Umuhimu Wa Kujitofautisha Na Wengine

Rafiki yangu mpendwa ili kufikia mafanikio makubwa na kutengeneza ubobezi wako, unahitaji kujitofautisha na wengine ambao wanafanya kile unachofanya wewe.

Lazima kuwe na kitu ambacho watu wanakipata kwako na hawawezi kukipata kwa mtu mwingine yeyote.

Na hili ni rahisi kujua na kutumia kama utajitafakari wewe binafsi na kuangalia maeneo yote ya maisha yako.

Angalia uzoefu wako wa nyuma, angalia vipaji ulivyonavyo kisha ona unawezaje kuvitumia kwenye kile eneo unalojenga ubobezi na kuweza kujitofautisha na wengine wanaofanya kile unachofanya.

Hakuna ubobezi kama hakuna kinachokutofautisha na wengine. Lazima kuwe na sababu kubwa ya watu kuja kwako.

Kabla hujafanya maamuzi, lazima watu wajue kuna kitu wanapata kwako ambacho hawawezi kukipata kwa wengine.

Habari njema ni kwamba ni rahisi sana kujitofautisha na wengine kama utaamua kuwa wewe. Kama utaacha kuiga na kujilinganisha na wengine, na kuchagua kuwa wewe, kwa kuweka utu wako kwenye kile unachofanya, basi utakuwa tofauti kabisa na wengine.

Kitu kimoja zaidi rafiki ni kuwa hakuna mtu anayefanana na wewe kwa kila kitu hapa duniani. Hivyo ukichagua kuwa wewe, utajitofautisha na wengine wote.

Chukua hatua, ili kufanya makubwa kwenye maisha yetu, tunapaswa kuanza sasa kukataa kuiga wengine na kuamua kuwa sisi na tutaweza kujitofautisha na wengine na kuweza kufanya makubwa.

Mwandishi na rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment