwenye maisha, tunapaswa kuwa watu shukrani na maisha yetu yataboreka bila shaka.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Njia 5 za kusisimua shukrani inayoweza kuboresha maisha yako.
Focus on gratitude.

Rafiki yangu mpendwa tuanze kwa kutazama jinsi ya kuifanya shukrani kuwa sehemu ya utaratibu wako wa kila siku, na hivyo kuweza kuboresha maisha yetu.
Hatua ya kwanza ni shukrani inaweza kuboresha afya yako ya akili. Utafiti katika chuo kikuu cha Indiana ulichunguza shukrani na afya ya akili.
Watafiti hao wanapendekeza kwamba ‘ kuandika barua ya shukrani hutokeza afya bora ya kiakili kwa kuondoa uangalifu wa mtu kutoka kwa hisia zenye sumu, kama vile chuki na wivu’.
Hatua ya pili ni shukrani inaweza kuboresha mahusiano yako. Haijalishi ni aina gani ya uhusiano ambao tungependa kuboresha, maneno ya shukrani ni hatua katika mwelekeo zaidi.
Hatua ya tatu ni shukrani inaweza kukufanya uwe na furaha zaidi. Watafiti katika uwanja wa saikolojia chanya wamepata uhusiano thabiti kati ya usemi wa shukrani na furaha iliyoongezeka.
Hatua ya nne shukrani inaweza kukusaidia kulala vizuri. Watafiti wanaamini kuwa manufaa yanaweza kupatikana kwa sababu wanaotoa shukrani hawana uwezekano mdogo wa kuzingatia mawazo hasi, yanayotokeza wasiwasi wakati wa kulala.
Hatua ya tano; Shukrani inaweza kukufanya uwe na matumaini zaidi. Kuongeza shukrani zako kunaweza kukufanya uishi maisha marefu.
Chukua hatua; Rafiki yangu ni muda nzuri sasa wa kuamua kuwa chanya na pia kuwa mtu wa shukrani muda wote. Tunapofanya hivyo, tunaishi kwa kufurahia maisha yetu hata kama tunapitia changamoto si hapa.
Pia, ningependa kukushukuru wewe, msomaji mpendwa, kwa kuchukua muda wa kufuata pamoja nami katika uchunguzi wetu mdogo wa shukrani.
Natumai umepata thamani katika kile tulichoshiriki kuhusu neno shukrani.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Njia 5 ya kushinda imani yako yenye ukomo.
Rafiki yangu mpendwa karibu kwenye makala hii ambayo itajadili kuhusu namna ya kushinda imani yenye mipaka.
Rafiki ni lini mara ya mwisho ulikata tamaa kwa jambo fulani na kwa nini? Ni lini mara ya mwisho ulishindwa, na ulijiambia nini kuhusu sababu ya kushindwa kwako?
Kushinda imani zenye ukomo si rahisi kila wakati. Wamejikita ndani yetu, mara nyingi tangu utoto. Lakini mara tu unapogundua ni nini na jinsi ya kuzitambua, unaweza kujifunza jinsi ya kushinda imani zako zenye mipaka.
Kwa kujumuisha mikakati inayoweza kutekelezeka ya kubadilisha imani zenye kikomo katika maisha yako ya kila siku, hatimaye unaweza kufikia kila kitu ambacho umewahi kitamani.
Hatua ya kwanza ni kutambua na kuondoa imani zenye mipaka. Kwa wengi wetu, imani zetu kuhusu sisi wenyewe ndio kitu pekee kinachotuzuia .
Imani hizi pungufu zinatuambia kuwa sisi hatuwezi, sisi si jasiri au tunastahili kupendwa. Mazungumzo mabaya kama mimi ‘siwezi kusimama mbele ya watu, siwezi fanya mazoezi’. Unapoweza kutambua mazungumzo haya mabaya ya kibinafsi na kuyaondoa kutoka kwa msamiati wako, unaweza kuwa bora katika hali yoyote.
Hatua ya pili ni kutafuta kusudi lako kuu. Mara tunapotupilia mbali imani zenye vikwazo ambazo zimekuwa zikikuzuia, ulimwengu mpya kabisa wa uwezekano utafunguka. Unaweza kufanya, kuwa na kuwa na chochote unachotaka. Kusudi lako ndilo linalokuongoza. Ndiyo sababu unatoka kitandani asubuhi. Kwa Nini unafanya maamuzi unayofanya. Usiogope kufikiria kubwa. Unapokuwa na kusudi dhabiti, unaweza kulitumia kukusukuma kuwa mtu bora zaidi. Utakuwa na maono makubwa sana kwa maisha yako, na hautazuilika . Hiyo ndiyo maana ya kuishi kwa kusudi.
Hatua ya tatu ni kuzingatia. Kugundua kusudi lako kuu kutakupa nguvu. Utakuwa na kiendeshi unachohitaji ili kuwa mtu bora zaidi.
Hatua ya nne ni kuunganisha muda wa net. Unapokuwa kwenye njia ya kuwa mtu bora zaidi, huna wakati wa kupoteza. Watu waliofanikiwa wanajua hili na hutumia wakati wao wote kwa busara. Watu hawa wanatumia kile ambacho Tonny Robbins anakiita wakati wa N. E. T. Au hakuna wakati wa ziada ili kuendelea na safari yao ya kujiboresha.
Wakati wa NET ni wakati wote unaotumia kufanya kazi za kila siku au kutofanya chochote. Kusafisha,usafiri,ununuzi wa mboga na mbio za marathoni za Netflix zote ni wakati wa NET. Unaweza kutumia wakati huu kugundua jinsi ya kuwa bora zaidi badala ya kuupoteza.
Hatua ya tano; Ondoka nje ya eneo lako la faraja. Iwapo umekuwa ukifanya kazi ili kuwa bora zaidi kwa muda, unaweza kuanza kuhisi umetulia, haijalishi umebakisha malengo mangapi ili kufikia.
Njia bora ya kuendeleza ukuaji ni kutoka nje ya eneo lako la faraja. Inamaanisha eneo lako la kustarehesha kimwili: kwenda kuruka angani, kuendesha baiskeli milimani au kupiga puto ya hewa moto.
Inaweza pia kumaanisha eneo lako la kufariji kiakili au kihisia: kwenda kwenye tukio ambalo humjui mtu yeyote au kujipa changamoto ya kuwa hatarini na mwezi wako.
Kumbuka daima kuna mengi zaidi ya kujifunza ikiwa uko tayari kufanya kile kinachohitajika ili kuwa bora zaidi.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Jinsi Ya Kufikiri Kwa Usahihi.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kufikiri kwa usahihi na umakini ni muhimu kuliko kuwa na akili.
Wapo watu wengi wenye akili sana ila hawana hekima na hivyo hawafanyi maamuzi sahihi.
Wewe unapaswa kujijengea uwezo wa kufikiri kwa usahihi na umakini, kwa kujua msingi wa kitu na kujua jinsi kinaungana na vitu vingine na unapofanya maamuzi, unajua kabisa ni matokeo gani yanakwenda kupatikana.
Ili kufikiri kwa usahihi unahitaji vitu viwili; Kitu cha kwanza ni kuepuka kuathiriwa na hisia zako wakati wa kufikiri na kufanya maamuzi. Hisia zinapokuwa juu, huwezi kufikiri kwa usahihi. Hivyo kuwa na njia ya kutuliza hisia zako au kuwa na subira mpaka zinapotulia ndipo ufikiri na kufanya maamuzi.
Kitu cha pili ni kujua misingi ya kitu kabla hujafanya maamuzi. Kila kitu kina msingi yake ambayo huwa haibadiliki, ukijua msingi hiyo inakusaidia sana kufanya maamuzi ambayo ni sahihi.
Utajua kama unafikiria kwa usahihi kuhusu kitu kama unaweza kumwelezea mtoto wa darasa la tano na akakuelewa au mzee ambaye hakuenda shule kabisa.
Kama chochote unachofanya huwezi kukielezea kwa namna sahihi kwa mtoto wa darasa la tano kuelewa, basi wewe mwenyewe hujui unachofanya na huwezi kufanya maamuzi sahihi kwenye eneo hilo.
Kwenye kila tasnia, kuna mambo mengi na mengi zaidi yanagunduliwa kila siku. Huwezi kupata muda wa kuweza kujifunza na kujua kila kitu, ila yale ya msingi huwa ni machache na hayabadiliki. Ukiyajua hayo ya msingi, utaweza kufanya maamuzi bora na sahihi kwenye eneo hilo.
Kuchukua hatua; rafiki yangu tunapaswa kuepuka sana kutumia lugha na dhana ngumu kwa wengine kuelewa Ili tuonekane kama tunajua, badala yake tunapaswa tukijue kitu kwa misingi yake, kwa namna ambayo tunaweza kumweleza yeyote na akaelewa, hapo tunakuwa tumekielewa vizuri na kuweza kufanya maamuzi sahihi.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.