Home

  • Mambo 8 Ya Kuzingatia Unapotengeneza Bajeti.

    Rafiki mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kujifunza kuhusu namna ya kuweka bajeti ni jambo la kutilia maanani kwenye maisha.

    Rafiki kwanza bajeti ni mpangilio wa kipato na matumizi kwa kipindi fulani. Kuna mitazamo potofu kuhusu bajeti kama kufikiri kuwa bajeti inabana, ni kwa matajiri, kuwa mtu unajitaji kuwa na elimu ya juu sana, kuwa na bajeti ni kuonyesha majivuno na bajeti inatengenezwa na taasisi kubwa.

    Rafiki hayo ni mitazamo potofu kabisa kuhusu bajeti. Basi tuangalie mambo ya kuzingatia tunapoweka bajeti ya kila siku kwenye maisha.

    Mambo hayo ni kama;

    1. Kukokotoa jumla ya kipato unachoingiza.
    2. Kokotoa jumla ya matumizi unayoyafanya, bajeti zinatakiwa kubadilika kulingana na matumizi ya mwezi husika.
    3. Chagua kanuni ya kugawa kipato chako.
    4. Gawa kipato kwenye mafungu kabla ya kutumia.
    5. Balance matumizi yako yasizidi kipato
    6. Kuwa na mpango wa kuongeza kipato.
    7. Bajeti ibadilike kulingana na malengo husika.
    8. Endelea kufuatilia bajeti ambayo umeiweka.

    Chukua hatua; Rafiki tunapozingatia mambo hayo wakati wa kuweka bajeti tutaweza kufikia malengo ya kifedha na kuweka matumizi mabaya ya fedha, na kwa kufanya hivyo, tutaweza kufikia uhuru wa kifedha.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Kauli 10 Chanya Ya Mafanikio Ya Kujiambia Kila Siku.

    Rafiki yangu mpendwa karibu leo tujitamkie kauli kumi chanya ya mafanikio ambazo zinaelekeza fikra kwenye malengo, zinapunguza mawazo hasi,zinaongeza motisha ya kuchukua hatua, zinaimarisha imani binafsi, na pia zinajenga nidhamu ya muda mrefu.

    Hizi ni kauli 10 chanya tunazoweza kujitamkia kila siku.

    1. Nina uwezo wa kujenga biashara yenye mafanikio na thamani kwa watu wengi.
    2. Kila siku nachukua hatua zinazonikaribisha kwenye uhuru wa kifedha.
    3. Nidhamu, uvumilivu na kujifunza kila mara vinanipeleka kwenye mafanikio makubwa.
    4. Ninaona fursa ambazo wengine hawazioni na nazitumia kwa hekima.
    5. Pesa ni matokeo ya thamani ninayotoa kwa wengine, na ninaongeza thamani kila siku.
    6. Biashara yangu inakua kwa utaratibu na mifumo inayoifanya ijiendeshe kwa ufanisi.
    7. Nina uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yanayojenga utajiri wa muda mrefu.
    8. Changamoto ni nafasi ya kujifunza, kuboresha na kukua zaidi.
    9. Ninavutia watu, washirika na wateja wanaochangia ukuaji wa biashara yangu.
    10. Ninaelekea kwenye uhuru wa kifedha, amani ya akili na maisha yenye kusudi kila siku.

    Hatua ya kuchukua, kaulia chanya ni kama ramani ya akili, lakini safari yenyewe inahitaji hatua za kuchukua.

    Tunahitaji kuchukua hatua kama tunataka kufikia uhuru wa kifedha kama kuongeza kipato, kuwekeza,kupunguza matumizi, kujenga biashara yenye mfumo, na kuwa na nidhamu ya muda mrefu.

    Rafiki yako,

    Maureen .

  • Njia Ya kuweza Kuitawala Siku Yako.

    Rafiki kwa mujibu wa falsafa ya utoa (stoism), kutawala siku yako kunamaanisha kutawala, mawazo matendo na mitazamo yako bali si kujaribu kutawala kila kitu kinachotokea.

    Baadhi ya mafundisho muhimu kutoka kwa wanafalsafa wa Ustoa ni kama yafuatayo;

    Anza siku yako kwa kusudi. Unapoamka asubuhi jiulize, ‘ leo nitakuwa mtu wa aina gani?’

    Fanya jambo moja kwa wakati mmoja. Epuka kurukaruka kutoka kazi moja kwenda nyingine.

    Kubali usichoweza kudhibiti. Kwa mfano unapokuwa foleni, au hali ya hewa inapobadilika kama ilikuwa jua na ikaanza kunyesha haifai kukukasirisha kwa sababu huna udhibiti nacho. Pia maoni ya wengine yasikuharibie siku.

    Tenda kazi zako kwa nidhamu. Rafiki tunapaswa kufanya yaliyo sahihi atakama hatujiskii kufanya .Ukipanga ratiba yako ya siku unapaswa kufuatilia hadi ukamilishe.

    Jitathmini jioni. Rafiki baada ya kufanya mambo zako zote au kufuatilia ratiba yako ya siku unapaswa kujifanyia tathmini ili uchunguze umefanya nini vizuri na nini kinahitajika uboreshe kesho.

    Hatua ya kuchukua; Marcus Aurelius alisema kuwa ‘ubora wa maisha yako hutegemea ubora wa mawazo yako .”

    Kwa mtazamo wa wastoa, siku nzuri si ile ambayo kila kitu kimeenda kama ulivyotaka, bali ni ile ambayo umeishi kwa hekima, nidhamu, ujasiri, na kujidhibiti licha ya changamoto.

    Rafiki kwa kuboresha mawazo yetu kila siku tutaweza kuishi na kuitawala siku yetu bila kuzuiliwa na mambo ya nje ambayo hatuyawezi kuyazuia.

    Rafiki yako,

    Maureen.

  • Njia 5 Ya Kujenga Uwezo Wa Kutokukata Tamaa.

    Rafiki, najua pia wewe una hamu ya kujua njia za kufanya ili usikate tamaa kwenye safari hii ya mafanikio.

    Basi usiwe na wasiwasi wowote kwa sababu niko hapa kwa ajili yako rafiki yangu, karibu tujifunze njia hizo ili kamwe tusikate tamaa kwenye maisha.

    Habari njema ni kuwa watu wengi ambao wamefanikiwa kwenye maisha yao wamekuwa wakitumia njia hizi ili wasikate tamaa kwenye safari ya mafanikio.

    Njia hizo ni kama yafuatayo:

    1. Kubali mapema kwamba safari itakuwa ngumu. Hakuna mafanikio bila changamoto.
    2. Weka mfumo, siyo hisia. Weka ratiba, weka malengo ya kila siku, weka viwango vya kazi . Fanya kazi hata kama hujiskii kufanya. Kocha Dr Makirita Amani huwa anasema usikubali mtu yeyote akushinde kwenye kujifunza au kusoma na kufanya kazi.
    3. Jifunze kutafsiri kushindwa kama somo. Rafiki badala ya kusema ‘nimeshindwa’ tunapaswa kusema “nimejifunza nini”.
    4. Punguza kutegemea matokeo ya haraka. Rafiki mafanikio ya kweli huchukua muda.
    5. Jikumbushe sababu yako [your why]. Kila unapochoka, jikumbushe kwa nini ulianza. Unapaswa kujitamkia kuwa “nataka maisha makubwa, na sitakata tamaa mpaka nipate.

    Hatua ya kuchukua; rafiki pata picha unapoyazingatia mambo hayo vizuri kwa sababu zinafanya kazi vizuri sana. Utafikia ndoto zako kubwa na utaweza kufanya makubwa na kuacha alama kwenye maisha yako.

    Rafiki yako,

    Maureen.

  • Jinsi Ya Kupata Maisha Mazuri Unayotaka Kwenye Maisha (falsafa ya Ustoa).

    Rafiki, karibu leo tunajifunza jinsi ya kuishi maisha ya furaha licha ya kukabiliana na magumu kwenye maisha yetu ya kila siku.

    Kwa mujibu wa wanafalsafa njia ya kupata maisha mazuri si kwa kulazimisha matokeo, bali kwa kujenga tabia na kufanya yaliyo ndani ya uwezo wako.

    Mambo ya kuzingatia ili kuishi maisha mazuri ni kama yafuatayo:

    1. Tenganisha unachoweza kudhibiti na usichoweza kudhibiti. Unaweza kudhibiti juhudi zako, maamuzi yako na mtazamo wako. Huwezi kudhibiti maoni ya watu, bahati, au matokeo yote.
    2. Fanya wajibu wako kila siku. Mafanikio makubwa hujengwa kwa hatua ndogo zinazorudiwa kila siku.
    3. Kubali changamoto kama sehemu ya ukuaji. Kikwazo kinaweza kuwa fursa ya kujifunza na kuwa imara zaidi.
    4. Tawala tamaa na hisia zako. Usifanye maamuzi muhimu ukiwa na hasira, woga, , au msisimko mkubwa.
    5. Thamini kile ulicho nacho sasa. Shukrani huleta utulivu na hukusaidia kuona fursa zilizopo.

    Hatua ya kuchukua; Lenga kuwa mtu bora kila siku; matokeo mazuri yatafuata.

    Rafiki yako,

    Maureen.

  • Jinsi Ya Kuondoka Kwenye Utegemezi Mkubwa Wa Familia.

    Rafiki karibu kwenye siku ya leo tunajifunza jinsi ya kuepuka utegemezi mkubwa kutoka familia na watu wa karibu.

    Familia haihitaji mafanikio ya mmoja kama nyenzo ya kufanya bidii maishani bali ni utegemezi mkubwa ambao huchosha kiakili na watu hutoa huku wakiwa na maumivu ndani yao.

    Baadhi ya mambo ya kufanya ili kuondokana na utegemezi huu ni kama yafuatayo;

    1. Jitoe kwenye janga la umaskini . Maisha ya watu huendelea hata nafasi ya wewe kusaidia watu ikipotea.
    2. Weka bajeti ya kusaidia watu. Mfano; fungu la mwezi la kusaidia watu labda ni 100,000. Budget ikiisha na shughuli imekwisha pia. Mpango wako ni muhimu kuliko chochote kile.
    3. Sio muda wote tatizo hutatuliwa kwa pesa. Mfano; mpe kazi mpe ushauri, mpe connection.
    4. Fundisha watu kujitegemea. Weka masharti ya pesa yako kwa maana pesa si rahisi.
    5. Jifunze kusema ‘hapana’ hakuna kusema ngoja tuangalie, unampa mtu matumain8 na usumbufu unakuwa mwingi.
    6. Tengeneza mfuko wa familia.
    7. Epuka maonyesho ya maisha yanakufanya uonekane una fedha nyingi.
    8. Badilisha falsafa ya familia.

    Hatua ya kuchukua; Rafiki tunapaswa kujenga familia sio za kutegemea bali kushirikiana kwa lengo la kuvunja umaskini na kujenga utajiri wa vizazi.

    Rafiki yako,

    Maureen.

  • Mambo 4 yakuzingatia ili kuwa na nidhamu kali ya kuamua na kutenda

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana kwenye blog hii ya kujifunza kila siku. Nimerudi sasa tusonge mbele na kujifunza kila siku, naamini uko salama sana.

    Leo tunajifunza kuhusu nidhamu ya kuamua kufanya, tunapopanga kufanya kitu lazima tupange na kufanya. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha kwa sababu ya kukosa nidhamu hii.

    Watu wengi hukosa nidhamu kwa sababu hawajaamua kwa dhati, hawana mifumo ya kuwasaidia na hawana watu wa kuwawajibisha.

    Mara nyingi mtu huanza jambo kwa hamasa kubwa, lakini hatua ya kuendelea kulifanya kila siku bila sifa wala makofi ndiyo sehemu ngumu na yenye mafanikio ya kweli.

    Mambo ya kuzingatia ili kuwa na nidhamu ni kama ifuatavyo;

    1. Badilisha utambulisho wako. Jione kama kile unachokitaka kuwa. Ukiwa mfanyabiashara tenda kama mfanyabishara, ukiwa mwandishi,andika kila siku.
    2. Tengeneza mifumo. Usitumie nguvu binafsi pekee kwa sababu unaweza kuchoka au kurudi nyuma ukipata changamoto. Mfumo mzuri hukusaidia kuendelea hata ukiwa huna hamasa.
    3. Tengeneza mazingira yanayokuunga mkono. Mazingira yana nguvu kubwa katika kufanikisha au kuharibu malengo yako.
    4. Kuwa na uwajibikaji. Pata mtu wa kukusimamia au coach wa kukuwajibisha ili usijidanganye na kuacha ulichoamua kufanya.
    5. Jamii ya watu wanaokuzunguka. Huwezinirudishia kufanikiwa katika jambo kubwa kama bado una tabia au watu wanaokurudisha nyuma.

    Mifano ya tabia zinazoweza kukukwamisha ni kama: visingizio, uvivu, kukosa uaminifu, uzinzi, uongo nk.

    Rafiki ukiwa karibu na watu wenye tabia hizo, ni rahisi kurudi kwenye mazoea mabaya na kushindwa kusonga mbele kadri muda unavyokwenda.

    Hatua ya kuchukua; rafiki washindi au wanaofanikiwa hufanikisha mambo yao kwa nidhamu kali ya kuamua na kufanya na si kwa bahati. Naamua leo kuwa naweka kali katika kazi na shughuli zangu za kila siku.

