Rafiki Keith J Cunningham ni mfanyabishara mkongwe na mwekezaji. Kitabu chake kinatofautiana na vitabu vingi vya biashara.
Kitabu hiki hakitoi njia za haraka za kufanikiwa badala yake kinazungumzia ukweli wa msingi. Watu wengi wanashindwa si kwa sababu hawana akili, bali kwa sababu wanafanya mambo makuu ya kijinga.
Lengo kuu ya kitabu ni kutufundisha jinsi ya kuacha ujinga katika uongozi na maamuzi ya biashara.
Falsafa ya msingi: “Fikiria zaidi, Fanya Upumbavu” Cunningham anasisitiza kuwa;
- Tunapaswa kutumia wakati wa kutosha kufikiria na kuchambua kabla ya kutekeleza. Mara nyingi tunajikuta uamuzi wa haraka unaoleta madhara makubwa.
- Saa moja ya kufikiri inaweza kuokoa miaka miwili ya kufanya kazi ngumu isiyo na tija.
- Wafanyabishara wengi hujikuta katika hali ya kukimbia mwendo wa kasi bila mwelekeo badala ya kukaa na kujiuliza: Ninafanya Nini? Kwa Nini Ninafanya hivyo? Je, ninafanya vizuri?
Dhana ya saa ya fikra ( The thinking hour). Hii ndiyo dhana muhimu zaidi katika kitabu. Cunningham anashauri kila siku, au angalau kila wiki, utumie saa moja bila usumbufu wa kufanya yafuatayo:
- Kuandika mawazo yako. Fikiria kwa kutumia kalamu na karatasi.
- Uliza maswali makuu kwa wewe mwenyewe . Ni wapi inaweza nifanya nivunje biashara yangu? Ni makosa gani ninafanya sasa? Ni mapungufu gani ya kifedha nimeyapuuza? Ni nini kinachokwenda vizuri zaidi?
- lengo siyo kuandika mpango, bali kuzua maswali mazuri na kuyajadili. Kwa kufanya hivyo, unaweza kugundua mapito na hatari kabla hujaathiri biashara yako.
Uchumi wa biashara (Business Acumen). Kitabu kinatoa mwongozo mzuri wa kuelewa kanuni za msingi za kifedha na biashara:
- Tofauti kati ya pesa na mapato: Unaweza kuwa na mapato makubwa lakini ukakosa pesa taslimu ( cash flow). Hii ndiyo sababu ya kufa kwa biashara nyingi.
- Umuhimu wa uwiano wa faida: Unauzungumziaje gharama zako? Faida halisi ni kiasi gani baada ya malipo yote.
- Uwekezaji wa mtaji. Tunapaswa kuwekeza pesa tu kwenye mambo yanayotoa faida au kuleta ufanisi.
Kupunguza Hatari na Kuepuka Mapito ( avoiding stupid mistakes). Cunningham anasema kuwa ushindi wa biashara haupo kwenye kufanikiwa kwa kushinda, bali kwenye kuepuka kufeli.
- “Wataalamu wa kifedha hushinda pesa. Wanaofanya makosa hupoteza.”
- Anatoa mifano ya makosa ya kijinga kama vile: kukopa kwa kasi mno, kupanua biashara bila kuhakikisha uwezo wa kifedha, kushindwa kusikiliza wateja, na kujifanya unajua kila kitu.
Uongozi na Uamuzi.
- Kuweka kipaumbele: Ni muhimu kujua ni shida gani ya kutatua kwanza. Cunningham anasema, “Usiwe na shida nyingi; weka kipaumbele na utatue moja moja.”
- Kujua kile usichojua: Mfanyabishara mzuri anajua mipaka ya ujuzi wake na anatafuta ushauri kutoka kwa wale walio na ujuzi zaidi.
- The road less stupid ni kitabu cha lazima kwa mfanyabishara yeyote ambaye amechoka na kufanya makosa yanayozuilika na anataka kujenga msingi imara kwa maamuzi yake.
Kitabu hiki ambacho kinatumika kama “bima ya kijinga” kinakusaidia kutambua na kuepuka makosa makubwa kabla hujaathiri biashara yako.
Hatua ya kuchukua; Kuanzisha saa ya kufikiri yaani the thinking hour. Huu ndio msingi wa yote. Usiwe na wasi wasi huhitaji kuanza kwa saa nzima bali unaanza kidogo kidogo.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.