Rafiki yangu mpendwa, mara nyingi mtazamo wako ndiyo unaokutofautisha na wengine. Nini mtazamo wako juu ya maisha, mafanikio na uwezo.
Kuna aliyefanya utafiti kidogo tu juu ya mtazamo ya watu. Aliweka maji kwenye glasi. Kuna aliyeona glasi imejaa nusu, kuna aliyeona nusu haijajaa au haikujaa nusu. Watu hao wawili wana mtazamo tofauti.
Mtazamo wako juu ya uwezo wako utakutofautisha na wengine. Kitu cha kushangaza ni kuwa mtazamo wako unatafsiri utendaji wako. Hivyo, unaweza kuathiri vitendo vyako chanya au hasi kulingana na mtazamo wako.
Kama mtazamo wako ni kuangalia udhaifu wako juu ya uwezo wako, ni lazima utakupeleka kushindwa kwa kila kitu unachokifanya.
Kuna mtazamo chanya na hasi. Unahitaji mtazamo chanya Ili uweze kusonga mbele. Kwa mfano ukimsikia mtu akisema ‘ hawezi’ kuna mawili;
- Yaweza kuwa anamaanisha hajui. Hivyo, anahitaji kufundishwa Ili ajue kuwa anaweza na inawezekana kufanya na kuwa chochote anachotaka.
- Anahitaji kufundishwa lakini uwezo wa kufanya jambo lolote uko ndani mwake na wala hauko mbali.
Kuchukua hatua rafiki yangu ni wakati sahihi wa kubadili mtazamo wetu, kama tunataka tuwe wa tofauti au kuondokana na kundi kubwa la wengi wanaoishi maisha ya kawaida, wakifanya mambo ya kawaida tu. Hatuna budi kuibadili mtazamo wetu yaani tuwe watu wenye mtazamo wa uwezekano,uchanya na ufaulu.
Mtazamo ni muono wa ndani yaani ni tofauti na kuona kwa macho. Macho yako yanaweza yakakusaidia kutengeneza mtazamo wako wa ndani, mtazamo chanya au mtazamo hasi.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com