    Rafiki yako,

    Maureen.

  • Mambo Makuu 5 Ambayo Nimejifunza Kutoka Kitabu Cha The Road Less Stupid Na Keith J. Cunningham.

    Rafiki Keith J Cunningham ni mfanyabishara mkongwe na mwekezaji. Kitabu chake kinatofautiana na vitabu vingi vya biashara.

    Kitabu hiki hakitoi njia za haraka za kufanikiwa badala yake kinazungumzia ukweli wa msingi. Watu wengi wanashindwa si kwa sababu hawana akili, bali kwa sababu wanafanya mambo makuu ya kijinga.

    Lengo kuu ya kitabu ni kutufundisha jinsi ya kuacha ujinga katika uongozi na maamuzi ya biashara.

    Falsafa ya msingi: “Fikiria zaidi, Fanya Upumbavu” Cunningham anasisitiza kuwa;

    1. Tunapaswa kutumia wakati wa kutosha kufikiria na kuchambua kabla ya kutekeleza. Mara nyingi tunajikuta uamuzi wa haraka unaoleta madhara makubwa.
    2. Saa moja ya kufikiri inaweza kuokoa miaka miwili ya kufanya kazi ngumu isiyo na tija.
    3. Wafanyabishara wengi hujikuta katika hali ya kukimbia mwendo wa kasi bila mwelekeo badala ya kukaa na kujiuliza: Ninafanya Nini? Kwa Nini Ninafanya hivyo? Je, ninafanya vizuri?

    Dhana ya saa ya fikra ( The thinking hour). Hii ndiyo dhana muhimu zaidi katika kitabu. Cunningham anashauri kila siku, au angalau kila wiki, utumie saa moja bila usumbufu wa kufanya yafuatayo:

    1. Kuandika mawazo yako. Fikiria kwa kutumia kalamu na karatasi.
    2. Uliza maswali makuu kwa wewe mwenyewe . Ni wapi inaweza nifanya nivunje biashara yangu? Ni makosa gani ninafanya sasa? Ni mapungufu gani ya kifedha nimeyapuuza? Ni nini kinachokwenda vizuri zaidi?
    3. lengo siyo kuandika mpango, bali kuzua maswali mazuri na kuyajadili. Kwa kufanya hivyo, unaweza kugundua mapito na hatari kabla hujaathiri biashara yako.

    Uchumi wa biashara (Business Acumen). Kitabu kinatoa mwongozo mzuri wa kuelewa kanuni za msingi za kifedha na biashara:

    1. Tofauti kati ya pesa na mapato: Unaweza kuwa na mapato makubwa lakini ukakosa pesa taslimu ( cash flow). Hii ndiyo sababu ya kufa kwa biashara nyingi.
    2. Umuhimu wa uwiano wa faida: Unauzungumziaje gharama zako? Faida halisi ni kiasi gani baada ya malipo yote.
    3. Uwekezaji wa mtaji. Tunapaswa kuwekeza pesa tu kwenye mambo yanayotoa faida au kuleta ufanisi.

    Kupunguza Hatari na Kuepuka Mapito ( avoiding stupid mistakes). Cunningham anasema kuwa ushindi wa biashara haupo kwenye kufanikiwa kwa kushinda, bali kwenye kuepuka kufeli.

    1. “Wataalamu wa kifedha hushinda pesa. Wanaofanya makosa hupoteza.”
    2. Anatoa mifano ya makosa ya kijinga kama vile: kukopa kwa kasi mno, kupanua biashara bila kuhakikisha uwezo wa kifedha, kushindwa kusikiliza wateja, na kujifanya unajua kila kitu.

    Uongozi na Uamuzi.

    1. Kuweka kipaumbele: Ni muhimu kujua ni shida gani ya kutatua kwanza. Cunningham anasema, “Usiwe na shida nyingi; weka kipaumbele na utatue moja moja.”
    2. Kujua kile usichojua: Mfanyabishara mzuri anajua mipaka ya ujuzi wake na anatafuta ushauri kutoka kwa wale walio na ujuzi zaidi.
    3. The road less stupid ni kitabu cha lazima kwa mfanyabishara yeyote ambaye amechoka na kufanya makosa yanayozuilika na anataka kujenga msingi imara kwa maamuzi yake.

    Kitabu hiki ambacho kinatumika kama “bima ya kijinga” kinakusaidia kutambua na kuepuka makosa makubwa kabla hujaathiri biashara yako.

    Hatua ya kuchukua; Kuanzisha saa ya kufikiri yaani the thinking hour. Huu ndio msingi wa yote. Usiwe na wasi wasi huhitaji kuanza kwa saa nzima bali unaanza kidogo kidogo.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei.

  • Siri Ya Kuvuka Vikwazo.

    Rafiki yangu mpendwa waliofika mbali waliamua kutokuogopa kushindwa.

    Wao wanajaribu hata kama wanashindwa. Mafanikio ni ung’ang’anizi.

    Mambo yakuzingazia ili kuvuka vikwazo.

    1. Kushindwa ni sehemu ya wastani. Baada ya hapana nyingi utapata ndio, hakuna kukata tamaa katika safari ya mafanikio. Wingi wa juhudi huleta kuua uoga wa kukataliwa.
    2. Kukataliwa hakumaanishi wewe ni tatizo bali ni bidhaa. Andika majibu ya mapingamizi ili utafute njia ya kuyavuka. Uliza maswali ili uweze kupata mapingamizi sahihi, kukataliwa ni kinga kukujenga uwe jasiri.
    3. Hakuna mafanikio bila kushindwa mara nyingi ni sehemu ya mchakato. Thomas Edison alishindwa mara nyingi kabla ya kupata mafanikio. Kushindwa siyo doa la aibu ni daraja la mafanikio.
    4. Kushindwa kunaonyesha ukweli wa juhudi zako. Mchakato uko ndani ya juhudi zetu na siyo matokeo. Frank Portugie alikuwa haweki kazi, alijitathmini na kuona ugumu na akaamua kufanyia kazi kwa kutaka matokeo. Ukiwa kinganganizi dunia inakupa kile unachokitaka. Fanya tathmini ujue ni juhudi ulizoweka ama ni uzembe uliokufikisha hapo, jiweke kitimoto.
    5. Ukiwa na hofu ya kushindwa utajifunga mwenyewe. Jaribu na kuwa kinganganizi hadi uweze kukubalika na wengine bisha mara nyingi au omba mara nyingi ili ukubalike.
    6. Kila hatua ya kushindwa inakusogeza kwenye kufanikiwa. Wingi wa majaribio unazalisha matokeo . Kukataliwa siyo wewe ni kile unachouza , jipime kwa juhudi zako.

    Kile nimejifunza, kujaribu mara nyingi utaishia kwenye kupata matokeo. Kushindwa ni sehemu ya ushindi lakini ukiendelea kujaribu mara nyingi.

    Rafiki yako,

    Maureen Kemei

  • Mambo Muhimu Ambayo Nimejifunza Kuhusu Nidhamu Ya Muda Na Utekelezaji.

    Rafiki yangu mpendwa muda una ukomo, muda ni sawa na kuna wanaofanikiwa na wasiofanikiwa.

    Kuwe na nidhamu ya muda, weka vipaumbele vyako hicho unachokifanya kinachangiaje kwenye malengo yako.

    Kama hauwezi kutawala maisha yako hauwezi kufanikiwa . Wengi hawafanyi kwa ufanisi na kuvipa muda vile vyenye vipaumbele.

    Weka tija kwenye vile vya msingi. Achana na kukimbilia fursa mpya.

    Nidhamu ya muda ni kufanya yale uliyopanga hata kama huna hamasa ya kufanya.

    Weka vipaumbele na kufuata kwa utekelezaji, kuahirisha jambo ni kujijengea tabia mbaya na kujidharau.

    Kamilisha vitu vitatu kwa uhakika kila siku kwa usahihi na yale yanayopelekea kufikia maono yako.

    Panga muda kwa vipindi na kublock mambo mengine . Weka muda maalum kwa kazi kubwa.

    Anza na kazi ngumu zaidi. ‘Eat that frog’ Chura ni vitu au kitu ambacho hukipendi. Anza na magumu wakati una nguvu. Wakati akili iko vizuri na uendelee na madogo.

    Pangilia muda na kufanya kazi kwa muda dk 25 kwa 5, unapiga kazi kwa dakika ishirini na tano na kupumzika kwa dakika tano.

    Fanya tathmini yako ya siku na kuona umekamilisha nini.

    Hatua za kuchukua:

    1. Tekekeza mambo 5
    2. panga muda.
    3. tekekeza mambo muhimu mapema.
    4. fanya tathmini ya siku.
    5. fanya tathmini ya wiki .

    Ukipanga muda vizuri utaondokana na mambo mengi.

    Kila siku tumia muda wako vizuri kupata matokeo mazuri.

    Rafiki yako,

    Maureen.