-
Uongo Wa Kufikiri Chanya.
Rafiki yangu mpendwa, bila shaka umekuwa ukisikia kufikiri chanya kunahubiriwa sana kwenye kutengeneza mtazamo sahihi wa mafanikio. Ni kweli kufikiri chanya kuna manufaa kuliko kufikiri hasi, lakini pia pasipokuwa na mpango sahihi, kufikiri chanya kunaweza kuwa tatizo kubwa.
Watu wengi wamekuwa wakitumia kufikiri chanya kama njia ya kukwepa na kujaribu kuzika hisia zao. Pale wanapokutana na tatizo au changamoto na kuibua hisia ndani yao, wanakimbilia kufikiri chanya ili kuondoa hisia hizo.
Kinachotokea ni hisia haziondoki, badala yake zinadidimizwa. Hilo linamtaka mtu atumie nguvu zake nyingi kuendelea kudidimiza hisia hizo ili zisipate nafasi ya kuibuka na kumsumbua.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini hivi ndivyo wengi wamekuwa wakitengeneza matatizo ya kisaikolojia kwa baadaye. Unachopaswa kufanya ni kutokutumia hisia zozote unazokuwa nazo.
Badala yake jipe muda wa kukaa na hisia zako, kuzielewa na kuzitatua. Fungua moyo wako na zielewe hisia mbalimbali unazopitia, Ili uweze kuzitatua na kuwa huru nazo. Baada ya kufanya hivyo, hapo sasa unaweza kufikiri chanya utakavyo na hilo litakusaidia.
Tambua hapa haimaanishi utawaliwe na hisia zako na zikusukume kufanya mambo fulani fulani. Bali inamaanisha kuzipa nafasi, kuzielewa na kutatua kile kinacholeta hisia hizo.
Kumbuka hisia zetu zina nguvu kubwa, ukijaribu kuzididimiza, zinazidi kupata nguvu na siku moja zitalipuka na kuleta madhara makubwa.
Hatua ya kuchukua, rafiki yangu tunapaswa kuzikabili hisia pindi zinapokujia, tatua kile kinachozileta na utakuwa huru kiakili na kihisia kitu kitakachokuwezesha kufanya makubwa.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kwa Nini Unapaswa Kujijengea Ujasiri Mkubwa.
Rafiki yangu mpendwa, sina uhakika kama itakufaa, lakini Robin ila Ro anatushirikisha hadithi ya Niki lauda, mshiriki wa mbio za magari ambaye alipata ajali mbaya kwenye mashindano na kuungua kichwa na uso.
Alipelekwa hospitalini akiwa taabani na kila mtu alijua hawezi kupona. Lakini siku 40 baadaye alirudi kwenye mbio za magari, kabla hata hajapona vizuri.
Alipoulizwa alieleza kilichomwezesha kupona ni alikataza akili yake kupumzika, kwani alijua kwa hali aliyokuwa nayo, angeruhusu akili ipumzike kingekuwa kifo.
Na pia alieleza baada ya kuona amepata nafuu, alichagua kurudi kwenye mbio za magari kwa sababu ndiyo kitu muhimu zaidi kwake.
Kupitia hadithi hii Robin anatupa mafunzo matatu makubwa.
Kwanza ni kujenga ujasi, hakuna anayezaliwa akiwa jasiri, Bali ujasiri hutengenezwa kadiri mtu anavyokabiliana na magumu. Hivyo unapokutana na magumu, usilalamike wala kuyakimbia, bali yakabili na yatumie kujenga ujasiri.
Mbili ni rudi kwenye mwendo mapema. Unapokutana na magumu ambayo yanakutoa kwenye mwendo, hakikisha unarudi kwenye mwendo mapema iwezekanavyo.
Magumu hayo yanaweza kukujengea hofu ambayo itaendelea kukupa hofu kadiri utakavyokuwa nje ya mwendo kwa kurudi kwenye mwendo mapema, utavunja hofu hiyo na kuimarisha ujasiri wako.
Tatu ni usistaafu. Hata baada ya Niki lauda kustaafu mbio za magari, aliendelea na ujasiriamali kwenye sekta ya usafiri. Licha ya kuwa alikuwa ameshafika kwenye kilele, hakuona huo ndiyo mwisho, aliendelea kujisukuma zaidi.
Hivyo ndivyo alivyopaswa kuwa pia, kutokukubali kustaafu baada ya kufika kileleni, badala yake kuendelea kujisukuma na kufanya makubwa zaidi.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kwa Nini Unapaswa Kuishi Maisha Yako Halisi?
Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo kwa akili ya kujijengea sifa baada ya kuondoka hapa duniani. Wanafanya kwa lengo la kuendelea kukumbukwa vizazi kwa vizazi kwa majina yao kuandikwa maeneo muhimu au kuchongwa sanamu.
Lakini kama ilivyo mambo mengine ya maisha, unapolazimisha kitu huwa hakitokei.
Unapofanya mambo Ili ukumbukwe, hakuna anayekukumbuka, kwa sababu unakuwa siyo halisi.
Rafiki unapaswa uachane na msukumo wa kufanya vitu ili kukumbukwa au kuacha alama.
Badala yake chagua kuishi maisha halisi kwako, simamia kile kweli unachoamini na utakuwa na maisha bora huku pia ukiwa na nafasi kubwa ya kuendelea kukumbukwa.
Watu hawatakukumbuka kwa sababu unataka wakukumbuke, bali watakukumbuka kwa aina ya maisha uliyoishi .
Kuchukua hatua, wajibu wako kubwa ni kuyaishi maisha yako kwa uhalisi na ukamilifu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Jiamini Na Utafikia Ndoto Zako.
Henry Ford aliwahi kunukuliwa akisema, kama unaamini unaweza au unaamini huwezi uko sahihi.” – Henry Ford
Kama unaamini kitu kinawezekana na mtizamo wako ni kuwa tayari kufanya chochote na kwa muda wowote kukipata, basi mafanikio kwako ni swala la muda tu.
Kwa hali hii unakuwa na uhakika wa kufikia mafaniko kwenye jambo lolote unalofanya. Unaweza kujiongezea kujiamini kwa kusoma vitabu vya kujijenga, kusoma blogu za kukufundisha na kukuhamasisha na hata kuhudhuria semina mbalimbali.
Hatua ya kuchukua leo; Amini unaweza na utaweza.
Kila kitu kinawezekana.Kama utaweka vitu vizuri kwenye akili yako, utakuwa imara na utajiamini zaidi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Kwa Nini Unapaswa Kuacha Kuahirisha Ndoto Zako.
Rafiki yangu mpendwa nianze kwa kusema kwamba kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake. Kuna picha ambayo kila mtu anayo ya namna maisha yake anataka yawe.
Lakini kwa kwa bahati mbaya sana, wengi wamekuwa wakiahirisha ndoto zao kila wakati. Wakijua kabisa wanapaswa kufanya nini, lakini wanaahirisha na kujitambua hawajawa tayari au muda bado.
Tunajua jinsi ambavyo hatuna uhakika wa muda wetu hapa duniani. Na tunajua jinsi wengi wanavyokuja kujuta maisha yao yanapofika ukingoni.
Rafiki, usiwe mtu wa aina hiyo, usiwe mtu wa kuahirisha ndoto zako. Badala yake zitekeleze ndoto zako kama unavyoziona kwenye akili yako.
Hata kama wengine hawatakuelewa, wewe fanya kile unachojua ni sahihi, maana kama ni majuto wewe ndiye utakayeyapata.
Muda ulionao ndiye huu, hakuna wakati utakuwa tayari zaidi ya ulivyo sasa.
Chukua hatua; anza kuziishi ndoto zako sasa, kwa pale ulipo na kwa kile ulichonacho. Hiyo ndiyo njia ya kuwa na maisha kamilifu kwako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Mambo 5 Yanayosababisha Changamoto Kubwa Kwenye Zama Hizi.
Rafiki yangu mpendwa jamii ya Kisasa zina maendeleo makubwa sana ukilinganisha na za asili.
Lakini zina changamoto makubwa ukilinganisha na za asili kama upweke ni mkubwa, magonjwa ya akili yapo kwa kiwango kikubwa na pia hali ya watu kujiua, ipo zaidi.
Changamoto hizi zinasababishwa na haya:
Moja; hali ya ubinafsi mkubwa, watu huweza kujitegemea kwa kila kitu, haoni umuhimu wa kushirikiana na wengine, hilo linafanya mtu awe pweke licha ya kuwa na kila kitu.
Pili; wingi wa watu, unafanya watu wasijuane kwa undani. Watu wanaweza kuwa wanakata eneo moja lakini hawajuani, kila mtu anakuwa na maisha yake, linafanya jamii kukosa ushirikiano.
Tatu; kukosekana kwa usawa baina ya watu kwenye jamii. Wachache wana mali sana huku wengine wakiwa hawana. Linafanya ushirikiano baina ya wanajamii ukosekane.
Nne; ubadhilifu, kuwa watu ni wengi na hakuna ile hali ya kujuana moja kwa moja, baadhi ya watu wanaweza fanya ubadhilifu na wasijulikane. Ni vigumu kuwatambua na kuwajibisha.
Tano; kutegemea zaidi mamlaka ambazo haziwezi kutafuta kila kitu kwenye jamii. Kukosekana kwa ushirikiano wa karibu wa wanajamii kunapelekea wategemee mamlaka za kiserikali ambazo sinasimamia sheria na taratibu mbalimbali.
Lakini haziwezi kufika mpaka ngazi za chini kabisa, kama ambavyo watu wangeweza kuwajibishana wenyewe kwa wenyewe pale wanapojuana kiundani.
Sababu hizi zinawasukuma watu kutaka kurudi kwenye jamii za asili, hata kama hawatakuwa na maendeleo na ustaraabu uliopo kwenye jamii za kisasa. Watakuwa na uhuru mkubwa na maisha yao yatakuwa na maana.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Falsaya Ya Kurudi Kwenye Ubinadamu.
Rafiki yangu mpendwa watu huwa wanasema ubinadamu ni kazi, lakini siyo kazi ngumu kama ukiishi kwa falsafa sahihi.
Robin Sharma anatushirikisha falsafa sahihi ya kuishi kwenye kitabu cha the daily manifesto ambayo huturudisha kwenye ubinadamu.
Falsafa hiyo ni kuzingatia yafuatayo;
Yaendee maisha kwa moyo uliojaa ushujaa na macho yanayoangalia nguvu kubwa iliyo ndani yako.
Tambua kuna wakati mambo yatakuwa magumu na mabaya, lakini mwisho wa siku maisha ni mazuri.
Kuna watu watakuchukia na kutamani uanguke, wasamehe na watakie mema. Usiruhusu chuki au hasira kuwa ndani yako.
Fanya kazi yako kwa bidii, juhudi na kutoa thamani kubwa zaidi kwa wale wanaopokea kile unachofanya. Heshimu upekee wako na uonyeshe kupitia kazi unayofanya badala ya kwenda na mazoea.
Yafanye maisha kuwa rahisi kwa kuhangaika na vitu vichache vyenye maana na tija kwako. Usihangaike na mengi yanayofanya maisha kuwa magumu.
Toa zaidi ya unavyopokea, kuwa na msaada na huduma kwa wengine na mchukulie kila unayekutana naye kwa heshima.
Furahia kukutana na watu wenye hekima, kusoma vitabu vinavyokuhamasisha na kuwa na mahusiano mazuri na wewe mwenyewe.
Kundi linapokulazimisha uwe kama wao, kataa na baki kuwa wewe halisi, kuwa mkweli kwako.
Kuwa jasiri, ukijua waoga huwa hawawi na maisha bora kwao. Kuhairisha maisha yako ni kukaribisha majuto.
Kumbuka wakati ambapo hofu inakuwa kubwa ndiyo wakati unaukaribia ushindi mkubwa. Na hofu hugeuka kuwa imani pale unapoikabili.
Furahia matunda ya kazi yako, ishi kwa upendo na jali wengine. Fanya haya yote kuungana na ukuu ulio ndani yako na kuwa shujaa wa kweli ambaye ndiyo asili yako.
Hatua ya kuchukua; rafiki yangu tunapaswa kufanyia kazi falsafa hayo na bila shaka tutaishi maisha yenye furaha.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Njia 8 za kukusaidia kutulia wakati wa mgogoro.
Rafiki yangu mpendwa karibu kwenye makala hii ambayo itajadili njia unazopaswa kuchukua wakati unapitia majaribu na changamoto mbalimbali.
Wengi waliofanikiwa zaidi duniani, wakiwemo wafanyabiashara, wanariadha na wasanii, hawakuweza kufikia kiwango chao cha mafanikio bila kujifunza jinsi ya kukaa watulivu sana chini ya shinikizo. Wana uwezo wa kukuza na kudumisha hali fulani ya utayari wa kisaikolojia, utayari wa kiakili wanaouita kwa mahitaji.
Kwanza; punguza polepole. Ikiwezekana, usichukue hatua mara moja. Badala yake, kuwa na subira na kukusanya taarifa nyingi iwezekanavyo. Mtazamo huu utakusaidia kubaki chini ya hisia na kuboresha uwezo wako wa kufanya maamuzi.
Pili; kaa chanya. Wakati hali zenye mkazo zinatokea, akili yako inaweza kwenda pande elfu moja na baadhi ya mawazo yako yanaweza kuwa hasi. Kadiri akili yako inavyozidi kutangatanga, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwako kubaki mtulivu. Acha mawazo hasi na uelekeze akili yako kwenye kitu chanya, haijalishi ni kidogo kiasi gani.
Tatu; usiulize kamwe ‘ nini kama ?’ Swali hili baya zaidi unaweza kujiuliza au wengine katikati ya mgogoro huanza na ‘ vipi kama’. Mstari huu wa kuhoji husababisha hofu kubwa na kukulazimisha kuishughulikia hali ambazo hazijatokea na ambazo huenda zisiwahi kutokea.
Nne; tunza mwili wako. Ikiwa unatanguliza afya yako ya kibinafsi, utakuwa na vifaa bora zaidi vya kuishughulikia shida. Kula mlo kamili, fanya mazoezi mara kwa mara na upate usingizi wa kutosha. Mazoezi hupunguza kiwango cha homoni za mkazo na kusaidia mwili kufanya kazi kwa kiwango chake cha juu. Kwa kuboresha afya yako, utaongeza uwezo wako wa kujidhibiti, kumbukumbu na akili ya kihisia sifa muhimu ambazo zitakusaidia kukabiliana vyema na dharura.
Tano; punguza kafeini. Unapokuwa katikati ya hali mbaya, unaweza kujaribiwa kukimbilia kwenye chumba cha mapumziko ili kunyakua kikombe cha kahawa. Kafeini inaweza kusababisha kutolewa kwa adrenaline, kukupa mlipuko wa haraka wa nishati na nguvu za kimwili, Kisha kufuatiwa na ajali inayoashiria uchovu na kuwashwa katika baadhi ya matukio. Badala ya kufikia kikombe hicho Cha kahawa, soda au kinywaji Cha kuongeza nguvu, jisafishe kwa maji.
Sita; piga simu kwa rafiki au mshauri unayemwamini. Tumia mfano wako wa usaidizi na usiogope kuomba ushauri katika hali ya mkazo. Mtu ambaye hajawekeza kihisia katika hali hiyo ataweza kuona tatizo hilo kwa mtazamo tofauti na anaweza kukusaidia kufikia suluhu zinazowezekana. Unapofikia watu unaowaamini na kuwaheshimu, utahisi kuwa na msingi zaidi. Usalama huo utakusaidia kudhibiti mfadhaiko na wasiwasi wako.
Saba; tenganisha. Ondoka kutoka kwa hali hiyo kwa muda, hata ikiwa na saa moja au mbili tu. Unapojipa muda wa kushughulikia tatizo na hisia zinazokuzunguka, utaweza kukabiliana na hali hiyo kwa mtazamo mpya.
Nane; tengeneza mkakati wa kukabiliana na hali hiyo. Mgogoro unaweza kuhitaji uweke saa nyingi ofisini au utumie wikendi ukifanya kazi nyumbani. Ukibaki katika hali ya mfadhaiko wa muda mrefu, unaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa afya yako na kudhoofisha uwezo wako wa kufanya maamuzi yanayopatana na akili.
Chukua hatua; rafiki yangu kwa kuzingatia mbinu hizi na zingine zinaweza kukusaidia kujisikia kuwezeshwa zaidi kushughulikia hali nyingi za mgogoro.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Jinsi Ya Kuivunja Tabia Ya Kukurupuka.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini hakuna kitu kinatuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu kama maamuzi ya kukurupuka.
Unakuwa unafanya maamuzi bila ya kufikiri kwa kina na mwishowe yanakuwa na madhara makubwa kwako. Wakati unafanya maamuzi hayo unaona kila kitu kipo sawa, lakini unapokuja kukaa chini na kufikiri kwa kina, unaona namna ulifanya maamuzi bila ya kuwa na taarifa sahihi.
Hii ni tabia ambayo unahitaji kuivunja haraka sana kama unataka kufanikiwa na kudumu kwenye mafanikio. Na jinsi ya kuivunja tabia hii ni kuzingatia yafuatayo;
Kwanza; jiridhishe na taarifa kabla hujafanya maamuzi. Kabla hujafanya maamuzi yoyote makubwa na muhimu, jiridhishe na taarifa unazopata. Je ni taarifa za kweli, je ni taarifa sahihi, je ni taarifa za kutosha. Mara nyingi watu wanaweza kuwa na taarifa ambazo siyo za kweli, au taarifa za kweli lakini hazijajitosheleza, wanatumia kufanya maamuzi na wanaumia. Chunguza taarifa ulizonazo kwa makini, usiamini maneno ya watu, nenda mbali zaidi kujiridhisha na kile unachoambiwa au unachoona.
Pili; muda ni silaha yako muhimu. Muda ni tiba ya kila kitu, hakuna kinachoweza kushinda muda. Siku zote kama siyo jambo la kufa na kupona, basi jipe muda. Kwa mambo mengine, jipe muda kabla hujafikia uamuzi kamili.
Tatu; epuka kuendeshwa na hisia. Maamuzi mengi tunayofanya kwenye maisha yetu, yanaendeshwa na hisia. Na hisia kuu zipo mbili, furaha na hasira. Usifanye maamuzi ukiwa na furaha sana au ukiwa na hasira sana, lazima tu utakosea.
Kwa sababu mara zote hisia zinazuia uwezo wetu wa kufikiri kwa kina. Hivyo unapokuwa kwenye hali ya furaha, au hali ya hasira, jizuie kabisa kufanya maamuzi yoyote, utakuja kuyajutia.
Nne; tumia kauli ya Richard Branson. Ni mjasiriamali bilionea wa nchini Uingereza, ana makampuni zaidi ya 400. Kuna kauli yake moja ambayo huwa inasema fursa za kibiashara ni sawa na mabasi ya abiria, mara zote kuna basi jingine linakuja . Kama ambavyo unajua, daladala moja ikipita, basi ipo nyingine inakuja.
Hii ni muhimu kuitumia kuepuka kukurupuka na kuvamia fursa kwa sababu tu watu wanakuambia inapita au hautaiona tena .
Usisumbuke kuingia kwenye fursa ambayo huijui vizuri, fursa zipo nyingi mno.
Hatua ya kuchukua; tunapaswa kufanyia kazi haya Ili kujijengea nidhamu ya kuwa na subira ya kufanya maamuzi makubwa kwenye maisha yetu. Tuepuke kukurupuka kwenye jambo lolote lile na pia tujifunze kwenye kila chochote tunachofanya.
Kila la kheri.
Wako Maureen Kemei,
Rafiki wako.
-
Kitu Kinachopoteza Zaidi Kwenye Maisha.
Rafiki yangu mpendwa, kinachokupoteza ni kujilinganisha na watu wa nje.
Unataka kuishi kama mtu ambaye tayari ameyapatia maisha, unataka kuishi kama mtu ambaye yuko katika nchi zilizoendelea na wakati wewe uko katika nchi zinazoendelea.Kwa mfano, kwenye kazi unataka kufanya kidogo huku ukiwa na matarajio ya mfano makubwa. Unajilinganisha na mabilionea ambao wakati wanaanza walikuwa hawaishi maisha ya anasa, walikuwa wanafanya kazi usiku na mchana halafu wewe hujafikia viwango hivyo unataka kuishi kama wao.
Rafiki yangu, maisha ya nchi zinazoendelea ukizaliwa tu tayari umeshafungwa tatu bila , unapambana kwanza uweze usawazishe ndiyo uweze kushinda.
Maisha ya nchi zinazoendelea ni kama kupanda mlima, hivyo linapokuja suala la kazi wewe fanya tu kazi hata muda mrefu. Usiwasikilize watu wanaokuambia kwamba fanya kazi kidogo tumia akili.
Kila kazi inahitaji kazi, weka juhudi kubwa, mpaka sasa bado umefungwa tatu bila pambana usawazishe.
Ukizaliwa nchi zilizoendelea tayari umeshinda tatu bila unaona hapo utofauti?
Kitu kikubwa ambacho kinafanya watu wengi wa nchi zinazoendelea kutokupiga hatua ni kuishi kama vile nchi zilizoendelea.
Bado huna anasa ya kuishi maisha hayo, bado hujakuwa huru kiasi hicho.
Kuwa huru ni gharama, tafuta uhuru wako kwa kujitesa sasa hivi, acha usingizi, acha anasaa zote na weka kujuhudi kubwa kwenye kufanya kazi.
Hatua ya kuchukua leo; kwenye maisha kuwa mtumwa wa kitu fulani ambacho unajua ukikomaa nacho kitakupa uhuru.
Kumbuka, ili uwe huru lazima uchague kuwa mtumwa wa kitu fulani. Unachagua nini? Usiishi maisha ya kuigiza pambana usawazishe magoli matatu ambayo tayari umefungwa.
Kama maisha yako bado, uko kwenye umasikini, unapambana kusawazisha hutakiwi kuwa na anasa, unatakiwa kuweka kazi. Na hata ukiifia kazini ni ushujaa, punguza kuridhika wakati maisha bado yanakupiga.Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.