Home

  • Tiba Ya Kuongeza kipato Kutoka Kitabu Cha The Richest Man in Babylon Na George Clason.

    Rafiki yangu mpendwa kwenye hii tiba ya kuongeza kipato nimejifunza vitu vifuatavyo.

    1. Ni lazima kutafuta namna yeyote ya kuongeza kipato ili kufikia uhuru wa kifedha.

    2. Kutamani tu kuwa tajiri hakutakufikisha popote. Ila kutamani kupata vipande vitano vya dhahabu ni kitu kinachoeleweka na kinaweza fanyiwa kazi hadi kikatimizwa.

    3. Lengo lako la kufikia utajiri iwe rahisi na kueleweka. itakuwa haina maana kama malengo yako ni mengi,hayaeleweki na yapo juu ya uwezo wako kuyatimiza.

    4. Kadiri tunavyoongeza maarifa ndivyo tutakavyoongeza kipato chetu. Mtu atakaye jitahidi kuijua kazi yake vizuri atapata mafanikio zaidi.

    5. Maisha ya mwanadamu hubadilika na kuwa bora kwa sababu ya watu wenye udadisi na wenye kutafuta ujuzi kwa faida ya wote.

    6. Mtu anayejiheshimu anatakiwa kufanya mambo kama haya yafuatayo;

    a). Anatakiwa kulipa madeni yake haraka iwezekanayo, hutakiwi kununua kitu usichoweza kumudu.

    b).Anatakiwa kujali familia yake, hilo litafanya imheshimu na imuongelee vyema .

    c).Anatakiwa kuacha wosia kwa maandishi ili siku akifa mali yake igawanywe kwa utaratibu.

    d).Aanatakiwa kuwa na huruma kwa wagonjwa, wasiojiweza na wale waliopatwa na majanga. Awasaidie kulingana na uwezo wake.

    e,).Anatakiwa kuwa mkarimu kwa wapendwa wake. kujifunza na kujizoeza kupata maarifa zaidi, kupata ujuzi zaidi na kujiendesha kwa heshima.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Sheria 5 Za Dhahabu.

    Rafiki yangu mpendwa leo tunajifunza sheria tano za dhahabu kutoka kitabu cha ‘ the richest man in Babylon.’

    Kati ya fedha na busara ama hekima, hekima ndio kitu cha kwanza kuchukua kabla hujachukua, nami nimechukua yafuatayo;

    1. Mbwa mwitu wanavyolia kwa kunung’unikia njaa, ukisema uwapatie chakula nini kitatokea??, watapigana zaidi na kuzurura basi, hivyo ndiyo binadamu walivyo ukisema uwape Dhahabu bila maarifa hutafanya kitu!!..

    2.Pesa ipo kwa wale wanaojua sheria zake na kuzifuata.

    3. Kiongozi mkubwa wa maisha katika uchumi ni sheria na hekima katika pesa ndio msingi na muhimu zaidi,,..

    4. Summary ya sheria hizo ndizo zifuatazo;

    a).Dhahabu huja kwa wingi kwa wale ambao huweka akiba moja ya kumi ya pato lake na kuwekeza kwa ajili ya wakati ujao.

    b).Dhahabu hufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu iwapo itampata mtu anayeipata kazi yenye faida.

    c).Dhahabu kung’ang’ania kukaa kwa mtu anayeilinda na mwenye tahadhari, anayeomba ushauri kutoka kwa wenye ujuzi na uzoefu wa kutunza.

    d). Dhahabu haikai na hupotea kwa mtu ambaye amewekeza kwenye biashara, au miradi ambao, haujui vizuri, au miradi ambayo haishauriwi na wale wenye uzoefu na ujuzi wa kuitunza .

    e). Dhahabu haikai kwa yule anayewekeza kwenye miradi inayodai kutoa fedha kubwa kuliko kawaida , wala kwa wanaodanganywa na matapeli au watu wajanja-wanjanja na wale wanaowekeza bila kupata ushauri kutoka kwa wale wenye uzoefu au na wale wanaoonekana kupenda miradi ya hivyo.

    5. Mwanzo wa kuweka akiba na kutunza pato moja ya kumi kuna mengi hutapata hivyo utaishi kibahili sana.

    6. Siku zote fuatana na watu wenye maarifa kuhusu pesa na kabla ya kuwekeza pesa yako, jadili kwa kina uwekezaji.

    7. Utajiri unaodumu na kufurahisha anayeumiliki huja polepole, huo ni mtoto anayezaliwa kutokana na maarifa na uvumilivu.

