Rafiki yangu mpendwa, sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna njia sita nzuri kabisa unazoweza kufanya ili kuwa na furaha siku zote za maisha yako.
Kwanza. Usiwe na kazi, kuwa na kile unachopenda kufanya. Furaha ni matokeo ya kufanya kile unachopenda kufanya.
Hivyo, unapaswa kupenda unachofanyana hapo hutafanya kazi kabisa. Kama unachofanya unakiona ni kazi tu, basi tayari unakosea.
Pili. Furahia kushindwa kwako. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa sana bila ya kushindwa. Hivyo unaposhindwa furahia, kwa sababu ni njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Tatu. Fedha siyo sawa na furaha. Lengo lako kuu kwenye kile unachofanya lisiwe fedha, bali anza kwa kupenda kile unachofanya na kutoka mchango wako kwa wengine. Na furaha unayoweza kuipata kwenye fedha ni kuwasaidia wengine.
Nne. Shukrani inaleta furaha. Unapokuwa mtu wa kushukuru, unakuwa na furaha. Kila siku orodhesha vitu unavyoshukuru kuwa navyo kwenye maisha yako na utakuwa na maisha yenye furaha.
Tano. Utajiri hauwezi kununua afya. Hivyo weka kipaumbele cha kwanza kwenye afya yako. Wengi wanasahau afya zao kwa kukimbizana na utajiri, halafu wakishaupata wanautumia kuboresha afya zao, huo ni ujinga. Zingatia afya yako, kula vizuri, fanya mazoezi na pata muda wa kupumzika.
Sita. Wakati sahihi kwako kubadili kazi au biashara ni pale kila unapoamka asubuhi hujiskii kabisa kwenda kwenye kazi au biashara yako. Unapoanza kujiona unafanya kazi, hapo umeshapoteza.
Kuchukua hatua, rafiki kumbuka ili kufanikiwa hupaswi kufanya kazi, basi unapaswa kufanya kile unachopenda.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafsi.com.