Mambo makubwa ya kujifunza kutoka kwa shujaa Desmond Tutu.

Mwandishi Robin Sharma kwenye kitabu chake cha “the everyday hero manifesto” anatushirikisha wakati alipokutana na Desmond Tutu, mwanaharakati wa Afrika kusini aliyefanya kazi kwa karibu na Nelson Mandela katika kuikomboa Afrika kusini na kuponya majeraha ya mfumo wa ubaguzi.

Robin anasema kitendo cha kukutana na Tutu kilileta nguvu kubwa na ya kipekee sana ndani yake. Kupitia yeye, kuna mambo makubwa muhimu aliyojifunza.

Mambo hayo ni kama : kuwa jasiri kusimamia kile kilicho sahihi bila ya kujali nani anayekupinga, lakini pia kuwa tayari kuwasamehe waliokuumiza kwa namna mbalimbali.

Kila binadamu hapa duniani ni muhimu bila kujali rangi, jinsia, dini au taifa. Na kila mtu anapaswa kuchukuliwa kwa heshima, uelewa na upendo.

Umuhimu wa kila mtu kuishi upekee ambao upo ndani yake, kuvunja minyororo ya ukomo ambayo tumejengewa na kuwa halisi, kitu ambacho kina mchango mkubwa hapa duniani.

Kila mtu ni kiongozi hata kama hana madaraka. Asili huwa haipendi kuwepo kwa utupu, hivyo popote ulipo, asili itatupa wajibu wa kuwa kiongozi ili kujaza ombwe lililopo. Ni wajibu wako kuwa na maono na kuwahamasisha wengine kuyaelewa na kujiunga na maono uliyonayo.

Hatua ya kuchukua, sisi binadamu tuna nguvu kubwa ambayo tayari ipo ndani yetu, ni wajibu wetu kuitambua na kuanza kuitumia ili kuweza kufanya makubwa.

Akujaliaye sana.

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment