Rafiki yangu mpendwa mwandishi Jaron Lanier kwenye kitabu chake cha Ten Arguments for Deleting Your Social Media Accounts Right Now.
Mwandishi anatushirikisha jinsi mtandao wa kijamii inavyofuatilia maisha ya watu na pia inatumia nguvu kuhakikisha unakuwa msikivu na mtii kwa mtandao hiyo. Nguvu iyo ni shinikizo la kijamii.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, tunajali sana jinsi ambavyo wengine wanatuchukulia kwa sababu huwa tunalinda hadhi zetu za kijamii na kushindana na wengine.
Kihistoria, binadamu waliopona na kuzaliana ni wale walioweza kwenda vizuri na kuwa sehemu ya jamii, wale ambao hawakuweza waliachwa na jamii na kupoteza maisha yao.
Watu huwa wanafanya vitu siyo kwa sababu wanapenda au vina manufaa kwao, bali kwa sababu wanataka kutunza hadhi yao kijamii au kufanana na wengine kwenye jamii wanaofanya hivyo.
Japo kwa sasa hakuna hatari kubwa kama mtu usipokuwa ndani ya jamii fulani, bado ile hali ya kuitegemea jamii iko ndani yetu. Na mtandao ya kijamii imejua jinsi ya kuitumia hali hiyo kwa manufaa yake.
Mtandao wa kijamii imeleta hali ya mashindano baina ya watu na watu wamekuwa wanaitumia kufuatilia maisha ya wengine na kijilinganisha nao. Mtandao hii imekuwa inaibua hisia chanya pale mtu anapojiona yuko juu ya wengine au hisia hasi pale mtu anapoona yuko chini ya wengine.
Sasa pia kwa kuwa watu hawaweki maisha yao halisi kwenye mtandao hiyo, kila mtu anaonekana ana maisha mazuri hivyo kila anayeangalia, anaona mwenzake yuko vizuri kuliko yeye. Hali hiyo imekuwa inaibua hisia za hasira kama chuki, wivu na hasira, kitu ambacho kinawafanya watu kuwa rahisi kupoteza utashi wao na kushawishika na chochote.
Pale hisia za mtu zinapokuwa juu huwa hawezi kufikiri na hivyo ndivyo mitandao hiyo inanufaika, inachochea hisia zako kwa kukulinganisha na wengine na zikishakuwa juu inakushawishi kuchukua hatua fulani zinazowanufaisha wao na kukuumiza wewe.
Kama tunavyojua, zawadi na adhabu zina nguvu ya kuwabadili watu, shinikizo la kijamii, linatumia nguvu hiyo kuwabadili watu kwenye utumiaji wao wa mitandao ya kijamii.
Kumbuka yote haya yanafanyika kwa mfumo wa mitandao hiyo, ambao haumjui hata mtu lakini unakusanya kila taarifa na kisha kuzitumia kwa namna inamfanya mtu awe mtumiaji zaidi na kuchukua hatua zenye manufaa kwa mtandao huo, hata kama hazina manufaa kwa mtumiaji.
Kuchukua hatua; kwa sababu lengo la mtandao wa kijamii ni kukufanya wewe uwe mraibu wa mtandao, ili kila mara unatamani kufuatilia habari zote zinazoendelea humo. Hivyo tunapaswa tuwe na ugomo wa utumiaji wa mitandao wa kijamii na badala yake tufanye yale yaliyo na tija kwenye maisha yetu.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.