    8. Kwa mtu mwenye kufikiri kwa kina, kupata utajiri si kazi ngumu wala mzigo mzito, siri ni kubeba mzigo huo mwaka hadi mwaka hadi mwaka na mwisho wa lengo lake utatimia.

    Kuchukua hatua, rafiki kazi kwetu kuweka kwenye matendo sheria hizi na bila shaka tutatoboa kwenye upande wa fedha.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Atomic Habits By James Clear.

    Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze pamoja kutoka kitabu cha atomic habits.

    1. Wewe Unajengwa au kubomolewa na tabia zako ( your habits). Matokeo yako ni kutokana na tabia zako.

    2. Pesa ulionayo ( either tajiri, masikini au wakati) ni matokeo ya tabia Yako ya kifedha.

    3. Mwili ulionao ( uzito , magonjwa, etc) ni matokeo ya tabia ya ulaji wako.

    4. Uwezo wako wa kuchanganua na kuelewa mambo ni matokeo ya tabia yako ya kujifunza.

    5. Kujifunza idea Moja haitakufanya uwe *Genius*, lakini uwezo na matamanio ya kujifunza kitu kipya kila siku ndio itakufanya uwe bora.

    6. Kila kitabu kipya unachosoma hakikifundishi tu mambo mapya bali ufunguo pia ya njia mbali mbali za namna ya kufikiri upya kwa msomaji.

    7. So tengeneza tabia chanya upate mambo chanya kwenye kila field, eg kimahusiano , pesa, elimu, biashara nk

    Chukua hatua, tumejifunza mambo sapa yatakayotusaidia kujenga tabia ya mafanikio, kazi kwetu kuweka kwenye matendo.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Jinsi Ya Kutengeneza Mchakato.

    Rafiki yangu mpendwa kila unayemwona ameweza kufanya makubwa kwenye maisha yake, haikutokea kama bahati au ajali. Bali ni matokeo ya mchakato ambao mtu huyo ameufuata kwa muda mrefu.

    Japo mchakato wowote hauna matokeo ya uhakika, kwa kufuata mchakato wengi wameweza kuzalisha matokeo bora.

    Mchakato unahusisha mitazamo na misingi ambayo mtu anatumia kufanya maamuzi. Hapa ni baadhi ya mitazamo na misingi inayosimamiwa na wengi walioweza kufanya makubwa.

    1. Ujuzi siyo sawa na kipaji.
    2. Mchakato mzuri unaweza kuzalisha matokeo mazuri, japo siyo uhakika.
    3. Kutaka ukamilifu siyo mpaka uwe mkamilifu.
    4. Kutaka uhakika ni kujidangnya.
    5. Kiburi ni kunyume na uaminifu.
    6. Mitazamo ni ujuzi.
    7. Mkwamo wa kiuandishi ni kitu ambacho hakipo.
    8. Wabobezi wanazalisha kwa nia, siyo hisia.
    9. Ubunifu ni kitendo cha uongozi.
    10. Viongozi ni waigizaji.
    11. Ukosoaji wote haufanani Tunakuwa wabunifu pale tunapozalisha kazi ya kibunifu.
    12. Kuweza kuchagua vizuri ni ujuzi.
    13. Hamada ni uchaguzi.

    Chukua hatua, tunapaswa kukaa kwenye mchakato kwa muda mrefu na bila shaka tunapata matokeo.

    Mimi wako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 10 Ambayo Brian Tracy Anatufunza Kuhusu Watu Waliofanikiwa.

    Rafiki mpendwa kwenye kitabu ambacho mwandishi Brian Tracy ameandika, anaeleza kuwa ni matokeo ya miaka 15 ya utafiti, kufundisha na mazoezi binafsi juu ya namna matajiri walivyotengeneza utajiri wao.

    Hayo ni mambo 10 ambayo nimetoka nayo:

