-
Madhara Ya Kufuata Mkumbo.
Rafiki yangu mpendwa kuna hali huwa zinajitokeza kwenye kundi ambapo watu wanakuwa wanafikiria kitu kimoja, hakuna anayehoji wala kukosoa pale mambo yanapoonekana hayaendi vizuri. Wanasaikolojia wanaita hali hii groupthink na imekuwa chanzo cha matatizo makubwa kwenye taasisi nyingi.
Kufikiri kwa kufuata mkumbo huwa kunachochewa zaidi na mtazamo mgando. Pale taasisi inapokuwa na kiongozi ambaye anachukuliwa kuwa na uwezo mkubwa na kuwa mwenye mtazamo mgando, kila mtu anaweka imani yake kwa kiongozi huyo na kuona kila analofanya kuwa sahihi.
Kuna mfano wa jinsi hali ya kufikiri kwa kufuata mkumbo ilivyowahi kuwa na madhara kwenye uvamizi wa siri uliopangwa na Marekani kupindua Castro wa Cuba yaani pay of pigs invasion.
Hilo lilikuwa tukio la kushindwa kwa aibu kwa taifa hilo kubwa dhidi ya taifa dogo na uchunguzi unaonesha kilichopelekea uvamizi huo kushindwa ni watu kuacha kufikiria kwa usahihi na kufuata mkumbo.
Chanzo kikuu cha kushindwa kwa uvamizi huo ilikuwa ni kiongozi wa wakati huo, Rais Kennedy ambaye alikuwa amejijengea sifa ya kufanya mambo mengi kwa usahihi. Watu walimwamini sana na kuona ana maono makubwa na yaliyo sahihi, ambayo hayapaswi kuhojiwa wala kukosolewa.
Hivyo alipopendekeza uvamizi wa Cuba, japo mpango haukuwa sahihi, washauri wake wote walikubaliana na yeye. Yeye alifikiri wanakubaliana naye kwa sababu ya mpango, kumbe wanakubaliana naye kwa sababu ya imani waliyonayo kwake.
Kilichotokea ni uvamizi kushindwa vibaya kwa sababu ya watu kufuata mkumbo kwenye kufikiri
Chukua hatua; rafiki tunapaswa wakati wote tusikilize kundi wanasema nini, lakini kwenye kufanya maamuzi ni sahihi kufikiri kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale.
Rafiki yako,,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Kutoa Zaidi Kupata Zaidi.
Rafiki yangu mpendwa kuna tafiti zinaonyesha kadiri watu wanavyotoa, ndivyo wanavyopata zaidi.
Utafiti uliofanywa kwa wale wanaotoa misaada ya fedha kwa wengine unaonesha kwa kila dola moja ambayo mtu anatoa kama msaada, anapata dola 3.75 zaidi kwenye kipato chake.
Kinachowapelekea wale wanaotoa kupata zaidi ni furaha wanayoipata kwenye utoaji ambayo inawapa msukumo wa kufanya kazi kwa juhudi zaidi na hivyo kupelekea kuongeza kipato zaidi.
Utafiti mwingine umewahi kufanywa ambapo watu walipewa dola 20 na kupewa nafasi kuchagua jinsi ya kuitumia. Wale waliotumia kuwasaidia wengine walikuwa na furaha kuliko wale walioitumia kwa mambo yao binafsi. Hivyo kuwasaidia wengine kunawapa furaha zaidi.
Kuna utajiri wa tafiti unaoonyesha kwamba watu wenye furaha huwa wanafanya kazi kwa juhudi zaidi, wanafanya kazi kwa muda mrefu na kutoa matokeo makubwa na mazuri.
Furaha pia inawafanya watu kufikiri kwa usahihi na haraka na kufanya maamuzi ambayo ni bora kwenye kile wanachofanya.
Kwa wastani, watu wenye furaha wana kipato zaidi, wana ufanisi mkubwa kazini, wanafanya maamuzi bora na kwa ujumla wana mafanikio zaidi.
Chukua hatua; toa kwa kupenda mwenyewe bila kulazimishwa.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Nafsi Yako Inapoongea Na Wewe.
Rafiki yangu mpendwa roho yako kuna vitu inajua lakini akili yako kuna vitu haiwezi kuvielewa.
Kuna wakati unasukumwa sana kufanya kitu fulani, ambacho huwezi kuelewa kwa nini, ila unapokifanya kinakuwa bora kwako.
Hayo ndiyo tunapoita machale,nafsi yako inapoongea na wewe. Unapaswa uisikilize nafsi yako, pale inapokusukuma sana ufanye kitu fulani, isikilize na ufanye.
Unaweza ukakosea, lakini mara nyingi matokeo yake huwa ni makubwa
Tofautisha machale instincts na emotions hisia. Hupaswi kutawaliwa na kuendeshwa na hisia, ila unapaswa kujua wakati nafsi yako inanena na wewe na kuisikiliza.
Tatizo ni kwamba hakuna yeyote anayekushauri lolote kuhusu machale, hilo ni la ndani yako na hata utakapoyasikiliza wengi hawatakuelewa.
Matokeo utakayopata ndiyo watu wataona labda una bahati au ulipata maono fulani. Ukweli ni nafsi yako ilijua kilicho sahihi kwako, na mara zote ndivyo ilivyo.
Chukua hatua; rafiki isikilize nafsi yako mara zote kabla hujafanya maamuzi yoyote kwenye maisha yako, na utaweza kufanya maamuzi yanayoleta matokeo bora zaidi.
Rafiki yako ,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Uwepo Wa Akili
Rafiki yangu mpendwa unaweza ukafanya kazi bora kabisa kama utaweka umakini wote kwenye kile unachofanya.
Na utaweza kuweka umakini kama utaacha kusumbuka na mengi na kuondokana na usumbufu.
Hilo ni gumu zama hizi kwa sababu watu wanatumia ubize kama sifa, anayeonekana kuhangaika na mengi ndiye anayeonekana mchapakazi.
Chukua hatua; rafiki chagua kuweka uwepo wa kiakili kwenye kile unachofanya ili ukifanye vizuri.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Jinsi Ya Kujua Shauku Yako.
Rafiki yangu mpendwa watu wengi wamekuwa wakiuliza wanawezaje kujua shauku yao, wanawezaje kujua kile wanachopenda kufanya, kinachotoka ndani yao.
Jibu la swali hili liko wazi kabisa, ukisikiliza sauti ya ndani yako na ukachukua hatua, utaijua shauku uako.
Shauku siyo kitu unachozaliwa nacho na wala haipo kwenye kitu kimoja.
Shauku ni matokeo ya mchakato ambao mtu ameufanyia kazi. Wachanga ndiyo husubiri mpaka wapate kile wanachopenda na wakifanye.
Wabobezi huwa wanachagua watakachofanya na kisha kukipenda.
Usijicheleweshe mpaka upate unachopenda wewe isikilize sauti ya ndani yako na kuwa na mchakato wa kufanya na hapo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupenda kile unachofanya.
Chukua hatua; Sikiliza sauti iliyo ndani yako na utaweza kujua shauku yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Jinsi Utulivu Unavyoibua Upekee Wako.
Rafiki yangu mpendwa unapokuwa na chanzo kimoja cha sauti inakupa uwezo mzuri wa kufikiri kwa kina.
Kuna wachache tu waliofanikiwa kutengeneza utulivu wao dhidi ya kelele za dunia zilizopo kila kona. Hii imewasaidia kuamsha uwezo wao halisi na kuleta mafanikio.
Jambo la kwanza; Ni kujitenga na kundi. Si rahisi kuamini upekee katika kundi. Kwa sababu kundi huamini kuwa watu wote ni sawa. Hii imekuwa sababu ya wengi kutoamsha uwezo wao halisi.
Pikli; Utulivu hukusanya nguvu, hii ni kwa sababu unasikia sauti moja tu, hivyo akili na nguvu zako zinajikita kwenye kufikiri na kutendea kazi sauti iyo moja.
Tatu; Moyo wako ndio wenye sauti yako; moyo una siri kubwa juu yake, na huu ndio kifaa cha sauti ya upekee wa maisha yako. Washa na sikiliza moyo wako ukiwa kwenye utulivu ( kujitenga na kundi).
Nne; Tenga muda wa kuwa wewe. Sina uhakika kama itakufaa, lakini kuwa wewe ni kujitenga kabisa na dunia, yaani kujitenga na shughuli na taarifa zote za dunia na kubaki wewe.
Hapo unajisikiliza mwenyewe, unajihoji mwenyewe, na kujijibu mwenyewe na kujitafakari mwenyewe ulivyo.
Tano; Kufanya tahajudi . Kwa kutafuta eneo tulivu, weka akili izingatie kwenye kile unachohitaji, kihisi kile unachokizungumzia, thibiti pumzi yako, fanya hivi kila siku. Muda mwingine unahitaji wazo moja tu ili kubadilisha maisha yako.
Hatua za kuchukua ; Unaweza tenga muda kila siku wa kutafakari kuhusu maisha yako na kuhusu wewe mwenyewe.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 28 Ambayo Nimejifunza Kwenye Safari Yangu Ya Maisha.
Rafiki yangu mpendwa, sina uhakika kama itakufaa, lakini naona bora nikushirikishe yale nimekuwa nikijifunza kwenye safari yangu ya maisha.
Ninaposherekea siku ya kuzaliwa kwangu, ikiwa leo nina miaka 28, yapo mambo mengi ambayo nimejifunza, ninapoendela kupigania ndoto ya maisha yangu ya kuwa mshauri, mwandishi na pia muuzaji bora kuwahi kutokea. Napenda kushukuru Mungu kwa uhai na uzima ambao amenijalia hadi leo.
Nashukuru pia watu wangu wa karibu ambao wamekuwa wakinishika mkono kama wazazi wangu wote mama na baba, ndugu zangu na pia mtoto wangu wa kipekee sana na marafiki wangu wote mbarikiwe sana.
Nawashukuru pia familia ya wanamafanikio hasa Kocha Makirita Amani, Songa mbele consultant na wapambanaji wote wa familia ya kisima cha maarifa KCM.
Nimejifunza mambo mengi ila baadhi ya hayo ni kama yafuatayo 28;
- Napaswa niwe na kusudi la maisha yangu.
- Kama sio sahihi nisifange, kama sio kweli nisiseme.
- Niwe tayari kwa mabadiliko, kwani kila kitu hubadilika.
- Sifai kushindwa kwenye kujifunza na kwenye kufanya kazi.
- Nidhamu ni kitu muhimu sana kwenye maisha.
- Niwe tayari kulipa gharama.
- Hakuna kitu cha bure chini ya jua.
- Nijihusishe na watu wa kuaminika kwenye maisha.
- Niwe mchangamfu hata kama nina matatizo.
- Nisiwe na chuki.
- Nisiwe na wivu.
- Nisitumie zaidi ya kipato changu na niwe naweka akiba cha asilimia kumi ya kila kipato.
- Nifanye yale ninayepaswa kufanya.
- Maisha hayafiki tamati pale ninaposhidwa, pali pale ninapokata tamaa.
- Elimu haina mwisho.
- Lazima nikae kwenye mchakato sahihi.
- Sifai kuwa kiranja wa dunia.
- Lazima niseme hapana kwenye mambo mengi.
- Niwe na utulivu kwenye maisha yangu ya kila siku.
- Nisipoendea chenye ninataka, hakitanikujia.
- Maisha yangu yanajengwa na kile ninachokila na kile ninachokilisha akili yangu.
- Niwe ninasoma angalau kitabu kimoja kila wiki.
- Hakuna kitu rahisi nisipoweka kazi.
- Nifanye tahajudi na sala kila mara.
- Niwe na malengo na mipango ninayofanyia kazi kila siku.
- Kuwa sahihi ni kukosea.
- Bora mtu anayetembea kuliko anayeongea.
- Niwe msikilizaji mzuri wakati wote.
Rafiki yako anayekupenda,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Jinsi Ya Kujijengea Tabia Za Furaha.
Rafiki yangu mpendwa hebu tuanzie kwa kuchunguza tabia za furaha. Kama inavyosemekana kwamba tabia tulizonazo zinaathiri sana furaha zetu.
Rafiki hapa kuna orodha ya tabia ambazo ukijijengea, utaweza kuwa na furaha kwenye maisha yako.
1. Kufanya tahajudi ( meditation).
2. Kuacha kuwalaumu wengine.
3. Kupata mwanga wa jua na tabasamu
4. Kuondokana na tamaa yoyote ile.
5. Kuachana na ulevi au vichangamsha akili kama kahawa.
6. Kufanya mazoezi ya mwili kila siku.
7. Kuwaambia wengine una furaha, kitu kitakachokulazimisha uwe na furaha kweli.
8. Kupunguza matumizi ya simu janja ( smartphone).
9. Kuepuka kuwa na siri nyingi.
10. Kusimama pale unapoteleza, mfano unapojikuta umevurugwa fanya tahajudi kurudi kwenye utulivu wako.
11. Usitegemee chochote cha nje kupata furaha.
12. Kuwa na kipimo binafsi unachojipima nacho mwenyewe na siyo kujilinganisha na wengine.
13. Kuwa na mtazamo chanya na matumaini kwenye kila jambo.
14. Epuka mchezo ya hadhi ambayo ili upande lazima uwashushe wengine.
15. Zalisha kemikali za furaha kwenye ubongo bila ya kutumia madawa ya kulevya, fanya mazoezi, kuwa na mtazamo chanya na kukaa kwenye asili.
