-
Njia 10 Bora Ya Jinsi Ya Kuimarisha Mahusiano
Rafiki yangu mpendwa yapo njia bora ya kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wengine kwenye maisha.
Njia hizo ni kama yafuatayo;
- Mawasiliano ya wazi. Zungumza kwa uaminifu na uwazi kuhusu hisia, matarajio, na changamoto. Mawasiliano mazuri ni msingi wa uhusiano mzuri.
- Kujifunza kusikiliza. Sikiliza mwenzi wako kwa makini bila kukatiza. Hii huonyesha heshima na kuimarisha uelewa kati yenu.
- Uaminifu. Jenga na linda uaminifu. Hakikisha kuwa vitendo vyako vinaendana na maneno yako.
- Kuheshimu tofauti. Tambua kwamba ninyi wawili mnaweza kuwa na maoni na mitazamo tofauti. Jifunze kuheshimu na kuthamini utofauti huo.
- Kutenga muda pamoja. Hakikisha unapata muda wa kuwa pamoja, hata kama ratiba zenu ni zenye shughuli nyingi. Hii huimarisha uhusiano wa kihisia.
- Kujifunza kuomba msamaha. Kukubali makosa na kuomba msamaha kunahitaji ujasiri, lakini ni muhimu kwa kurudisha maelewano.
- Kuonyesha Shukrani. Tambua na shukuru juhudi na matendo mazuri ya mwenzi wako. Hii kuongeza furaha na upendo.
- Kusaidiana katika changamoto. Kuwa nguzo ya kuaminika kwa mwenzi wako wakati wa changamoto. Ushirikiano huimarisha uhusiano.
- Kupunguza mizozo kwa upole. Badala ya kugombana, tumia njia za kushughulikia mizozo kwa njia za heshima na kuelewana.
- Kujali maendeleo binafsi. Endelea kujiboresha binafsi, kimwili, kihisia, na kiakili. Uhusiano imara hujengwa na watu waliokamilika kihisia.
Chukua hatua; kwa kufanyia kazi hayo mawazo kutasaidia mahusiano yako kuwa na afya ,furaha na uimara zaidi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Je Unajua Mazuri Unayoyafanya Yanadumu Milele?
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kumekuwa na uhaba wa watu kufanya mambo mazuri kwa sababu wanaona hakuna anayejali.
Lakini huo siyo ukweli, mambo mazuri unayofanya, hata kama ni madogo kiasi gani, huwa yanagusa maisha ya wengine na huwa hawasahau.
Robin anatushirikisha hadithi mbili kwenye hili.
Moja ni utaratibu ambao mama yake alikuwa nao wa kumletea chakula shuleni alipokuwa mtoto. Ndani ya chakula aliweka ujumbe wa jinsi alivyokuwa anampenda. Mpaka sasa Robina anakumbuka ujumbe huo.
Mbili ni mchezaji maarufu aliyekuwa anaambatana naye ambaye alikuwa tayari kusimama pale watu walipomwomba wapige naye picha.
Alipomwuliza kwa nini ana utayari wa aina hiyo alimjibu unahitaji kufanya vitu vidogo vidogo kuwafurahisha wengine.
Na hapo ndipo Robin alijifunza umuhimu wa vitu vidogo vidogo vizuri kwa wengine, kwako inaweza kuwa kawaida, lakini kwa wengine ikawa ni kitu kikubwa ambacho hawatakisahau maisha yao yote.
Chukua hatua; hatupaswi kuchoka kwenye kutenda mema kwa wengine kwani huwa inawagusa sana na huwa wanaikumbuka kwenye maisha yao yote. Tunafaa kuendelea kutenda mema hata kama hamna anayetambua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Misingi 10 Ya Kuwa Na Maisha Ya Furaha.
Maisha ya furaha maana yake nini? na misingi gani unaitumia ili kuishi maisha ya furaha?
Maisha ya furaha ni kuwa na amani na utulivu.
Misingi 10 ya kuwa na maisha ya furaha ni kama yafuatayo;
- Tegemea kukutana na watu wabaya.
- Ipime siku yako kabla ya kulala. Fanya tahajudi kabla ya kulala kwa kufikiria siku yako. Je, vitu gani umefanya kwa ubaya au kwa namna isiyo sahihi. Vitu gani umefanya vizuri au vitu gani utavifanya kwa utofauti siku inayofuata. Usikubali usingizi ufumbe macho yako kabla hujahesabu kila tendo ambalo umefanya. Jifokee kwa kila tendo baya na jipongeze kwa kila tendo jema.
- Fanya kilicho sahihi lakini usitegemee chochote. Mtu mwenye hekima hafanyi chochote kitakachomuumiza.
- Jijengee tabia njema. Tabia njema ndiyo zao la furaha.
Kwenye USTOA tuna tabia njema 4
A. Hekima
B. Haki
C. Ujasiri
D. Kiasi- Mahusiano Bora. Ukitafuta ubaya kwa mtu tegemea kuupata lakini tusiangalie ubaya wa mtu bali tuangalie mazuri. Tuangalie namna nzuri ya kushirikiana na siyo kupingana kila wakati.
- Dhibiti hisia zako ili kuishi maisha ya furaha
- Kuwa mstahimilivu. Kushindwa na kukata tamaa visipatikane kwako.
- Ishi kulingana na asili. Jua unachopaswa kukifanya na ufanye hakuna chochote kilicho kibaya au kizuri. Jua unachopaswa kukifanya na ukifanye.
- Jua yaliyo ndani ya uwezo wako na yaliyo nje ya uwezo wako.
- Una muda wa kutosha kufanya chochote unachokitaka. Maisha yako ni marefu kama utafanya yaliyo mazuri
Chukua hatua; rafiki kuishi maisha ya furaha na utulivu unategemea na sisi wenyewe, hamna yeyote anayeweza kukuletea furaha ila wewe mwenyewe ujitafutie furaha na utulivu kwenye maisha yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Sababu 5 zilizopelekea Al Rida Kuwa Muuzaji Bora Kuwahi Kutokea Kwenye Kipindi Hiki.
Rafiki yangu mpendwa Al Rida anaweza kuwa rejeleo kwa mtu, kampuni, au falsafa fulani ya biashara, na sifa za kuuza bora mara nyingi zina uhusiano na vipengele vya kipekee vinavyomtofautisha na wengine.
Hapa kuna sababu tano zinazoweza kuelezea kwanini Al-Reda alifanikiwa kuwa muuzaji bora.
- Uwezo wa kujenga uhusiano imara na wateja. Al- Reda aliweza kujenga mahusiano ya dhati na wateja wake, alihakikisha wanahisi kuthaminiwa.
- Ufahamu wa kina wa mahitaji ya soko. Alijitahidi kuelewa changamoto za wateja na kutoa bidhaa au huduma zinazotatua matatizo hayo moja kwa moja.
- Ubunifu na ubora wa bidhaa au huduma. Al- Reda alileta bidhaa au huduma zilizo na tofauti za kipekee ambazo hazikupatikana kwa washindani.
- Ujuzi bora wa uwasilishaji na ushawishi. Alitumia mbinu za ushawishi, kama hadithi, kithibithisha thamani ya bidhaa zake kwa kutumia mifano halisi.
- Ushindani wa bei na huduma bora kwa wateja. Alihakikisha kuwa huduma kwa wateja ni ya kiwango cha juu, aliweka kipaumbele katika kuridhisha wateja hata baada ya mauzo. Aliweka bei zake kwa busara, alihakikisha wateja wanapata thamani zaidi ya pesa zao.
Chukua hatua rafiki tunapaswa kujenga urafiki na umoja ili watu wasinunue kwa mtu mwingine. Tunapaswa kupiga kelele sana kwa watu wengi ili watu wajue uwepo wetu kwenye soko.
Ukitaka kitu kifanyie kazi na utaweza kufanikiwa kwa hali ya juu.
Rafiki yangu,
Maureen Kemei.
-
Hatua 5 Za Kutoka Kwenye Madeni.
Rafiki yangu mpendwa 99% ya watu wengi wamo kwenye madeni mabaya. Lakini hatua za kujitoa kwenye madeni mabaya kunahitaji kazi unapaswa kuweka utaratibu wa kuanza kulipa.
Hapa kuna hatua 5 Za kujikwamua kwenye haya madeni mabaya. Ni kama yafuatayo;
- Kujua kiasi gani cha deni unalodaiwa. Unakuwa na mahali pa kuanzia na unaanza kulipa.
- Tengeneza mpango mpya wa kuongeza kipato k.m kuongeza muda wa kufanya kazi, kuongeza biashara.
- Weka kipaumbele cha kulipa madeni. Mpangilio wa kipato unachokitaka ili kulipa madeni. Njia kwa mfano, snowball, deni lenye riba ndogo zaidi. Avalanche unaanza na madeni lenye riba kubwa.
