Dhibiti Kile Kinachoingia Kwenye Akili Yako.

Rafiki yangu mpendwa tunaishi kwenye zama ya mafuriko ya taarifa na maarifa, tuna mengi yanayopigania kupata umakini wetu kuliko muda tulionao wa kuhangaika na mambo yote hayo.

Watu wengi wamekuwa wakijidanganya kwa kukimbizana na maarifa zote ili wasipitwe, lakini kwa kumezwa na taarifa hizo, wanakosa muda wa kufanya mambo mengine muhimu.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini usikubali hili litokee kwako, badala ya kuhangaika na kila aina ya taarifa na maarifa yanayosukumwa kuja kwako, dhibiti ni aina gani ya maarifa zikufikie na kwa muda gani.

Fikiria jinsi ambavyo huwa unajisikia unapoamka asubuhi na mapema, kabla siku hazijaanza kuingia na hujaanza kuzurura mitandaoni. Unakuwa na utulivu mkubwa sana ndani yako, unaweza kufanya makubwa na mazuri.

Chukua hatua, rafiki sasa tengeneza hali kama hizo kwenye maisha yako, tenga muda wa kuwa mbali na maarifa na taarifa na kuweza kufikiri kwa kina na kufanya kazi ambayo inahitaji utulivu wako.

Muda huo kaa mbali kabisa na simu yako na hata watu wengine, ili uepukane na usumbufu utakaoathiri kile unachofanya.

mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment