-
Njia Kuu 2 Za Kuishi.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna njia mbili ya kuishi.
Njia ya kwanza ni kuishi kama ambavyo watu wanataka wewe uishi. Kwa kufanya na kuishi kama vile wengine wanataka ni kujichelewesha mwenyewe na pia ni kama kuruhusu wengine waendeshe maisha yako.
Sifanyi kile ambacho kila mtu anafanya hata kama sina msukumo wowote wa kufanya hivyo.
Njia ya pili ni kuishi kama vile ambavyo mimi mwenyewe nataka kuishi. Kufanya kile ambacho ni muhimu kwangu.
Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa hili kuweza kufikia ndoto zangu kubwa, bila kujali wengine wanafanya nini au wanasema nini.
Hatua ya kuchukua; najua maisha ni kuchagua, na kuna njia mbili za kuweza kuishi maisha yangu.
Mimi nachagua kuishi njia yangu ya kuishi kama vile nataka na nitafanya mambo ninayopenda hili kuhakikisha maisha yangu yanakwenda vile nilivyopanga.
Mwandishi na rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
www uamshobinafsi.com.
-
Hatua Ya 1 Kuchukua Ili Kubadili Maisha Yako.
“The moment you accept responsibility for everything in your life is the moment you can change anything in your life.” Hal Elrod.
Rafiki yangu hatua ya kwanza kuchukua ili kubadili maisha yako, ni kukubali kwamba kila kitu kwenye maisha yako ni wajibu wako.
Hapa unaondokana kabisa na kulaumu na kulalamikia wengine pale ambapo maisha yako hayaendi vizuri.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini pale ambapo unaona maisha yako hayako kama unavyotaka yawe, basi jua hilo ni jukumu lako.
Hivyo basi, kama unashindwa, jua wewe ndiye mwenye jukumu la maisha yako.
Kama unataka kufanikiwa, jua ni wewe pekee unayeweza kujifikisha kwenye mafanikio yako.
Hata kama kuna wengine wanakukwamisha kufanikiwa, kubali hilo kama jukumu na tatizo lako, kisha chukua hatua sahihi za kulitatua ili kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.
Kulalamika na kuwalaumu wengine ni kujiondoa kwenye nafasi ya kufanikiwa. Kwa sababu unapolaumu mtu mwingine, maana yake unampa jukumu la maisha yako, na hakuna aliye tayari kubeba jukumu la maisha yako.
Kuchukua hatua; kama unataka kufanikiwa, kama unataka kuwa na maisha unayotaka na kuondoka kwenye maisha magumu, kubali maisha yako na kila kinachotokea kama wajibu wako, na kisha chukua hatua sahihi za kukutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha mbali zaidi.
Mwandishi na rafiki wako,
kemeimaureen7@gmail.com
uamshobinafsi.com.
-
Umuhimu Wa Kuacha Kutumia Maneno Hasi.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini maneno tunayotumia huwa yana maana kubwa na kuathiri sana maisha yetu.
Maneno unayotoa yanatuma ujumbe ni aina gani ya fikra zinazotawala akili yako.
Aina ya fikra zinazotawala akili yako ndiyo zitaamua kama utafanikiwa au kushindwa.
Kuna maneno hasi huwa tunayatumia kama utani kivumishi cha vitu mbalimbali.
Mfano, umefanya kazi nzuri na watu wanasema umepambana kishenzi. Au umefanya vizuri na watu kusema umeua kabisa.
Maneno ya aina hiyo, japo yanaonekana ni sifa, lakini kwa kuwa ni hasi yanaathiri matokeo yako.
Pia kuna maneno hasi tunayojiambia kwa nia nzuri tu, labda ni ndoto kubwa sana unazokuwa nazo na kujiambia haziwezekani.
Kitendo tu cha kujiambia kitu hakiwezekani, unatengeneza utabiri ambao unakuja kuwa wa kweli.
Kwa kuamini kitu hakiwezekani unaacha kuziona fursa nzuri zinazokuzunguka za kuiwezesha kuwezekana.
Kamwe usikubali kutumia maneno au fikra hasi kwenye uwezo wako, ndoto zako au matokeo unayoyataka.
Hatua ya kuchukua; rafiki tunapaswa kufuta kabisa maneno haiwezekani, mbaya, ngumu na mengine ya aina hiyo ambayo tumezoea kuyatumia na mtazamo wetu utabadilika sana.
Tutaona uwezekano kwenye kila kitu, tutaziona fursa nzuri za kufanya tunayotaka na hilo litatupa mafanikio makubwa.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Je, Unajua Wewe U Adui Wako M8wenyewe?
Rafiki yangu mpendwa moja ya changamoto kubwa zinazowazuia watu wengi kufuata kile wanachotaka ili kufikia mafanikio wanayotarajia ni kuwa wapinzani wao wenyewe.
Kuwa adui wangu mwenyewe ni kikwazo namba moja kwangu kwenye kubadili maisha yangu na kufikia mafanikio makubwa.
Kama sitaacha kuwa adui wangu mwenyewe hakuna kitakachobadilika maishani mwangu.
Safari ya kuibadili maisha yangu na kufikia mafanikio sio rahisi kama ninavyofikiria , nitapata upinzani mkubwa kuanzia ndani yangu mwenyewe na hata kwa wale wanaonizunguka .
Kama nataka kufaulu kwenye mambo ninayofanya nahitaji kukataa kabisa kuwa mpinzani wangu mwenyewe na kuanza kujikubali na kujitamkia maneno chanya yatakayonisaida kufikia ndoto zangu kubwa.
Najua mara nyingi nimekuwa mpinzani wangu mwenyewe nimekuwa napanga kubadili maisha yangu ili kufikia mafanikio, Lakini mimi mwenyewe naanza kupinga vile nilivyopanga kufanya .
Chukua hatua; kuanzia leo naondoa kabisa upinzani mkubwa ambao nimekuwa najiwekea mwenyewe.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
-
Sababu Ya Kusema Hapana Kwa Mengine Yote.
Rafiki yangu mpendwa unapochagua kitu ambacho utakifanya, unapaswa kukifanya kweli hadi kikamilike.
Wengi hushindwa kwenye hili kwa sababu huhadaiwa na fursa nyingi mpya zinazowajia. Wanaacha kile walichochagua kufanya na kuanza kuhangaika na vitu vingine.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini kama unataka kufanikiwa usiwe kama hao wengi. Tumia kigezo cha NDIYO KUBWA kuchagua kile muhimu kwako kufanya.
Na ukishasema NDIYO kwenye kitu kimoja, sema HAPANA kwenye vingine vyote mpaka utakapokamilisha hicho kimoja muhimu kabisa.
Chukua hatua; rafiki ni bora tunaposema NDIYO kwa kitu kimoja, tuseme HAPANA kwenye vingine vyote.
Uwe na wakati mwema.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafsi.com.
-
Changamoto 2 Kubwa Kwenye Mabadiliko Ya Tabia.
Rafiki yangu mpendwa tunapojaribu kubadili tabia, iwe ni kujenga tabia mpya au ni kuvunja tabia mbaya. Huwa tunakwama kwa sababu ya changamoto kubwa mbili.
Moja tunajaribu kubadili kitu kisicho sahihi, yaani tunachobadili siyo kinachoweza kutuletea matokeo tunayoyataka.
Mbili ni tunajaribu kubadili tabia kwa njia isiyo sahihi.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye kubadili kisicho sahihi, huwa kuna ngazi tatu za kubadili tabia.
Ngazi ya kwanza ni kubadili matokeo, hapa mtu unahangaika kubadili matokeo. Malengo mengi huwa unawekwa kwenye ngazi hii ya kwanza.
Ngazi ya pili ni kubadili mchakato, hapa unabadili njia unayotumia kufikia matokeo. Hapa ndipo mtu unapojenga tabia.
Ngazi ya tatu ni kubadili utambulisho wako,kubadilika wewe kulingana na kile unachotaka kubadili. Hapa unabadili imani na msimamo yako juu ya kitu fulani.
Unapotaka kuleta mabadiliko ya kweli na ya kudumu kwenye maisha yako, basi unapaswa kuanza kubadilika wewe mwenyewe, kisha kubadili mchakato na hapo ndipo matokeo yatabadilika.
Watu wengi wanakwama kwenye mabadiliko kwa sababu wanakazana na matokeo, huku mchakato na utambulisho wako ukipaki vile vile.
Chukua hatua; rafiki yangu ngangana kubadilika wewe mwenyewe kisha kubadili mchakato na hapo ndipo matokeo yatabadilika.
Uwe na siku njema kutoka kwa rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafi.com.
-
Uwekezaji Bora Na Rahisi Kufanya .
Rafiki yangu mpendwa uwekezaji bora kabisa na muhimu kwenye maisha yako, tena ambao hautakugharimu ni kwenye vitabu.
Kwa gharama ndogo sana utanunua uzoefu wa watu walioishi miaka mingi na kufanya makubwa.
Hivyo kila unapopata, fanya uwekezaji huu, nunua vitabu vingi kuliko hata unavyoweza kuvisoma.
Na katika usomaji wa vitabu, jua havifanani, kuna vitabu ambavyo hutamaliza hata kuvisoma. Kuna vitabu utasoma mara moja tu. Halafu kula vitabu utarudia kuvisomaara nyingi.
Kwa vitabu bora na unavyochagua kurudia kuvisoma, mara nyingi nunua nakala nyingi za kitabu husika. Hilo litakusaidia kuwa na kitabu hicho wakati wote lakini pia utaweza kuwapa wengine kitabu hicho kama zawadi. Robin anatuambia huwa ana nakala mpaka 40 za kitabu kimoja.
Unaporudia kusoma kitabu bora, unajifunza vitu vipya ambavyo hukujifunza wakati unasoma mwanzo. Kwa sababu umekuwa mtu mpya na hivyo uelewa wako unabadilika pia.
Chukua hatua; rafiki yangu wekeza sana kwenye vitabu na chagua vitabu vichache ambavyo utakuwa unarudia kusoma mara kwa mara.
Rafiki wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobianfsi.com
-
Maadili 13 Ya Benjamin Franklin.
Rafiki yangu mpendwa tunajifunza leo kuhusu msingi wa maisha ambao Benjamin Franklin alijijengea kwenye maadili 13 aliyochagua kuyaishi na kujipima nayo.
Maadili hayo ni kama yafuatayo;
Moja. Ujasiri kuwa makini kwenye unywaji na vyakula.
Pili. Ukimya kuepuka mazungumzo yasiyo na maana na kuepuka kutumia maneno machafu
Tatu. Mpangilio kila kitu kifanyike kwa mpangilio mzuri.
Nne. Maamuzi fanya ukichoahidi bila ya kuahirisha.
Tano. Ubahili kuwa makini na matumizi yako na ebuka upotevu.
Sita. Kazi tumia muda wako vizuri na epuka kufanya mambo yasiyo na umuhimu.
Sapa. Ukweli usidanganye yeyote na kuwa mkweli kwako mara zote.
Nane. Haki watendee watu kwa usawa na mara zote fanya kilicho sahihi.
Tisa. Kiasi ebuka kuzidisha chochote kile, kiwe kuzuri au kibaya.
Kumi. Usafi uweke mwili wako, makazi yako na mazingira yako kwenye hali ya usafi.
Kumi na moja. Utulivu kuwa na amani ya ndani na usisumbuke na vitu vidogo vidogo.
Kumi na mbili. Uadilifu usijihusishe na zinaa.
Kumi na tatu. Unyenyekevu waige wale waliofanya makubwa hapa duniani.
Ili kuhakikisha anayaishi maadili haya 13, Franklin alichagua kuyageuza kuwa tabia kwake. Maana tabia ina nguvu kuliko kipaji au maamuzi.
Alitengeneza chati ya kujipima kila siku na kabla ya kulala alijitathmini jinsi alivyoishi maadili hayo kwenye siku husika.
Hapa rafiki tunajifunza mambo kmakubwa mawili;
- Kuwa na maadili ambayo mtu unasimamia na kujipima nayo kwenye maisha yako.
- Kuyageuza maadili hayo kuwa tabia kwa kujifanyia tathmini kila siku na kurekebisha pale unapokosea.
Chukua hatua; rafiki yangu tunapaswa kufanyia kazi maadili hayo ambayo tumejifunza siku ya leo kutoka kwa muuzaji bora kuwahi kutokea Benjamin Franklin.
Rafikj na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
uamshobinafsi.com
-
Uhitaji Wa Kuwa Tayari Kujaribu.
Rafiki yangu mpendwa mara kwa mara umekuwa ukipata mawazo mazuri na bora sana ambayo yana nguvu ya kuleta mafanikio makubwa.
Labda ni namna ya kufanya kazi yako kwa ubora zaidi. Au namna unaweza kuifanya biashara yako kwa viwango vya juu.
Lakini kadiri unavyoendelea kuyafikiria mawazo hayo mazuri, wasiwasi unaibuka ndani yako, unaona huwezi kuyatekeleza , kwa sababu ni makubwa na magumu.
Unaona ukijaribu utashindwa, na hapo unaamua kuachana na mawazo hayo mazuri.
Rafiki yangu hapo unakuwa umechagua kushindwa kabla hata hujaanza. Badala ya kwenda hivyo, chagua kuwa mtu wa kujaribu.
Kwa wazo lolote kubwa na bora unalokuwa nalo, hakikisha kuna hatua unachukua ili kuanza kulitekeleza. Hata kama ni hatua ndogo kiasi gani, ina uwezo wa kufungua fursa kubwa mbele yako.
Kwa kujaribu hakuna matokeo ya kushindwa. Maana kama utafanikiwa utakuwa umepata matokeo mazuri. Na kama hutakuwa umefanikiwa utakuwa umejifunza kitu ambacho hukuwa unakijua awali.
Kuchukua hatua; rafiki usikubali kupoteza mawazo mazuri yanayokujia, badala yake yafanyie kazi na hutabaki pale ulipo.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafsi.com
-
Hofu 1 Inayoongoza Kwa Kuua Ndoto Za Watu
Rafiki yangu mpendwa kama kuna kitu ambacho kinawazuia watu wengi kufanikiwa ni hofu.
Hofu imekuwa kikwazo kwa watu wengi kuchukua hatua na kuweza kufanikiwa kwenye maisha yao.
Watu wanakuwa na ndoto kubwa, wanaweka mipango mizuri, lakini inapofika kwenye utekelezaji ndipo hofu huchukua nafasi hiyo na basi watu hawaanzi.
Zipo hofu nyingi, lakini hofu moja kubwa inayoongoza kwa kuua ndoto za watu ni hofu ya kushindwa.
Hii imekuwa inawazuia watu wengi kuchukua hatua na kuweza kufanya makubwa. Hii ni kwa sababu kwa lolote kubwa ambalo mtu anapanga kufanya, ipo hatari ya kushindwa.
Ukweli ni kwamba, mambo huwa hayawi mabaya kama tunavyofikiria yatakuwa. Huwa yanakuwa kwenye hali ya tofauti na tulivyotegemea, lakini maisha bado itaendelea.
Dawa ya hofu ya kushindwa ni kuanza kidogo kidogo kabisa, kwa hatua ndogo kabisa ambayo ukishindwa hutajali au maisha yako hayatakuwa hatarini kama ulivyofikiria.
Mfano, weka lengo dogo kabisa unaloweza kulifanyia kazi kwa siku moja, alafu jifanyie tathmini, umeweza kufanya kwa kiasi gani. Wapi umefanya vizuri na wapi una changamoto.
Kisha, panga kuchukua hatua nyingine ndoto na endelea kupiga hatua hivyo kila siku, baada ya muda utakuwa upo mbali sana.Ukilinganisha na kama usingeanza kabisa.
Kwa kuanza kufanya ukianzia hatua ndogo ndogo unaiua hofu kabisa kwa sababu kwanza unajizoesha kufanya kile ambacho hujazoea kufanya na unafanya kwa ngazi ya chini kabisa.
Na pili unajijengea kujiamini kwa kuwa unafanya, tofauti na pale unaponga pekee. Unapofanya kitu na kukamilika, hata kama ni kidogo, unajijengea kujiamini na baadae utaweza kufanya kwa uzoefu ambayo utakuwa umejijengea kwa kufanya.
Rafiki, chochote unachopanga tu bila kuanza kufanyia kazi, nakushauri leo uanzie hapo kwa kufanya kwa udogo bila kuacha na utaweza kushinda hofu.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com
uamshobinafsi.com