-
Ushindi Mkuu Wa Maisha.
Rafiki yangu mpendwa, bila shaka natumia u buheri wa afya, nikukaribishe siku ya leo twendelee mbele kwenye kujifunza kama kawaida yetu. Karibu sana .
Leo tunajifunza mambo ya kufanya ili tuweze kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yetu ya kila siku
1.Ukweli ni kwamba kila kitu tunachohangaika nacho kwenye maisha kuna hatari yakukipoteza
2.Ushindi ulio mkuu ni kuwa wewe kwenye dunia inayokazana kukubadilisha uwe kama wengine ni mafanikio makubwa.
3. Ni kupitia mtu kujitambua ndio anaweza kuwa yeye na kufanya makubwa kwenye maisha yake.
4. Jitambue uimara na udhaifu wako na kuutumia vizuri.
5. Kila mtu hawezi kuwa kama wewe, kwani wewe ni WA kipekee sana.
6. Zamanı tulikuwa tunashindana binadamu kwa binadamu ila kwa sasa tunashindana na maroboti (Artificial Intelligence) ushindani ambao ni wa hatari na utawapoteza wale ambao hawajajitambua na kuishi maisha yao.
7. Wape watoto uhuru na waunge mkono kwa kile wanachojaribu, wajifunze na kuona kama wanataka kwenda nacho au la.
8. Ushindi mkuu kwenye maisha na utakaoweza kudumu nao kwenye kipindi chote cha maisha yako ni kuchagua kuwa wewe na kubaki kuwa wewe kwa maisha yako
Chukua hatua, ni wakati Sasa wa kuamua kuwa wewe na kuhakiksha unafanya yale unayopaswa kufanya na ka kufanya hivyo utaweza kuwa mshindi kwenye maisha yako ya kila siku.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com
-
Vipengele 10 Vya Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Katika Babeli Kutoka Kitabu Cha (the richest man in Babylon).
Rafiki yangu mpendwa pata picha kwenye kila eneo la maisha yako, kila jambo unalofanya una bahati ya kufanikisha. Sio tu bahati unakujia hivyo tu, bali kuna vipengele muhimu unayopaswa kuzingatia.
Hapa kuna vipengele kumi ambayo tunapaswa kuzingatia kwenye maisha.- Ukiwa na pesa kwenye maisha hata kama umri umeenda bado utaonekana kuwa kijana.
- Kwenye maisha tusijilinganishe na wengine bali tupambane kutafuta mali ili tufurahie maisha yetu ya baadaye.
- Tujifunze kwa wengine waliofanikiwa ili na sisi tufanikiwe.
- Tujifunze kutunza siri hata iwe nzito kiasi gani.
- Tusijiingize kwenye vitu ambavyo vinatuletea matatizo kwenye maisha yetu kama vile kamari na pombe.
- Tusitegee kufanya kazi. Mtu hawezi fika popote kwa kutegea kazi.
- Tupende kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Hakuna rafiki mzuri kama kazi. Jitahidi uipende kazi usijali hata kama ni ngumu kiasi gani.
- Mtu anayetaka kujenga nyumba nzuri hatawaza sana juu ya uzito wa nguzo au umbali wa kufuata maji ya kujengea.
- Tuthamini kazi tunayofanya. Kumbuka kuwa kazi ikifanywa vizuri inamnufaisha anayeifanya.
- Fanya kazi ili kujipatia kipato uweze kununua uhuru wako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Hatua 10 Ambazo Mjasiriamali Anapaswa Kupitia Kabla Hajafanikiwa.
Rafiki yangu mpendwa hofu ya kushindwa ndiyo sababu kuu kwa nini watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha.
Mfumo wetu wa elimu na hata ajira umetengenezwa kwenye msingi wa kutokufanya makosa, kwa sababu ukikosea shuleni au kazini basi unaadhibiwa.
Lakini ulimwengu wa biashara upo tofauti kabisa, kama hukosei, huwezi kupiga hatua na kufanikiwa. Ni kupitia kukosea ndiyo uvumbuzi mpya unapatikana. Ni kupitia kukosea ndipo mtu unajifunza na kuwa bora.
Ili kufanikiwa, mjasiriamali mpya anapaswa kupita hatua hizi.
1. Kuanza biashara
2. Kushindwa na kujifunza.
3. Kutafuta menta.
4. Kushindwa na kujifunza.
5. Kujifunza kupitia kozi mbalimbali.
6. Kuendelea kushindwa na kujifunza.
7. Kusimama pale anapofanikiwa
8. Kusherekea ushindi.
9. Kuhesabu fedha zake, faida na hasara.
10.. Kurudia mchakato mzima.
Chukua hatua; rafiki kujifunza hakuna mwisho, makosa hayana mwisho, utaendelea kujifunza kadiri biashara inavyokwenda.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Hatua 5 Muhimu Za Kupiga Ili Kutoka Kwenye Uathirika Victim Kwenda kwenye Ushujaa Hero.
Rafiki yangu mpendwa ili uweze kufanya makubwa, lazima kwanxa utoke kwenye hali ya uathirika kwenda kwenye hali ya ushujaa.
Hili ni zoezi ambalo linapaswa kuanzia ndani yako, zoezi ambalo siyo rahisi, lakini ukilifanya utapiga hatua kubwa.
Hatua ya kwanza; Ondoka kwenye mtazamo wa haiwezekani kwenda kwenye mtazamo wa inawezekana. Waathirika huwa wanaona mambo hayawezekani wanaona kikwazo kwenye kila jambo na hilo kiwazuia kuchukua hatua na kufanya makubwa.
Mashujaa Wana mtazamo wa tofauti, wanaona mambo yote yanawezekana na hakuna kinachowazuia kupata wanachotaka. Hilo huwasukuma kuchukua hatua na kufanya makubwa.
Hatua ya pili; Acha kutoa sababu na anza kutoa matokeo. Unaweza kutoa sababu au kutoa matokeo, huwezi kutoa vyote kwa pamoja. Waathirika hutoa sababu kwa kila jambo kuonesha kwamba haiwezekani.
Mashujaa huwa wanatoa matokeo, hawahangaiki kutafuta sababu na visingizio, bali wanazalisha matokeo. Kwa njia hiyo wanafanya makubwa bila kujali wanapitia nini.
Hatua ya tatu; Acha kuishi jana, tengeneza kesho bora. Waathirika huishi kwenye wakati uliopita na kutumia yale yaliyotokea uko nyuma kama sababu ya wao kuwa pale walipo sasa.
Mashujaa wanapambana kujenga kesho iliyo bora wakitumia waliyopitia uko nyuma kama somo na msukumo wa kufanya makubwa zaidi.
Hatua ya nne; Acha kuwa bize, zalisha matokeo. Waathirika wanapenda kuwa bize, kwa sababu wanaona hilo ni sifa. Siku yao nzima imejaa mambo ya kufanya, lakini mengi katika hayo siyo muhimu.
Hawana vipaumbele vyovyote hivyo, lakini wanaimaliza siku wakiwa wamechoka, lakini hakuna matokeo makubwa wanayozalisha.
Mashujaa wanajua kinachohitajika ni kuzuia matokeo muhimu , hivyo hupangilia muda na kuweka vizuri vipaumbele vyao. Hilo huwawezesha kufanya vizuri machache yaliyo muhimu na yenye tija, kitu kinachowapa matokeo makubwa.
Hatua ya Tano; Acha kuwa mchukuaji na anza kuwa mtoaji. Waathirika huwa na mtazamo wa uhaba . Wanaona rasilimali muhimu ni chache na zipo kwa uhapa, hivyo hukazana kupata zaidi ya wengine. Mtazamo huo hugeuka kuwa kikwazo kwao wasipate mafanikio makubwa.
Mashujaa wana mtazamo wa utele, wanajua rasilimali muhimu zipo kwa uwingi kiasi cha kila mtu kuweza kupata kadiri anavyopata.
Na wanajua ili wapate wanachotaka, wanapaswa kuwapa kwanza wengine kile wanachotaka. Na kadiri wanavyotoa, ndivyo wanavyopata zaidi na zaidi.