    1. Safari ya mafanikio inahitaji kujifunza kwa waliofanikiwa au wanaofanya mambo unayotaka kujifunza.
    2. Kuna tabia, mtindo wa maisha na nidhamu zipo kwa watu waliofanikiwa tunazohitaji kujifunza kutoka kwao.
    3. Utafiti ni sehemu muhimu/nyenzo katika kujenga utajiri.
    4. Mafanikio yanahitaji kujenga tabia ya kujifunza hata kwa kusoma vitabu ( tawasifu na wasifu wa watu walofanikiwa)
    5. Ukiwa kijana unajawa na maono makubwa na shauku kubwa ya kuona mambo unayowaza yatokee haraka pengine bila kuangalia gharama ya kujitoa na muda.
    6. Maisha yetu yanaweza kubadilika kwa kujifunza kujiuliza maswali sahihi.
    7. Kabla ya mtu kuwa na shauku ya kupata hela ni vyema kujijengea uwezo ambao utafanya pesa ije yenyewe bila kutumia nguvu. Lazima mtu awe ili pesa ije.
    8. Si jambo baya kujifunza na kukubali kuwatumia waliofanikiwa ni walimu wetu katika safari ya kufanikiwa
    9. Maswali kuhusu utajiri yanaweza kuanzia katika kujiuliza waliofanikiwa wamewezaje ? Na ambao bado kufanikiwa hawafanyi nini kinachowakwamisha kufanikiwa kwao.
    10. Utajiri unatengenezwa kwa kuweka mikakati halisi.

    Chukua hatua tunapaswa kufanyia kazi mambo hayo ili kupata mafanikio tunayoyataka kwenye maisha yetu.

    Rafiki Yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com

  • Njia 2 Ya Kuyakabili Magumu.

    Rafiki yangu mpendwa, wastoa wanatushirikisha njia kuu mbili tunazoweza kuzitumia kuyakabili magumu ili yasivuruge maisha yetu.

    Njia ya kwanza ni kutambua wema pekee ndiyo kitu bora. Hapa ustoa unatukumbusha kurudi kwenye asili yetu binadamu ambayo ni viumbe wa kufikiri. Hivyo tunapaswa kuziweka fikra zetu vizuri na tusitawaliwe na hisia zozote mbaya.

    Kwani kinachofanya mambo kiharibike tunapopitia magumu ni tunaporuhusu kutawaliwa na hisia.

    Njia ya pili ni kutambua baadhi ya mambo yapo nje ya uwezo wetu. Kwamba tunaweza kufanya kila kinachopaswa kufanya lakini bado tutakutana na magumu kwa sababu kuna yaliyo nje ya uwezo wetu yanayokuwa yameingilia.

    Ni muhimu kujua mambo yapi yapo ndani ya uwezo wetu na kuyafanyia kazi, huku yale yaliyo nje ya uwezo wetu kuyapokea kama yalivyo.

    Kwa kutumia njia hizi mbili kwa pamoja, hakuna gumu lolote linaloweza kututikisa, kwani tunafikiri kwa usahihi na kujua yaliyo nje ya uwezo wetu hatuna namna ya kuyaathiri.

    Hata pale magumu yanapotokea hatupati taharuki au kuumia sana kwa sababu siyo kitu kinachokuja kwetu kwa mshangao.

    Rafiki Yako.

    Maureen Kemei.

  • Jinsi Unavyoweza Kuwa Kioo Ambacho Hakijakamilika.

    Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kama kuna kitu umekipenda na kujikubali sana kutoka kwa watu wengine, kiige, kuna kazi ya sanaa umekipenda kutoka kwa wengine iige.

    Kuna biashara nzuri umeona wengine wanafanya na ukakubali sana, iige.

    Huwa tunafikiria ili ufanikiwe lazima uje na kitu kipya na cha kipekee sana. Huo siyo ukweli, kwanza itakuwa vigumu sana kuwashawishi watu wakubaliane na wewe pale unapokuwa na kitu kipya ambacho hawakijui kabisa.

    Hivyo iga kile kilichopo, lakini kifanye kwa ubora ambao utafanya watu wasukumwe kuja kwako.

    Usiishie tu kuiga kwa namna kitu kilivyo. Bali iga na boresha zaidi kwa namna ambayo watu wanapata thamani kubwa zaidi.

    Chukua hatua hivyo basi, kama hujui ukifanye nini, angalia kile unachokikubali zaidi kwa wengine na ukiige huku ukiboresha zaidi, utaweza kufanya makubwa.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

  • Mambo 5 Ya Kusema Hapana Kwenye Maisha Yako.

    Rafiki tangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, ni kwenye muda pekee ndipo penye demokrasia ya kweli duniani.

    Ndiyo kitu pekee ambacho wote tumepewa kwa usawa.Sasa kwa kuwa tumepewa kwa usawa, ila wapo ambao wanafanya makubwa sana kwenye muda huo huo, ina maana kuna vitu wanafanya kwa utofauti.

    Na hapo ndipo muda unapokuwa muhimu sana.Na ndiyo maana muda ni kitu kingine ninachokiamini mno.

    Naamini ukitumia muda wako vizuri, utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.Kwa yote ambayo watu wengi wameweza kufanya, ni kwa sababu wamekuwa wanakazana kutumia muda wao vizuri.

    Na siri kuu ya kutumia muda vizuri ni kusema HAPANA kwenye mambo yote ambayo hayana mchango kwenye maisha yako na mafanikio unayotaka.

    Kwa mfano, haya ni mambo ambayo watu wanaofazidi kufanikiwa wanasema hapana kwenye maisha yao na kutokuyafanya kumeokoa muda wao mwingi.

    1. Kufuatilia habari kwa tv, redio, magazeti na vyombo vingine vya habari.

    2. Matumizi ya mitandao ya kijamii, hawatumii muda wao kuzurura kwenye mtandao wowote wa kijamii.

    3. Ushabiki wa mchezo wa aina yoyote ile, huwa hawafuatilii.

    4. Ulevi na starehe mbalimbali, wengi hawatumii kilevi chochote.

    5. Vikao na shughuli nyingi za kijamii, shughuli ambao siyo muhimu kwako hawahudhurii.

    Kwa kusema hapana kwenye hayo, wanabaki na muda mwingi ambao wanaweza kuutumia kwenye mambo yenye tija zaidi.

    Rai yangu kwako rafiki yangu ni hii, linda sana muda wako. Tumia neno HAPANA kwa yote yasiyokuwa na mchango kwenye mafanikio unayoyataka.

    Tahadhari;Jamii ina mbinu nyingi sana za kunasa muda wako.Inakulazimisha ufanye yale ambayo kila mtu anafanya ndiyo uonekane wa kawaida.

    Chagua kama unataka kuwa wa kawaida na usifanikiwe.Au kuwa wa ajabu na ufanikiwe.

    Huwezi kufanikiwa bila kuonekana wa ajabu kwenye jamii.Kwamba hufuatilii habari, haupo kwenye mitandao na hushabikii chochote!Wengi watakuona una tatizo, ila wao ndiyo wenye tatizo kubwa zaidi.

    Rafiki yangu, kutoka ndani ya moyo wangu kabisa hayo ni mambo ninayoyaamini bila ya shaka yoyote ile.

    Mwandishi wako,

    Maureen Kemei.

  • Umuhimu Wa Kuzungukwa Na Watu Sahihi.

    Rafiki yangu mpendwa kufanya makubwa siyo kitu rahisi kuna changamoto na vikwazo, kuna kushindwa na kukata tamaa.

    Utaweza kuyavuka hayo kama utakuwa umezungukwa na watu sahihi. Tafuta watu ambao wanafanya makubwa, k7isha zungukwa nao, kuwa na kikundi cha watu wanaofanya makubwa ambao mnapeana moyo wa kuendelea na mapambano.

    Usisubiri mpaka watu waje wakuite na kukuweke kwenye kikundi cha aina hiyo tafuta kikundi ambacho tayari kipo na kama hakuna, anzisha kikundi cha aina hiyo.

    Wale wanaokuzunguka wana mchango mkubwa kwenye yale unayoyafanya. Kama unataka kufanya makubwa, lazima uzungukwe na wanaofanya makubwa pia.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.

  • Kile Kinachodhihirisha Thamani Yetu.

    Rafiki yangu mpendwa kabla hujafanya maamuzi, unaweza kusema utakavyo, lakini watu wataamini zaidi kile unachofanya kuliko unachoongea.

    Maneno ni rahisi kila mtu anaweza kusema atakavyo, lakini matendo ni magumu na hayo na ndiyo yanadhihirisha kweli mtu anasimama wapi.

    Kama kweli kitu ni muhimu kwako utakifanya, hutaishia tu kusema. Kama unakitaka kitu kweli utakifanya kila namna mpaka ukipate, hautakubali kuzuiwa na chochote. Hivyo angalia yake unayofanya hayo ndiyo yanaonyesha nini unajali zaidi.

    Na hata kwa wengine, usisikilize wanasema nini, wewe angalia wanafanya nini. Kama maneno na matendo ya mtu vinatofautiana, amini zaidi matendo kuliko maneno.

    Hivyo kwa wale ambao kila mwaka wanasema wanataka kuanza biashara ila hawana mataji, au wazo, au muda au kingine chochote, jibu unalo hapa hawataki kuanza biashara. Wangekuwa wanataka kweli wangeshaanza.

    Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili thamini yetu idhihirike kwa watu ni kwa kuweka matendo zaidi kuliko maneno.

    Rafiki wako,

    Maureen Kemei.

    kemeimaureen7@gmail.com.