- Kuepuka madeni mabaya. Epuka kukopa ili kulipa madeni.
- Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Epuka mihemko ya harambee.
- Tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato chako.
Chukua hatua; kulipa deni ni tabia, tunapaswa kujifunza kuwa na tabia ya kuepuka kuingia kwenye madeni au kama tayari tupo kwenye madeni tujaribu kulipa na kutafuta njia za kuongeza kipato.
Rafiki y’all,
Maureen Kemei.
-
Namna 10 Ya Jinsi Unavyoweza Kushukuru.
Rafiki yangu mpendwa Mwenyezi Mungu (au kwa namna yoyote unavyoitambia nguvu hii kuu) ametupatia baraka nyingi pengine kuliko yale ambayo tumekua tukiyaona kama kero katika maisha yetu.
Hivyo basi, yatupasa kushukuru kwa yale ambayo tayari tumebarikiwanayo kabla ya kudhihirishwa kwa yale ambayo bado yapo tu katika hisia na mapenzi yetu.
Haijalishi uwezo ulionao, popote pale ulipo na kwa namna yoyote uliyonayo, bado unaweza kushukuru kwa namna tofauti.
1️⃣Tafakari kila siku jipatie muda wa kutafakari kila jioni kuhusu mambo mazuri yaliyotokea katika siku yako. Andika mambo matatu unayoshukuru kila siku.
2️⃣Toa sadaka kwa wenye mahitaji tembelea watu wenye mahitaji maalum, kama vile watoto yatima au wagonjwa hospitalini, na wape msaada wa vyakula, mavazi, au hata maneno ya faraja.
3️⃣Shukuru kwa maneno na vitendo wakati mwingine kusema “Asante” kunaweza kuwa na maana kubwa kwa wengine. Pia, jitahidi kuonyesha shukrani zako kwa vitendo kama kuwasaidia wengine bila malipo.
4️⃣Andika ujumbe wa shukraniA andika barua au ujumbe mfupi wa shukrani kwa mtu aliyekusaidia au aliyefanya jambo zuri kwako.
5️⃣Sali au fanya maombi shukuru kwa yale uliyonayo kupitia sala au maombi kwa Mungu au nguvu ya juu unayoiamini.
6️⃣Onyesha ukarimu kwa wengine kuwa mtu wa kutoa msaada, hata kwa vitu vidogo kama tabasamu, msaada kazini, au kuwajulia hali wengine mara kwa mara.
7️⃣Sherehekea/furahia mafanikio ya wengine jifunze kushukuru kwa ajili ya furaha ya watu wengine. Sherehekea mafanikio ya watu wa karibu yako na uwapongeze.
8️⃣Ishi katika hali ya kuridhika jifunze kuwa na moyo wa kuridhika na kile ulicho nacho badala ya kulalamikia unachokosa. Hii itakusaidia kuona mazuri zaidi maishani.
9️⃣Jitolee katika jamii yako jiunge na vikundi vya kujitolea kusaidia jamii yako. Hii si tu kuwasaidia wengine bali pia kukuza moyo wa shukrani.
🔟Jali mazingira na asili tembelea maeneo ya asili, kama misitu au bahari, na ujifunze kushukuru kwa uwapo wa uzuri huu katika dunia.
Chukua hatua rafiki yangu hifadhi mazingira kwa kupanda miti na epuka uchafuzi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 10 Ya Kuzingatia Tunapokosa Kile Ulichokuwa Unakitarajia
Rafiki yangu mpendwa matarajio yanapokuwa makubwa na uhalisia mdogo kuna asilimia kubwa ya kukosa hicho kitu. Kiwango cha furaha hupungua pia na msongo kuongezeka.
Lakini matarajio yanapokuwa madogo na uhalisia kuwa mkubwa kuna asilimia kubwa sana ya kupata hicho kitu. Kiwango cha furaha kuongezeka na msongo hupungua.
Baadhi ya mambo hayo kumi ni kama ifuatavyo;
- Kutambua jambo lililo ndani ya udhibiti wako.
- Kukabiliana na hali halisi.
- Punguza matarajio kwa mambo ambayo hayapo kwenye udhibiti wako.
- Fanya mazoezi ya shukran kwa jambo ambalo umekosa tafuta mambo 3 ya kushukuru kwanza.
- Jitayarishe kwa mambo ambayo hayajatokea sawa na ulivyotaka.
- Simama kwenye msingi wa tabia na maadili mema
- Tambua hali iyo ni ya muda tu.
- Angalia tukio kwa mtazamo wa juu.
- Nenda kwenye hatua inayofuata.
- Kujijenge uwezo wa kisaikolojia.
Rafiki, kukata tamaa, kukosa furaha, kupata msongo ni kaa sababu ya kukosa ustahimilivu.
Chukua hatua; ili kupata ustahimilivu fanya tahajudi na kujifunza. Kwenye hayo maisha utakosa mengi kuliko utakayoyapata.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 12 Ambayo Ninajifunza kutoka Kitabu Cha Don’t Go Back To School By Kio Stark.
Rafiki yangu mpendwa karibu tena siku ya leo nikishirikishe mambo muhimu 12 Ambayo naendelea kujifunza kutoka kitabu hiki kuzuri cha don’t go back to school.
Mambo hayo ni kama yafuatayo;
6. Alama zako ulizopata darasani hazina maana kama huna ujuzi. Ujuzi ndio unaotumika katika maisha na siyo alama ulizopata darasani. Tunapojifunza tutumie ujuzi zaidi tulionao kuliko alama tulizopata darasani. Kujua kila siku ndio alama nzuri.
7. Siku zote kama unataka kuwa mtu fulani na una kiu ya kupata anza kudhubutu. Kama unataka kuwa mwandishi mzuri kuandika na kuwa msomaji mzuri. Uzoefu unaupata pale unapokuwa unafanya, uzoefu hauji huku mikono iko mifukoni unatakiwa kudhubutu kwa vitendo.
8. Shule tunajifunza mawazo. Ukitaka kujifunza kwa vitendo na siyo nadharia ingia kwenye tukio husika na jifunze kwa watu wanaofanya kwa vitendo ndio utajifunza kwa kiuhalisia. Hata ukisoma shule kwa nadharia lazima ujifunze tena mafunzo kwa vitendo mtaani.
9. Kuwa na mawazo peke yake haitoshi unatakiwa kuyawekeza mawazo yako katika uhalisia wa vitendo. Kuwa na mtu ambaye atakua anakuongoza katika jambo lako yaani mshauri ambaye yeye ameshalipitia jambo hilo na yuko vizuri katika idara hiyo.
10. Dunia ni shule ukiitumia vizuri itakufundisha chochote unachotaka. Sio mpaka uende darasani ukasome darasani la mtaani la kujifunza kwa watu wanaofanya jambo fulani kwa vitendo.
11. Kufeli shule sio kufeli maisha. Kama una kipaji chako unaweza kujifunza kwa watu wenye aina ya kipaji chako ulichonacho. Muda mwingine angalia ni nini shauku ya maisha yako unataka nini katika maisha yako ukijua unataka nini utatafuta ili ufanikishe hitaji lako.
12. Kujifunza kupitia watu ni njia bora ya kupata uzoefu. Mtu anayejifunza kwa vitendo na yule wa kukaa darasani wako tofauti sana. Hivyo ni muhimu kujifunza kwa vitendo.
13. Njia nzuri ya kujifunza na kukufanya uwe na uwezo wa kujiamini katika mambo yako bila ya kuyumbishwa na kelele za dunia ni njia ya kusoma vitabu bila sababu na ni niia nzuri ya kujifunza sana ni wewe tu kuwa tayari kuchukua hatua.
14. Wajasiriamali ni shule ambayo kila mtu anaweza kujifunza kupitia kwao na ukapata ujuzi tosha kupitia wao. Shule hii ni nzuri kwani unajifunza kwa vitendo tofauti na shule ya darasani ambapo unajifunza kwa nadharia.
15. Kujifunza vitu mbalimbali ni muhimu sana hata kama siyo utamaduni wako au falsafa yako. Ni muhimu kujifunza vitu mbalimbali ili kuwa mjuzi wa vitu vingi. Teknolojia itakusaidia sana.
16. Zungukwa na watu chanya ambao watakusaidia kukufikisha sehemu fulani unapotaka kwenda. Kuwa na shauku ya kujua kitu fulani halafu tafuta watu wenye shauku kama yako halafu ambatana nao nawe utafika. Epuka kukaa na watu ambao wanakurudisha nyuma kwani watakua kikwazo kwako kukufikisha kule unakitaka kwenda.
17. Teknolojia imerahisisha maisha sana. Ukitaka kusoma siku hizi sio mpaka uende chuo, darasani au shule, ila siku hizi ukitaka kujifunza shule iko mikononi mwako. Huwezi kuleta sababu tena za kwanini hujifunzi kwa bidii wakati elimu inapatikana hapo ulipo ni wewe tu kuchukua hatua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mambo 5 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Don’t Go Back To School
Rafiki yangu mpendwa karibu siku ya leo nikishirikishe mambo 5 nininayo jifunza kutoka kitabu cha don’t go back to school.
Mambo 20 ninayojifunza katika kitabu Cha (Don’t Go Back To School) by Kio Stark ni kama ifuatavyo;
- Watu waliofanya machaguo katika kazi zao ndio wale wenye furaha. Mtu ambaye anafanya kazi asiyoipenda anakua hana furaha na kazi yake inamsababisha hali ya kutokuwa hata mbunifu katika KAZI yake na kuleta matokeo ambayo si mazuri. Ubunifu ni chanzo cha furaha kwa hiyo ukikosa furaha ni mbaya katika utendaji wa kazi. Fanya kazi au kitu unachokipenda kitakuletea furaha.
- Kuna njia mbili za kupata taarifa nazo ni ; kusoma, kusikiliza. Maarifa yanapatikana katika kusoma vitabu huwezi na maarifa mengi kama wewe siyo mtu wa kujifunza na njia ya kusikiliza, kusikiliza ni bora kuliko kuongea. Mtu anayesikiliza anajifunza zaidi kuliko mtu anayeongea. Jifunze kusikiliza ili kuchota maarifa mengi.
- Siku hizi kujifunza sio mpaka uende shule ukasome . Shule unatembea nayo siku hizi ukitaka kujifunza kuhusu kitu fulani unaingia katika mtandao na kujifunza kitu huko. Vitabu viko vingi online ni wewe kushindwa kujifunza tu. Maarifa huwezi kupata shule peke yake.
- Kujifunza nje ya shule kama vile kujisomea kitabu inahitaji motisha, hamasa ya kutoka moyoni. Ni injini ya ndani ndio inaweza kuratibu mambo binafsi ya kujifunza. Ukikosa hali ya kupenda kujifunza bila sharti unakua ni mtumwa.
- Njia ya kujifunza na kumfundisha mwenzako ni njia nzuri sana ili ukae na maarifa wapatie na wenzako kile ulichojifunza. Njia nzuri ya kujifunza ni kushirikisha wengine uliyojifunza.
Chukia hatua huwezi kuleta sababu tena za kwa nini hujifunzi kwa bidii wakati elimu inapatikana hapo ulipo ni wewe tu kuchukua hatua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
Mitazamo 6 Sahihi Kuhusiana Na Utajiri.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna mitazamo sahihi ambayo unapaswa kuijenga ili uweze kupata mafanikio na utajiri ambao unaitamani kwenye maisha yako.
Yafuatayo ni njia sita ya kujenga mtazamo sahihi.
- Una uwezo mkubwa ndani yako kuliko vile ambapo wewe unautumia. Bado unaitumia asilimia chache zaidi ya uwezo ulio ndani yako.
- Utajiri ni haki na wajibu wako wa kimsingi. Unapaswa kukiri mwenyewe kwa mdomo wako kuwa utajiri ni haki yako na ni wajibu wangu kutafuta utajiri huo.
- Njia bora ya kuwasaidia maskini ni kutokuwa maskini. Wanaposema tunapaswa kuwasaidia maskini, inatupasa sisi wenyewe tuwe matajiri kwanza ili tuwasaidie maskini.
- Kila kitu kinasababishwa, kuna kichochea cha kila kitu, kwa hivyo ili uwe tajiri lazima uchochee kwa kutafuta na ukiwa maskini pia ni wewe umechochea umaskini huo.
- Hakuna njia moja pekee ya kujenga utajiri. Yapo njia nyingi halali mno za kujenga utajiri.
- Kama wengine wameweza kuwa matajiri na mimi ninaweza kupata utajiri mkubwa. Naamini kabisa ndani yangu kuwa, naweza kuwa tajiri na wewe rafiki unaweza kuwa tajiri.
Chukua hatua; rafiki moja kati ya mafanikio kwenye maisha ni kuwa na mtazamo sahihi juu ya mafanikio yako kwa ujumla. Kwa hivyo basi tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi ili tuweze kuijenga utajiri.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.