Chukua hatua, rafiki kazi kwetu kuweka kwenye matendo haya ambayo tunajifunza siku ya leo, ili tutoke kwenye mtazamo wa uathirika kwenda kwenye mtazamo wa hero.
Rafikk yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Naendelea Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Success Codes Na Joel Arthur Nanukaa.
Rafiki yangu mpendwa karibu pia siku ya leo tujifunze zaidi kutoka kitabu cha Success codes na Joel Arthur Nanukaa. Leo tunajifunza mambo kumi ambayo yanatusaidia kwenye safari yetu ya mafanikio, karibu sana.
1.Tunatakiwa kufanya kazi ili kuvutia fursa kubwa kwenye maisha haijalishi zipo kwa muda huo au hazipo tunatakiwa kujiandaa muda wote ili zikitokea zitukute tupo tayari.
2. Ili kupata zaidi ya ulichonacho unatakiwa kutumia kile kidogo ulichonacho ili kupata kikubwa zaidi ambacho kitachukua muda kufika.
3. Nimetambua kwamba mafanikio yako yamejificha kwenye mabadiriko tunayoyaogopa.
4. Nimejifunza kuanza kuona faida kwenye kila badiliko badala ya kutangulia kuona hasara au kuona hofu ya kupoteza mamlaka tuliyonayo.
5. Nimejifunza kujenga uwezo wa kuyakabiri mabadiriko. Badala kuogopa tunapaswa kupambana ili kupata matokeo bila kujali.
6. Daima siku zote tunatakiwa kuziambukiza akili zetu tabia ya ushindi ili kupambana na mabadiriko yanayoweza kujitokeza.
7. Katika Safari ya mafanikio tunapaswa kuziambukiza akili zetu kuwa safari hii ya mafanikio ni yangu hivyo sihitaji kujua watu wangapi wako nami au wangapi hawako pamoja na mimi kikubwa nikusonga mbele kwani ni safari yako sio safari yao.
8. Nimejifunza kwamba maamuzi magumu na makubwa kwenye maisha yetu huongozwa na maono ya ndani ya mioyo yetu ambayo mtu mwingine anaweza asikuelewe kabisa unachokiona na kinachokusukuma.
9. Nimejifunza kupitia nyakati ngumu hata kwani mashaka katika mafanikio niyakawaida kwani hata waliofanikiwa wakuwa na mashaka hivyo natakiwa kusonga mbele daima.
10. Nimejifunza kuamini kwamba maisha ni ya kwangu na ninaiishi mara moja hivyo natakiwa kuchukua hatua mapema .
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com
-
Suluhisho La Ugumu Wa Kifedha Kutoka Kitabu Cha Success Codes Na Joel Arthur Nanukaa.
Rafiki yangu mpendwa watu wengi tumejikuta katika changamoto kubwa ya pesa hasa kipato kisicho tosheleza matumizi na hapa ndipo pagumu kutoka mwandishi anakuja na suluhisho:
- Kila matumizi yanapoongezeka jitahidi kuwa na mpango wa kuongeza kipato chako
- Kama huna mbinu ya kuongeza kipato acha kuongeza matumizi.
- Hakuna utajiri unaopatikana kama zawadi hivyo tunapaswa kuweka mikakati na mipango itasaidia kuondoka kwenye changamoto ya kupoteza pesa ili kupata pesa nyingi
- Kujenga nidhamu ya kutumia pesa bila papara.
- Nimbaya sana kukopa pesa ambayo hujui kabisa unakwenda kuifanyia nini
- Huwezi kubadili maisha yako hadi ubadilishe mambo unayoyafanya kila siku maana siri ya mafanikio ipo kwenye mambo unayoyafanya kila siku.
- Tengeneza malengo au majukumu ya kutekeleza kila siku kwa maana hii itasaidia kuwabize kwa mambo ya msingi .
- Weka vipaumbele katika shughuli zako ili uwe mtu ambae unajua nini unafanya na wapi unaelekea.
- Kumbuka kuanza kufanya jambo la muhuimu zaidi na mengine yafuate kwa kuzingatia umuhimu wake.
- Jambo la muhuimu zaidi katika kujikwamua na changamoto ya kifedha na kuwa mtu bora nikupunguza mtumizi nakuwa na mapango sahihi wa matumizi ya pesa .
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com
-
Mambo 10 Ambayo Nimejifunza Katika Kitabu Cha The Success Codes Na Joel Arthur.
Rafikj yangu mpendwa karibu sana siku ya leo ambapo bado tunaendelea kujifunza katika kitabu hiki cha Joel Arthur Nanukaa, ambacho anatufunza siri za mafanikio.
- Namna nzuri ya kuondoka kwenye changamoto ya kifedha.
- Kubadiri mtazamo na Imani katika kuelekea kwenye mafanikio ya kifedha.
- Kujenga Iman ya kufanikiwa bila kujali changamoto ulizonazo.
- Namna nzuri ya kujikwamua baada ya kutambua sababu iliyosababisha kuingia kwenye changamoto ya kifedha.
- Nimetambua nguvu yakujisamehe katika kuponya maumivu yandani ili ufanikiwe tena.
- Ili uweze kuvuka maumivu yanakurudisha nyuma hunabudi kuzika historia yako iliyopita na kukili tatizo na kutafuta msaada mahari sahihi.
- Kujenga mtazamo wa kufanikiwa hata kama upo katika wakati ambao huoni mlango wa kutokea kabisa .
- Nimetambua nguvu ya Imani katika kuvuka changamoto yoyote na wakati wowote .
- Kujipa muda katika kutatua changamoto zinazokukabiri bila papara.
- Kujenga Imani ya ushindi bila kujali changamoto yoyote.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 10 Nimejifunza Katika Kitabu Cha Success Codes Cha Joel Arthur Nanukaa.
Rafiki yangu mpendwa karibu sana tujifunze kutoka vitabuni, leo nimebahatika kusoma kitabu hiking kizuri, karibu nikushirikishe.
1.Ili kufanikiwa unatakiwa kufanya vitu bila kuogopa changamoto ambazo zitatokea pamoja na kuishinda hofu katika maisha.
2. Kuna maumivu ya aina mbili moja ni maumivu ya kuikabili hofu leo ni ndogo ukilinganisha na maumivu utakayoyapata utakapo gundua hauna nguvu, muda na uwezo wa kufanya ambacho ulikuwa unakitamani kila siku .
3. Lazima kuchukua hatua leo na ufanye unachotakiwa kufanya ili baadae usijute.
4. Tunatakiwa kujifanyia tathimini kila siku katika maisha pamoja na kuacha kuishi kwa mazoea.
5. Nimejifunza kutokata tamaa pamoja na kujipa moyo pale unapoona umekata tamaa unatakiwa kutambua kwamba umefanya kazi kwa asilimia 40% tu hivyo unatakiwa kujilazimisha kufanya tena kwani kuna asilimia 60% bado hujazifanyia kazi hivyo unatakiwa kujipa moyo na kuendelea kufanya kazi zaidi .
6. Badala ya kulalamika na kulaumu pamoja na kunungunika unatakiwa kuvunja mipaka uliyojiwekea na amini kuwa unaweza kufanya na kupata unachotaka .
7. Kuna vita nyingi huwa zinaibuka katika kila unapokaribia kufanikiwa hivyo unatakiwa kutumia hekima kuchagua vita ya kupigana nayo na nyingine ambazo hutakiwa kupigana nazo .
8. Kuepuka watu walioshindwa katika maisha kwani walioshindwa wanatamani na wewe ushindwe kama wao walivyoshindwa hivyo unatakiwa kuwa makini sana na watu hao.
9. Lazima kufuatilia ndoto yako hata bila kuogopa hofu ya kutokubalika au kutokubaliana na wewe.
10. Katika jambo lolote unalotaka kufanya lazima kupambana kwa moyo wote bila kuchoka wala kukata tamaaa kikubwa kujiamini na kuamini njia yako kuwa ni sahihi pambana mpaka mwisho utapata matokeo mazuri tu.
Chukua hatua; rafiki yangu tuchukue hatua ya kupambana ndoto yetu baada ya kusoma na kuelewa mambo haya kumi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Ni Wakati Wa Kuwa Wewe.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini ndani yako kabisa unajua nini ambacho unataka kwenye maisha yako.
Kuna sauti inayokuambia nini unapaswa kufanya na hata ukiipuuza sauti hiyo, bado haiondoki. Kuna mambo ukiyaona huwezi kuyavumilia, ungependa yawe bora zaidi.
Huu ndiyo wakati wa wewe kuwa wewe na kuacha kupoteza muda wako na maisha yako kwa mambo yasiyo kuwa na tija kwako
Fanya zaidi ya ulivyozoea maana ndiyo njia ya kuweza kufanya makubwa zaidi. Kumbuka hamasa na msukumo uliokuwa nao tangu utotoni na uamshe tena ndani yako sasa. Hayo hayakuondoka, ila tu uliyazima, unaweza kuyawasha tena sasa.
Pima ushindi wako kwa hatua unazopiga na siyo kwa vitu unavyokuwa navyo au unavyowazidi wengine.
Chukua hatua; ongoza hata kama huna cheo, shawishi hata kama huna nafasi na fanya kazi kwa viwango vya juu sana na utaweza kufanya makubwa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Kitu Ambacho Watu Wanakihofia Kuliko Hata Kifo.
Rafiki yangu mpendwa watu wengi husema kitu kikubwa ambacho kila mtu anahofia ni kifo, hilo siyo kweli. Kitu kikubwa ambacho kila mtu anahofia ni kuishi maisha yake kwa uhalisi wake.
Watu wengi hawana uthubutu wa kuchagua kuyaishi maisha yao kwa namna wanavyochagua wao, hivyo wanalazimika kujificha kwenye utumwa wa jamii.
Tumefundishwa kuyaishi maisha yetu ili kuwaridhisha wengine, wakubaliane na sisi na kutuona ni watu wazuri, hata kama inabidi tuigize maisha ili kukamilisha hilo. Tumezoea kuishi kama wengine wanavyotaka tuishi ili wakubaliane na sisi.
Kuchagua kuwa wewe na kuyaishi maisha yako kwa namna unavyochagua mwenyewe ni kitu ambacho watu wanakihofia zaidi kuliko hata kifo. Wengi wapo tayari wafe kuliko kuchagua kuyaishi maisha yao.
Maisha ambayo wengi wanaishi siyo maisha halisi kwao, bali ni maisha ambayo wengine wanawategemea wawe hivyo. Dini ambazo wengi wanazo, kazi wanazofanya na maisha wanayoishi, siyo kwa sababu wamechagua wenyewe, bali kwa sababu ndivyo jamii inawategemea wawe. Kwa njia hiyo wengi wanaishi maisha yasiyo yao, maisha ya utumwa.
Kwa kuwa maisha ambayo watu wanaishi siyo yao, wanaacha kujiheshimu na kujiamini . Wanajiona ni watu ambao hawajakamilika na hivyo kuzidi kutafuta njia za kuwafurahisha wengine, hapo wanazidi kuwa watumwa zaidi kwenye jamii.
Watu wamekuwa wanajidharau wao wenyewe ili kuwafurahisha wengine.. Wamekuwa wanajiumiza miili yao ili tu kuwafurahisha na kukubalika na wengine. Angalia vijana wanaoingia kwenye ulevi na madawa ya kulevya, siyo kwa sababu vina manufaa kwao, ila kwa sababu wanataka wakubaliane na wengine.
Hata watu wazima kuna mambo wanafanya ambayo hayana manufaa kwao na tena yanawaumiza, lakini wanataka wakubalike na wengine.
Watu wanajiumiza na kutokujikubali kwa sababu hawana uthubutu wa kuyaishi maisha yao. Wanajiadhibu na kuruhusu wengine wawaadhibu ili tu wakubalike ndani ya jamii. Hili limewafanya wengi kuendelea kubaki kwenye utumwa.
Chukua hatua ; rafiki tunapaswa kuishi maisha halisi, kwa sababu kuishi maisha ya kufurahisha wengine ni kujitesa na kupotezauda wako hapa duniani.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com