Chukua hatua tunapaswa kujijengea na kuishi tabia hizo kila siku na tutaweza kuwa na furaha kwenye maisha yetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Mambo 10 Ya Kufanya Yatakayo Badili Maisha Yako.
Rafiki yangu mpendwa yapo mambo kumi tunayopaswa kufanya yatakayo badili maisha. Yafuatayo ni mambo hayo kumi;
- Kupenda ninachofanya.
Nahitaji niwe na hamasa kubwa kwenye kile ninachofanya na kuipenda kuliko kitu chochote. Kubadili ninachofanya. Mfano kama nataka kuanzisha biashara, nikae chini na kupanga kuweka akiba, mtaji wa biashara na ya matumizi binafsi iwapo nitaacha kazi. - Kubali kwamba mabadiliko yapo na yataendelea kuwepo. Ni muhimu kukubali na kukiri kwamba matokeo yanakuja, hutakuwa na mtu wa kumlaumu pale ambapo mabadiliko yatakukuta hujajiandaa.
- Kujifunza sana kuhusiana na unachofanya.Nijifunze sana kuhusiana na kile ambacho nakifanya.Kufanyia kazi utalaamu wako,kujua mabadiliko kwenye taaaluma yako. Kufanyia kazi eneo la kazi.
Kama unafanya biashara una majukumu mengi zaidi.
a).Unatakiwa kujijua wewe mwenyewe, kujua uwezo wako, ni vitu gani kwenye biashara yako ambavyo uko vizuri. Pia kujua ni maeneo gani haupo vizuri sana una madhaifu gani.
Kinahitaji jitihada za ziada za kutafakari na kuchukua hatua.
b). Ukishajua wewe mwenyewe unatakiwa kujua biashara yako vizuri, kuijua nje na ndani.
c).Uhitaji wa kuwajua wateja wako vizuri, kujua sifa zote za mteja wako. Kujua umri wake, kipato wake, hadhi yake ya maisha, eneo analoishi na hata mahitaji yake kulingana na biashara ninayofanya.
Litakuwezesha kujua njia za kuongeza wateja zaidi na hata pale ambapo wateja wako wanabadilika.
d). Kujua nani ni mpinzani wako, anaweza kuwa mpinzani wa moja kwa moja au asiye moja kwa moja.
- Kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana, usiweke mazoea. Kwa kufanya kitu cha ziada, kwa kuongeza ubora na thamani.Kuhakikisha hufanyi mambo kimazoea, kuhakikisha leo hufanyi kama vile ulifanya Jana.
- Nusa mabadiliko, kuwa mdadisi.Kuwa mdadisi, usikubali majibu ya haraka, kutokubaliana na kila kitu, kuhoji kila kitu, kujihoji mwenyewe, kutumia udadisi huu kwenye mambo chanya.
- Kuchukua hatua mapema.Hili kunufaika na mabadiliko ni vizuri kujua na pia kuchukua hatua ambayo itakuwezesha kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunufaika na mabadiliko hayo.
- Kujua kwamba hakuna atayekuja kukutoa hapo ulipo.
- Kushirikiana na wengine.
- Kuwa tayari kusimama mwenyewe.
- Kubali na kusonga mbele.
Kuchukua hatua hayo ni mambo muhimu tukizingatia na kuweka kwenye matendo tutaweza kupata kile tunachokitaka na pia kufikia malengo yetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
- Kupenda ninachofanya.
-
Njia 5 Zinazoweza Kuwahamasisha Wengine Kuchukua Hatua.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye maisha Kuna mambo ambayo tukizingatia yanaweza kutuhamasisha kuchukua hatua.
Kwanza; Hadhi, ubongo wetu unajali sana hadhi yetu kwa kujilinganisha na wengine. Unapopewa hadhi ya juu, unajisukuma kufanya vizuri zaidi.
Pili; Uhakika, ukiwa na uhakika wa jambo fulani, ubongo unakuwa tayari kuchukua hatua fulani.
Tatu; Udhibiti, unapokuwa na udhibiti wa maisha yako, unasukumwa kuchukua hatua zaidi.
Nne; Uhusiano, unapowaona wengine wanafanya kitu fulani, unahamasika kufanya.
Tano; Haki, inapoonekana ni haki kufanya kitu fulani, mtu anasukumwa kufanya zaidi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com