Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini ikiwa unataka kuboresha mahusiano yako na wengine, falsafa ya ustoa inaweza kuwa mwanga mzuri.
Hapa chini mna njia kadhaa unavyoweza kuitumia.
- Kuelewa na kukabiliana na wengine. Huwezi kubadilisha mtu bali ni kumuelewa na kukubali au kumkubali jinsi alivyo. Kwa hivyo pamoja na udhaifu wake Kuna kitu kizuri unachokipata. Usiangalie ubaya bali angalia ni kitu gani kizuri utapata kwake.
- Kudhibiti hisia na mawazo. Tunapaswa kudhibiti hayo ili kuweza kuishi na watu vizuri kama wivi,ghadhabu na mengine. Turuhusu hisia lakini ila tujicheleweshe kuchukua hatua fulani.
- Kuishi kwa maadili na heshima. Fanya kilichosahihi na kuheshimu . Tusitafute manufaa binafsi bali tumpe kila mtu heshima yake
- Onyesha huruma kwa wengine. Hasa wakati wa changamoto, tuwavumilie na kuwaelekeza wawe bora. Tuwape jukumu lililoko ndani ya uwezo wao.
- Thibiti matarajio ya wengine . Binadamu wanabadilika na kukugeuka.
- Ishi kwa amani iliyo ndani yako. Usikubali utawaliwe na furaha ya nje. Tegemea kupata wanyanganyi na wadhulumu.
- Kuwa mtu wa kuwajibika kwa matendo yako. Kuwa tayari kukiri makosa yako na kuwajibika kwa matendo yako. Uwe mfano wa wema .
- Kuepuka tabia zisizofaa. Kukosa maadili na udanganyifu. Mambo mengi yanayotokea siyo mabaya ni kujifunza kutokana na changamoto hiyo.
- Uzuri au ubaya wa kitu ni tafsiri ya mtu. Inategemea jinsi utakavyoichukulia.
- Ishi kadiri ya uwezo wako. Usiishi maisha ya juu kama kipato chako bado iko chini.
- Kukuza sehemu ya mahusiano. Tunaishi kwa kutegemeana katika umoja wa kijumuia. Huwezi ukawa bora ukiwa peke yako lazima uwe na uhusiano na watu.
- Usiruhusu mambo ya nje yakuumize.
- Jijali na kujipa muda. Watu wengi hawajijali wala hawajipi muda . Unapaswa kujipenda na ndipo uwapende wengine. Jitunze wewe mwenyewe kula vizuri, lala vizuri nk.
- Kubaliana na mabadiliko. Kukabiliana na mabadiliko ni sehemu nzuri hivyo pokea..
- Uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine.
Chukua hatua, rafiki tutakuwa bora na tutakuwa na furaha pale tu tutakapokuwa na falsafa ya ustoa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .